Kinara wa Nusra adaiwa kuuawa syria
Vyombo vya habari vya Serikali ya Syria vimesema jeshi limemuua kamanda wa kijeshi kutoka kundi la waasi lenye uhusiano na Al Qaeda, la Nusra Front.
Taarifa zinasema aliuawa katika mji wa Idlib ambapo viongozi wa Nusra Front walikuwa wanakutana.
Nusra front ni moja kati ya makundi yenye nguvu yanayopambana ili kumuangusha Rais wa Syria, Bashar Al Assad, kundi hilo pia lilihusika na shambulizimjini Alepposiku ya jumatano.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria ameweka wazi nia yake ya kufanya mazungumzo na Nusra Front ikiwa sehemu ya jitihada za kurejesha utulivu mjini Aleppo.
Staffan de Mistura ameiambia BBC kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na yeote ili kuokoa maisha ya Watu mjini humo.

Venezuela yatoa Masharti kwa Marekani
Serikali ya Venezuela imeipa Marekani muda wa wiki mbili kupunguza idadi ya wanadiplomasia wake walio nchini Venezuela.
Waziri wa mambo ya nje Delcy Rodriguez ametoa kauli hiyo baada ya kukutana Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani mjini Caracas.
Waziri huyo amesema ni juu ya marekani sasa kuamua nani kati ya mamia ya wanadiplomasia walio nchini Venezuela arudishwe nyumbani.
Nia imeelezwa kuwa awali ilihitajika idadi ya wanadiplomasia 17 ambao idadi hiyo ina uwiano sawa na wanadiplomasia wa Venezuela walio Marekani.
Mwanzoni mwa mwezi huu Marekani iliweka vikwazo kupata viza za kusafiri dhidi ya Maafisa wa Venezuela ambao Marekani inawashutumu kuwa wamekiuka haki za binaadam na waliojihusisha na vitendo vya rushwa.
Serikali ya Venezuela imeipa Marekani muda wa wiki mbili kupunguza idadi ya wanadiplomasia wake walio nchini Venezuela.
Waziri wa mambo ya nje Delcy Rodriguez ametoa kauli hiyo baada ya kukutana Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani mjini Caracas.Waziri huyo amesema ni juu ya marekani sasa kuamua nani kati ya mamia ya wanadiplomasia walio nchini Venezuela arudishwe nyumbani.
Nia imeelezwa kuwa awali ilihitajika idadi ya wanadiplomasia 17 ambao idadi hiyo ina uwiano sawa na wanadiplomasia wa Venezuela walio Marekani.
Mwanzoni mwa mwezi huu Marekani iliweka vikwazo kupata viza za kusafiri dhidi ya Maafisa wa Venezuela ambao Marekani inawashutumu kuwa wamekiuka haki za binaadam na waliojihusisha na vitendo vya rushwa.
kukoma kwa mapigano Ukraine bado Ndoto
Viongozi wa Urusi, Ukraine,Ujerumani na Ufaransa wamefanya mazungumzo zaidi kwa njia ya simu kuhusu jitihada za kuhakikisha mapigani yanakoma Mashariki mwa Ukraine.
Wamekubaliana kupeleka waangalizi katika maeneo kumi ambako makubaliano ya kusitisha mapigano yalikiukwa ukiwemo Mji wa Shchastya,Volnovakha na maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Donetsk.
Viongozi hao wamesisitiza kuhusu uhitaji wa kuwaruhusu waangalizi kufuatilia na kuhakikisha uondolewaji wa Silaha.
Petro Poroshenko, Angela Merkel na Francois Hollande kadhalika wamemtaka Rais wa Urusi Vladmir Putin kumuachia huru Nadya Savchenko, Rubani wa Ndege wa Ukraine aliyeshikiliwa tangu mwaka jana, amekuwa katika mgomo wa kutokula kwa siku 80
Viongozi wa Urusi, Ukraine,Ujerumani na Ufaransa wamefanya mazungumzo zaidi kwa njia ya simu kuhusu jitihada za kuhakikisha mapigani yanakoma Mashariki mwa Ukraine.
Wamekubaliana kupeleka waangalizi katika maeneo kumi ambako makubaliano ya kusitisha mapigano yalikiukwa ukiwemo Mji wa Shchastya,Volnovakha na maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Donetsk.Viongozi hao wamesisitiza kuhusu uhitaji wa kuwaruhusu waangalizi kufuatilia na kuhakikisha uondolewaji wa Silaha.
Petro Poroshenko, Angela Merkel na Francois Hollande kadhalika wamemtaka Rais wa Urusi Vladmir Putin kumuachia huru Nadya Savchenko, Rubani wa Ndege wa Ukraine aliyeshikiliwa tangu mwaka jana, amekuwa katika mgomo wa kutokula kwa siku 80
Profesa Tibaijuka: Niliondoka kwa bahati mbaya
NA CHRISTINA MWAGALA, Dar
*Simbachawene aahidi uwazi mikataba ya madini
*Sitta: Mimi ni mtu mzima, sipendi kudanganywa
ALIYEKUWA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,
amekabidhi ofisi kwa Waziri mpya, William Lukuvi huku akisema aliingia
wizarani humo kwa bahati nzuri, ameondoka kwa bahati mbaya.
Profesa
Tibaijuka alisema wakati Rais Jakaya Kikwete alipomteua kuongoza wizara
hiyo, alitambua kuwa yeye ni mtu makini na ndio maana, licha ya watu
kuona kwamba hajafanya kitu, amefanikiwa kuiongoza vyema wizara hiyo kwa
miaka minne.
Mwishoni
mwa mwaka jana, Rais alitengua uteuzi wa Profesa Tibaijuka kwa kukiuka
maadili ya uongozi wa umma baada ya kuwekewa Sh. bilioni 1.6 kwenye
akaunt yake na Mkurugenzi wa VIP Engineering, James Rugemalira.
Fedha
hizo ni zilitokana na malipo kutoka kwenye Akaunti ya Escrow, kashfa
iliyotikisa taifa mwaka jana na kusabaisha mawaziri wawili kuondoka
madarakani.
“Licha
ya kuondolewa hapa, kuna mengi niliyafanya. Sikuja hapa kwa bahati
mbaya, Rais aliona utendaji wangu, akaniamini na kunikabidhi nifanye
kazi.
“Lakini
nimeondoka kwa bahati mbaya, ninakukabidhi wizara hii na pia
ninakukaribisha jimboni kwangu, huko kuna maeneo mengi hayajapimwa,”
Profesa Tibaijuka aliwambia Lukuvi, akiongeza:
“Lakini
pamoja na kuondoka kwa bahati mbaya, wakati naingia katika wizara hii,
nilikuwa sijui kitu na sasa ninajivunia kuondoka nikiwa mtalamau wa
masuala ya ardhi.
“Hii
ni moja ya wizara ngumu. Hii ndio figo yenyewe, utakachokifanya hata
kama ni kizuri, hakiwezi kuonekana. Ni sawa na figo ambayo inafanya kazi
kwenye mwili wa mtu ila mwingine hajui kuwa inafanya nini na kwa kiasi
gani. Na wewe utakapokutana na ugumu huo, usije kushangaa.”
Alimtahadharisha
Lukuvi kujiandaa na changamoto ya mipanhgo miji na kumwomba aendelee
pale alioachia yeye huku akimshauri kusali sana kumwomba Mungu kusizuke
moto utakaoteketeza nyaraka za serikali.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi, Lukuvi alisema:
“Kukabidhiwa
wizara hii si kwamba sitambui ugumu uliopo, hii ni kama kaa la moto.
Ninaingia hapa sio kwamba sina akili au wizara hii siitambui, ninaijua
vizuri! Nina akili timamu na si kwamba sina macho. Nitaondoa migogoro
yote iliyopo hapa kwa sababu ninaimudu.”
Aliahidi kuanza kazi tofauti na wengine waliokuwa wakikaa mijini kwani yeye ataanzia vijijini.
“Vijijini
ndiko kwenye matatizo yenyewe. Nataka kukomesha huu mgogoro wa ardhi
ambao umekuwa ukifanya watu waonekane hawafanyi kazi. Nitakuja tofauti,
nitasikiliza shida zao, na kuona wapi nitanzia,” alisema.
Alikiri kufahami kuwa wizarani humo wapo watendaji ambao si waminifu, akisema hao ni mafisadi na kuahidi kupambana nao.
Naibu
Waziri wa wizara hiyo, Angela Kairuki, alisema katika utendaji wao,
watahakikisha wanaongeza nguvu katika mabaraza ya ardhi kuepusha
usumbufu kwa wananchi.
Wakati
huo huo, mwndishi wetu NA SHARIFA MARIRA, anaripoti kwamba Waziri wa
Nishati na Madini, George Simbachawene, ameahidi kutoa usiri kwenye
mikataba ya gesi na kwamba ndani ya siku tatu atatoa tamko la kuwawekea
wazi wananchi kuhusu mikataba hiyo.
Akizungumza
kwa mara ya kwanza ofisini kwake jana, Simbachawene alisema ataangalia
ni kitu gani kilichopo katika mikataba hiyo au ambacho kinazungumziwa
ili ajenda hiyo ifungwe na kazi nyingine ziendelee.
“Tumekuja
kwenye wizara ambayo ina changamoto na wafanyabiashara kutoka ndani na
nje ya nchi wanaiangalia kwa hiyo tutajaribu kufanya kazi kwa
kuziangalia sekta binafsi kwani ina mchango mkubwa katika maendeleo ya
taifa,” alisema Simbachawene.
Alisema
watahakikisha kuwa wachimbaji wakubwa na wadogo hawalumbani na
kuwatengenezea mazingira ya usawa kwa kujitahidi kuwakuza wadogo ili
kusiwe na malalamiko.
“Katika
suala la kupeleka umeme vijijini tutaanza na kasi ile ile iliyokuwepo
na tutahakikisha muda uliobakia tunaweka mambo sawa ili wananchi
wachekelee kama inavyotakiwa. Tutashirikiana na Ewura kuhakikisha bei ya
mafuta inapungua na kuendana na soko la dunia,” alisema Simbachawene.
Kwa
upande mwingine, Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, aliyefika ofisi yake
mpya saa 8:07 mchana na kupokewa kwa shangwe, aliwataka wafanyakazi wa
Wizara hiyo kumpa ushirikiano na kutokusema uongo katika utendaji kazi
kwani yeye ni mtu mzima na hatofanya kama alivyokuwa anafanya
aliyekuwapo hapo awali, Dk. Harrison Mwakyembe.
“Mimi
ni mtu mzima unatakiwa unieleze ukweli hata kama umekosea ili tutafute
suluhisho, sitofanya kama alivyokuwa anafanya Dk. Mwakyembe kwa sababu
mimi kidogo utu uzima umenipa busara,” alisema na kumshukuru Rais kumpa
nafasi ya kuongoza wizara ambayo alisema tayari mambo mengi makubwa
yalishafanyika hivyo anachotakiwa kukifanya ni kuendeleza juhudi za Dk.
Mwakyembe.
Akizungumza
ofisini hapo jana, Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Mwakyembe alisema
kupewa Wizara aliyokuwa anaiongoza Sitta ambaye ni kaka yake na
alichangia kumfundisha kazi, ni faraja na kwamba hatosita kumuomba
ushauri atakapokwama katika mambo mbalimbali ya kuiongoza Wizara hiyo.
“Furaha
yangu ni kubadilishana Wizara na kaka yangu nina imani yale niliyokuwa
nikiyafanya atayaendeleza kwa kiasi kikubwa sina shaka na utendaji wake,
najua wizara unayoniachia itakuwa ipo vizuri umeifagia vya kutosha
hivyo sitapata changamoto kubwa naahidi kuenzi jitihada zako,” alisema
Dk Mwakyembe.

Rais Kikwete awateua mawaziri 8 Tanzania
Rais Jakaya kikwete wa Tanzania ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano.
Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na kawi wa Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema leo pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliwachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa ardhi, George Simbachawene
Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya hii leo katika tangazo lililorushwa hewani na runinga ya taifa moja kwa moja.
Hii ndio orodha ya mawaziri walioteuliwa
MAWAZIRI
George Simachawene waziri wa nishati na madini
Mary Nagu- waziri wa nchi [afisi ya rais] mahusiano na uratibu
Christopher chiza -waziri uwezeshaji na uwekezaji
Harisson Mwakyembe[waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki]
William Lukuvi -waziri wa ardhi nyumba na makaazi
Steven Wasira -waziri wa kilimo chakula na ushirika
Samwel Sita -waziri wa uchukuzi
Jenista Muhagama -waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge
MANAIBU WAZIRI
Stephen Masele -naibu waziri afisi ya makamu wa rais muungano
Angela Kariuki -naibu waziri wa ardhi nyumba na makaazi
Ummi Mwalimu- naibu waziri wa katiba na sheria
Anna Kilango naibu waziri wa elimu na mafunzo ya kiufundi
Charles Mwijage-naibu waziri wa nishati na madini

Rais Obama ataka mgao sawa wa rasilimali
Rais wa Marekani Barak Obama, amesema Marekani inafanya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii baada ya miaka mingi ya kujirudia kwa mdororo wa uchumi na vita, huku uchumi ukiongeza ajira kwa kasi kubwa kuliko wakati wowote tangu mwaka 1999.
Pia amesema Wamarekani wengi zaidi wana bima za afya kuliko wakati wowote kabla ya hapo.
Akihutubia taifa kupitia baraza la Congress lenye wajumbe wengi kutoka chama cha Republican, Rais Obama ametumia hotuba hiyo kutangaza mpango wa kujenga uchumi wa kati kwa wananchi wote wa Marekani, ambapo wananchi wa kipato cha chini watapata huduma za afya na elimu kwa gharama nafuu.
Rais Obama ametangaza hatua za kusaidia familia za wafanyakazi kunufaika kutokana na kukua kwa uchumi.Mkakati wa Bwana Obama anaouelezea kama uchumi wa daraja la kati, unahusisha kupandisha kodi kwa matajiri.
Hotuba ya Rais Obama ilibeba mapendekezo kuhusu kodi, vyuo vya jamii, huduma za internet, usalama katika mtandao wa komputa na likizo ya ugonjwa.
Bwana Obama amesema hali ya kutoka katika mdororo wa uchumi imetoa fursa ya kuongezeka kwa kipato na fursa kwa kila mtu.
Amesema uchumi wa daraja la kati ni wazo kwamba nchi hiyo inafanya vizuri kabisa wakati kila mtu anapata haki katika mapato na kila mtu anatendewa haki kama ilivyoanishwa katika sheria za nchi hiyo.
Mpango wake wa kuongeza kodi kufikia dola bilioni 320 katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi ni pamoja na kuziba mianya ya kukwepa kodi kwa wenye vipato vikubwa, ambapo matajiri wakubwa watalipa kodi ya kukua kwa mtaji kutoka asilimia 23.8% hadi asilimia 28%.

Waasi 'waiteka' ikulu ya Rais Yemen
Uchaguzi wa Zambia kufanyika leo
Hatimaye leo wananchi wa Zambia wanapiga kura kuchagua Rais wa nchi hiyo, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Michael Sata Oktoba mwaka jana.
Chama tawala cha Patrioyoc Front kinauhakika wa kushinda katika uchaguzi huo licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka upinzani.
Waangalizi wa kikanda katika uchaguzi huo, wanasema wameridhishwa na maandalizi ya zoezi zima la upigaji kura.Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kati ya Edgar Lungu anayegombea nafasi hiyo kupitia chama tawala na mpinzani wake HAKAINDE Hichilema kutoka United Party for National Development.
Wagombea wote katika nafasi hiyo ya Urais wakati wakijinadi wameahidi kuimarisha mfumo wa elimu nchini humo, kutengeneza ajira. Huku wapiga kura nao wakitumaini kuwa wanasiasa hao watatimiza ahadi zao.Ikiwa ni miaka 50 toka nchi hiyo ilipojipatia uhuru, Zambia imekuwa imara na imeendelea na msimamo wake wa kufanya uchaguzi tangu kumalizika kwa siasa za chama kimoja nchini humo.
Hata hivyo mshindi katika uchaguzi huo wa leo atatumikia kipindi cha miezi 18 iliyobakia, katika awamu iliyobaki, aliyoiacha marehemu Michael Sata, wakati nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwakani 2016.
Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 12 kamili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni. Tume ya Uchaguzi nchini Zambia imesema zoezi la uhesabuji kura, linatarajiwa kuanza muda mfupi tu baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika, huku matokeo yakitarajiwa kutangazwa katika kipindi cha saa 48.

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI CHA KWANZA KWA MWAKA HUU WA 2015
Republican yampinga Obama
Wabunge wa chama cha Republican ambao ni wengi Marekani wanapinga mipango ya Rais Barack Obama kuzifanyia mabadiliko sera za Uhamiaji nchini humo.
Spika wa bunge la Marekani John Boehner amesema hatua ya serikali iliyotangazwa na Rais Obama mwezi Novemba mwaka jana haikuwa imeidhinishwa na bunge la taifa hilo.
Lakini Ikulu ya Marekani imesema chama cha Republican kimechukua hatua ambazo si sahihi kupinga hatua ya Rais Obama akuhusiana na marekebisho ya sera ya uhamiaji ili kuwapa uraia wasioa raia wa taifa hilo.

Hatutawabagua Waislam:Ujerumani
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck amewahakikishia uvumilivu na ustahimilivu waislam million nne waliopo nchini humo pamoja na tukio la shambulizi nchini Ufaransa.
Katika kumbukumbu ya shambulio la mjini Paris Ufaransa mbele ya umati, Rais Gauck alisema “sisi wote ni Wajerumani”. Amesema kuwa walitekeleza shambulio Charlie Hebdo nia yao ni kutaka kuwagawa watu kwa matabaka ya dini,lakini Ujerumani kamwe haiwezi kufuuata mgawanyiko huko kwa Waislam waliopo Ujerumani. Awali viongozi wa kidini na kisiasa pamoja na Kansela Angela Merkel walitoa salam zao za rambi rambi kwa kuweka maua ubalozi wa Ufaransa nchini Ujerumani kama hatua ya kulaani shambulio hilo.

Zanzibar na miaka 51 ya Mapinduzi
12 Januari 2015 Imebadilishwa mwisho saa 04:56 GMT

Vita vipya dhidi ya waasi wa FDLR
Serikali ya Angola inasema kuwa uamuzi umechukuliwa na mataifa ya Afrika kuingilia kijeshi harakati za waasi wa kihutu kutenda uhalifu Mashariki mwa Congo.
Afisaa mmoja mkuu (Joaquim do Espirito Santo) anasema kuwa mkutano wa kikanda uliotarajiwa kufanyika leo, umefutiliwa mbali kwa sababu ya hofu ya kuchelewesha mipango ya kijeshi dhidi ya waasi hao.
Umoja wa mataifa ulithibitisha mwishoni mwa wiki jana kwamba waasi wa FDLR wamepitwa na muda waliowekewa wa mwisho kwao kusalimisha silaha.
Wiki jana Rais wa DRC, Joseph Kabila, aliambia katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kuwa jeshi la nchi yake liko tayari kupambana na waasi hao.
Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Mataifa, (Martin Kobler) amesema kuwa hatua za kijeshi ndizo pekee zinahitajika kuchukuliwa dhidi ya waasi hao kwa sasa.

CCM wamshambulia mdhamini
MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Muslim Hassanali, amedai kushambuliwa na Katibu Kata wa Kisutu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Sauda Addey, baada ya mjumbe huyo kukataa kubandikwa kipeperushi cha wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali za mitaa kupitia CCM mbele ya eneo lake la biashara.
Hassanal, anadai tukio hilo lilitokea Jumamosi saa tano asubuhi, baada ya wafuasi wa CCM kubandika kipeperushi chao katika eneo lake la biashara lililopo mtaa wa Mali Kisutu jijini Dar es Salaam.
Kushambuliwa kwa Hassanal, kumekuja ikiwa ni siku chache zimepita huku baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa katika maeneo mbalimbali nchini wakiwa wameshashambuliana na wengine kupoteza maisha.
Akizungumzia namna alivyoshambuliwa, Hassanal alisema baada ya kufika ofisini kwake, alikuta kipeperushi hicho na alipouliza watu aliowakuta wakamuambia kuwa makarataisi hayo yamewekwa usiku na kwamba hawamjui aliyeweka.
“Kisheria lile ni eneo langu ninalolimiliki kibiashara, hivyo yeyote anayetaka kulitumia ni lazima aonane na mimi nimpe ruhusa ama la, sasa hawa CCM wamekuja kuweka pasipo ridhaa yangu na mimi siipendi CCM, nikiona hata rangi zao nasikia kichefu chefu nikaona ngoja niziondoe,” alisema Hassanal na kuongeza;
Unajua ile ni sehemu ya biashara wanafika watu wa kila itikadi, sasa kubandika picha kama zile zinaweza kuvuruga biashara zangu, isitoshe kwa kulitambua hilo ndio maana nimeshindwa hata kubandika picha za wagombea wa CHADEMA ambacho ni chama changu.
Alidai kuwa, baada ya kuyaondoa matangazo hayo viongozi wa Kata hiyo wa CCM wakiambatana na wafuasi wao, walimvamia na kumfanyia vurugu zilizosababisha uharibifu wa miwani yake ya macho, vifaa, nyaraka na upotevu wa baadhi ya vitu.
Alisema kutokana na fujo hizo, alifika kituo cha Polisi Kisutu, ambako wakamueleza hawana mamlaka ya kushughulikia kesi za kisiasa, hivyo alifikishe suala hilo kituo kikuu cha kati.
Hassanali, alisema baada ya kushauriwa hivyo, aliamua kwenda kituo hicho lakini cha kusikitisha hakuweza kupata ushirikiano wa kutosha na alitakiwa kurudi kituoni hapo Jumatatu, ambako alifanya hivyo.
“Leo kama mnavyoniona hapa bado nasumbuliwa, nataka kufungua jalada lakini bado wahusika wanazunguka tu kwa kunieleza kuwa msimamizi wa shauri langu hajafika, hata hivyo niliweza kuhojiwa na kuandika maelezo yangu,” alisema.
Wakili wa Hasanali, Fredrick Kihwelo, alikiri mteja wake kufanyiwa vurugu na kwamba baada ya kufika polisi, waliandika maelezo na kuambiwa uchunguzi unaendelea.
“Pamoja na kukwama siku ya Jumamosi, leo tumekuja tena, tangu asubuhi tuko hapa na hatimaye tumefungua kesi ya jinai, kimsingi suala hili litakuwa kwenye uchunguzi baada ya hapo litapelekwa kwa DPP ambaye ndio ataamua kama litapelekwa mahakamani,” alisema wakili huyo.
Kwa upande wake, Sauda alisema zoezi la kubandika picha za wagombea limefanyika Jiji zima kisheria tangu miaka ya nyuma na hakutegemea katika eneo hilo kama angekuwepo mtanzania mwenye asili ya Asia asiwe mfuasi wa CCM.
“Sisi hatukujua kama pale kuna mtu wa CHADEMA tena Muhindi, kama tungejua tusingebandika, kwani kwa zaidi ya miaka 25 tumekuwa tukibandika,” alisema Sauda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Mary Nzuki, alisema suala hilo bado liko kwa mkuu wa kituo kwa ajili ya uchunguzi na mara litakapokamilika litafikishwa kwake kwa hatua zaidi.

Maandamano ya umoja yaanza Paris.
Maandamano ya umoja nchini Ufaransa yameanza baada ya makundi ya watu kukongamana katika eneo la de la Republique katika mji mkuu wa Paris nchini Ufaransa ,kama kigezo cha kuonyesha umoja dhidi ya mashambulizi ya wiki iliopita yaliotekelezwa na waislamu wenye itikadi kali.
Zaidi ya watu millioni moja wanashiriki katika maandamano hayo.
Makumi ya viongozi wa nchi tofauti duniani wako mji paris ambapo usalama umeimarishwa huku maafisa zaidi wa jeshi na wale wa polisi wakiwekwa kupiga doria.
Ghasia hizo nchini Ufaransa zilianza siku ya jumatano kutokana na shambulizi la gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Hatahivyo maafisa wa polisi waliwazingira na kuwapiga risasi mandugu wawili waliohusika na shambulizi hilo.

Azimio kuhusu Palestina lakataliwa
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limekataa azimio lililoandaliwa na Palestina ambalo limewasilishwa na Jordan linalopendekeza kusitishwa kwa mpango wa Israel wa kuyakalia maeneo ya Palestina kwa miaka miaka mitatu.
Jordan iliwasilisha azimio hilo baada ya kukubaliwa na nchi 22 za kiarabu ikiwemo mamlaka ya Palestina.
Kura tisa zilihitajika ili kupitisha azimio hilo lakini azimio hilo lilipigiwa kura nane pekee.
Nchi mbili zilipiga kura ya hapana kupinga azimio hilo ambazo ni Australia na Marekani zilizokataa mpango huo wa mwisho na kusema hautasaidia katika masuala ya usalama wa Israel.
Nchi tano hazikupiga kura ambazo ni Uingereza, Lithuania, Nigeria, Jamuhuri ya Korea na Rwanda, huku Urusi, China, Ufaransa, Argentina, Chad, Chile, Jordan na Luxembourg zikilipigia kura ya ndio azimio hilo

NAIBU WAZIRI MHE. JANUARY MAKAMBA AZINDUA KUNDI LA KAONE SANAA GROUP DAR LIVE
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba akiongea na wasanii....
Akiwa pamoja na wasanii

ESCROW YAMFUKUZISHA KAZI PROFESA TIBAIJUKA, MUHONGO AWEKWA KIPORO
Rais wa Jamhuri wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kutengua uteuzi wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka baada ya vyombo vya Serikali kubaini na kijiridhisha kuwa amekiuka maadili ya utumishi wa Umma kwa kuingiziwa fedha kiasi cha Sh1.65bilioni kwenye akaunti yake binafsi.
Rais kikwete ametangaza kufukuzwa kazi kwa Waziri huyo leo alipokuwa anazungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa, na baada ya kutangaza kufukuzwa kwake maelfu ya wazee waliohudhuria kwenye mkutano huo walipiga kelele za kumpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake.(MM)
Rais kikwete amesema miongoni mwa mapendekezo ya Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Escrow Tegeta yaliyofikishwa kwenye Serikali ni pamoja na kuwajibishwa kwa Bodi ya Shirika la umeme (Tanesco), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Rais Kikwete amesema baada ya uchunguzi wa vyombo husika viliweza kubaini kuwa kiasi cha Sh1.65bilioni kiliingizwa kwenye akaunti binafsi ya Profesa Tibaijuka, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa Umma.
"Tumezungumza na Profesa Tibaijuka na tumemuomba atupishe ili tuweze kuteua waziri mwingine kwani viashiri vyote vinaonyesha kuwa alikiuka kanuni na sheria ya maadili ya Umma," anasema Rais Kikwete.
Aidha Rais Kikwete amesema katika suala la Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo analiweka kiporo maana bado hajapata ufafanuzi kuhusu mambo kadha wa kadha, hivyo pindi atakapopata ufafanuzi na kujiridhisha ataujulisha umma .
Amesema kuhusu suala la bodi ya Tanesco hana shida nalo kwa sababu tayari bodi hiyo imeshamaliza muda wake hivyo ni kama imekwishajifuta yenyewe, na kuongeza kuwa tayari Ikulu imeshapewa taarifa za kumtaka achague bodi nyingine, hivyo ndani ya siku chache bodi mpya ya Tanesco itatangazwa.
Amesema suala la Katibu Mkuu wa Nishati na Madini na viongozi wengine wa utumishi wa Umma ambao wametajwa katika sakata hilo tume ya maadili, Taasisi ya Kuzuia na Kupapambana Rushwa (Takukuru) pamoja na jeshi la polisi wanaendelea kufanya uchunguzi wao, na ikithibitika kuwa walikiuka maadili yao ya kazi sheria stahiki zitachukuliwa.

Marekani yaitupia lawama Korea kaskazini
Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.
Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala wake utafanya hivyo baada ya kuilaumu nchi hiyo kufanya uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony Pictures.
Amesema mara tu mchakato wao huo utakapokamilika, watajibu mashambulizi hayo. Korea kaskazini imeziita tuhuma hizo zilizotolewa na Marekani dhidi yake kuwa ni za uzushi.
Korea kaskazini ilikuwa katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, kabla ya kuondolewa wakati wa utawala wa Rais George Bush wa Marekani mwaka 2008.

Essebsi ajitangaza kushinda Tunisiaako
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais nchini Tunisia yanaonesha kuwa Beji Caid Essebsi anaongoza kwa zaidi ya asilimia 55 ya kura
Licha ya Kujitangaza mshindi, mpinzani wake ambaye ameshika nafasi ya pili Moncef Marzouki amesema matokeo hayo yanakaribiana mno.
Wakati wafuasi wa Beji Caid Essebsi wakishangilia ushindi, kiongozi wa kampeni ya uchaguzi wa Bwana Essebsi, Mohsen Marzouk, amedai ushindi.
‘’…Kulingana na matokeo ya awali kutoka katika vituo vya kupigia kura tunaweza kusema kuwa Beji Caid Essebsi ameshinda katika duru ya pili...'' Anasema Marzouk.
Hata hivyo wakosoaji wake wanasema, ushindi wa bwana Essebsi ni ishara kurudi tena uongozi usioaminika.
Lakini mwenyewe anasema ni mtendaji ambaye ataimarisha nchi hiyo.
Uchaguzi huo unaonekana kama kilele cha mageuzi ya kisiasa ambayo nchi hiyo imepitia kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyotokea takriban miaka minne iliyopita.

Uchaguzi wa maseneta wafanyika Liberia
Shughuli za upigaji kura zinaendelea nchini Liberia kuwachagua maseneta wapya licha ya kuwepo kwa hofu kwamba kura hiyo huenda ikachangia kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.
Uchaguzi huo umehairishwa mara kadha lakini rais Ellen Johnson - Sirleaf anasema kuwa kura hiyo ni lazima ifanyike wakati huu ili kuzuia msukosuko .
Mikutano ya kisiasa ilipigwa marufuku kufuatia hatari iliyotokana na ugonjwa wa ebola ambao umewaua maelfu ya watu magharibi mwa afrika.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi nchini Liberia wanaamini kuwa kura hiyo ni hatari sana na kesi ya kuizuia isifanyike imepelekwa kwenye mahakama ya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka.
Kenyatta anasema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab.
Amesisitiza kuwa sheria hio haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza.
Mnamo siku ya Alhamisi, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana makonde bungeni wakijadili marekebisho kwa mswada kabla ya Rais kuupitisha kuwa sheria.
Katika vurugu hizo mmoja wa wabunge wa upinzani alimmwagia maji naibu spika.
Sheria hizo mpya zilipitishwa na bunge licha ya pingamizi kubwa na vurugu kutoka kwa wabunge hao.
Vyombo vya habari vimesema baadhi ya vipengee vya sheria hio ninabana uhuru wa vyombo vya habari na hata kutishia kwenda mahakamani.
Mswada huo kabla ya kutiwa saini na kufanywa sheria,ulifanyiwa mabadiliko kadhaa katika vipengee ambavyo vilionekana na baadhi ya wabunge kama vilivyokua vikali na kwenda kinyume na katiba.
Polisi sasa watakuwa na jukumu la kuidhinisha taarifa au picha za uchunguzi wa maswala ya usalama na hasa kuhusiana na ugaidi.
Polisi pia ndio watapaswa kuidhinisha picha za waathiriwa wa ugaidi kabla ya kuchapishwa au kuonyeshwa katika vyombo vya habari.
Vyombo vya habaro vinasema haya yanakwenda kinyume na uhueu wa vyombo vya habari.
Adhabu itakayotolewa kwa watakaokiuka sheria hii ni hadi faini ya shilingi milioni tano au dola elfu sitini ama kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitatu.
Rais Jakaya Kikwete, ametupiwa lawama na makada wa CCM kwa kusababisha kushindwa CCM viti vingi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, kutokana kuchelewa kutoa maamuzi juu ya sakata la wizi wa Tsh 306 bilioni katika akaunti ya Tegeta Escrow.(MM)
Liyewahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali nchini, Lapilali Ole Molloiment alisema kitendo cha Rais Kikwete kuchelewa kutoa maamuzi, katika sakata la Escrow kumechangia sana kuondoa imani ya wananchi kwa CCM."Kama Bunge letu, tayari lilitoa mapendekezo, kwanini Rais amechelewa kutoa maamuzi, hili ni tatizo ambalo limechangia CCM kushindwa,"alisema.
Alisema Watanzania wa sasa ni tofauti na zamani, wanajua vitu vingi hivyo, ni vigumu kuwaficha mambo ambayo yapo wazi na ambayo yanagusa maisha yao. "Mimi ninachoona washauri wa Rais ndio wanampotosha hili suala la Escrow, jambo hili lilitawala kampeni za Ukawa, hivyo ilipaswa kulifanyia maamuzi mapema na kuzima maneno kuwa CCM inawatetea waliohusika,"alisema. "Mimi ni Kada wa CCM, nasema tusipobadilika na kuwaondoa wachache wanaotuvuruga, tujiandae kuwa chama kikuu cha upinzani mwaka 2015,"alisema.
Kada Mwingine wa CCM, Joram Kaaya alisema, matokeo wa Uchaguzi wa Serikali za mtaa yana maana kubwa kwa uchaguzi ujao hivyo, ni muhimu kwa CCM kujipanga. "Lazima CCM tujipange haiwezekani watu wachache wavuruge chama alafu tubaki, mimi naungana na Katibu Mkuu wetu, Kinana wote waliohusika na haya mambo ya Escrow waondoke,” alisema Kaaya.
No comments:
Post a Comment