Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Tuesday, November 4, 2014

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UZALISHAJI WA AJIRA NCHINI

Mkurugenzi wa Ajira toka Wizara ya kazi na Ajira Bw.Ally Msaki akiongea na waandishi wa habari kuhusu kasi ya uzalishaji wa nafasi za ajira nchini ambapo katika kipindi cha miezi 3 kuanzia Julai hadi Septemba 2014 jumla ya ajira 139,361 zimezalishwa. Kushoto ni Msemaji wa Wizara hiyo Ridhiwani Wema.Posted By  Tupambane blog
Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Ridhiwani Wema akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mikakati ya Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya waajiri kuongeza fursa za ajira hapa nchini.kushoto ni Afisa Kazi Mkuu Bi Amina  Likungwala.
(Picha na Frank Mvungi)
………………………………………………………………………..
Frank Mvungi
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuimarisha mazingira ya uzalishaji ajira katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ambapo ajira 139,361 zimezalishwa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya kazi na Ajira Bw. Ridhiwani Wema wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika Mkutano huo Wema alisema kuwa kati ya ajira zilizozalishwa 3,657 ni ajira za Serikalini na 135,704 ni ajira kupitia sekta binafsi.
Akifafanua zaidi Wema amesema, kwa kipindi cha mwaka 2011/12 ajira zilizolalishwa ni 250,678 ambapo mwaka 2012/2013 zilizalishwa ajira 274,030.
Kwa mwaka 2013/2014 ajira 408,756 zilizalishwa na mwaka 2014/15 jumla ya ajira 560,000 zilitarajiwa kuzalishwa katika sekta binafsi rasmi.
Aidha katika kipindi cha mwaka 2013/14 sekta binafsi rasmi imezalisha ajira 408,706 kupitia uwekezaji binafsi ambapo baadhi ya maeneo hayo ni Viwanda vidogo na kati ,Uwekezaji kupitia TIC,Sekta ya Mawasiliano na  nyingine.
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa sekta binafsi itafanya vizuri zaidi kwa kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa waajiri ili waweze kuongeza  fursa za ajira hapa nchini ambapo baadhi ya hatua zinazochukuliwa kwa sasa ni pamoja na kufanya marekebisho ya Sera ya Ajira ya mwaka 2008,Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini No. 6 ya mwaka 2004.
Marekebisho mengine yanayofanyika yanahusisha sheria ya Taasisi za Kazi na Ajira Na.7 ya mwaka 2004 pamoja na kutunga sheria mpya ya ajira za wageni Nchini ambayo imelenga kulinga ajira za watanzania,kuboresha mazingira ya Biashara na kuhamasisha uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG