Baadhi
ya mwashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 wakishangilia kwa hisia,wakati
shoo ikiendelea jukwaani ndani uwanja wa Namfua mjini Singida.
Kundi
mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando
wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua
mjini Singida.(P.T)
Sehemu
ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la
Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida.
Mmoja wa mashabiki akishangilia huku akiwa amebebwa
Msanii
wa muziki wa bongofleva,Mr Blue a.k.a Kabyssal akiimba mbele ya umati wa
wakazi wa mji wa singida waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta
lililofanyika hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua.
Sehemu ya umati wa watu ndani ya tamasha la Fiesta mjini Singida hapo jana katika uwanja wa Namfua
Ilikuwa ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Namfua wakati tamasha la Fiesta likiendelea.
Msaniii
mwingine anaefanya vyema katika anga ya muziki wa bongofleva,kupitia
kundi la WEUSI,Niki wa Pili akiwaimbisha mashabiki wake
Shabiki kapagawa na yaliyokuwa yakijiri jukwaani.
Badala ya kuwa watazamaji tu,nao pia walikuwa wakijimwaya mwaya taratiibu.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael
akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta
likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
Msanii
mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake wa
Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya
uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
Mmoja wa
wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kizazi kipya atambulikae kwa jina
kisanii Mwana-FA akiimba mbele ya umati wa wakazi wa Singida
waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika jana ndani ya
uwanja wa Namfua.
Mashabiki wakishangilia
Wasanii
mahiri wa muziki wa Bongofleva,Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia
jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa jina la Huko kweni
Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa
Namfua mjini Singida.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Singida wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ndani ya tamasha la Fiesta.PICHA NA TUPAMBANE-SINGIDA.
No comments:
Post a Comment