Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, August 14, 2014

UGAIDI

Ugaidi dili mpya ya kuwaandama waislamu ?

victor-arusha


  • Victor, Maofisa wa Polisi siwo tena ?
  • Na THOMMY KUNDY
    Anaitwa Ambrose Victor Calist ambae ndie aliyekamatwa baada ya kutokea mripuko wa bomu katika Kanisa Catholic La Olasiti Mjini Arusha, Tarehe 5 May 2013. Bomu hilo la kivita liliua watu wa tano na kujeruhi 60 (sitini),ilikuwa ni siku ya ufunguzi wa Kanisa hilo.
    Kukamatwa Kwa Victor kulitokana na watu kumuona akitupa kitu kilichoripuka akiwa anaendesha Pikipiki. Amefikishwa Mahakani mara moja au mbili na mpaka leo kimyaaa.Hajuulikani Victor yuko wapi, kesi yake imefikia wapi na hakuna taarifa zinazotolewa kuhusu yeye.
    Ilikuwa ni Juni 15, 2013 katika viwanja vya Soweto mkoani Arusha,mripuko wa bomu ulipotokea katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na kusababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi zaidi ya 60.
    Jeshi la Polisi lilishindwa kuwakamata wahusika huku viongozi wa Chadema wakidai kuwa na ushahidi wa picha za video zinazowaonyesha maofisa wa polisi kuhusika.
    Ushahidi wa Chadema kuwa afisa wa Polisi anahusika hatukuusikia tena, hatukujua nini kinaendelea.Ushahidi huo hadi leo hakuna ajuwaye Jeshi la polisi limeutumiaje katika kumkamata huyo afisa ambaye video ilimuonesha kuhusika.
    Wiki iliyopita nikiwa napitia kurasa mbali mbali katika mitandao kuisoma hii habari, moja ya taarifa iliyonishangaza ni taarifa niliyoipata kupitia page ya facebook ya EATV inayosomeka :
    Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetaja majina ya watuhumiwa 19 wanaodaiwa ndio kuwa ndio vinara wa mtandao wa matukio yote ya miripuko ya mabomu
    Vile vile nalo gazeti la Mwananchi la Ijumaa,Agosti 1 mwaka huu linatueleza kuwa:
    Hatimaye Polisi limewakata watu 12 likiwatuhumu kuhusika kuushambulia kwa bomu mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) uliofanyika kwenye Viwanja vya Soweto jijini hapa.
    Katika Gazeti la Mtanzania na Waandishi Eliya Mbonea na Janeth Mushi, Arusha linasema gazeti hilo: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Lebaratusi Saba aliwataja watumiwa waliokamatwa na matukio waliyohusika nayo kama ifuatavyo:-
    Kanisa la Olasiti
    Aliwataja waliohusika na tukio la ulipuaji wa bomu kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasiti jijini Arusha Mei 5, mwaka 2013, kuwa ni Yusuph Huta (30), Ramadhan Waziri (28), Abdul Humud (30) na Wakala wa Mabasi ya Mohamed Trans (ambaye amefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama).
    Wengine ni Jafar Lema (38), ambaye alikuwa Imamu wa Msikiti wa Quba (ambaye amefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama), Said Mohamed Temna (42), (ambaye amefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama).
    Wengine ni Kassim Ramadhan (34), Abashar Omar (24), ambao ni madereva bodaboda, Abdulrahman Hassan (41), pamoja na mfanyakazi wa Benki ya Stanbic Arusha.
    Wengine ni Morris Muzi (44), mkazi wa Kalinzi mkoani Kigoma, Niganya Niganya (28), mkazi wa Businde Ujiji Kigoma, Baraka Bilango(40), mkazi wa Kalinzi Kigoma na Hassan Omar (40).
    Mripuko mkutano wa Chadema
    Alisema Jeshi la Polisi limewanasa watuhumiwa kadhaa ambao walihusika katika tukio la uripuaji wa bomu Juni 15, mwaka jana kwenye mkutano wa kampeni za udiwani za Chadema.
    Watuhumiwa hao ni Yusuph Huta (30), Abdul Humud (30), pia wapo Said Temba (42), ambao wamefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama na Jafar Lema (38).
    Wengine ni Imamu wa Msikiti wa Quba, Sheikh Abuu Ismail, ambaye amefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na bomu la Mgahawa wa Vama. Wengine ni Kasim Ramadhan (34), ambaye ni dereva wa bodaboda, Ramadhan Waziri (28).
    Alitaja watuhumiwa wengine kuwa ni Abashar Hassan Omar (24), Abdulrahman Hassan (41), mfanyakazi wa Benki ya Stanbic Arusha, Morris John Muzi (28). Wengine ni Niganya Niganya (28), Baraka Bilango (40) na Hassan Omar (40).
    Kila mtu kasoma vizuuri majina ya wahusika wa bomu la Olasiti, lakini jina la Ambrose Victor Calist limekosekana. Pia mripuko wa Soweto kamanda Lebaratus Sabas alisema kuwa waliotiwa mbaroni wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani, hakuna ofisa wa polisi hata mmoja. Kisha Kamanda huyo akadai kwamba Chadema iligoma kutoa ushahidi huo wa picha za video.
    Kama Chadema hawana ushahidi basi washitakiwe kwa kulisingizia uovu Jeshi la Polisi. Mbona hata hilo halifanyiki? Wapelekeni mahakamani wale wanaosema mumwehusika. Ili nasi tuamini kweli hamujahusika.
    Huenda kuna kamchezo tu kanachezwa-chezwa, atiwe matatizoni asiyehusika. Na waliohusika wapate kujisafisha. Unadhani Polisi kama hajahusika wangekubali kuchafuliwa ?Nina uhakika kama hawajahusika wangekuwa wameshaishitaki zamani Chadema.
    Nani anakubali kuchafuliwa? Nani atakubali kutiwa dosari isiyomuhusu? Wangekubali kweli kuzuliwa? Wangekuja na mambo meengi mno, “ohh Chadema tunawashtaki kwani wanaondosha uwaminifu wetu kwa raia”. Lakini sijalisikia hili.
    Mbali na matukio hayo ambayo watuhimiwa wa mwanzo walipatikana lakini haijuulikani wameishia wapi, kilchpofanyika na kutafuta watuhumiwa wapya na kuwapachika mzigo.
    Hao sasa wamekuwa kama chambo kwani matukio yote hayo sasa wahusika wamekuwa wao na hata yale matukio ya Bomu nyumbani kwa Katibu wa Bakwata, Kumwagiwa tindikali Sheikh Makambawa,Kumwagiwa tindikali Sheikh Mustapha, Tukio la Arusha Night Park, Bomu nyumbani kwa Sheikh Sudi n.k. Matukio yooooote hayo wao ndio wamekuwa wahusika.
    Ni kama palikuwa anatafutwa ni nani tumtwike huu mzigo, lakini inavyoonekana wamewapata wa kuwatwika mizigo na kuwakumbizia yoote hayo. Hata ile mizigo ya Maofisa Polisi na mzigo wa Ambrose Victor Calist yote wamebebeshwa wao na wao ndio wahusika. Polisi na Victor siwo tena!!
    Hatuingilii masuala yao lakini pia tunayo haki ya kuhoji, uko wapi ushahidi wa video na picha ambao Cahadema walikuwa nao? Yuko wapi Victor mshukiwa wa bomu la Ollasiti?
    Aliyefanya uovu achukuliwe hatua lakini asitafutwe mtu asiyehusika akatwishwa mizigo si yake. Kila muovu alipwe kwa uovu wake na mwema asitafutiwe matatizo na kuingizwa katika mambo asioyajua.
    Tunaelezwa kuwa Kenya baadhi ya watu walikuwa wanabambikiziwa mabomu na bunduki kisha wanauwawa bila hata ya kufikishwa mahakamani. Musione aibu kusema kuwa aliyehusika bado hatujampata hata kama itachukua miaka mingi lakini musitake kuonekana ni wafanya kazi bora kwa kuwaingiza wasio husika matatizoni.
    Mtenda muovu na ahukumiwe kwa uovu wake lakini, wasiingizwe matatizoni wasiohusika. Tusiige mifumo ya wenzetu wa Kenya. Kenya imeanza kuvuruga katika suala la amani kwa sababu za kutaka kuonekana ni wapambanaji wazuri wa kinachoitwa ugaidi. Lakini kumbe wanazidi kuichafua hali ya hewa.
    Baada ya kupewa misaada na Wazungu hutafuta watu na kuwabambikizia makosa ya ugaidi ili waletewe misaada zaidi na waonekane ndio anapambana na ugaidi. Tuwe tunajifunza makosa ya majirani zetu sisi tusiyarudie

    No comments:

    Post a Comment

    TUPAMBANE BLOG