Posted by tupambane blog
In Summary
Ni hivi majuzi tu vyombo vya habari vilitawaliwa na
habari ya aibu kuhusu Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali
(Shimiwi) baada ya timu ya Mchezo wa Pete (netiboli) ya Uchukuzi
kuondolewa mashindanoni katika hatua ya nusu fainali.
Ni hivi majuzi tu vyombo vya habari vilitawaliwa
na habari ya aibu kuhusu Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali
(Shimiwi) baada ya timu ya Mchezo wa Pete (netiboli) ya Uchukuzi
kuondolewa mashindanoni katika hatua ya nusu fainali.
Timu hiyo iliyoibuka mshindi katika mchezo huo
iliondolewa ilipobainika kuwatumia wachezaji mamluki katika mechi yao na
timu ya netiboli ya Mahakama.
Tukio kama hilo linaonyesha ni vipi Watanzania
wanaamua kujidanganya wenyewe hata katika mashindano yaliyoandaliwa kwa
ajili ya kujifurahisha na kujumuika pamoja nje ya shughuli zao za kila
siku za maofisini.
Katika soka mchezo unaopendwa na wengi nao
umetawaliwa na hujuma na udanganyifu wa kila aina mambo ambayo tunaamini
ni sehemu ya tatizo au kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya mchezo huo.
Katika soka usiposikia hujuma za wizi wa tiketi,
utasikia hujuma za kupanga matokeo, usiposikia hujuma za wachezaji
kununuliwa utasikia hujuma za waamuzi kuhongwa.
Haya ni baadhi ya matatizo ambayo ni muhimu
yakadhibitiwa ili harakati za maendeleo ya soka ziweze kufikia malengo
yanayokusudiwa.
Kati ya yote hayo udanganifu ambao umekuwa
ukitukera mara kwa mara ni ule wa kudanganya umri kwa wachezaji, jambo
ambalo hufanyika mara kwa mara katika mashindano mbalimbali ya vijana
wadogo yenye lengo la kuibua vipaji.
Hili kwa sasa ni tatizo sugu ambalo linakwamisha
juhudi za kuibua vipaji na kibaya ni kwamba hazionekani dalili zozote za
kukabiliana na tatizo kwa nia ya kulimaliza.
Nia ya kuyazungumzia yote haya ya udanganifu na
hujuma ni kuweka msisitizo katika hoja iliyotolewa hivi karibuni na
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij aliyelalamikia kitendo cha timu hiyo
kumtegemea mno Mbwana Samatta.
Nooij alisema kwamba ni vyema juhudi zikafanyika kuibua vipaji vya wachezaji ili kuachana na utegemezi wa mchezaji mmoja.
Ni ukweli ulio wazi kwamba mshambuliaji huyo
anayeichezea Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni
mchezaji mzuri na tegemeo katika Taifa Stars.
No comments:
Post a Comment