Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, August 22, 2014

Olle Anasema; " Kuna Ndoto Zitakufa Leo'

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter Share on linkedin
1 2297c
Olle Anasema; " Kuna Ndoto Zitakufa Leo'
Leo ni ' Super Sunday!'
Kuna ndoto zitakufa leo. Katika vyombo vya habari vya Uingereza, leo ni 'Super sunday!' Ni kwa kuwa kuna mechi mbili kali sana!
Ni Manchester United dhidi ya Liverpool, na Arsenal dhidi ya Tottenham. Kwa mtazamo wangu, mechi ya kwanza niliyoitaja hapo juu ni muhimu zaidi. Ukweli ni huu: kama Manchester United wanafungwa au wanatoka sare leo, basi, nafasi yao ya kuchukua nafasi ya nne ni ndogo sana, na wakifungwa naamini watashindwa kuchukua nafasi hii.
Vile vile mechi hii ni muhimu sana kwa Liverpool. Kama Liverpool wanashinda leo naamini watacheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Na kama Liverpool wanashinda, Brendan Rodgers atabadilisha lengo lake. Mwanzoni mwa msimu huu Brendan Rodgers alisema lengo la Liverpool msimu huu ni kuchukua nafasi ya nne.
Lakini, kama Liverpool wanawafunga Manchester United ugenini, bila shaka 'The reds' wana nafasi na uwezo wa kushinda ligi na hii itakuwa lengo la Rodgers. Arsenal pia wana ndoto ya kushinda ligi msimu huu.
Jana Chelsea walifungwa na Aston Villa na kwa hiyo, Arsenal wanaweza kupunguza pointi ambazo wanazihitaji kuwafikisha Chelsea. Lakini, kama Arsenal wanafungwa leo, 'The gunners' watakuwa na mlima mkubwa kuwakamata Chelsea, Man City na labda hata Liverpool.
Vile vile kama Manchester United, Tottenham pia wana ndoto na lengo la kuchukua nafasi ya nne. Kwa sasa wameshika nafasi ya tano lakini Arsenal ambao wapo katika nafasi ya nne wamewapita kwa pointi sita na Tottenham wamewazidi Arsenal mechi moja. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwamba Tottenham hawafungwi.
Waingereza wana msemo: 'The ball is round'. Wana maana, kwamba chochote kinaweza kutokea katika mpira. Na chochote kinaweza kutokea katika mechi za leo. Siwezi kutabiri matokeo ya mchana huu, lakini, ninachojua ni kwamba, lazima kuna ndoto zitakufa leo!

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG