Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

UFUGAJI


UFUGAJI BORA WA VIFARANGA VYA KUKU

Ni muhimu kuzingatia utunzaji wa vifaranga

Vifaranga waliyotunzwa vizuri
Vifaranga wanapotunzwa vizuri kama hawa hukua vizuri na kuwa kuku wenye afya

Kwa karne na miaka mingi, ufugaji wa kuku imekuwa ni kazi muhimu na inayokubalika katika jamii nyingi. Ni kazi isiyohitaji gharama kubwa sana, ambayo imekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa kwa wanaiofanya kibiashara.

Tatizo ambalo limekuwa sugu na kusababisha hasara kwa wafugaji walio wengi, ni kutofahamu namna bora ya kuwatunza vifaranga kuanzia siku ya kwanza wanapoanguliwa hadi kuwa kuku wakubwa. Hali hii imekuwa ikiwasababishia wafugaji hasara na kuwakatisha tamaa.

Hii inatokana na wafugaji kuzingatia kuwa na banda na chakula tu, bila kuzingatia aina nyingine ya matunzo muhimu yanayohitajika kwa ajili ya kuwafanya vifaranga waishi na kukua wakiwa na afya.

Haya ni baadhi ya mambo muhimu kuanzia siku ya kwanza ili vifaranga wako wasipate madhara na hatimaye kufa:

• Mara baada ya kuanguliwa, vifaranga wawekwe sehemu yenye joto kwa wastani unaohitajika.Kuku wenye afya 1
• Hakikisha sehemu ya banda ulipowaweka vifaranga ni kavu, na isiyokuwa na vimelea.
• Hakikisha vifaranga wote wanapata chanjo ya mahepe (mareks) siku ya kwanza.
• Siku ya saba, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa kideri.
• Inapofika siku ya 14, vifaranga wachanjwe dhidi ya ugonjwa wa gumboro.
• Rudia chanjo ya kideri katika siku ya ishirini na moja.
• Siku ya ishirini na nane, rudia tena chanjo ya gumboro
• Baada ya wiki nane, hakikisha kuwa vifaranga wako wanapata chanjo ya ndui.

Kwa kuzingatia mtiririko huo, utakuwa na uhakika kuwa kuku wako ni salama. Watakuwa bila tatizo, jambo ambalo litakupa uhakika wa kuwa na mazao bora, na hatimaye kupata faida.
Pamoja na hayo, hakikisha kuwa unazingatia lishe bora. Hii itasaidia kuwapa kuku afya njema na kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa.

**Kamwe usiwape kuku vyakula vilivyooza. Hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa kuku na kusababishia hasara.

 

SAMAKI WA MAKUNDUCHI HAWA...


  • Share on facebookShare on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Wako tayari sokoni...

Epuka kuchunga mifugo kwenye maeneo hatarishi


Licha ya kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazozalisha mifugo ya aina mbalimbali na kwa wingi kama vile ng’ombe, mbuzi, kondoo lakini inakabiliwa na upungufu mkubwa wa maeneo ya ufugaji sambamba na malisho ya kutosha kwa ajili ya mifugo hiyo.


Mbuzi barabaraniWafugaji walio wengi, wameshindwa kukabiliana na changamoto hizo hasa kwa kutenga maeneo maalum ya kuchungia au kufuga majumbani, na badala yake wanalazimika kuchunga mifugo hiyo katika maeneo hatarishi na yasiyofaa kwa shughuli hizo.

Maeneo hatarishi ambayo mara nyingi yamekuwa yakitumika kwa ajili ya kuchungia mifugo ni pamoja na pembezoni mwa barabara zinazopita vyombo vya moto kama magari, kwenye maeneo ya migodi, kwenye mashimo makubwa yaliyotokana na uchimbaji wa mawe, na hata katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa taka bila kujua madhara yanayoweza kuikabili mifugo yao.


Madhara yanayotokana na kuchunga katika maeneo hatarishi


eneo hatarishiMajalala
• Mifugo inapochungwa katika maeneo yanayotumika kutupa taka hula makaratasi, au nailoni ambazo huharibu mfumo wa chakula na kuzuia mfumo mzima wa umeng’enyaji.
• Mifugo huweza pia kula vitu vilivyotupwa vyenye sumu ambazo huharibu mfumo wa chakula vile vile na hata kusababisha vifo.
• Wanyama huweza kuchomwa na vitu vyenye ncha kali kama vile vyuma wakiwa katika harakati za kula. Vyuma hivyo vinaweza kuwadhuru kwenye miguu au hata mdomoni wakati wa kula na kuwajeruhi hata kupelekea kifo kutokana na kuwa vitu hivyo wakati mwingine huweza kuwa na sumu ambayo huleta madhara kwenye mwili wa mnyama.


Migodini
• Mifugo inapochungwa katika maeneo ya migodi au pembezoni mwa migodi kwa mfano migodi ya dhahabu, huweza kula sumu (mercury poison) inayotokana na maji yaliyotumika kusafishia dhahabu.
• Sumu hiyo huharibu mfumo wa neva (nervous system) na huweza kusababisha mnyama kufa.


Maeneo yenye mashimo makubwa

• Mifugo inapofugwa kwenye maeneo yenye mashimo makubwa hasa yaliyotokana na uchimbaji wa mawe huweza kuumizwa na wanyama wakali kama vile nyoka ambao huwadhuru mifugo na kusababisha madhara makubwa mwilini na hata kusababisha mnyama kufa.
• Ikiwa wanyama wanachungwa katika maeneo ya mashimo makubwa huweza kuanguka na kuvunjika miguu na hata kupoteza uhai.
• Wakati mwingine mifugo huweza kupotea. Mfano; ndama wanaweza kuachwa wakiwa wamelala na wasijue kama mifugo mingine imehama na kwenda eneo lingine au wakati mwingine wakatumbukia kwenye mashimo na wasiweze kutoka.



Barabarani
• Mifugo kama itachungwa katika maeneo ya barabarani kunakopita magari, pikipiki na baiskeli huweza kupata ajali kwa kugongwa na hatimaye kuumizwa vibaya na hata kusababisha kifo.
• Majani yanayopatikana pembezoni mwa barabara yanapotumiwa na mifugo kama chakula huweza kuwadhuru kwani yana sumu (lead poison) ambayo hutokana na moshi wa vyombo vya usafiri. Ng’ombe anapokula majani hayo hupata matatizo kwenye mfumo wa neva na unaosababisha kupata upofu na kupoteza nguvu na hatimae kufa.


Mambo ya kufanya kuepukana na hayo;

• Kabla ya kuanza kufuga ni muhimu mfugaji ukatambua eneo ulilo nalo na
kiasi cha mifugo utakaoweza kuwafuga katika eneo hilo.
• Hakikisha eneo hilo litatosha kulisha mifugo yako hivyo hautohitaji kwenda kuchunga mifugo katika maeneo hatarishi kwa lengo la kukidhi lishe na kuwe na uwiano wa eneo na mifugo.
• Hakikisha unakuwa na malisho ya kutosha kwa wakati wote wa kufuga.
• Jenga mazoea ya kulisha mifugo yako nyumbani.
• Kata majani na wapatie wanyama katika mabanda uliyoandaa kwa ajili ya kulishia.
• Ikiwa utalazimika kutafuta malisho kwa ajili ya mifugo, basi epuka kuchunga
katika maeneo hatarishi, ni vyema ukachunga kwenye mashamba yaliyokwisha kuvunwa vyakula au katika maeneo maalumu yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya kulishia.
• Ni muhimu kutenga malisho maalumu ya mzunguko. Kuwa na maeneo mbalimbali kwa ajili ya kulishia kwa nyakati tofauti. Hii itasaidia kukidhi chakula cha mifugo hata wakati wa ukame.






ZAKANUNI  UFUGAJI BORA WA MBUZI NA KONDOO




1.. Utangulizi
Mbuzi na kondoo wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu nakuishi katika mazingira magumu kama ya maradhi na ukame ikilinganishwa na ng’ombe. Kutokana na umbillao dogowanaweza kufugwa katika eneo dogo na pia wanaweza kuhudumiwa na familia yenye nguvukazi na kipato kidogo. Uzaowa muda mfupi unamwezesha mfugaji kupata mbuzi/kondoo wengikwa kipindi kifupi. Wanyama hao hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwangozi, sufu na mazao mengine kwa matumizi ya familia nakuongeza kipato. Ufugaji bora wa mbuzi na kondoo uzingatie kanuni zifuatazo:-
i)       Wafugwe kwenye banda au zizi bora,
ii)      Wachaguliwe kutokana na sifa za koo/aina na lengo la uzalishaji
(nyama, maziwa au sufu),
iii)      Wapatiwe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili,
iv)      Kuzingatia mbinu za kudhibiti magonjwa kama inavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo,
v)      Kuweka na kutunza kumbukumbu sahihi za uzalishaji; na
vi)      Kuzalisha nyama, maziwa au sufu yenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko

2. Zizi au Banda la Mbuzi/Kondoo

Mbuzi/kondoo wanaweza kufugwa katika mifumo ya huria, shadidi na kwa kutumia njia zote mbili. Zizi hutumikakatika mfumo huria ambapo mbuzi/kondoo
huchungwa wakati wa mchana na kurejeshwa zizini wakati wa usiku. Zizi bora nlillenye sifa zifuatazo:-
•    Lililo imara linaloweza kumkinga mbuzi/kondoo dhidi ya wanyama hatari na wezi,
•    Lililojengwa mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama,
•    Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo. Ni vema mbuzi/kondoo watengwe kulingana na umriwao; na
•    Liruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.

Palambapo mbuzi/kondoo wanafugwa kwa mfumo wa shadidi hufugwa katika banda wakati wote. Bandabora la mbuzi/kondoo linatakiwa kuwa na sifzifuatazo:-
•    Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali,upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari,
•    Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi,
•    Lijengwe sehemu isiyoruhusu maji kutuama na liwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu. Pia ujenziuzingatie mwelekeo wa upepo ili hewa kutoka bandani isiende kwenye makazi,
•    Liwe na sakafu ya kichanja chenye urefu wa mita 1 kutoka ardhini (Kwa banda la mbuzi),
•    Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji na mahali pa kuweka jiwe la chumvichumvi; na
•    Liwe na vyumba tofauti kwa ajili ya majike na vitoto, mbuzi/kondoo wanaokua, wanaonenepeshwana wanaougua.

3. Vifaa vya Kujengea na Vipimo vya Banda
Inashauriwa banda la mbuzi/kondoo lijengwe kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi katika eneo husika. Ukubwa wa  banda utategemea idadi  ya

mbuzi/kondoo wanaofugwa humo na ukubwa wa umbo kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na. 1
JedwalNa 1: Eneo la mbuzi/kondoo linalotakiwa
Kundla Mbuzi/Kondoo               Eneo kwa Mnyama Mmoja
(Mita2)
Vitoto                                                                  0.3
Wasio na mimba                                                  1.5
Wenye mimba                                                     1.9
Dume                                                                   2.8

•    Paa lijengwe kwa kutumia vifaa kama miti, mbao, na kuezekwa kwa nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati au hata vigae kwa kutegemea uwezo wa mfugaji,
•    Kuta zijengwe kwa kutumia mabanzi, mbao, nguzo, wavu wa waya, fito na matofali. Kutziwe imarazinazoruhusu hewa na mwanga wa kutoshaMlango uwe na ukubwa wa sentimita 60 x 150,
•    Sakafu inaweza kuwa ya udongo au zege. Sakafu ya kichanja inaweza kujengwa kwa kutumia miti,fito, mianzi, mbao au mabanzi na iweze kuruhusu kinyesi na mkojo kupita. Chumba cha majike navitoto kiwe nnafasi ya sentimita 1.25 kati ya papi na papi, fito na fito au mti hadi mti. Chumba chambuzi/kondoo wakubwa iwe sentimita 1.9 kati ya mbao na mbao.

4. Uchaguzwa Mbuzi/Kondoo wa Kufuga
Madhumuni ya kuchagua mbuzi au kondoo wa kufuga ni kuboresha uzalishaji na kuendeleza kizazi bora. Kunaaina nyingi za mbuzi/kondoo wanaoweza kufugwa kulingana na mazingira na mahitaji ya mfugaji. Uchaguzihufanyika kwa kuangaliumbile, uzalishaji na kumbukumbu za wazazi kama vilumbo kubwa, ukuaji waharaka, uwezo wa kutunza vitoto na kutoa maziwa mengi.
Mbuzi wanaofaa kwa ajili ya maziwa ni aina ya Saanen, Norwegian na Toggenburg pamoja na chotara wao.

Mbuzi wanaofaa kwa ajili ya nyama nBoer na chotara wao, mbuzi wa asili kama vile Pare white, Newala na Ujiji.Mbuzi aina ya Malya (Blended) wanafaa kwa ajili ya nyama na maziwa. Aidha, kondoo aina ya
Aidha, kondoo aina ya Black Head Perrsian (BHP), Masai na Red Suffalk Hampshire wanafaa kufugwa kwa ajili yanyama. Merino na Lincoln hufugwa kwa ajili ya sufuwakati Corriedale na Romney hufugwa kwa ajili ya nyama nasufu. Hapa Tanzanikondoo wanaopatikana kwa wingi ni Black Headed Persian, Masai Red Dopper na kondoowengine wa asili.

Mbuzi/kondoo jike wanaofaa kwa ajili ya kuzalisha maziwa na nyama wawna sifzifuatazo:-
•    Historia ya kukua upesi, kuzaa (ikiwezekana mapacha) na kutunza vitoto vizuri,
•    Umbo la mstatili linaloashiria utoaji wa nyama nyingi; na
•    Asiwe na ulemavu wa aina yoyote

Sifa za Ziada kwa Mbuzwa Maziwa

•    Awe na miguu ya nyuma iliyo imara na iliyonyooka na yenye nafasi kwa ajili ya kiwele; na
•    Awe na kiwele kikubwa na chuchu ndefu zilizokaa vizuri
  Sifa za Dume

Dume bora awe na sifzifuatazo:-
•    Miguu iliyonyooka, imara na yenye nguvu,
•    Asiwe na ulemavu wa aina yoyote,
•    Mwenye uwezo na nguvu ya kupanda; na
•    Mwenye kokwa mbili zilizo kaa vizuri na zinazolingana
Angalizo: Dume lichaguliwe kwa makini kwa sababu “dume ni nusu ya kundi”.

5. Utunzajwa Vitoto vya Mbuzi/Kondoo
Utunzaji huanza mara tu baada ya kuzaliwaMfugaji ahakikishe:-
•  Kitoto cha mbuzi/kondoo kinapata maziwa ya mwanzo (dang’a) ndani ya masaa 24 tangu kuzaliwa nakwa muda wa siku 3,
•  Kama kinanyweshwa maziwa, kipewe lita 0.7- 0.9 kwa siku. Maziwa haya, ni muhimu kwani yana viinilishena kinga dhidi ya magonjwa,
• Iwapo mama hatoi maziwa au amekufa, inashauriwa kutengeneza dang’a mbadala au kama kunambuzi/kondoo mwinginaliyezaanaweza kusaidia kukinyonyesha kitoto hicho,
•    Kitoto cha mbuzi/kondoo kiendelee kunyonya kwa wiki 12 - 16. Wiki baada ya kuzaliwa, pamoja namaziwa, kianze kupewa vyakula vingine kama nyasi laini na chakula cha ziada ili kusaidia kukua kwatumbo. Aidha, kipewe maji wakati wote,
•    Vyombo vinavyotumika kulishia vinakuwa safi muda wote,
•    Kitoto cha mbuzi/kondoo kiachishwe kunyonya kikiwa na umri wa miezi 3 hadi
4 kutegemea afya yake; na
•    Vitoto vipatiwe kinga na tiba ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam wa mifugo.

6. Matunzo Mengine
Utambuzi

Mbuzi huwekewa alama ili atambulike kwa urahisi na kuwezesha utunzaji wa kumbukumbu zake. Shughuli hiihufanyika kwa mbuzi/kondoo akiwa na umri wa siku 3 - 14. Njia zitumikazo ni pamoja na:
•         Kuweka alama sikioni kwa kukata sehemu ndogo ya sikio,
•         Kumpa jina kwa wafugaji wenye mbuzi wachache,
•         Kumvisha hereni ya chuma au plastiki yenye namba kwenye sikio,
•         Kumvalisha mkanda wenye namba shingoni; na

•         Kuweka namba kwa kuunguza sehemu ya ngozi ya mbuzi. Pale mfugajanapotumia njia hiiinashauriwa aweke alama kwenye eneo ambalhalitaathiri ubora wa ngozi
Kuondoa vishina vya pembe

Mbuzi/kondoo aondolewe vishina vya pembe akiwa na umri kati ya siku hadi 14Visipoondelewa hukua nakusababisha kuumizana na kuhitaji nafasi kubwa
kwenye banda. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo.
Kuhasi

Vitoto vya mbuzi/kondoo ambavyo havitatumika kwa ajili ya kuendeleza kizazi vihasiwe kabla ya kufikia umri wamiezi 3. Kazi hii ifanywe na mtaalam wa mifugo.

7. Utunzajwa Mbuzi/Kondoo wa Miezi 4 - 8

Mbuzi wa miezi 4 mpaka 8 ni walambao wameacha kunyonya mpaka umri wa kupandishwa kwa mara yakwanzaMbuzi wa umri huu wana uwezo wa kula aina mbalimbali za malisho kama nyasi, mikunde, miti malishona mabaki ya mazao wakati kondoo hupendelea zaidi nyasi fupi. Wakati wa kiangazi huhitaji kupatiwa chakulacha ziada au kupewa pumba znafaka mbalimbali, mashudu ya alizeti, pamba na dengu, majani ya mikunde yaliyokaushwa, madini na vitamini.
Katika ufugaji huria ni vema kuzingatia idadi ya mbuzi/kondoo inayoweza kuchungwa katika eneo, ainana hali ya malisho.

Ili mbuzi/kondoo aweze kukua na kufikia uzito wa kuchinjwa/kupevuka mapema, mfugaji anapaswa kufuatakanuni zufugaji bora zifuatazo:-
•    Kumpatia vyakula vya ziada kwa muda wa miezi 2 mfululizo kiasi cha kilo 0.2 –0.7 kwa siku kuanziaanapoachishwa kunyonya,
•    Kumpatia dawa ya kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3 na kutoa kinga za magonjwa mengine kamaitakavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo,

•    Kuchanja na kuogesha ili kuzuia magonjwa mbalimbali,
•    Kukata kwato mara zinapokuwa ndefu; na
•    Kuhasi madume yasiyotumika kuzalisha.

8. Umri wa Kupandisha Mbuzi/Kondoo
Mbuzi/kondoo wakitunzwa vizuri wanaweza kupandishwa wakiwa na umri wa
miezi hadi 12 kwa mbuzi/kondoo walioboreshwa na miezi 18 hadi 24 kwa mbuzi wa asili kutegemea afya yake.Hathivyo, inashauriwa wapandishwe wanapofikiuzito wa kilo 12 au zaidi na wasipandishwe mbuzi/kondoo waukoo mmoja.
Dalilza joto

Mfugaji anashauriwa asimpandishjike kabla hajafikisha umri wa kupandwa wa miezi hadi 12 kwambuzi/kondoo walioboreshwa na miezi 18 hadi 24 kwa mbuzi wa asili hata kama ataonyesha dalili ya kuhitajidume. Mbuzi/kondoo aliyezaa anaweza kupandishwa siku 30-60 baada ya kuzaa. Mbuzi/kondoo aliyeko kwenyejoto huonyesha dalili zifuatazo:-
•    Hutingisha/huchezesha mkia,
•    Hupanda na kukubali kupandwa na wengine,
•    Hutoa ute mweupe ukeni,
•    Huhangaika mara kwa mara na kupiga kelele,
•    Hufuata madume,
•    Hamu ya kula hupungua,
•    Hukojoa mara kwa mara,
•    Uke huvimba na huwa mwekundu kuliko ilivyo kawaida; na
•    Kwa mbuzi anayekamuliwa hupunguza kiwango cha maziwa

Mbuzi/kondoo apelekwe kwa dume mara tu dalili za joto zinapoonekana kwanjoto hudumu kwa wastani wasiku (saa 48). Chunguztena dalili zjoto baada ya siku 1hadi 2na kama dalili hazitaonekana tena kunauwezekano mkubwa
kuwa   mbuzi/kondoo   amepata   mimba.   Mfugaji   apange   msimu   mzuri   wa mbuzi/kondoo kuzaaMsimumzuri ni mara baada ya mvua.

9.   Utunzajwa Mbuzi/Kondoo MwenyMimba

Kwa kawaida mbuzi/kondoo hubeba mimba kwa muda wa miezi 5. Utunzaji wa mbuzi/kondoo mwenye mimbani muhimu kwani ndiyo chanzo cha kupata vitoto vyenye afya bora. Mfugaji anashauriwa kufuata kanunizifuatazo:
•    Apatiwe vyakula vya ziada kilo 0.2 – 0.7 kwa siku ili kutosheleza mahitaji yake na kitoto kinachokuatumboni,
•    Apatiwe nyasi, miti malisho na mikunde mchanganyiko kilo 1.8 – 2.5 kwa siku.
Dalilza Mbuzi/Kondoo Anayekaribia Kuzaa

•    Huhangaika kwa kulala na kuamka mara kwa mara,
•    Sehemu ya nje ya uke hulegea,
•    Hujitenga na kundi na hutafuta sehemu kavu na yenye kivuli,
•    Hupiga kelele; na
•    Hutokwa na ute mzito ukeni.
Mfugaji akiona dalili hizi anashauriwa asimruhusu mbuzi/kondoo kwenda machungani, bali amtenge kwenyechumba maalum, ampatie maji ya kutosha na kumuandalia sehemu ya kuzalia.

10.  Utunzaji wa Mbuzi/Kondoo Anayenyonyesha
Mbuzi/kondoo anayenyonyesha huhitaji chakula kingi zaidi ili kukidhi mahitaji ya mwili na kuzalisha maziwa kwaajili ya kitoto/vitoto. Pamoja na nyasi, mikunde na majani ya miti malisho kilo 1.8 – 2.5 kwa siku ni muhimuapewe chakula cha nyongeza kilo 0.3 – 0.8 kwa kila lita ya maziwa inayoongezeka baada ya lita 2 na maji safi,salama na ya kutosha wakati wote.

Taratibu za Kuzingatia Katika Ukamuaji wa Mbuzi wa Maziwa
Lengo la ufugaji wa mbuzi/kondoo wa maziwa ni kupata maziwa mengi, safi na salama pamoja na mazaoyatokanayo na maziwaMambo muhimu ya kuzingatini:-
•    Sehemu ya kukamulia iwe safi na yenye utulivu,
•    Mbuzi/kondoo awe na afya nzuri, msafi, na kiwele kioshwe kwa maji safi ya uvuguvugu,
•    Mkamuaji asibadilishwe badilishwe awe msafi, mwenye kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza,
•    Vyombo vya kukamulia viwe safi; na
•    Maziwa ya mwanzo kutoka kila chuchu yakamuliwe kwenye chombo maalu(strip cup) ilikuchunguzugonjwa wa kiwele.

11. Utunzaji wa Dume Bora la Mbegu
Dume bora la mbegu ni muhimu litunzwe ili liwe na uwezo wa kutoa mbegu bora, kupanda na kuzalisha. Dumebora huanza kupanda akiwa na umri kati ya miezi.8 -
10 kwa mbuzi walioboreshwa. Katika msimu wa kupandisha dume moja liruhusiwe kupanda majike 40 hadi 50.Aidha, inashauriwa madume wenye umri wa miezi 8 –
9 waruhusiwe kupanda majike ambao ndio mara ya kwanza kupandwa.

Dume apatiwe:-
•    Malisho ya kutosha na vyakula vya ziada kiasi kisichopungua kilo 0.2 – 0.7 kwa siku na maji ya kutosha,
•    Majani ya miti malisho, mikunde na nyasi mchanganyiko na mabaki ya mazao; na
•    Kilo 0.45 hadi 0.za chakula cha ziada za nyongeza kwa siku kulingana na uzito wake na wingi wamajike anayopanda.wiki 2 kabla na baada ya kuanza kupanda.


12.    Matunzo Mengine

Kukata Mkia

Mara nyingine kondoo hukatwa mkia ili kuruhusu mtawanyiko mzuri wa mafuta katika misuli mwilini. Piakondoo aliyekatwa mkia huwa msafi. Kazi hii ifanywe kama itakavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo kwakutumia vyombo maalum. Inashauriwa mkia ukatwe urefu wa sentimita 2.5 – 3.8 kutoka kwenye shina la mkiawakati kondoo akiwa na umri wa siku 3 mpaka mwezi 1.
Kumnyoa Kondoo wa Sufu

Sufu hunyolewa wakati kondoo akiwa hai au amechinjwa. Kwa kawaidhunyolewa miezi hadi mwaka 1ambapo sufu huwa imefikia urefu wa sentimita
15 – 20. Vifaa vinavyotumika ni pamoja na mikasi au visu maalum. Uangalifunahitajika wakati wa kunyoa ilingozi ya kondoo isiharibike. Unyoaji ufanyike wakati wa kiangazi na siyo wakati wa mvua, kondoo akiwa namimba au kipindcha majani kutoa mbegu.

13.  Udhibitwa Magonjwa ya Mbuzna Kondoo
Magonjwa husababishwa na vimelea jamii ya virusi, bakteriaprotozoa na riketsiaMagonjwa menginehusababishwa na upungufu wa viinilishe, vitamini na protini. Dalili za mbuzi/kondoo mgonjwa ni pamoja na:-
 Manyoya husimama,
 Kuzubaa, kusinzia, kukohoa na kupiga chafya,
 Kukosa hamu ya kula na kunywa maji,
  Kujitenga na kundi,
  Kuvimba taya la chini,
  Kupumua kwa shida,
 Kutokwa na machozi na makamasi,
 Kuwa na upelau uvimbe kwenye sehemu ya mwili; na
 Kutupa mimba.
•    Hatua za haraka za kumuona mtaalamu wa mifugo zichukuliwe iwapo baadhi ya dalili hizizitaonekana,

•    Mbuzi na kondoo wachanjwe dhidi ya magonjwa ya homa ya maapafu.
Ugonjwa huu ni hatari sana na huenea kwa njia ya hewa na unaweza kusababisha vifo kati yaasilimia 60-100,
•    Kila baada ya miezi 6 mifugo ipatiwe kinga dhidi ya ugonjwa wa miguu na midomo na magonjwa mengine kama Kimeta, bondla ufa, kutupa mimbna chambavu (BQ) zitolewe kulingana na ushauri wa mtalaam wa mifugo,
•    Kama kuna wanyama walioathirika watengwe kwenye kundi, wasisafirishwe au kuuzwa,
•    Mbuzi/kondoo wapatiwe dawa ya minyoo Vitoto vya mbuzi/kondoo vipatiwe dawa ya minyoo vinapofikiaumri wa mwezi 1. Viendelee kupatiwa dawa ya minyoo kila mwezi hadi vinapofikia miezi na baada yahapo vipatiwe dawa ya minyoo kila baada ya miezi 3 - 4; na
•    Zingatia usafi wa banda ili kuwakinga na ugonjwa wa kuharisha na kuharisha damu na magonjwambalimbali.

14.  Utunzajwa Kumbukumbu za Mifugo
Kuweka kumbukumbu za mifugo ni muhimu katika uzalishaji kwa ajili ya kutambua kosaafu, gharama za utunzajina faida. Piahumsadia mfugaji kufanya maamuzi katika uendelezaji wa ufugaji wake. Mtalaamu wa mifugo piaanaweza kutumia kumbukumbu hizi ili kumsaidia mfugaji kuboresha ufugaji wake.
Kumbukumbu muhimu zinazohitajika kutunzwa ni:-
•    Kumbukumbu za idadi na ukuaji wa wanyama waliopo, jinsi zao, uzito wa mbuzi/kondo kwa  kil mwezi il kufuatili ukuaj wake tareh ya kuachishwa kunyonya na idadi ya waliouzwa,
•    Kumbukumbu ya uzazi zinazoonyesha tarehe ya kuzaliwa, namba yake, jinsi yake, aina (breed)namba yadume/jike, na uzito wa kuzaliwa,
•    Kumbukumbzupandishaj zinazoonyesh namba  ya  mbuzi/kondoanayepandwatarehe ya joto naya kupandwa, namba ya dume lililotumika kupanda, tarehe ya joto la pili kama atarudia na tarehe ya kuzaa,
•    Kumbukumbu   za   chanjo   na   matibabu   zinazoonyesha   namba   ya mbuzi/kondoo, tarehe yamatibabu, aina ya chanjo au ugonjwa, dawa iliyotumikaidadi ya waliokufa na waliopona na jina la mtaalamaliyetibu,
•    Kumbukumbu za maziwa zinazoonyesha namba ya mbuzi/kondoo, tarehe ya kuzaa, kiasi cha maziwa kwasiku, na kiasi cha maziwa kwa kipindi chotcha kukamuliwa, tarehe ya kuacha kukamua na idadi ya sikualizokamuliwa,
•    Kumbukumbu za mapato na matumizi zinazoonyesha mapato na matumizi, vitu vilivyouzwa au kununuliwakwa siku, kiasi cha fedha unachokuwa nacho kila wakati, kiasi cha fedha unachodai na kudaiwa.

Dalili za mwanzo za joto

Kusimama: Ng’ombe kusimama anapopandwa na wenzake au dume ni dalili tosha kuwa yupo katika wakati muafaka na joto linalostahili kufanyiwa uhamilishaji. Ng’ombe wanahitaji nafasi ya kutosha ili kuchangamana. Hili halitawezekana kwa ng’ombe anaefugwa ndani, na endapo ni ng’ombe mmoja tu anafugwa. Muda wa wastani wa joto la kusimama ni kati ya saa 15 hadi 18, lakini pia huweza kutofautiana kutoka saa 8 hadi 30.














Dalili zinazofuata 
Dalili hizi huweza kutokea kabla, wakati au baada ya joto la kusimama. Mfugaji anatakiwa kumchunguza ng’ombe husika kwa ukaribu zaidi hasa katika kipindi cha awali cha dalili za joto.

Kupanda ng’ombe wengine: Ng’ombe anayeonesha tabia hii huweza kuwa katika joto au kukaribia joto.













Kutokwa ute: Hii ni dalili isiyofungamana moja kwa moja na joto la kusimama. Ute huzalishwa kutoka katika mfuko wa uzazi na hujilimbikiza pamoja na majimaji mengine katika uke kabla na muda mfupi baada ya kipindi cha joto kupita.

Kuvimba na wekundu katika uke: Wakati wa joto vulva huvimba, huwa na unyevu na wekundu kwa ndani. Kwa ujumla dalili hizi huonekana kabla ya joto na hubaki kwa muda mfupi baada ya joto.

Kutokutulia: Ng’ombe anapokuwa katika hali hii huwa hatulii, huhangaika, hukosa kupumzika na hata hula kidogo sana kuliko wengine.

Kunusa: Ng’ombe anapokuwa kwenye joto hunusa na kulamba uke wa ng’ombe wengine mara kwa mara.

Mambo yanayoathiri uhitaji wa ng’ombe kupandwa

Mambo mbalimbali yanayohusiana na mazingira, afya ya ng’ombe na lishe yanaweza kuathiri uhitaji wa ng’ombe kupandwa.

Banda: Mpangilio wa banda linaloruhusu ng’ombe kuingiliana au kuwa pamoja wakati wote hutoa mwanya kwa ng’ombe kupandwa na tabia ya kusimama hudhihirika kwa urahisi.

Sakafu: Tendo la kupanda hufanyika mara nyingi zaidi ikiwa ng’ombe wapo katika eneo la udongo au kwenye nyasi badala ya sakafu ya saruji. Hali ya utelezi, tope pamoja na kukosekana kwa nafasi ya kutosha huzuia kupandana.

Matatizo ya miguu: Ng’ombe mwenye matatizo au kidonda miguuni huwa na kiwango cha chini cha kupandisha kutokana na sababu kuwa hushindwa kuonyesha ushirikiano kwani hukwepa zaidi kupata maumivu.

Joto: Ng’ombe huonyesha zaidi kuhitaji kupandwa hasa katika kipindi cha baridi kuliko kipindi cha joto.

Muda wa kupandisha: Kupandisha mara nyingi hufanyika wakati wa asubuhi au mapema wakati wa jioni. Ng’ombe akionekana kuwa kwenye joto kabla ya 12:00 asubuhi ni lazima apandishwe siku hiyo hiyo, wakati ng’ombe aliyeonekana kwenye joto baada ya mchana ni lazima kupandishwa mapema siku ya pili.

DALILI ZA KUTAMBULISHA NG'OMBE ALIYE KWENYE JOTO

Uzalishaji wenye faida kwa ng’ombe wa maziwa huhitaji uangalizi wa karibu, unaowezesha kutambua ni wakati gani ng’ombe ana joto, hivyo kufanya uhamilishaji kwa wakati unaotakiwa.


Kushindwa kutambua joto ni chanzo kikubwa cha urutubishaji hafifu. Mbali na Tanzania, kulingana na utafiti uliofanywa na chuo cha PennState huko Marekani, takriban nusu ya joto hushindwa kutambulika katika uzalishaji wa maziwa nchini humo.

Hata hivyo, kutokana na utafiti juu ya kiwango cha homoni kilichopo kwenye maziwa, inaonekana kuwa takribani asilimia 15 ya ng’ombe waliotakiwa kufanyiwa uhamilishaji hawakuwa katika joto sahihi. Kutokana na hali hiyo, husababisha hasara kiuchumi kutokana na kuongezeka kwa vipindi tofauti vya kuzaa pamoja na kuongezeka kwa gharama za ziada za uhamilishaji.

Ni muhimu kuweka kumbukumbu ya taarifa zote za joto kuonesha kama ng’ombe anafaa kuhimilishwa au hapana. Utambuzi wa joto husaidia kujua kama kuna matarajio ya kuwepo kwa joto linalostahili hapo baadaye. Hata hivyo, mzunguko mrefu usio wa kawaida pamoja na vipindi virefu kutoka kuzaa kwa mara ya kwanza vyaweza kufuatiliwa.

Kwa kawaida, ng’ombe huwa katika joto mara moja kila baada ya siku 17 hadi 25. Ng’ombe huonyesha ishara ya kwanza ya joto ndani ya wiki 3 hadi 4 baada ya kuzaa.
Wakati muafaka wa kumshughulikia ng’ombe ni kati ya siku 45 hadi 90 baada ya kuzaa. Uhamilishaji wa aina yoyote utakaofanyika kabla ya siku 45 baada ya kuzaa hutoa mwanya finyu wa ng’ombe kushika mimba.

UFUGAJI WA KUKU AINA OTE

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa utasaidia Wananchi wetu kimahitaji.
LEKIDEA inalenga kuhamasisha na kukuza ufugaji wa Kuku wa Kisasa kwa Wananchi wetu

Ufugaji wa Mbuzi yafaa uwe wa Kisasa zaidi

Ufugaji wa Mbuzi wa Kisasa

Mbuzi wa Kisasa huzaa kwa Manufaa na pia hufanikisha kukua kwa idadi ya mifugo.

LEKIDEA ina malengo ya kuhamasisha Wananchi wa Ukanda wetu Kufuga Mbuzi wa Kisasa kwa ajili ya Nyama na Maziwa kama wanaoonekana na inapowezekana waweze kupatiwa misaada ya huduma za Tiba ya mifugo na ukaguzi.

Uugaji wa Nguruwe unanufaisha Wananchi kibiashara.
Matunzo ya Nguruwe haka hivi, hasa kwa maeneo ya Vijijini kwetu ni wa muhimu na unatekelezeka endapo wananchi watahamasishwa na kuwezeshwa ipasavyo.

Nguruwe wakitunzwa vyema huzaliana haraka na hivyo kukuza kipato cha wananachi. Lengo la LEKIDEA ni kufanya mafanikio kama haya yaweze kutekelezeka kwa manufaa ya Wananchi wetu vijijini.
  
Ufugaji wa Ngombe wa Kisasa pia utawasaidia sana wanaviji wetu kujikwamua kiuchumi

Wananchi wetu wanaweza kuwezeshwa katika mikopo ili waweze kuimarisha ufugaji wa Ngombe kama hawa kwa ajili ya Maziwa, Nyama na Mbolea, na hivyo kukuza kipato na maendeleo yao na kufuta kabisa umaskini.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG