- Written by Tupambane Blog
BUNGENI |
Suala la
Mahakama ya Kadhi limechafua hali ya hewa bungeni mjini Dodoma baada ya
wajumbe Waislamu kutishia kupiga kura ya hapana kama halitaingizwa
katika Rasimu inayopendekezwa.
Wakati
Waislamu wakishikilia msimamo huo, wajumbe ambao ni Wakristo nao
wamejipanga kupiga kura ya hapana endapo Mahakama ya Kadhi itaingizwa
katika Katiba inayopendekezwa.
Dalili za
mpasuko huo zilianza kujitokeza jana asubuhi baada ya mjumbe mmoja,
Jaku Ayub Hashim kuwasha kipaza sauti akitaka kuzungumza akisema ana
jambo muhimu.(t.k)
"Mheshimiwa
tangu jana (juzi) ulisema utanipa nafasi ya mwanzo nizungumze," alisema
Jaku, lakini Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu alimtaka aketi chini na
suala lake limesikika.
Suluhu
akaendelea kuwapa wajumbe wengine kuendelea kuchangia na baadaye alimpa
Jaku muda wa dakika saba ili kuwasilisha kile alichotaka kukizungumza
ndani ya Bunge hilo.
Jaku
alisema walipendekeza kifungu kinachotaka uamuzi unaohusu ndoa, talaka
na mirathi iliyoamuliwa kwa misingi ya dini ingizwe kwenye Katiba
inayopendekeza lakini hakimo.
"Ni kitu
kidogo kabisa tuliomba kiongezwe lakini cha kusikitisha kikundi cha
sanaa kimeingizwa. Mimi binafsi yangu sitaunga mkono wala mguu wala
sitaipigia kura hii," alisema Jaku.
Suluhu
akamweleza kuwa angalizo lake limechukuliwa, na uongozi wa Bunge pamoja
na kamati ya Uandishi wanajitahidi kuingiza kila kitu kinachowezekana,
lakini kwa misingi na sheria za nchi.
Baadaye
Sheikh Masoud Jongo alipopewa nafasi ya kuchangia, naye alitahadharisha
kuwa mambo yaliyopendekezwa na Waislamu yasipoingizwa kama ilivyo kwa
sasa, hawatakuwa tayari kwa lolote.
"Msimamo
wetu sisi Waislamu kama mambo yetu tuliyoleta katika mapendekezo
hayataingizwa, basi yatabomokea hapa na hatutakuwa tayari tena," alisema
Sheikh Jongo, kauli iliyowashtua wajumbe.
Akihitimisha
majadiliano hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge
alisema kamati yake imefanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kwa masilahi ya
Watanzania. Akiahirisha Bunge, Suluhu alisema kesho Bunge litaanza kwa
kupitia baadhi ya mambo yaliyoibuka katika uhakiki kisha kupitisha
azimio la upigaji wa kura. Kura zitapigwa kati ya kesho hadi Oktoba 2.
Baada ya
kuahirishwa kwa Bunge, Sheikh mwingine, Hamid Jongo alimwendea Askofu
mstaafu Donald Mtetemela na kumkumbatia, kisha kumvuta pembeni na kisha
kuteta kwa dakika tano.
No comments:
Post a Comment