- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter
Stori: Mayasa Mariwata na Rhoda Josiah
Usilolijua
litakusumbua! Msichana aliyejitambulisha kwa jina moja la Mary (23),
mkazi wa Dar ambaye ni mwenyeji wa Nyegezi, Mwanza, ameangua kilio na
kusema; ‘nabebeshwa madawa ya kulevya (unga), nalipwa kiduchu hadi
nimechoka’.
Msichana anayetambulika kwa jina moja la Mary (23) anayedai kuchoshwa na kazi ya kubebeshwa madawa ya kulevya.G.P.L (MC)
Awali, gazeti hili lilitonywa na vyanzo vyake juu ya kuwepo kwa ishu…
Stori: Mayasa Mariwata na Rhoda Josiah
Usilolijua
litakusumbua! Msichana aliyejitambulisha kwa jina moja la Mary (23),
mkazi wa Dar ambaye ni mwenyeji wa Nyegezi, Mwanza, ameangua kilio na
kusema; ‘nabebeshwa madawa ya kulevya (unga), nalipwa kiduchu hadi
nimechoka’.
Msichana anayetambulika kwa jina moja la Mary (23) anayedai kuchoshwa na kazi ya kubebeshwa madawa ya kulevya.
Awali,
gazeti hili lilitonywa na vyanzo vyake juu ya kuwepo kwa ishu hiyo
maeneo ya Manzese, Dar ambapo uchunguzi ulifanyika na kumnasa binti huyo
ambaye alifunguka kila kitu.
Akizungumza na wanahabari wetu kwa uoga mkubwa, Mary alidai kwamba alichukuliwa kutoka kijijini kwao huko Nyegezi ambapo alipofikishwa Dar, alijikuta akiunganishwa kwenye mtandao wa kuuza ‘unga’.
Akizungumza na wanahabari wetu kwa uoga mkubwa, Mary alidai kwamba alichukuliwa kutoka kijijini kwao huko Nyegezi ambapo alipofikishwa Dar, alijikuta akiunganishwa kwenye mtandao wa kuuza ‘unga’.
“Nililetwa
Dar mwaka jana na mwanaume mmoja, aliniahidi kunitafutia kazi, niliishi
naye kama mtoto wake.“Zilipita kama wiki mbili tangu aliponileta bila
kuniambia nitafanya kazi gani, siku moja ndipo akanipeleka Mitaa ya
Magomeni (Dar) na kuniambia nitakuwa nafanya shughuli za kuuza unga huku
nikiishi nyumbani kwake na yeye ndiye bosi wangu.
“Nilishangaa
sana kuona ile ndiyo kazi niliyoahidiwa kuja kuifanya Dar. Nilianza
kumlilia bosi wangu anirudishe kwetu Mwanza lakini alinigomea, hata pale
nilipotafuta kisingizio cha kumwambia nimemkumbuka mama yangu,
aliniambia nimtumie nauli aje Dar,” alisema binti huyo akilengwalengwa
na machozi.
Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyowahi kunaswa.
Aliendelea
kusimulia kwa majonzi kwamba, siku hadi siku amekuwa akiiona dunia
ikimuelemea kwa kuwa amechoka na hayupo radhi kufanya shughuli hiyo,
kwani mbali na hatari yake haoni manufaa anayopata.
Alisema,
awali alikuwa akilipwa Sh. 3,000 kila siku kwa kupakia kwenye paketi na
alipobadilishiwa kitengo na kuanza kuhesabu kete na kubebeshwa amekuwa
akilipwa kiduchu, yaani Sh. 50,000 kwa mwezi.
“Hii kazi
sitaki hata kuisikia, nimeshafanya kwa mwaka mmoja sasa, sijapata faida
yoyote kwani nalipwa kiduchu huku nikiishi kwa hofu muda wote hivyo
nimechoka.“Kuna kipindi mama yangu alikuja na kufikia kwake,
alimnyanyasa na kumnyima nauli ya kurudi Mwanza. Alikuwa ananiambia kama
vipi nikajiuze nipate nauli ya mama yangu.
Kamanda Godfrey Nzowa.
“Sikuwa tayari kufanya hivyo, mama yangu akasaidiwa na jirani akasafirishwa kurudi kijijini Mwanza,” alisema na kuongeza:
“Kuna wakati ananitishia maisha endapo nitatoa siri popote, jambo ambalo limenifanya nikose uhuru na amani ya maisha, ndiyo maana nimeshukuru kukutana na magazeti ya Global Publishers nitue huu mzigo.”

Katika
kile kinachozidi kumtia hofu ni pale alipoambiwa siku chache zijazo
ataanza kusafirisha unga nchi mbalimbali na kupata utajiri mnono jambo
ambalo hataki kulisikia, kwa kuwa anaogopa kuozea jela hivyo kikubwa
anachohitaji ni msaada wa nauli ya kurudi kwao Mwanza akamsaidie mama
yake ambaye ni mzee na ni mgonjwa.
No comments:
Post a Comment