Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, October 12, 2014

Ndani Ya Miaka Kumi, Nyerere Alituvusha Kwenye Mitihani Migumu Mitano, Na Hakuwa Dikteta...


  • Written by Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter 

Ndugu zangu,
Nimeyaandika haya kufuatia mada niliyoianzisha juu ya hamu inayojengeka kwenye jamii ya kutamani udikteta.
Nimemjibu ndugu Galinoma kama ifuatavyo;
"Galinoma, foleni za unga haikumaanisha udikteta. Dunia ilikuwa tofauti na sasa. Dunia ilikuwa kwenye vita baridi na mapambano ya kiitikadi; Ujamaa dhidi ya Ubepari. Mimi ni Mjamaa, na zaidi ni Social Democrat.
Nimekulia katikati ya mapambano hayo ya kiitikadi. Nchi yetu wakati huo ilipitia mitihani migumu mitano kama taifa; Mtihani wa kwanza; migogoro miwili ya mafuta duniani.
Ni kati ya 70 na 73. Mtihani wa kwanza wa mafuta ni mwaka 1970. Wa pili mwaka 1973. Mtihani wa tatu ni ukame wa mwaka 74. Watanzania tulikula 'Unga wa Yanga' kwa maana ya unga wa njano. Mtihani wa nne ni kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977. Mtihani wa tano ni Vita vya Kagera 1978-79.
Ndani ya miaka kumi nchi yetu ilipitia mitihani migumu mitano. Nilikuwa na miaka kumi na moja pale Kinondoni Biafra, nilipomsikia kupitia redio, Julius Nyerere akitangaza vita dhidi ya dikteta Idd Amin aliyetuvamia na kuchukua sehemu ya ardhi yetu.
Usiku ule niliyaona magari ya kijeshi yakipita nje ya nyumba yetu, Morocco rd, yakitokea kambi ya Lugalo kwenda mpakani. Ndio, nimeishi na kushuhudia mwaka ule wa 79, pale uwanja wa taifa, mbali ya kumpoteza rubani wetu kwenye ndege ya kivita iliyokuwa ituangukie uwanjani, lakini rubani akajitahidi aende akaanguke nayo nje ya uwanja, Julius Nyerere alitoa hotuba muhimu yenye kutuandama hadi leo. Alirudia kusema kuwa vita si lelemama, na kwamba Watanzania tujiandae kufunga mikanda kwa miezi kumi na nane. Na hakika imekuwa zaidi ya miaka 18, na hadi leo tuna makovu ya vita. Ni makovu ya kiuchumi.(T.K)
Naam, ndani ya miaka kumi nchi yetu ilipitia mitihani mitano migumu. Nyerere hakuwa dikteta, alijenga uongozi wa kitaifa uliojenga ushawishi na mshikamano wa kitaifa tukaweza, hata kwa tabu, kuvuka mitihani hiyo mitano na tukabaki kama taifa.
Ndio maana leo, inashangaza, wakati tumepoteza ndugu zetu kupambana na kumng'oa dikteta Idd Amin, tunajadili hamu ya kuwa na rais dikteta. Historia ni mwalimu mzuri, tuipitie historia yetu. Uganda wamekuwa na dikteta Idd Amin kwa miaka 8, lakini, hata Amin hakumaliza rushwa kwa vifaru vyake vya jeshi. Badala yake alisambaza hofu kwa Waganda na kuwaandama na hata kuwapoteza wapinzani wake.
Na kwa vile , kama taifa, tumepigana na kumshinda dikteta, basi, tusikubali kumkaribisha wenyewe dikteta ndani ya ua wetu...
Maggid Mjengwa.
59 mins · Like
Joey Galinoma Nashukuru kwa somo lililojitosheleza sana. Nadhani somo litasaidia kuelimisha wengine waliochangia uzi huu. Usiku mwema.
33 mins · Unlike · 1
Maggid Mjengwa Asante sana Galinoma kwa kunielewa. Tofauti za kimawazo ni jambo la siha kwa jamii ili iendelee, ingawa kwenye udikteta yaweza kuwa nongwa!

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG