Raia wa
Sierra Leone wamesalia majumbani mwao kwa siku ya pili mfululizo wakati
ambapo taifa hilo linatekeleza agizo la kutotoka nje la masaa 72 ili
kujaribu kusitisha ueneaji wa ugonjwa wa Ebola.
Mwandishi wa BBC
katika mji mkuu wa Freetown anasema kuwa barabara nyingi za miji ambazo
zimekuwa zikijaa watu hazina watu kwa sasa.Mwandishi wetu anasema kuwa kituo cha oparesheni za dharura kilipokea zaidi ya simu 900 katika siku ya kwanza ya agizo hilo,kupitia kuwaripoti wagonjwa ama kutaka miili ya wafu kuchukuliwa.
Amesema kuwa kuna vituo viwili pekee katika taifa hilo na kwamba kituo kimoja katika eneo la Kenema kimejaa wagonjwa.
No comments:
Post a Comment