Mwili wa aliyekuwa rais wa Burkina fasso marehemu Thomas Sankara kufukuliwa
Serikali Burkina Fasso imeagiza kufukuliwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Thomas Sankara .
Watu wa familiaya rais huyo wamekuwa na wasiwasi kuhusu utambuzi wa maiti ya kiongozi huyo wa zamani.
Mjane wa marehemu Miriam,akizungumza kupitia njia ya simu kutoka Parisamesema, kuwa ufukuaji wa mwili huo utafanywa kulingana na agizo la mahakama ili kusaidia katika kuwatafuta waliotekeleza mauaji yake.
Bwana Sankara aliuawa mnamo mwaka wa 1987 katika mapinduzi yaliomfanya aliyekuwa rafikiye na mshirika wake mkuu Blaise Campaore kuchukua mamlaka.
Blaise Campaore aliondolewa mamlakani katika mapinduzi ya kiraia mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita.
Serikali mpya inayoongozwa na Michael Kafando ,ilisema kuwa italiangazia suala hilo wakati ilipochukua madaraka.
Mwili wa Sankara ulizikwa katika kaburi lisilotambulika miongoni mwa makaburi yaliopo mashariki mwa mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Viapo vya ndoa havitekelezeki.
Harusi na viapo visivyotekelezeka.
Ahadi ya kuwa pamoja maishani katika shida na raha,taabu na shida viapo hivi ama ahadi hizi zinaonekana kuchukuliwa kirahisi mno na wanandoa wapya, lakini kwa muujibu wa utafiti mpya uliotolewa hivi karibuni unathibitisha kuwa ni rahisi mno kutamka kuliko utekelezaji wa viapo vyenyewe .
Mtafiti uliofanywa kwa wanandoa wenye bahati 2,700 waliooana umegundua kwamba ,ikiwa mwanamke katika ndoa hiyo ataugua kwa muda mrefu asilimia sita hukaribia kupewa talaka kuliko wale ambao wana afya njema .
Ukilinganaisha na wanaume ambao huugua wakiwa kwenye ndoa,hatari ya kuvunjika kwa ndoa ni ndogo mno,hatahivyo upendo huendelea hadi hapo mmoja wao atakapo baki kuwa mgane ama mjane.
Utafiti ulioongozwa na wanazuoni wa chuo kikuu nchini Marekani,kinapendekeza kwamba kwa asili, wanawake wao wameumbwa kutoa huduma katika familia zao nah ii inamaanisha kwamba wanaume wao huwa hawana uvumilivu wake zao pindi wanapokumbwa na maradhi ya muda mrefu ,ambayo pia yanweza kuwa hayatabiriki kuyakabili.
Walifanyiwa utafiti wanandoa nchini Marekani,ambao wote walikuwa na umri wa miaka 50, mnamo mwaka 1990 ambao waliulizwa juu ya afya zao kuhusiana na maisha yao wakichnugza kwa miaka miwili,miwili ndani ya utafiti uliofanywa kwa miaka ishirini.
Asilimia thelathini na mbili ya ndoa ziliishia kwa kuachana na asilimia ishirini na nnenzilivunjika kutokana na vifo vya mmoja wa wanandoa.
Kikosi cha utafiti kiliongozwa na Amelia Karraker, ambaye ni profesa msaidizi juu ya masuala ya maendeleo ya binaadamu na utafiti juu ya familia kutoka katika chuo cha Iowa State University,analinganisha matukio ya namna nne kansa,magonjwa ya moyo,kiharusi na magonjwa ya njia ya hewa kwa wanawake na wanaume na matokeo ya ndoa.
Tamu na chungu ya ndoa
Utafiti huo umebainisha kwamba , kuna tofauti ya kujisikia mgonjwa sana na huwezi kupika chakula cha jioni, ama unahitaji mtu hasa wa kukulisha masuala haya yanaweza kubadili upepo ndani ya ndoa .
Katika hali hiyo,utafiti huo hauoneshi dhahiri kuwa mume ama mke anadai talaka,takwimu kamili zinaonesha kwamba wanawake ni wepesi zaidi kuomba talaka kuliko wenza wao.
Bi Karraker anasema amegundua kwamba kwamba inawezekana baadhi ya wanawake ambao huachwa kwasababu ya huduma zao ama kushindwa kuhudumia
Tafakari juu ya Uhai ama kifo husababisha watu wajitafiti wenyewe na kujiuliza maswali muhimu kuwa ni nini muhimu maishani mwao? Anaeleza mtafiti huyo.
Wanawake wakati mwingine huribuka kwa kusema kuwa waume zao hawawajali,na hawafurahishwi na suala hilo ama husema sikufurahishwa na mwanzo wa mahusiano yao, na wansema kwamba wako radhi kubaki peke yao kuliko kujitosa katika ndoa isiyofaa.
Mali haina wagonjwa wapya wa Ebola
Waziri wa Afya wa Mali amesema nchi hiyo kwa sasa haina maambukizi ya virusi vya Ebola baada ya siku 42 za kutokuwa na wagonjwa wapya walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo .
"Natangaza siku hii, mwisho wa ugonjwa wa virusi vya Ebola nchini Mali," amesema Ousmane Kone.Mtu wa mwisho kuambukizwa Ebola nchini Mali alipona na kuruhusiwa kutoka hospitali mapema mwezi Desemba.
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa nchi tatu za Afrika magharibi zilizokuwa zimeathirika zaidi zote zimeshihudia kupungua kwa wagonjwa wapya wa Ebola.
Sierra Leone na Guinea zote zimekuwa na jumla ya chini kabisa ya wagonjwa waliothibitika kila wiki kuambukizwa virusi vya Ebola tangu mwezi Agosti, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa zilizotolewa Alhamisi.
Liberia, ambayo haikuripoti wagonjwa wapya kwa muda wa siku mbili wiki iliyopita, ilikuwa na idadi ya chini kabisa kwa wiki ya mambukizi ya Ebola tangu mwezi Juni.
Idadi ya watu waliokufa kutoka na virusi vya Ebola imefikia watu 8,429, huku 21,296 wakiwa wameambukizwa.
Mali iliandikisha mgonjwa wa kwanza wa Ebola mwezi Oktoba, wakati mtoto wa miaka miwili kutoka Guinea alipougua na kufa.
Katika kipindi cha hali mbaya kabisa ya ugonjwa wa Ebola nchini humo watu 300 waliwekwa chini ya uchunguzi kuhusiana na maambukizi ya virusi vya Ebola.
Lakini nchi hiyo kwa sasa imeepukana na ugonjwa huo, amesema Ibrahima Soce Fall, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Mali kuhusu Ebola (UMEER).
Ugonjwa wa Ebola unachukua siku 21 tangu mtu kuambukizwa hadi kujitokeza kwa dalili za ugonjwa huu na nchi ili kutangaza kuwa zimeondokana na maambukizi ya ugonjwa Ebola lazima zisiwe na wagonjwa wapya kwa vipindi viwili vya matazamio yaani siku 42.
VIJANA WATAKIWA KUJITUMA NA KUFANYA
KAZI KWA KWA MAENDELEO YAO
Ndugu Elly David Akitoa Mada Kuhusu Vijana kujituma na kufanya kazi kwa Bidii Kwa maendeleo ya taifa.Mtoa Mada huyo amesema kutokana na Ukosefu wa ajira hususani kwa vijana ni vyeme vijana kujituma na kuwa w abunifu na waweze kujiajiri kwa lengo la Kupambana katika M aisha.Katika Kongamano hilo la Vijana lililofanyika Jijini dar es salaam Liliwapa Fursa vijana kueleza Changamoto zinazowakabili na namna ya Kuzikabili.Kongamano hilo lililoandaliwa na Elly David mara baada ya ya kuona changamoto zinazowakabili vijana wa itazania ili kuwapa fursa vijana kukutana kubadilishana mawazo Pamoja na Kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana wa Kitanzania
Hatukushambulia raia Somalia:Marekani
Mpiganaji wa Al ShababMarekani imesema kuwa bado inatafakari matokeo ya shambulio la anga lililofanyika Kusini mwa Somali kumlenga kiongozi mwandamizi wa kundi la wapiganaji wa Al Shabab.
Ndege za Marekan
Msemaji wa idara ya usalama ya Marekani amesema shambulio la anga katika karibu na eneo la Saakow halikuwa na dalili zozote za kuleta madhara kwa raia na hakuna raia waliodhurika.
Shambulio hilo limetekelezwa siku chache tangu mtu anayedhaniwa kuwa ni mfuasi wa kundi hilo kushambulia kambi ya majeshi ya Somalia na Jeshi la Muungano wa Afrika.
Marekani yatuma meli ya kivita
Indonesia
Manowari ya Marekani
Wanamaji kutoka Marekani wamesema kuwa wanapeleka moja ya Manowari ya kivita kutafuta ndege ya AirAsia iliyopotea tangu jumapili katika Bahari za Indonesi.
Manowari hiyo ijulikanayo kwa jina la USS Sampson inatarajiwa kufika leo katika eneo la Java Sea today ikiwa ni siku ya tatu tangua kuanza msako dhidi ya ndege hiyo. Idadi ya wataalamu wa kimataifa wanaoitafuta ndege hiyo imeongezeka ambapo kwa sasa nchi za Singapore, Malaysia ,Australia, Korea Kusini,Thailand na China wanashiriki katika kazi hiyo. Mkuu wa Operesheni ya uokoaji na utafutaji ndege hiyo Henry Bambang Soelistyo amesema kwa sasa kuna jumla ya Meli 30,ndege 15 na Helkopita katika eneo la tukio. Ndege hiyo ilipotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Surabaya Indonesia kuelekea Singapore ikiwa na abiria 162.
Bus la Zuberi No. 3 Limegongana uso kwa uso na costa. Hakuna aliyetoka kwenye costa na imekwisha nyang'anyang'a. Hali hii imepelekea waliokua kwenye magari mengine kushuka na kuokoa majeruhi. Ni Mbele kidogo ya singida mjini.
Ajali yaua 10 Mbeya, wanane wajeruhiwa
WATU 10 wakiwemo watoto wadogo wawili, wamekufa papo hapo baada ya gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace kulivaa lori aina ya Fuso katika eneo la Mbalizi mkoani Mbeya.
Katika ajali hiyo iliyotokea jana saa 4 asubuhi, watu saba walijeruhiwa miongoni mwao wakiwa katika hali mbaya.
Watu walioshuhudia ajali hiyo waliliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa gari la abiria aina ya Hiace yenye namba za usajili T237 iliyokuwa ikitokea jijini Mbeya kwenda Mbalizi, ililivaa lori aina ya T 158 CSV lililokuwa ikitokea kwenye kituo cha mafuta kilichopo eneo la Mbalizi.
Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema kuwa jeshi lake linachunguza chanzo, taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda zinaeleza ajali hiyo ilisababishwa na dereva wa Hiace ambaye alishindwa kulidhibiti gari lake lililokuwa likishuka kwenye mteremko mkali wa Mlima Mbalizi.
Maelezo ya watu mbalimbali walioshuhudia tukio hilo pia yalionekana kumuelekezea lawama dereva wa lori ambaye walidai kuwa aliingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Kamanda Msangi kwa upande wake aliwataja miongoni mwa waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni dereva wa Hiace aliyetambulika kwa jina la Petro Mngo’ngo.
Aliwataja wengine waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni watoto wawili wa kiume, wanawake wanne na wanaume wanne.
Kwa upande wa majeruhi, Kamanda Msangi alisema wanne kati ya saba wanapatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ifisi na watatu wamekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Gazeti hili lilifika katika Hospitali Teule ya Ifisi, ambako Muuguzi Mkuu, Sikitu Mbilinyi alilithibitishia kupokea miili 10 na majeruhi saba.
Alisema majeruhi waliopokelewa ni wanawake watatu na wanaume wanne, kati yao wanaume wawili na mwanamke mmoja walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa kutokana na hali zao kutokuwa nzuri.
Muuguzi huyo alisema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo ya Ifisi na kuwataka ndugu na jamaa kufika kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya kutambua marehemu hao.
Aidha, MTANZANIA lilifanikiwa kuzungumza na kondakta wa Hiace ambaye kutokana na hali yake kutokuwa nzuri aliweza kujitambulisha jina lake kuwa ni Justin Chaula na mwingine ni Neima ambao wote wamelazwa katika hospitali hiyo ya Ifisi.
Akielezea kutokea kwa ajali hiyo, shuhuda Saidi Nzowa (44) ambaye ni dereva wa lori la mafuta Kampuni ya ASAS, alisema:
“Inavyoonyesha gari ya abiria ilifeli breki ndio maana dereva alishindwa kuisimamisha na kulivaa lori hilo ambalo lilikuwa tayar limeingia barabarani.
Mtanzania
JOKATE MWEGELLO ATOA MSAADA KITUO CHA YATIMA
CHA EXTREM CHA TANDALE
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, J
okate
Mwegello, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika
Kituo cha
Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne,
alipotembelea
kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.
Zawadi alizotoa
ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye
nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu,
Jokate Mwegello, akimpa zawadi ya ndala mmoja wa watoto wanaolelewa
katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua
Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na
Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni
na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu,
Jokate Mwegello, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa
katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua
Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na
Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni
a ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
MISS Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za
kibongo, Jokate Mwegelo 'Kidoti', jana ilitoa msaada wa vitu mbalimbali
katika Kituo cha Kulea Yatima cha Extrem kilichopo Tandare kwa Bi
Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mrembo huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti
inayojihusisha na masuala ya urembo, alitoa msaada huo kama
zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya kwa watoto
hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na
wengineo wanaioshi nawazazi wao.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Jokate
alisema kuwa ameguswa na kituo hicho ambacho huwa
hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo hilo.
"Nimefika hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha
ninavyoguswa na jamii ya watoto kama hawa, lakini pia nikiwa
na lengo la kuwafariji ili nao kujiona ni sehemu ya jamii ya
Watanzania," alisema.
Kidoti alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo,
kampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia
makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki
ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.
Msaada aliokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell,
ni mchele, unga wa sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye
nembo za Kidoti.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa
watoto hao, Mwamvua Jumanne, alitoa pongezi kwa Kidoti
na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo kusaidia
makundi maalum.
Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mwamvua
alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto
wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za
matibabu pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji
Wakenya wakiandamana kupinga kuzorota kwa usalama nchini Kenya
Bunge la Kenya limepitisha mswada unaolenga kuwapa
nguvu zaidi maafisa usalama kukabiliana na ugaidi
pamoja na maswla mengine ya usalama.
Wabunge walihusika na mjadala mkali Alhamisi kabla ya
mswada huo kupitishwa huku upinzani ukisema kuwa ikiwa
itakuwa sheria itakuwa inakiuka haki za wananchi.
Wabunge hao pamoja na mashirika mengine ya kutetea haki
za binadamu yanasema kuwa watafanya maandamani ikiwa
mswada huo utapitishwa bila ya kufanyiwa mabadiliko ili
isikiuke haki za binadamu.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al shabaab limekua
likishambulia Kenya mara kwa mara wataalamu wa wakisema
kuwa Kenya haina mikakati mizuri ya kudhibiti usalama wake.
Sheria hizo mpya zinampa Rais na mashirika ya ujasusi
mamlaka mapya.
Viongozi wa kiisilamu wamekuwa wakilaumiwa kushindwa kuwazuia waumini wa kiisilamu kujihusisha na vitendo vya kigaidi
Wito ulitolewa kutoka pande zote bungeni kwamba baadhi ya
vipengee vya mswada huo ambavyo ni tatanishi kufanyiwa
marekebisho.
Badhi ya vipengee hivyo ni:
Uhuru wa maafisa wa usalama kuwazuia washukiwa wa
ugaidi kwa karibu mwaka mmoja.
Uhuru wa mashirika ya kijasusi kudukua simu za watu bila
ya idhini ya mahakama.
Na mashirika ya habari kupata udhini ya polisi kabla ya
kupeperusha au kuchapisha taarifa za uchunguzi kuhusu
usalama wa nchi na maswala ya ugaidi nchini.
Mswaada huo sasa utapelekwa kwa kamati ya usalama
bungeni kufanyiwa marekebisho kabla ya kupelekwa kwa
Rais kuidhinishwa na kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wamelaani mswada huo na kusema
unakwenda kinyume na katiba ya nchi.
Wakenya waliouawa na Al Shabaab mjini Madera wakichimba machimbo ya mawe
Rais Kenyatta amesema anataka mswada huo uwe sheria haraka
iwezekanvyo.
Vipengee vingine vye sheria hio inayopendekezwa vinampa Rais
mamlaka ya kuwafuta kazi na kuwaajiri maafisa wakuu wa
usalama, kuyapa mashirika ya ujasusi uhuru wa kuwakamata
washukiwa wa ugandi na sharti kwamba watu wanaopatikana
na silaha katika sehemu za maombi kufungwa jela miaka 20.
POLISI WAZUIA MAZISHI YA MNENGUAJI
AISHA MADINDA KUFANYIKA
Share on facebookShare on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Mazishi ya aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta, Aisha Madinda yaliyokuwa yafanyike Alhamis hii yameahirishwa hadi Ijumaa ili kufanyika uchunguzi wa kifo chake chenye utata.
Aisha alifariki jana na kwa mujibu wa mwanae wa kiume aitwaye Feisal, mama yake hakuwa mgonjwa.“Kimetokea tu ghafla, ni kifo ambacho sio cha kawaida ni cha utata. Serikali nayo imeamua kufanya mambo yake imeamua kuingilia kati ili tumzike tukiwa tunafahamu nini kimemfanya mpaka afariki,” Feisal ameiambia 255 ya XXL, Clouds FM.
Ameongeza kuwa mwanamke ambaye aliupeleka mwili wa Aisha hospitali anashikiliwa na polisi kwenye kituo cha Oyster Bay.(MM)
No comments:
Post a Comment