Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, September 10, 2014

ODAMA: SIWEZI KUWASAHAU YATIMA

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter 

Stori: Gladness Mallya
MWANADADA Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa katika maisha yake hawezi kuwasahau watoto yatima na kuanzia sasa, kila mwaka lazima asherehekee nao katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Mwanadada Jennifer Kyaka ‘Odama’
Odama ambaye hivi karibuni alifanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kutoa misaada ya vyakula na vitenge kwa watoto yatima na walezi wao wa kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Dar huku akiangusha sherehe ya nguvu ndani ya ukumbi wa Vijana na kuungana na watoto hao, alisema huu ni wakati wa watoto kufurahi naye.
“Nimeshasherekea sana bethdei baa na marafiki zangu, lakini kwa sasa nimebadilika na ndiyo nimeanza mwaka huu nitakuwa na watoto yatima kila mwaka nikikumbuka siku yangu ya kuzaliwa kwani kama hivi wamejisikia faraja sana kuja kula pamoja na mimi, kucheza muziki pia kuwaona waigizaji mbalimbali imekuwa ni furaha kwao,”alisema Odama

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG