Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, October 9, 2014

Madhara ya kufanya mapenzi kupita kiasi


Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini
linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo
huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.
Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine
wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha
usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya
hivyo kwa sababu amelipa mahari.
 Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi
unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za
kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.
Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa
na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema
tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika
kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya
miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika.
Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO.
Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi
kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza
wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.
Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha
kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.
Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana
na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine
sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza
kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza
hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA.
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni
mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa
kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye
uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi
na kwa wakati gani?
Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale
ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake.
 Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au
kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa
zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.
 Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa
kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na
houseboy ili akukate kiu ya penzi.
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO.
Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi
na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila
mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha
ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.
 Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako
utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI.
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara
ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.
 Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu
nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa
wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya
kimaisha.
Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya
mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.
KUPATA MAGONJWA.
Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na
tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia
magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na
msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na
kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko
wakati wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza
kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG