Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, October 16, 2014

Semina za kidini zawabadili vijana wa Puntland kutoka katika

Zaidi ya vijana 600 kutoka Puntland walishiriki katika mfululizo wa semina za mwezi mmoja ambazo zililenga kuongeza amani na kupambana na tabia mbaya katika jamii kupitia mafundisho ya dini, waandaji wa mkutano waliiambia Sabahi

  • Vijana wanaume na wanawake waliohudhuria mfuatano wa semina walihusika katika mijadala kuhusu jinsi wanavyoweza kusaidia kurejesha utulivu nchini Somalia. [Hassan Muse Hussein/Sabahi] Vijana wanaume na wanawake waliohudhuria mfuatano wa semina walihusika katika mijadala kuhusu jinsi wanavyoweza kusaidia kurejesha utulivu nchini Somalia. [Hassan Muse Hussein/Sabahi]
  • Wanazuoni wa kidini kutoka Puntland wakitoa mhadhara kuhusu umuhimu wa kuwaelimisha na kuwaajiri vijana ili wasitekwe na itikadi za siasa kali. [Hassan Muse Hussein/Sabahi] Wanazuoni wa kidini kutoka Puntland wakitoa mhadhara kuhusu umuhimu wa kuwaelimisha na kuwaajiri vijana ili wasitekwe na itikadi za siasa kali. [Hassan Muse Hussein/Sabahi]
Mkutano ambao uliitwa "al-Risala" (ujumbe), uliandaliwa na shirika la Garowe linaloitwa al-Minhaj, na kumalizika Jumatano (tarehe 18 Julai).
"Lengo la tukio ni kuzuia vijana wasitumiwe kwa manufaa [na wenye siasa kali]," mratibu wa tukio la al-Minhaj Abdirahman Ibrahim Dirie aliiambia Sabahi.
Semina za kila siku zilikuwa za muda wa saa tano za masomo shirikishi ambayo yalianza mara tu baada ya sala ya asubuhi na kumalizika baada ya sala ya mchana katika Msikiti wa al-Hudda huko Garowe. Sehemu ya programu ilitumiwa na wazungumzaji na wahadhiri, na kisha ilitoa nafasi kwa maswali na majadiliano miongoni mwa waliohudhuria.
Lengo la mkutano lilikuwa ni kuwaelimisha vijana wanaume na wanawake kuhusu mafundisho sahihi ya Uislamu na falsafa ya sheria za Kiislamu.
"Mihadhara ilikuwa ya kina," alisema. "Ilihusisha [mafundisho] kuhusu Uislamu ni nini na [ujumbe] mzuri unaowakilishwa, umuhimu wa vijana kufuata dini [kwa haki], historia na utamaduni wa Somalia, [kuelewa] uraia na wajibu wao kwa nchi."
Mihadhara zililenga katika jukumu na uwajibikaji wa vijana katika kulinda amani, alisema.
Ni muhimu kujadili usalama na vijana ili wasipotoshwe katika kujiunga na al-Shabaab, Dirie alisema. "Ni muhimu kulieleza hili kwao ili wawe na ulinzi dhidi ya wale wanaotaka kuwatumia katika kuvunja amani."
Waandaaji walisema wamechagua kufanya semina wakati wa majira ya kiangazi na kabla ya Ramadhani ili kutumia muda wa kufungwa kwa shule na kuwapa wanafunzi wa sekondari ya juu na chuo kikuu kitu cha manufaa kufanya wakati wa mapumziko yao ya shule.
"Ni mara yangu ya kwanza kuwa sehemu ya mkutano kama huu," alisema Mohamed Abdullahi Ali, mwanafunzi wa sekondari ya juu mwenye miaka 20 aliyehudhuria mkutano. "Tulikuwa na majadiliano kuhusu masuala mengi, na ulikuwa ni mkutano ambao ungeweza kufanyika zamani."
Ali alisema kimsingi alifikiria programu ingekuwa kama mafunzo fulani, lakini baadaye alifurahishwa kuona kwamba ilikuwa ni semina shirikishi iliyozungumzia masuala mengi na vipengele vya maisha ambavyo vinamgusa.

Wataalamu wa dini wazungumza dhidi ya al-Shabaab

"Al-Shabaab wamekuwa wakiwalenga vijana katika matangazo yao ya vyombo vya habari, na kuwataka kuwa sehemu ya jihad," alisema Sheikh Yusuf Abdiaziz Mohamed, mmoja wa wataalamu wa dini aliyezungumza katika semina. "Ni muhimu kwa vijana kujitenga na itikadi kama hizo."
Mohamed, ambaye ni mjumbe wa bodi katika Bariga Afrika, chuo kikuu chenye kampasi huko Bosaso na Garowe, aliiambia Sabahi ilikuwa ni muhimu kuweka mkazo kwa vijana ili kuwazuia kutekwa nyara na kampeni za vyombo vya habari za al-Shabaab.
Mtaalamu mwingine wa dini aliyezungumza katika semina alikuwa Sheikh Abdulqadir Nur Farah, mmoja wa wataalamu wanaojulikana sana Puntland. Alizungumza kwa kirefu kuhusu umuhimu wa amani kwa vijana, pamoja na kwa nchi.
"Kila mtu anawajibika kwa nafsi yake na kuhakikisha kwamba hakuna madhara yanayotokea katika mwili wake. Vijana wanapaswa kulifahamu hili," Farah alisema.
Zaidi ya mihadhara, waandaji walitoa nafasi kwa washiriki wanafunzi kuonyesha vipaji vyao katika namna mbalimbali, ikiwa ni pamoja na katika ushairi, fasihi, mila na desturi, na masomo ya utamaduni, ili kuhamasisha kujifunza na kuelewa somo na kukuza hisia ya uwezeshaji.
Waziri wa Kazi, Vijana na Michezo wa Puntland Abdiweli Hirsi Abdulle, aliyehudhuria sherehe za kufunga siku ya Jumatano, alisema uongozi ulifurahishwa na misheni ya tukio na jinsi lilivyofanyika.
"Tungependa programu iendelee, na [kwa waandaaji] kuandaa matukio mbalimbali," aliiambia Sabahi. "Nilifurahishwa na jinsi vijana walivyowasilisha mawazo yao na kujadiliana miongoni mwao."
Wizara ya Elimu ilisaidia programu kwa kutoa viandikia na vitabu.
Hii ni mara ya kwanza semina kama hii kufanyika kwa vijana wa Puntland na waandaaji bado hawajasema kama watarudia tena tukio hili na lini.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG