- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter
Na Mwandishi Wetu, Katavi
YULE mtoto wa umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Regina Geofrey aliyeuawa kikatili kwa kunyongwa kisha kuzikwa na baba yake mzazi, Geofrey Kilangwa ‘Simbaiwe’ (27) kwa kuwa alizaliwa akiwa ametanguliza makalio yake, amezidi kuibua maswali.

Mtuhumiwa Geofrey Kilangwa ‘Simbaiwe’( katikati) aliyemuua mwanaye mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, Regina Geofrey.
Baadhi ya
wakazi wa Katavi waliozungumza na gazeti hili juzi, walihoji uhalali wa
baba kumjadili mtoto katika kuzaliwa kwa sababu ya kutanguliza kiungo
fulani.
Wengine walitaka kujua ni kwa nini kama kumuua mtoto wake, mzazi huyo alisubiri kwa mwaka mmoja na miezi miwili?(P.T)
Wengine walitaka kujua ni kwa nini kama kumuua mtoto wake, mzazi huyo alisubiri kwa mwaka mmoja na miezi miwili?(P.T)
Mtuhumiwa
ambaye pia ni mganga wa kienyeji anayeishi Kitongoji cha Mwikang’ombe,
Kijiji cha Katuma wilayani Mpanda, alitenda unyama huo kwa madai kuwa
mtoto huyo alizaliwa akiwa ametanguliza makalio, hivyo ni nuksi kubwa
katika shughuli zake za uganga wa kienyeji, madai yaliyopingwa na watu
mbalimbali, zikiwemo taasisi za kutetea haki za binadamu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, akizungumza na waandishi
wa habari mjini hapa, alidai mzazi huyo alitenda uhalifu huo Agosti
20, mwaka huu ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi, Agosti 26.
Ilidaiwa
siku hiyo ya tukio, mtuhumiwa huyo baada ya kumnyonga hadi kufa binti
yake, alimzika kwa siri katika kibanda chake anachofanyia shughuli za
uganga.
Kamanda Kidavashari alisema mtoto Regina alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa ambao haukufahamika kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Kamanda Kidavashari alisema mtoto Regina alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa ambao haukufahamika kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari.
“Ndipo
baba mzazi wa binti huyo alipomchukua marehemu na kwenda kumuuguza
kwa siri pasipo mama yake mzazi kufahamu kwani alimdanganya kuwa mtoto
wao amepelekwa kutibiwa na babu yake mkoani Mwanza,” alisema
Kidavashari.
Kwa
mujibu wa Kamanda Kidavashari, wakazi wa kitongoji hicho wakiongozwa na
mwenyekiti wao, walimtilia shaka mtuhumiwa kutokana na tetesi
zilizosambaa kwamba, Regina aliuawa na baba yake mzazi na kuzikwa kwa
siri.
Mwenyekiti
huyo na wakazi wa eneo hilo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa na kuhoji
alipo binti yake, aliposhindwa kujibu wakasema wampekue ambapo alipinga
vikali lakini alipopekuliwa kibandani kwake walibaini kuwepo kwa tuta
dogo lililokuwa limechimbwa siku za karibuni.
Wakazi hao walifukua tuta hilo na kukuta kichwa cha mtoto Regina na ndipo wakalitaarifu jeshi la polisi.
Mama wa marehemu, Maria Exavery (22) alisema hakupewa taarifa kwamba binti yake amekufa.
“Mimi nilikuwa nafahamu Regina yuko kwa babu yake Mwanza akitibiwa,” alisema huku akimwaga machozi.
Mama wa marehemu, Maria Exavery (22) alisema hakupewa taarifa kwamba binti yake amekufa.
“Mimi nilikuwa nafahamu Regina yuko kwa babu yake Mwanza akitibiwa,” alisema huku akimwaga machozi.
Naye
Regina Kaboni (40), mkazi wa Isamilo Mwanza ambaye alikuwa akitibiwa na
mtuhumiwa, anadai kuwa alishirikishwa katika maziko ya binti huyo
baada ya kufa.“Hata hivyo, nilishtushwa sana kwa kitendo cha mtuhumiwa
kumzika mwanaye bila mkewe, nilipomuuliza akadai mila za kwao mtoto
aliyezaliwa kwa kutanguliza makalio, mama mzazi wa mtoto ni mwiko
kushirikishwa katika maziko.
Kwa
mujibu wa Kidavashari watu wanne, wakiwemo wazazi wa marehemu
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi ambapo watafikishwa
mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika.Wengine wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni Regina Kaboni na Msolwa Jacob (29), mkazi wa Kitongoji cha Mwikang’ombe
No comments:
Post a Comment