Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, October 30, 2014

GAMA AHIMIZA UFUGAJI WA NYUKI KILIMANJARO



Na Mwandishi Wetu, KILIMANJARO
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amewaagiza wataalamu wa ufugaji wa Nyuki katika Halmashauri za mkoa, kuhakikisha wanaenda vijijini kutoa elimukwa wananchi juu ya ufugaji bora wa Nyuki.
Gama ametoa agizo hilo baada ya kukabidhi mizinga 150 ya Nyuki na pikipiki 10 iliyotolewa na shirika la UNDP kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Tanzania.
Amesema ufugaji wa nyuki unahitaji uwepo wa mazingira mazuri yatakayoruhusu kuwepo kwa miti ya kutosha ambayo nyuki watatumia maua yake kuzalisha asali na kuwataka wanchi kuendelea kuhimizwa kutekeleza amri ya kutokata miti  ikiwa ni pmoja na kusisitizwa kupanda miti kwa wingi.
 
Aidha Gama amelishukuru shirika la UNDP kupitia kwa mwakilishi wake mkoani hapa, ndugu Francis Mkanda kwa juhudi wanazofanya kuboresha maisha ya wana Kilimanjaro kupitia kilimo na ufugaji.
 Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa, amesema Ufugaji wa ni Nyuki fursa ya ajira binafsi kwa mtu yeyote Yule, kaya au kikundi na kuongeza kuwa kwa kutambua hilo, serikali ilishaanza kuzuia ukataji, upasuaji na usafirishaji wa mbao kuanzia Februari 29 mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG