Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Tuesday, September 2, 2014

DALEY BLIND TUMAINI JIPYA LA ULINZI MANCHESTER UNITED

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter

NaThommy kundy Tupambane Blog
Hatimae klabu ya Manchester United imefanikiwa kumnasa beki wa Ajax, Daley Blind kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 14. Ujio wa beki huyo huenda ukashusha presha ya mashabiki wa timu hiyo. Daley Blind ambaye msimu uliopita alikuwa mchezaji bora wa Uholanzi, sasa anajiunga na aliyekuwa kocha wake kwenye timu ya taifa Uholanzi. Kwa matatizo ya ulinzi ya Manchester United anaweza kuwa ni msaada tosha kwa timu hiyo.
Lakini kocha Louis Van Gaal anatakiwa kubadilisha mfumo anaoutumia kwenye timu hiyo. Tumeshuhudia mechi kadhaa za timu hiyo wachezaji wakishindwa kuumudu mfumo anao utumia kocha huyo. Kama kusipofanyika mabadiliko ya mfumo basi, hata usajili alioufanya utakuwa ni sawa na kuziba shimo la panya kwa mkate. Kwa maana kwamba hatafanikiwa kutatua tatizo kwa muda lakini tatizo litabaki pale pale.
Manchester United inahitaji msingi mpya kwenye eneo la ulinzi baada ya kuondokewa na safu yake karibu yote. Safu ambayo ilikuwa inaundwa na Patrice Evra, Rio Ferdinand na Nemanja Vidic ambao waliunda ukata imara kwa timu hiyo. Niseme tu kuwa kwa sasa Manchester United inapita kwenye kipindi kigumu. Kipindi ambacho kinahitaji uvumilivu kwa wamiliki wa timu ili kumpa nafasi kocha aweze kuijenga upya timu hiyo.
Kocha Louis Van Gaal baada ya matokeo mabaya kwa kikosi chake imemlazimu kusajili ili kukipa uhai kikosi hicho.Lakini pia tusubiri kuona zama mpya za timu.Tumaini pekee la ulinzi litabaki kwa Daley Blind ambae atakuwa ni sawa na ufunguo wa wa peponi kwa timu hiyo.Tumesoma vitabu vya Rio Ferdinand na Nemanja Vidic sasa ni zamu ya kusoma kitabu cha Daley Blind. Karibu Old Traffod ulete tumaini jipya.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG