Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, August 30, 2014

Majeshi yakwamisha 'First 11' ya Minziro

30th August 2014

Fredy Felix Minziro
Kocha mkuu wa timu JKT Ruvu, Fredy Felix Minziro amesema kikosi kamili cha timu yake kitajulikana mara baada ya baadhi ya wachezaji wake kurejea kutoka kwenye michezo ya majeshi ya Afrika Mashariki inayoendelea Zanzibar.
 
Michuano hiyo inayoshirikisha michezo tofauti kutoka kwa timu mbalimbali za majeshi za Ukanda huo, inafikia ukingoni kesho.
 
Akizungumza na NIPASHE jana, Minziro alisema kipa Shaaban Dihile na wachezaji Damasi Makwaya na George Minja ambao wana mchango mkubwa JKT Ruvu ni miongoni mwa wachezaji wake walio Zanzibar.
 
Kutokana na kuwepo kwa hali, alisema Minziro, hatoweza kutaja kikosi cha kwanza mpaka Septemba Mosi ambapo wachezaji hao watakuwa wameungana na wenzao katika maandalizi ya ligi kuu ya Bara inayoanza Septemba 20.
 
Alisema anaendelea na mazoezi ya kila siku kwa timu hiyo, ikiwemo kuinoa safu ya ushambuliaji zaidi ambayo ikiimarika itaipa nafasi JKT Ruvu kupachika mabao zaidi kwenye ligi kuu.
 
"Tumecheza mechi nyingi za majaribio, zimenisaidia kiasi kikubwa kufanya marekebisho kwa wachezaji wangu," alisema Minziro.
Alisema bado anaendelea kutafuta mechi nyingine za majaribio kabla ya ligi kuu kuanza.
 
Minziro alisema JKT imesajili wachezaji chipukizi na wazoefu, ambao anaamini wakiungana pamoja, kikosi hicho kitafanya maajabu kwenye ligi kuu ya Bara.
Alisema chipukizi waliopo wameonyesha uwezo mkubwa katika mazoezi na mechi za kirafiki ambazo wamecheza, na akaeleza zaidi kuwa hali hiyo inampa moyo wa kujiamini kuwa timu itafanya vizuri msimu huu.
JKT inafungua pazia la ligi kuu ya Bara dhidi ya Mbeya City iliyoshika nafasi ya tatu mwaka jana

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG