- Written byTupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Ligi kuu
ya England imeendelea jana usiku ambapo Manchester United ilijikuta
ikibanwa mbavu na kushindwa kufurukuta ugenini kwa Westbromwich Albion
na kutoka sare ya mabao 2-2 licha kwamba ilitawala mchezo huo.
Mchezo
huo wa pekee kwa ratiba ya ligi hiyo ulishuhudiwa Man United ikishindwa
kupata walau ushindi wake wa kwanza nje ya uwanja wake wa nyumbani tangu
timu hiyo iwe chini ya kocha Louis Van Gaal.
Ni bao la
Daley Blind katika dakika za mwisho za mchezo ambalo limeiokoa
Manchester United kuzama katika mpambano huo. Awali Stephane Sessegnon
wa Westbrom aliitungua United kwa bao la mapema kabla ya Marouane
Fellaini aliyeingia kipindi cha pili kusawazisha muda mfupi tu baada ya
kuingia uwanjani.
Mshambuliaji
kijana Saido Berahino aliipatia Westbrom goli la pili ambalo lilidumu
hadi pale Blind aliposawazisha na kuinusuru United na kichapo katika
mtanange huo uliochezeshwa na mwamuzi Mike Dean.
No comments:
Post a Comment