Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, October 8, 2014

JK KUPEWA ‘KATIBA MPYA’ LEO

  • Written by  Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter 

Stori:  Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete, leo atapokea ‘Katiba Mpya’ inayopendekezwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samuel Sitta, katika tukio linalotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Rais Jakaya Kikwete,
Bunge hilo maalum, lilihitimisha kazi yake ngumu ya kujadili rasimu ya katiba mpya iliyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba Oktoba 4 mwaka huu, baada ya Kamati ya Uandishi chini ya Andrew Chenge kuwa imewasilisha katiba inayopendekezwa iliyokubaliwa na wajumbe kutoka Bara na Visiwani.
Katiba hiyo inayopendekezwa, ilipatikana licha ya baadhi ya wajumbe kutoka vyama vya upinzani kujitoa kwa madai ya kuburuzwa na wenzao wa chama tawala, kitendo kilichoibua mjadala wa kitaifa huku makundi mbalimbali yakipingana, wengine wakiwaunga mkono na wengine wakiwapinga

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG