Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, August 29, 2014

kuhusu Taifa stars mimi nilisema ivunjwe je wadau mnasemaje?


  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Maoni (2)
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter
STARSNAUGANDA4 7517d
4-1 Unaonaje matokeo haya kwa timu ambayo tunaambiwa ni timu nzuri ina kocha mzuri na maandalizi ni mazuri, tumeshindwa World cup, tumeshindwa CAN na sasa CHAN, Jamani ndugu zangu watanzania tutaweza mashindano gani?
Nilisema toka awali ni vyema sasa tukajipanga upya kwa kuisuka timu yetu tukianzia na timu za vijana nashauri udhamini mkubwa kwa Taifa stars sasa upelekwe kwenye timu za vijana za mitaani ili kuweza kuibua vipaji ambavyo vitajenga timu zenye ushindani kwenye ligi zetu.
Hivyo kwa hatua hii ilivyofikia Timu ya Taifa nadhani ni wakati wa TFF kufanya maamuzi magumu ya kuivunja Timu hii na kuisimamisha kushiriki mashindano ya kimataifa hata kwa miaka miwili na kupeleka nguvu kwenye academy za soka zilizopo sehemu mbali mbali nchini kama hizo academy hazitoshi nadhani huu ni wakati wa wizara ya Elimu na wizara ya Michezo kuweza kushirikiana kuibua vipaji katika mashule nina hakika tukitumia mfumo huu baada ya miaka michache tutakuwa na Timu bora ya Taifa

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG