TUPAMBANE

Pages

  • Home
  • HABARI
  • MICHEZO
  • BURUDANI
  • MATANGAZO
  • DINI
  • PICHA
  • SIASA
  • CONTACTS
  • UFUGAJI
  • KILIMO
Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

HABARI

B Fasso:Mwili wa Sankara kufukuliwa




Mwili wa aliyekuwa rais wa Burkina fasso marehemu Thomas Sankara kufukuliwa
Serikali Burkina Fasso imeagiza kufukuliwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Thomas Sankara .
Watu wa familia ya rais huyo wamekuwa na wasiwasi kuhusu utambuzi wa maiti ya kiongozi huyo wa zamani.
Mjane wa marehemu Miriam,akizungumza kupitia njia ya simu kutoka Parisamesema, kuwa ufukuaji wa mwili huo utafanywa kulingana na agizo la mahakama ili kusaidia katika kuwatafuta waliotekeleza mauaji yake.
Bwana Sankara aliuawa mnamo mwaka wa 1987 katika mapinduzi yaliomfanya aliyekuwa rafikiye na mshirika wake mkuu Blaise Campaore kuchukua mamlaka.
Blaise Campaore aliondolewa mamlakani katika mapinduzi ya kiraia mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita.
Serikali mpya inayoongozwa na Michael Kafando ,ilisema kuwa italiangazia suala hilo wakati ilipochukua madaraka.
Mwili wa Sankara ulizikwa katika kaburi lisilotambulika miongoni mwa makaburi yaliopo mashariki mwa mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Viapo vya ndoa havitekelezeki.






Harusi na viapo visivyotekelezeka.

Ahadi ya kuwa pamoja maishani katika shida na raha,taabu na shida viapo hivi ama ahadi hizi zinaonekana kuchukuliwa kirahisi mno na wanandoa wapya, lakini kwa muujibu wa utafiti mpya uliotolewa hivi karibuni unathibitisha kuwa ni rahisi mno kutamka kuliko utekelezaji wa viapo vyenyewe .
Mtafiti uliofanywa kwa wanandoa wenye bahati 2,700 waliooana umegundua kwamba ,ikiwa mwanamke katika ndoa hiyo ataugua kwa muda mrefu asilimia sita hukaribia kupewa talaka kuliko wale ambao wana afya njema .
Ukilinganaisha na wanaume ambao huugua wakiwa kwenye ndoa,hatari ya kuvunjika kwa ndoa ni ndogo mno,hatahivyo upendo huendelea hadi hapo mmoja wao atakapo baki kuwa mgane ama mjane.
Utafiti ulioongozwa na wanazuoni wa chuo kikuu nchini Marekani,kinapendekeza kwamba kwa asili, wanawake wao wameumbwa kutoa huduma katika familia zao nah ii inamaanisha kwamba wanaume wao huwa hawana uvumilivu wake zao pindi wanapokumbwa na maradhi ya muda mrefu ,ambayo pia yanweza kuwa hayatabiriki kuyakabili.
Walifanyiwa utafiti wanandoa nchini Marekani,ambao wote walikuwa na umri wa miaka 50, mnamo mwaka 1990 ambao waliulizwa juu ya afya zao kuhusiana na maisha yao wakichnugza kwa miaka miwili,miwili ndani ya utafiti uliofanywa kwa miaka ishirini.
Asilimia thelathini na mbili ya ndoa ziliishia kwa kuachana na asilimia ishirini na nnenzilivunjika kutokana na vifo vya mmoja wa wanandoa.
Kikosi cha utafiti kiliongozwa na Amelia Karraker, ambaye ni profesa msaidizi juu ya masuala ya maendeleo ya binaadamu na utafiti juu ya familia kutoka katika chuo cha Iowa State University,analinganisha matukio ya namna nne kansa,magonjwa ya moyo,kiharusi na magonjwa ya njia ya hewa kwa wanawake na wanaume na matokeo ya ndoa.





Tamu na chungu ya ndoa

Utafiti huo umebainisha kwamba , kuna tofauti ya kujisikia mgonjwa sana na huwezi kupika chakula cha jioni, ama unahitaji mtu hasa wa kukulisha masuala haya yanaweza kubadili upepo ndani ya ndoa .
Katika hali hiyo,utafiti huo hauoneshi dhahiri kuwa mume ama mke anadai talaka,takwimu kamili zinaonesha kwamba wanawake ni wepesi zaidi kuomba talaka kuliko wenza wao.
Bi Karraker anasema amegundua kwamba kwamba inawezekana baadhi ya wanawake ambao huachwa kwasababu ya huduma zao ama kushindwa kuhudumia
Tafakari juu ya Uhai ama kifo husababisha watu wajitafiti wenyewe na kujiuliza maswali muhimu kuwa ni nini muhimu maishani mwao? Anaeleza mtafiti huyo.
Wanawake wakati mwingine huribuka kwa kusema kuwa waume zao hawawajali,na hawafurahishwi na suala hilo ama husema sikufurahishwa na mwanzo wa mahusiano yao, na wansema kwamba wako radhi kubaki peke yao kuliko kujitosa katika ndoa isiyofaa.


Mali haina wagonjwa wapya wa Ebola



Waziri wa Afya wa Mali amesema nchi hiyo kwa sasa haina 
maambukizi ya virusi vya Ebola baada ya siku 42 za 
kutokuwa na wagonjwa wapya walioambukizwa virusi vya 
ugonjwa huo .
"Natangaza siku hii, mwisho wa ugonjwa wa virusi vya Ebola 
nchini Mali," amesema Ousmane Kone.Mtu wa mwisho 
kuambukizwa Ebola nchini Mali alipona na kuruhusiwa 
kutoka hospitali mapema mwezi Desemba.
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa nchi tatu za 
Afrika magharibi zilizokuwa zimeathirika zaidi zote 
zimeshihudia kupungua kwa wagonjwa wapya wa Ebola.
Sierra Leone na Guinea zote zimekuwa na jumla ya 
chini kabisa ya wagonjwa waliothibitika kila wiki 
kuambukizwa virusi vya Ebola tangu mwezi Agosti, 
kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa 
zilizotolewa Alhamisi.
Liberia, ambayo haikuripoti wagonjwa wapya kwa muda 
wa siku mbili wiki iliyopita, ilikuwa na idadi ya chini 
kabisa kwa wiki ya mambukizi ya Ebola tangu mwezi Juni.
Idadi ya watu waliokufa kutoka na virusi vya Ebola 
imefikia watu 8,429, huku 21,296 wakiwa wameambukizwa.
Mali iliandikisha mgonjwa wa kwanza wa Ebola mwezi 
Oktoba, wakati mtoto wa miaka miwili kutoka Guinea 
alipougua na kufa.
Katika kipindi cha hali mbaya kabisa ya ugonjwa wa 
Ebola nchini humo watu 300 waliwekwa chini ya 
uchunguzi kuhusiana na maambukizi ya virusi vya Ebola.
Lakini nchi hiyo kwa sasa imeepukana na ugonjwa huo, 
amesema Ibrahima Soce Fall, mkuu wa ofisi ya 
Umoja wa Mataifa nchini Mali kuhusu Ebola (UMEER).
Ugonjwa wa Ebola unachukua siku 21 tangu mtu 
kuambukizwa hadi kujitokeza kwa dalili za ugonjwa 
huu na nchi ili kutangaza kuwa zimeondokana na 
maambukizi ya ugonjwa Ebola lazima zisiwe na
 wagonjwa wapya kwa vipindi viwili vya matazamio 
yaani siku 42.

VIJANA WATAKIWA KUJITUMA NA KUFANYA 

KAZI KWA KWA MAENDELEO YAO

Ndugu Elly David Akitoa Mada Kuhusu Vijana kujituma na 
kufanya kazi 
kwa Bidii Kwa maendeleo ya taifa.Mtoa Mada huyo 
amesema 
kutokana na Ukosefu wa ajira hususani kwa vijana ni vyeme 
vijana kujituma na kuwa w
abunifu na waweze kujiajiri kwa lengo la Kupambana katika M
aisha.Katika Kongamano hilo la Vijana lililofanyika Jijini 
dar es salaam Liliwapa 
Fursa vijana kueleza Changamoto zinazowakabili na namna ya Kuzikabili.Kongamano hilo lililoandaliwa na Elly David mara 
baada ya ya kuona changamoto zinazowakabili vijana wa 
itazania ili 
kuwapa fursa vijana kukutana kubadilishana mawazo Pamoja na 
Kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana wa 
Kitanzania

Hatukushambulia raia Somalia:Marekani















Mpiganaji wa Al ShababMarekani imesema kuwa bado inatafakari matokeo ya shambulio la anga lililofanyika Kusini mwa Somali kumlenga kiongozi mwandamizi wa kundi la wapiganaji wa Al Shabab.





Ndege za Marekan









Msemaji wa idara ya usalama ya Marekani amesema shambulio la anga katika karibu na eneo la Saakow halikuwa na dalili zozote za kuleta madhara kwa raia na hakuna 
raia 
waliodhurika.
Shambulio hilo limetekelezwa siku chache tangu mtu 
anayedhaniwa kuwa ni mfuasi wa kundi hilo kushambulia 
kambi ya majeshi ya Somalia na Jeshi la Muungano 
wa Afrika.

Marekani yatuma meli ya kivita 

Indonesia










Manowari ya Marekani

Wanamaji kutoka Marekani wamesema kuwa wanapeleka 
moja ya Manowari ya kivita kutafuta ndege ya AirAsia 
iliyopotea tangu jumapili katika Bahari za Indonesi.
Manowari hiyo ijulikanayo kwa jina la USS Sampson 
inatarajiwa kufika leo katika eneo la Java Sea today 
ikiwa ni siku ya tatu tangua kuanza msako dhidi ya 
ndege hiyo. Idadi ya wataalamu wa kimataifa 
wanaoitafuta ndege hiyo imeongezeka ambapo 
kwa sasa nchi za Singapore, Malaysia ,Australia,
Korea Kusini,Thailand na China wanashiriki katika 
kazi hiyo. Mkuu wa Operesheni ya uokoaji na 
utafutaji ndege hiyo Henry Bambang Soelistyo 
amesema kwa sasa kuna jumla ya Meli 30,ndege 
15 na Helkopita katika eneo la tukio. Ndege hiyo 
ilipotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Surabaya 
Indonesia kuelekea Singapore ikiwa na abiria 162.



BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YATOKEA SINGIDA MCHANA HUU KATI YA BASI LA ZUBERI NA COSTA...AMBAPO KATIKA COSTA HAKUNA ALIYEPONA

Bus la Zuberi No. 3 Limegongana uso kwa uso na costa. 
Hakuna aliyetoka kwenye costa na imekwisha  
nyang'anyang'a. Hali hii imepelekea waliokua kwenye 
magari mengine kushuka na  kuokoa majeruhi. Ni 
Mbele kidogo ya singida mjini. 






Ajali yaua 10 Mbeya, wanane wajeruhiwa




 WATU 10 wakiwemo watoto wadogo wawili, wamekufa papo 
hapo baada ya gari 
dogo la abiria aina ya Toyota Hiace  kulivaa lori aina ya 
Fuso katika eneo la 
Mbalizi mkoani Mbeya.
Katika ajali hiyo iliyotokea jana saa 4 asubuhi, watu saba 
walijeruhiwa miongoni 
mwao wakiwa katika hali mbaya.
Watu walioshuhudia ajali hiyo waliliambia MTANZANIA 
Jumamosi kuwa gari la 
abiria aina ya Hiace yenye namba za usajili T237
 iliyokuwa ikitokea jijini Mbeya 
kwenda Mbalizi, ililivaa lori  aina ya T 158 CSV lililokuwa 
ikitokea kwenye kituo 
cha mafuta kilichopo eneo la Mbalizi.
Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi 
akithibitisha kutokea 
kwa ajali hiyo huku akisema kuwa jeshi lake linachunguza
chanzo, taarifa za 
awali kutoka kwa mashuhuda zinaeleza ajali hiyo 
ilisababishwa na dereva wa 
Hiace ambaye alishindwa kulidhibiti gari lake lililokuwa
 likishuka kwenye 
mteremko mkali wa Mlima Mbalizi.
Maelezo ya watu mbalimbali walioshuhudia tukio hilo 
pia  yalionekana 
kumuelekezea lawama dereva wa lori ambaye walidai 
kuwa aliingia barabarani 
bila kuchukua tahadhari.
Kamanda Msangi kwa upande wake aliwataja miongoni 
mwa waliokufa 
katika ajali hiyo kuwa ni dereva wa Hiace aliyetambulika
 kwa jina la Petro 
Mngo’ngo.
Aliwataja wengine waliopoteza maisha katika ajali hiyo 
kuwa ni watoto 
wawili wa kiume, wanawake wanne na wanaume wanne.
Kwa upande wa majeruhi, Kamanda Msangi alisema 
wanne kati ya saba 
wanapatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ifisi na 
watatu 
wamekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Gazeti hili lilifika katika Hospitali Teule ya Ifisi, ambako 
Muuguzi Mkuu, 
Sikitu Mbilinyi alilithibitishia kupokea miili 10 na majeruhi saba.
Alisema majeruhi waliopokelewa ni wanawake watatu na 
wanaume wanne, 
kati yao wanaume wawili na mwanamke mmoja 
walikimbizwa katika 
Hospitali ya Rufaa kutokana na hali zao kutokuwa nzuri.
Muuguzi huyo alisema miili ya marehemu hao 
imehifadhiwa katika
 chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo ya
 Ifisi na kuwataka 
ndugu na jamaa kufika kwenye hospitali hiyo kwa ajili 
ya kutambua 
marehemu hao.
Aidha, MTANZANIA lilifanikiwa kuzungumza na
 kondakta wa Hiace 
ambaye kutokana na hali yake kutokuwa nzuri 
aliweza kujitambulisha
 jina lake kuwa ni Justin Chaula na mwingine ni 
Neima ambao wote 
wamelazwa katika hospitali hiyo ya Ifisi.
Akielezea kutokea kwa ajali hiyo, shuhuda Saidi 

Nzowa (44) ambaye ni 
dereva wa lori la mafuta Kampuni ya ASAS, alisema:
“Inavyoonyesha gari ya abiria ilifeli breki ndio maana 
dereva alishindwa 
kuisimamisha na kulivaa lori hilo ambalo lilikuwa tayar
 limeingia barabarani.
Mtanzania 





JOKATE MWEGELLO ATOA MSAADA KITUO CHA YATIMA 

CHA EXTREM CHA TANDALE

2
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, J
okate
Mwegello, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika
Kituo cha
Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne,
alipotembelea
kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.
Zawadi alizotoa
ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye
nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
7
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu,
Jokate Mwegello, akimpa zawadi ya ndala mmoja wa watoto wanaolelewa
katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua
Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na
Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni
na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
IMG_2647
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu,
Jokate Mwegello, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa
katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua
Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na

Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni
a ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
.....................................................................................
MISS Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za
kibongo, Jokate Mwegelo 'Kidoti', jana ilitoa msaada wa vitu mbalimbali
katika Kituo cha Kulea Yatima cha Extrem kilichopo Tandare kwa Bi
Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mrembo huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti
inayojihusisha na masuala ya urembo, alitoa msaada huo kama
zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya kwa watoto

hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na
wengineo wanaioshi nawazazi wao.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Jokate
alisema kuwa ameguswa na kituo hicho ambacho huwa

hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo hilo.
"Nimefika hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha
ninavyoguswa na jamii ya watoto kama hawa, lakini pia nikiwa
na lengo la kuwafariji ili nao kujiona ni sehemu ya jamii ya
Watanzania," alisema.
Kidoti alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo,
kampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia
makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki
ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.
Msaada aliokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell,
ni mchele, unga wa sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye

nembo za Kidoti.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa
watoto hao, Mwamvua Jumanne, alitoa pongezi kwa Kidoti
na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo kusaidia
makundi maalum.
Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mwamvua
alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto
wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za
matibabu pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji









Wakenya wakiandamana kupinga kuzorota kwa usalama nchini Kenya

Bunge la Kenya limepitisha mswada unaolenga kuwapa
nguvu zaidi maafisa usalama kukabiliana na ugaidi
pamoja na maswla mengine ya usalama.
Wabunge walihusika na mjadala mkali Alhamisi kabla ya
mswada huo kupitishwa huku upinzani ukisema kuwa ikiwa
itakuwa sheria itakuwa inakiuka haki za wananchi.
Wabunge hao pamoja na mashirika mengine ya kutetea haki
za binadamu yanasema kuwa watafanya maandamani ikiwa
mswada huo utapitishwa bila ya kufanyiwa mabadiliko ili
 isikiuke haki za binadamu.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al shabaab limekua
likishambulia Kenya mara kwa mara wataalamu wa wakisema
kuwa Kenya haina mikakati mizuri ya kudhibiti usalama wake.
Sheria hizo mpya zinampa Rais na mashirika ya ujasusi
mamlaka mapya.












Viongozi wa kiisilamu wamekuwa wakilaumiwa kushindwa kuwazuia waumini wa kiisilamu kujihusisha na vitendo vya kigaidi

Wito ulitolewa kutoka pande zote bungeni kwamba baadhi ya
vipengee vya mswada huo ambavyo ni tatanishi kufanyiwa
marekebisho.
Badhi ya vipengee hivyo ni:
  • Uhuru wa maafisa wa usalama kuwazuia washukiwa wa 
  • ugaidi kwa karibu mwaka mmoja.
  • Uhuru wa mashirika ya kijasusi kudukua simu za watu bila 
  • ya idhini ya mahakama.
  • Na mashirika ya habari kupata udhini ya polisi kabla ya 
  • kupeperusha au kuchapisha taarifa za uchunguzi kuhusu 
  • usalama wa nchi na maswala ya ugaidi nchini.
Mswaada huo sasa utapelekwa kwa kamati ya usalama
bungeni kufanyiwa marekebisho kabla ya kupelekwa kwa
Rais kuidhinishwa na kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wamelaani mswada huo na kusema
unakwenda kinyume na katiba ya nchi.











Wakenya waliouawa na Al Shabaab mjini Madera wakichimba machimbo ya mawe

Huenda kamati hio ikafanya marekebisho yanayohitajika kwani
pande zote zinayaunga mkono.
Rais Kenyatta amesema anataka mswada huo uwe sheria haraka
iwezekanvyo.
Vipengee vingine vye sheria hio inayopendekezwa vinampa Rais
mamlaka ya kuwafuta kazi na kuwaajiri maafisa wakuu wa
usalama, kuyapa mashirika ya ujasusi uhuru wa kuwakamata
washukiwa wa ugandi na sharti kwamba watu wanaopatikana
na silaha katika sehemu za maombi kufungwa jela miaka 20.

POLISI WAZUIA MAZISHI YA MNENGUAJI 

AISHA MADINDA KUFANYIKA

  • Share on facebookShare on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Mazishi ya aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta, Aisha 
Madinda yaliyokuwa yafanyike Alhamis hii yameahirishwa hadi 
Ijumaa ili kufanyika uchunguzi wa kifo chake chenye utata.

Aisha alifariki jana na kwa mujibu wa mwanae wa kiume aitwaye 
Feisal, mama yake hakuwa mgonjwa.“Kimetokea tu ghafla, ni kifo 
ambacho sio cha kawaida ni cha utata. Serikali nayo imeamua 
kufanya mambo yake imeamua kuingilia kati ili tumzike 
tukiwa tunafahamu nini kimemfanya mpaka afariki,” Feisal 
ameiambia 255 ya XXL, Clouds FM.
Ameongeza kuwa mwanamke ambaye aliupeleka mwili 
wa Aisha hospitali anashikiliwa na polisi kwenye kituo cha 
Oyster Bay.(MM)

Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Home
Subscribe to: Posts (Atom)
TUPAMBANE BLOG

WELLCOME TUPAMBANE BLOG

ALL HITS

BLOGGER

BLOGGER

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

  • UTAMU WA BOSS
    Hadithi yangu Inaitwa "Utamu wa Bosi" naomba tuwe pamoja mwanzo paka mwisho fatilia sasa  ..................Ooops,Ooooh?Aaah,M...
  • WAKUBWA TU 19+: SIMULIZI YA MAPENZI
      (((PICHA SIYO YA MUHUSIKI))) Janifa ni dada fulani huko Dar es Salaam. Ana miaka 32, ana kazi ya maana na ana mtoto moja wa kike. A...
  • 18+>>USIKU WA WAKUBWA>>>JE UNAJUA JINSI YA KUFANYA MAPENZI KWA KUTUMIA SIMU BASI SOMA HAPA(SEX PHONE
    Mapenzi ni k2 cha ajabu sana katika hii dunia maana kuna njia nyng sana za kufanya mapenz na bila kuingiza uume wala mwanamke kuing...
  • KILIMO BORA CHA NYANYA- MAGONJWA NA WADUDU
    Utangulizi Nyanya ni zao la chakula na biashara. Kilimo cha zao hili hufanyika majira yote (masika na kiangazi), na faida hupat...
  • SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UZALISHAJI WA AJIRA NCHINI
    Mkurugenzi wa Ajira toka Wizara ya kazi na Ajira Bw.Ally Msaki akiongea na waandishi wa habari kuhusu kasi ya uzalishaji wa nafasi ...
  • KIZAZA CHA MASTAA WA BONGO :TAZAMA PICHA 30 HAPA ZA ...............KWENYE 6*6 :( ONYO 81+)
    Na mwandishi wa Xdeejayz Afrika...
  • ZIJUE HASARA ZA KUTOKUFANYA MAPENZI KWA MUDA MREFU
    Aise, kwa kawaida kama wewe si mgonjwa wa aina yoyote ile, kwa maana ya ugonjwa ku-offset system ya mwili, madhara ya kutofanya te...
  • LEO NI STORY TU.
    Ilikuwa mida ya saa mbili jioni nikiwa natoka kazini na uchovu kiasi,nikaingia chumbani halafu nikaenda kuoga ili kupunguza uchovu.Nilipo...
  • SHAMBA LA MITIKI LINAUZWA
      Shamba lipo Morogoro, Turiani   Lina ukubwa wa ekari 5 Lina miti ya mitiki kati ya 4,000 na 4,500 yenye umri wa miaka ...
Copyright by Tupambane Blog. Simple theme. Powered by Blogger.