Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, October 29, 2014

MAPOROMOKO YA UDONGO YAUA 10 SRI LANKA


  • Written by Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter 

Wananchi wakishuhudia baadhi ya nyumba zilizofunikwa na maporomoko hayo.
WATU 10 wamepoteza maisha huku zaidi ya 300 wakiwa hawajulikani walipo baada ya kutokea maporomoko ya udongo katikati mwa nchi ya Sri Lanka leo.
Maporomoko hayo yametokea kufuatia kunyesha kwa mvua kubwa ambapo takribani nyumba 140 zimefunikwa na udongo katika Wilaya ya Badulla.
Msemaji wa Kitengo cha Kukabiliana na Maafa nchini humo, Sarath Kumara amethibitisha taarifa hizo.
Vyombo mbalimbali vya uokoaji vipo eneo la tukio kujaribu kuokoa majeruhi wa tukio hilo.
Maporomoko hayo pia yamelikumba shamba kubwa la chai la Meeriyabedda lililopo karibu na mji wa Haldummulla, uliopo kilomita 200 (maili 120) mashariki mwa mji mkuu Colombo

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG