Marekani inasema kuwa haina thibitisho lolote kuhusu mkataba wa
kusitisha mapigano uliotangazwa kati ya jeshi la Nigeria na kundi la
wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa rais nchini Nigeria amesema
kuwa makubaliano hayo yalihusu kuachiliwa kwa zaidi ya wasichana 200 wa
shule waliotekwa na Boko Haram miezi sita iliyopita.Makubaliano hayo yaliafikiwa baada ya wiki kadha za mazungumzo yalioongozwa na Chad na mikutano zaidi inahitajika ili kuafikia jinsi wasichana hao watakavyoachiliwa.


No comments:
Post a Comment