Mtungaji:
Thommy kundy
Mfasiri:
ombeni james
Kwa jina
la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Jaribio
la Kumfahamu
Kabla ya kufikia umri wa miaka kumi
na mitano kwa kipindi kidogo, mwanadamu hukabiliana na kipindi muhimu na cha
hatari katika uhai wake, nacho ni kipindi cha ujana (ubarobaro) ambacho
huendelea nacho hadi kufikia umri wa miaka ishirini au ishirini na tano hivi.
Hiki ndicho kipindi cha ubarobaro (ushababi), nacho ni kipindi muhimu na cha hatari. Hebu tujiulize kwa nini kuwa ni muhimu na hatari?
Ni muhimu kwa kuwa huihukumu hali
ya baadaye ya umma na mwisho wake. Vijana hawa wanaokua hivi leo
bila shaka wao ndio umma wa kesho.
Umma huu ulioko hivi sasa utaondoka na
pahali pao na vyeo vyao vitachukuliwa na hawa vijana. Naam,
utawaachia pahali pake umma unaokuja, umma mpya. Nao huo umma mpya ni hawa vijana wa leo na mabarobaro wa sasa.
Kwa hakika ni kweli kabisa kwamba
mwanachuoni wa leo wa kidini hatakuwa ndiye mwanachuoni wa kesho, bali hapana
shaka yoyote kwamba pahali pake na cheo chake ataviacha kisha atakuja mtu
mwingine miongoni mwa hawa vijana mabarobaro iIi achukue pahali pake.
Mkuu wa mkoa au wilaya wa leo
hatakuwa ndiye mkuu wa mkoa au wilaya wa siku zijazo, bali hapana budi nafasi
yake itafikia kikomo, atakufa na pahali pake patachukuliwa na mtu mwingine.
Vivyo hivyo, rais wa nchi wa leo, hakimu, amiri, waziri,
kiongozi, n.k.
watakufa na pahali pao patachukuliwa na vilana wa leo.
Hii ndiyo tabia ya uhai na tabia ya
maumbile. Huu ndio mwenendo wake kwamba kizazi kimoja kinapoondoka badala yake
huja kizazi kingine.
Je, hao watu wengine watakaochukua nafasi ya jamii ya sasa
katika siku zijazo ni akina nani? Hakika wao ni hawa vijana wa leo, kwani wao ndio watakaounda jamil ya
kesho.
Siku moja Imam Hasan bin Ali AS aliwakusanya watoto wake na kuwaambia: "Nyiny leo ni watu wadogo, mnatarajiwa
kuwa watu wazima kwa wengine."
Vijana wetu wa leo ikiwa watalelewa vyema hadi wawe wema na
wanyofu, tunaweza kubashiri kuwa umma wetu na jamii zetu bali na vizazi vyetu
vijavyo vitakuwa na mustakbali mwema; lakini wasipokuwa wema au wasipofuata
njia nyofu basi itamaanisha kuwa huenda mustakbali wao ukawa mwovu, mweusi na
wenye giza.
Kipindi cha ushababu ni muhimu sana kwa sababu ndicho upeo
wa mustakbali wa umma na mustakbali wa wananchi, na kutokana na sababu hii ndio
mafundisho bayana ya dini yanatilia mkazo sana kukizangatia kipindi hiki
kutokana na umuhimu wake.
Kwa mfano kauli ya Mtume Muhammad SAW aliposema:
"Hakika nyayo za mja hazitaweza kunyanyuka katika siku ya Kiyama hadi
aulizwe ameumaliza umri wake katika nila gani na
ameutumia ujana wake katika nini."
Wakati kama huu ni wa hatari kwa
kijana kwa kuwa huishi katika hali maalum inayoathirika kimwili, kifikra na
kijamii.
Katika hali hii ya pekee anayoishi kijana katika kipindi cha
ujana, inatakikana ama ajiimarishe katika mazingira yaliyo mema na maongozi
yaliyo salama ili aweze kuvuka kipindi hiki akiwa ni kijana mwenye juhudi sana
ambaye ataweza kuunufaisha umma kutokana na kuwepo kwake na harakati zake; au
aondokee kuwa ni kijana aliyeharibika katika mazingira ya ufisadi na matokeo
yake iwe ni kuibomoa nafsi yake na kuibomoa jamii yake.
Vipambanuzi
vya Kipindi cha Ujana
Kipindi cha ubarobaro kinajipambanua kwa
wingi wa sifa na vipawa. Sifa hizi na vipawa hivi
hupatikana kwa wingi katika shakhsia ya barobaro katika pande zote za maisha
yake.
Upande
wa Kimwili:
Katika kipindi cha uvulana na
ubarobaro, mwili wa mwanadamu hutangaza kuwasili kwake kwenye kilele cha
kukomaa na kukamilika, kwani huchukua umbile
lake
halisi
na nguvu zake hukamilika na kimo chake humuongezea urembo wa kitabia. Qur'ani
Tukufu yaelezea kuwa wakati wa uvulana ndio wakati wa
nguvu.
Mwenyezi Mungu
amesema: "Mwenyezi Mungu (ndiye) ambaye amewaumba nyinyi kutoka unyonge
kisha akajaalia baada ya unyonge nguvu, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge na uzee, Mwenyezi Mungu huumba anachokitaka na Yeye ndiye
Mjuzi na Mwenye uwezo." (30:54)
Mwanadamu huja kwenye uhai akiwa yu mtoto mdogo dhaifu,
hawezi hata kumwondoa nzi aliyetua usoni mwake, kisha hukipita kipindi hicho
cha udhaifu (utoto) huenda katika kipindi cha uvulana, kipindi chenye nguvu na
nishati; kisha unyonge humjia tena na kumtawala mara nyingine kwa jinsi ambayo
huingia katika zama za uzee na ukongwe.
Vilevile katika wakati wa ujana,
hisia za mwanadamu hulipuka na hisia za jinsia hazimpi nafasi. Kijana huishi
katika hali ya zahama, dhiki na vurugu za kijinsia
(shahawa) na huendelea katika hali hii. Hisia hizi huwa zinahitaji kushibishwa
na kuondoshewa kiu yake.
Upande
wa Kijamii:
Baada ya kukipita kipindi cha utoto alipokuwa mdogo
akinyenyekea amri za wakubwa, akiwa hana rai wala hamiliki jambo lolote, sasa
huona kuwa ni barobaro. Nafsini mwake anajihisi kuwa
ana nguvu, na kifuani mwake amejawa na hisia ya
kujamini dhati yake. Wakati huo hutafuta jukumu Ia
kutekeleza katika jamii.
Sasa yeye si mtoto tena, bali
hujihisi kuwa ni mtu mzima (mme) aliyekamilika uume (utu), na ni wajibu wake
kufanya yale yanayofanywa na wakubwa.
Umekwisha ule wakati aliokuwa akitendewa kama
mtoto mdogo, wakati alipokuwa akitii amri za wakubwa na kunyenyekea matakwa
yao. Hivi
sasa yeye amekuwa mkubwa si mdogo tena. Anayo rai anataka aitekeleze na anatafuta jukumu katika jamii alitekeleze ili aijaze hi
faragha ya kinafsi aliyokuwa nayo muda mrefu.
Upande
wa Kinafsi:
Katika kipindi hiki cha ubarobaro, ndani mwa nafsi ya
ubarobaro huwemo matakwa ya kutaka kukataa kila jambo na roho ya kutaka kuasi,
kama kulipizia kisasi kwa aliyofanyiwa alipokuwa mdogo, wakati alipokuwa akitii matakwa
ya wazazi wake na vilevile kuzinyenyekea ada za jamii yake bila ya kuweza
kupinga au kuhalifu na kujitenga.
Kijana anapokuwa mkubwa na mwenye
nguvu hupendelea naye atekeleze haki yake katika kupinga au kukubali na kuwa na
rai huru. Huu ndio wakati ambao hukua nafsini mwake roho ya kutaka kupinga na kuasi.
Tena hapa kuna sifa nyingine anayosifiwa barobaro kuwa nayo
katika wakati huu wa uvulana na ujana, nayo ni ule
upendo wake wa kujitolea na kuwa tayari kwake kujitoa mhanga.
Tabia ya binadamu na umbile
lake
kila
anapoishi muda mrefu hapa duniani, tamaa na pupa
lake
Ia
kutaka kubakia zaidi hapa duniani huzidi kuambatana naye.
Ama tunapomzingatia barobaro kwa
kuwa ni chipukizi anayeanza kukua katika hii dunia, yeye hawi mwingi wa tamaa
na pupa Ia kutaka kubakia hapa duniani
kama
anavyokuwa mzee mwenye umri mkubwa.
Mwenye kuyachunguza kwa makini
matendo ya barobaro atagundua kuwa ana tabia ya kujiingiza kwenye hatari au
kushikilia lilelile analolitaka, kupambana bila ya kujali kufa hasa anapojawa
na hamasa. Ama mtu mkubwa wa umri, yeye hujihifadhi,
tena huwa mwenye utulivu na husara katika matendo yake na shughuli zake. Kule
kuwa kwake na majaribio humpa aina fulani ya kuwa na
mizani na kujihifadhi, tena pupa
lake
Ia kubakia duniani
halimkubalii kuwa na upendo wa kujiigiza katika mambo bila ya kuzingatia.
Hapa kuna mfano mwepesi kuhusu hakika
hii. Hebu mpeleleze barobaro anapoendesha gari, kisha mpeleleze
mtu wa makamo uendeshaji wake uko namna gani.
Imerekodiwa kwamba katika zama za
khallfa wa Kiabbasi Harun Rashid, aliambiwa kuwa yuko mtu aliyeishi na Mtume
Mtukufu na akasikia hadithi zake. Yeye ni sahaba
aliyekuwa na umri mrefu ambaye aliishi tokea zama za Mtume Mtukufu hadi zama za
Harun Rashid. Umri wake ulikaribia miaka mia moja na
thelathini (130)
Kwa vile sahaba huyu ana heshima kuu,
Harun Rashid alipendelea kukutana naye. Harun Rashid
akaamuru aletwe na akaletwa kwake huku amebebwa. Harun
Rashid akamwuliza:
"Je, wewe
umekutana na Mtume wa Mwenyezi Mungu?"
Mzee
akainamisha kichwa chake
kama
kuonyesha alama ya kujibu ndio.
“Je,
umewahi kuyasikia mazungumzo (hadithi) ya Mtume wa Mwenyezi
Mungu?"
"Ndio.”
"Je,
unakumbuka mazungumzo yoyote miongoni mwa mazungumzo ya Mtume wa
Mwenyezi Mungu?"
"Ndio”
"Hebu nizungumzie iIe hadithi unayoikumbuka uliyoipokea
kwa Mtume Mtukufu."
Mzee akasema kwa sauti dhaifu
sana: "Nimemsikia
Mtume wa Mwenyezi Mungu siku moja akisema: 'Mwanadamu huzeeka na hubakia ndani
mwake sifa mbili -tamaa na matumaini.”
Mzee akayakata mazungumzo huku akiwa hana uwezo wa kuendelea nayo.
Harun Rashid akaamuru apewe zawadi, nayo ilikuwa ni kiwango fulani cha
mali, na iliwekwa juu ya kitanda
chake. Kisha wakambeba ili kumrudisha nyumbani kwake.
Harun Rashid akahisi kwamba mdomo wa sahaba mzee ulikuwa
ukichezacheza kana kwamba alikuwa akisema kitu.
Akaamuru arejeshwe. Watumishi wakaja naye hadi
ubavuni karibu na Harun Rashid. Akamwuliza:
"Nimeiona mdomo wako ukichezacheza wakati ulipokuwa ukirudishwa kana
kwamba ulikuwa ukisema kitu."
Mzee akasema: "Ndio, nilikuwa nikiwauliza waliokuwa
wakinibeba: 'Je, huyu Harun Rashid ataifanya zawadi hii iwe ni
ya kila mwaka, awe akinipa mfano wake ili niweze kumzuru mwanzo wa kila
mwaka?'”
Harun Rashid akacheka, kisha akasema: "Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema kweli kabisa katika ile hadithi
uliyolsema hivi sasa kwamba: 'Mwanadamu huzeeka na hubakia ndani mwake sifa
mbili - tamaa na matumaini.’”
Hivi ndivyo ilivyo.
Tamaa ya mwanadamu na matumaini yake ya kutaka kuishi
duniani huzidi kukua nafsini mwake kila umri wake unapozidi. Hubakia ana busara
na hujihifadhi katika matendo yake na mambo yake yote,
ambapo barobaro huwa yuko tayari kujitoa sadaka na kujiingiza katika mambo ya
hatari bila ya kujali hatari zilizoko mbele yake.
Upande
wa Kifikra:
Aghlabu vijana na barobaro katika
kipindi hiki cha ujana huwa na faragha na udhaifu wa kiakili katika kufungamana
kwao na watu.
Katika kipindi hiki cha ubarobaro akili ya binadamu hufumka na vipawa vyake hufunguka. Huanza kuyafikiria mambo kwa undani. Akilini mwake huchoreka maswali mengi kuhusu
maisha yake na maisha ya jamii. Maswali
ambayo hayana budi kujibiwa wazi.
Vilevile hujiona kwamba halazimiki tena kuzikubali fikra za
watu wake na mazingira yao, madamu ameamini nafsini mwake kuiamini dhati yake,
na kupendelea kufuata mtindo wa kukataa na kupinga kila jambo na kupondokea
zaldi upande wa kubeba majukumu mazito mazito na ya hatari.
Kwa ajili hiyo, barobaro huwa yuko tayari kuipokea na kuifuata fikra yoyote mpya japo iwe ya hatari namna gani.
Ama mtu mkubwa yeye ana ukinaifu, imani na
fikra anazoziamini na kuzitukuza miaka mingi. Yeye hana faragha ya kiakili wala
hahisi kuwa na haja ya kuwa na itikadi nyingine mpya,
bali yeye hayuko tayari kuiacha fikra aliyoiamini muda mrefu na kuitukuza miaka
mingi.
Kwa ajili hiyo utaona kwamba kila ujumbe na
mafunzo kutoka mbinguni yalisimama na kupata nguvu kutokana na mabarobaro
(vijana) wale ambao kwamba wao huwa wepesi kuziamini hizo fikra mpya na huwa
tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya kuzitetea.
Tuchukue mfano mmoja: Nabi Ibrahim AS alipowapelekea watu
wake ujumbe wa kumpwekesha na kutomshirikisha
Mwenyezi Mungu, ni nani aliyemwamini na kuukubali wito wake? Watu wake
hawakuukubali ujumbe wake, isitoshe wakamtuhumu kwa
kuwa aliaminiwa na kikundi cha vijana maskini,
kama
Qur'ani Tukufu inavyosema: "Na hatukuoni wamekufuata isipokuwa wale
wanyonge katika sisi wenye fikra ya mwanzo." (11:27)
Naye Nabii wetu Muhammad SAW pia.
Wale waliofanya upesi
kumwamini na kuufuata ujumbe wake walikuwa ni kikundi cha mabarobaro,
wadogo kwa umri,
kama Ali bin Abu Talib AS,
Bilal Mhabeshi na Ammar bin Yaasir, n.k.
Jambo hili liliwafanya wazee na
viongozi wa Makureshi kumtuhumu Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba yeye amewaharibu
vijana wao na wakayasema hayo hayo katika mashitaka
yao waliyoyapeleka kwa ami yake, Abu Talib.
Wakasema: "Hakika mwana wa nduguyo amewatusi miungu wetu, na amezipuuza
ndoto zetu na amewaharibu mabarobaro wetu."
lli
kuitilia nguvu hakika hii, Mtume Mtukufu amesema: "Nawausia kuwafanyia
mabarobaro wema, kwani wao wana mioyo laini zaidi. Hakika Mwenyezi Mungu
amenituma mimi (niwe)
mbashiri na mhofishaji, mabarobaro wakaapa kushikamana nami na wazee
wakanihalifu... Na muda wao (wa kuishi duniani) ukawa mrefu
na nyoyo zao zikasusuwaa (zikawa ngumu)."
Amirul Mu'miniyn Ali bin Abu Talib amesema:
"Hakika moyo wa kijana ni
kama
ardhi isiyokuwa na kitu (isiyolimwa) chochote kinachoingizwa (kinacholimwa)
ndani yake hukikubali."
Vipi Tufaidike
katika Kipindi cha Ubarobaro
Hayo yote yaliyotangulia ndiyo mambo
muhimu na sifa muhimu zinazompambanua barobaro
zikiwemo sifa za machimbuko yaliyo hatari pia.
Kwa hivyo, imetubainikia kwamba ni kwa
miongozo mema na taratibu zilizo salama tu, ndipo itamkinika kufaidika na hivi
vipawa na kuvipatiliza katika kuujenga utu wa Kiislamu unaotakikana ili vijana
wetu wawe ni mfano halisi wenye kufanana na maisha ya vijana wa Kiislamu
waliopigana jihadi kama Ammar bin Yaasir, Mus'ab bin Umayr, Malik Ashtar na Al
bin Husayn al-Akbar.
Ikiwa tutawapuuza vijana wetu na
kutowajali katika wakati huu ulio hatari au tukawatendea vibaya katika sifa zao
na vipawa vyao vya kifikra, huenda tukaonjwa kwa kupata umma mpya uliopotoka na
kuharibika. Umma huu mpya utapotosha njia na lengo, na
vilevile utaubomoa mustakbali wake mwema.
Swali Ietu hivi sasa ni hili: Ni kwa njia gani
tutafaidika na wakati
huu wa ubarobaro (uvulana)? Vipi tutavikuza vipawa
vyake na kumpangia nyadhifa kwa ajili ya maslahi yake
na kuujenga utu wake, ili aweze kuubeba wajibu wa ujumbe huu wa Kiislamu? Haya ni miongoni mwa yale yatakayomfanya kijana awe ni msingi
mwema wenye utendaji katika maendeleo ya kijamii na kuuendeleza mbele ujumbe
huu wa Kiislamu.
Hapa napendelea kuelezea kwa kirefu
kila kipawa cha kipindi hiki cha uvulana, na kuyaelezea mambo yenye kumpangia
wadhifa na kumwongoza kwa ajili ya kujenga viongozi miongoni mwa vijana na umma
wa Kiislamu unaokuja. Hapo tutaona vipi tutaweza kufaidika na
kila kipawa chake, miongoni mwa hizi sifa tulizozitaja wakati atalelewa na
kukua katika maongozi sahihi.
Vikwazo vya
Matamanio ni
Fursa
Nzuri ya Kuimarisha Matakwa
Ikiwa vijana wa umma wanamiliki
irada (matakwa) na nguvu ya nafsi iliyo thabiti ambayo inashinda matamanio ya
nafsi, nia na Irada thabiti yenye kupambana na ghururi, hakika umma utakuwa
umetukuka na kupata heshima kuu. Tena umma
kama huu utakuwa una uwezo wa kukabiliana na
maadui na kupambana na wakoloni. Hautaweza kurukuu na kuyaitikia matakwa ya
wakoloni, na hautamnyenyekea dhalimu au
kuridhia kuwa watumwa wa wadhalimu na wakoloni.
Umma ni muundo wa mkusanyiko wa
watu. Ikiwa watu wanaounda umma ni watu waliopondokea kwenye uharibifu na
maovu, na ni wenye tabia ya ghururi na shahawa, basi msimamo wa umma na muamala
wao kwa maadui zao utakuwa ni baridi na wenye kukubaliana na maovu hayo na
dhuluma hiyo.
Ama ikiwa watu wanamiliki irada (nia thabiti), nguvu ya
nafsi na uwezo wa kupambana na vikwazo, hakika umma
ukishikana na vijana wake unaweza kukabiliana, kupinga na kusimama kwa ushujaa
dhidi ya tamaa za maadui na njama za madhalimu na wakoloni.
Wakati huu wa uvulana ni fursa nzuri
yenye thamani ya kuikuza irada (matakwa) ya mtu katika umma. Sababu ni kwamba irada ya binadamu haipati nguvu mara moja kwa
kuipa mawaidha au kuipa miongozo, bali hupata nguvu kwa kupitia ukinzani na kwa
kupambana na ghururi na vikwazo vya kila aina.
Kwa mfano, mtu ambaye ataikuta nafsi yake imezingirwa na
mambo yenye udanganyifu na hadaa zenye nguvu, tena ikawa nafsi imebanwa katika
vikwazo vyenye shahawa kali, yamkinika kwake kuilelea nafsi yake kwa matendo,
kwa kuwa mgumu wa kutoyatii matamanio yake, aikuze kwa kuiviza irada yake kwa
majaribio ya kimatendo. Mtu kama huyu anaweza kupata ushindi, hasa pale
atakapoitukuza nafsi yake na kuzidharau zile ghururi na shahawa na aikanye nafsi yake kuvinyenyekea
vikwazo vya matamanio.
Vivyo hivyo, kipindi hiki cha ujana kwa
vijana ni kipindi cha kuipa mazoezi irada na kuifanyia majaribio nafsi yake.
Kijana akipata miongozo iliyo salama na
kupata mafunzo (elimu) sahihi yaliyojaa ubinadamu katika malezi yaliyo mema,
ataweza kuyapita majaribio haya kwa ushindi mkubwa, na baada ya mtihani huu
atakuwa mwenye irada yenye nguvu na ushujaa.
Hakika mara nyingi mabarobaro husumbuliwa na hisia kali za
matamanio nafsini mwao, vilevile hupambana na ghururi (hadazi) za aina
mbalimbali zenye nguvu, lakini huweza kupata ushindi upesi hasa anapoweza
kuitawala nafsi yake, kuuhifadhi utu wake na heshima yake, akaweza kupambana na
hadazi zote na akaweza kujiepusha na vitimbi vikubwa vya matamanio yenye kiwi,
hasa katika hizi jamii zetu kunakopatikana kwa wingi upondokeaji kwenye uharibifu
na ufisadi. Barobaro akiweza kuyashinda hayo yote, yamaanisha kwamba ameimiliki
irada yake iliyo thabiti na amemiliki nafsi yenye
kutoteteleka. Wakati ambapo umma utamiliki watu pamoja na
vijana wa namna hi basi hapo utaweza kuwa na matumaini ya kuwa na mustakbali
mwema.
Riwaya na hadithi tukufu
zilizopokewa katika mafunzo matukufu ya Qur'ani zimeelezea kwamba barobaro
anayo sifa tukufu ya kuyapa nyongo mambo yenye ghururi na ya haramu kwa kutubu,
kwani toba inadhihirisha kujihifadhi kwake na kulingana kwake. Mtume Mtukufu
amesema: "Toba ni nzuri, na kwa barobaro ni nzuri zaidi."
Pia
imepokewa
kwake kuwa amesema: "Hakuna kitu kizuri kinachopendeza zaidi kwa
Mwenyezi Mungu kuliko kumwona barobaro mwenye kutubu."
Ni kwa nini kitendo hiki
kinamfurahisha Mwenyezi Mungu? Sababu ni kwamba
barobaro anapojiondoa kwenye maasi na kuyadhibiti matamanio yake huwa amefanya
ukinzani mkubwa dhidi ya nafsi yake, vilevile huwa anailelea nafsi yake juu ya
misingi ya kupania, kukakamia na kushikamana na imani yake.
Tunapoidurusu historia ya viongozi wakubwa wa historia ya binadamu, tunakuta kwamba aghlabu
yao walikuwa na jitihada ya hali ya juu
sana wakati wa ujana wao katika kuzijenga
nafsi zao na kuzielekeza kwenye maongozi matukufu yenye utu na ukamilifu. Na
sababu ni kwamba wao walishikamana na mkondo wa matukufu na kulazimiana nayo,
na wakakataa kupomoka kwenye lindi Ia matamanio na upotevu wenye kutenganisha
na haki, pamoja na kwamba kulikuweko hali zenye kusaidia kuwavuta kwenye
matamanio na kuzama zaidi kwenye mambo ya ufisadi.
Hebu tujionee baadhi ya kumbukumbu za maisha ya baadhi ya
viongozi wakuu ambao wamefaidika kwa kuziviza irada
zao katika wakati wa ujana wao, wakazipa nguvu nafsi zao kwa kukakamia
kujiepusha na shahawa za nafsi. Kutokana na kufuata
njia hii, walizipa nafsi zao nafasi ya kwanza ya kuyavaa matukufu na kuvikwea
vilele vya matukufu na ukamilifu.
1.
Hebu tuitazame historia ya Nabii wa Mwenyezi Mungu, Yusuf bin
Yaakub
AS akiwa ameyakosa malezi ya wazazi wake
pamoja na huruma
yao
tokea udogoni mwake baada ya kumpoteza mama yake, ndugu zake walimlia njama na
kumtupa kisimani, kisha akanunuliwa na mmoja wa misafara ya Misri kwa thamani
ya chini ya dirhamu chache.
Tazama ndugu msomaji, majaaliwa yalitaka aishi katika zama
zake za ubarobaro ndani mwa nyumba ya Mfalme wa Misri pamoja na mkewe Zulaikha
ambaye alivutwa vilivyo na uzuri wa Nabii Yusuf
AS uliojulikana na uliokuwa ukipigiwa mfano. Ashiki ya kumpenda Yusuf
ikavama moyoni mwa Zulaikha, na nyumba walimokuwa wakiishi haikuwa
na yeyote mwenye kutia zahama, na
hali haikuwa na pingamizi yoyote ya kuzuia kutekeleza hila za kishetani.
Hebu sawirisha ewe kijana uliye barobaro, kuwa wewe umeingia
kwenye mtego wa Nabli
Yusuf
AS. Pia chukulia kuwa uko katika mazingira yanayosaidia kupotoka, Je,
ungefanya nini? Na wajibu wako ungekuwa ni nini
katika hali
kama hii?
Naam, ukweli ni kwamba wengi wa
barobaro wetu wa sasa, mara nyingi wanatatizwa na ghururi zilezile ambazo
zilimtatiza huyu barobaro mtukufu Yusuf, vilevile wanaishi katika mazingara
sampuli ileile aliyoishi.
Kwa hivyo, ni juu ya vijana wetu
kumfanya Nabii Yusuf AS kuwa ni kiongozi wao na kugizo chao, wamwige katika
kupambana kwake na ghururi kama zile katika kukabiliana kwake na hali
kama zile. Hebu tutazame msimamo wake ulikuwa namna gani?
Qur'ani Tukufu yatusimulia kwa
ufasaha mkubwa ikitumia njia yake ya kimbinguni. Yatutolea baadhi ya visa
vinavyoelezea baadhi ya ile mikasa hatari aliyoipata Nabii Yusuf AS katika
nyumba ya Mfalme wa Misri, pamoja na tukio Ia kurukiwa
na Zulaikha. Mwenyezi Mungu asema:
"Na
akasema yule aliyemnunua huko Misri kumwambia mkewe: 'Mweke pahali pazuri
huenda akatufaa au tukamfanya mwana. 'Na hivi ndivyo
tulivyommakinisha Yusuf katika ardhi (nchi,) ili
tumfundishe taawili (ufafanuzi) za hadithi na Mwenyezi Mungu ni Mshindi juu ya
jambo
Lake
lakini watu wengi hawajui. Na alipofikia ukamilifu wake tukampa hukumu na elimu na vivi hivi huwalipa wonaofanya wema. Na akamtaka
[Yusuf kutenda haramu]
yule [Zulaikha] ambaye yeye yuko nyumbani kwake nafsi yake, na akafunga milango
[ili asikimbie] na akasema: 'Ni toyari njoo [nimejitayarisho kwa ajili yako].'
Akasema [Yusuf]: 'Namwogopa Mwenyezi Mungu, Yeye ni Mlezi wangu, ameyafanya
mazuri makao yangu. Hakika madhalimu hawafuzu.' " (12:21-23)
Qur'ani inaendelea kuyafafanua baadhi ya maelezo ya kisa
chenyewe kutokana na umuhimu wake hadi pale
ilipomdondoa Zulaikha akisema:
Hakika
nilimtaka nafsi yake akajizuia (akakataa) na ikiwa hatafanya ninayomwamuru,
atafungwa na atakuwa katika wanyonge.'
Akasema [Yusuf]: 'Mola wangu, jela ni boro zaidi
kwangu kuliko yale wonayoniita kuyafanya, na ikiwa hutaniepusha na vitimbi
vyao, nitapondokea kwao na nitakuwa miongoni mwa wajinga.' Basi Mola wake
akamjibu, akamwepushia vitimbi vyao; hakika Yeye ni
Mwenye kusikia na ni Mjuzi." (12:32-34)
Vivi hivi Yusuf
alimwomba Mwenyezi Mungu amsaidie katika kupambana na
ghururi za matamanio na hali za upotofu. Naye Mwenyezi Mungu akayajibu maombi
yake, na Nabii Yusuf akazishinda zile hali zote za
uharibifu na ufisadi ingawa alistahamilia maovu na kwa muda mrefu alibaki jela
kwa azma, nia thabiti na nafsi yenye ushujaa. Na hivi ndivyo
inavyotakikana kijana mwema awe.
2.
Kuna kisa kingine chenye kuvutia
na kustaajabisha
kama kinachoelezwa
katika historia. Kisa chenyewe kinamhusu Sayyid Mir Damad, aliyekuwa
mwanachuoni mashuhuri
sana
nchini
Iran.
Yaelezewa kwamba Sayyid huyu alifikiwa na
kisa hiki wakati akiwa kijana mbichi mwanzo wa kubalehe kwake, naye alikuwa ni
mwanafunzi katika madrasa moja ya kidini katika jiji Ia Tehran. Katika usiku
mmoja wakati binti wa Shah wa Iran katika zama hizo alipokuwa akitembea mitaani
pamoja na vijakazi na watumishi wake, kwa ghafla kukanyesha mvua kubwa na
kukavuma upepo mkali na kila mmoja miongoni mwa watumishi wa binti wa Shah
akakimbia kutafuta mahali pa kujificha kibinafsi. Binti wa
Shah akabakia peke yake mitaani katika lile janga Ienye kutisha na kuhofisha,
ikawa naye hana budi kutafuta pahali pa kujificha. Katika kutazamatazama kwake
huku na huko iIi angaa naye apate pahali pa kujificha na
kujistiri, akauona mlango wa madrasa uko wazi, akaingia madrasani. Kwa bahati
akagonga mlango wa chumba cha huyu Sayyid kijana na
akamkuta yuko kando ya moto akijiota ili ajiondoshee baridi aliyokuwa nayo.
Binti huyu akamwelezea huyu Sayyid kijana kisa chake, kwamba
yeye ni msichana aliyepotea njia na anachohitaji ni
msaada, pahali pa kulala na kujistiri usiku ule, hadi hali ya anga iwe tulivu
na ipambazuke.
Sayyid aliona hana budi kulijibu ombi lile Ia msichana, hivyo akamkaribisha
chumbani mwake, yeye akakaa katika kipembe kimoja na msichana naye
akakaa katika kipembe kingine.
Baada ya kupita muda katika usiku huo, shetani akaanza
kucheza mchezo wake mwovu katika hali kama hii,
kama ilivyopokewa katika hadithi ikisema: "Mwanamume
hakai faragha na mwanamke ila shetani anakuwa wa tatu wao."
Shetani akawa anamshawishi Sayyid huyo kijana namna ya
kuipatiliza hii fursa na kutenda haramu kwamba mambo
yote yako sawa kwa kila njia, mlango umefungwa, wala msichana hana njia yoyote
na kujikinga au kujitetea.
Lakini vipi itakuwa?
Kwani Sayyid huyo alikuwa ni kijana mwema na mwongofu,
anayetambua hila na vitimbi vya Shetani. Akawa anafikiria njia ya kujiepusha
kutokana na makucha haya ya shahawa na mtego huu wa
Shetani. Mwishowe akafikia kwenye uamuzi mgumu.
Akaamua kuitumia njia hii kwa ajili ya kupambana na
shahawa zake na kuutatua wasiwasi wa shetani. Uamuzi wenyewe ukawa ni kuweka kidole chake juu ya kaa Ia moto, hadi
ashughulishwe na uchungu wa kuchomeka ili asifikirie mambo ya haramu. Naam,
aliendelea kujichoma hivihivi usiku kucha, huku akistahmilia uchungu na maumivu na huku akiihutubia nafsi yake: "Onja moto
wa dunia ili uuogope moto wa Akhera!"
3.
Je, ndugu! Vijana wamewahi
kukisikia kisa cha lbn Siriin ambaye alikuwa mwanachuoni mkubwa wa elimu ya nafsi na aliyejulikana kwa kufasiri ndoto?
Katika wakati wa ubarobaro wake Ibn Siriin alikuwa mwenye umbo jema,
kiwiliwili kizuri, mwenye uso mwangavu na uzuri wa kitabia wenye kuvutia.
Alikuwa akifanya kazi kwa mfanya biashara mmoja wa
nguo. Siku moja alifika mwanamke dukani kununua vitambaa, alipomaliza kununua
mahitaji yake, akamtaka yule mfanya biashara amtume mfanyakazi wake Ibn Siriin ili ambebee mizigo yake aliyonunua hadi nyumbani kwake,
kisha ampe ujira. Ibn Siriin akabeba mizigo na
kuandamana naye hadi nyumbani, walipoingia nyumbani mwanamke huyo akafunga
milango, kisha akamtaka afanye naye kitendo cha haramu, lakini yeye akakataa. Mwanamke alipoona amekataliwa akazidi kutumia hila za kumlazimisha
zaidi. Mwisho Ibn Siriin alijiona kuwa ametumbukia mtegoni, na hapana budi kufikiria njia ya kujisalimisha kutokana na
mtego huo Alipoigundua hila yenyewe alimwomba huyo mwanamke amruhusu aende
chooni kujisaidia. Mwanamke akamruhusu kufanya hivyo, naye alipoingia chooni tu
alijipaka mavi mwili mzima, kisha akamtokea mwanamke yule akiwa katika hali
kama hii ya kunuka. Mwanamke
alipomwona katika hali
kama
ile, akamkimbia na kumfukuza nyumbani. Na kutokana na
hila
kama hii lbn Siriin alijiokoa kutoka
mtego huu wa matamanio yaliyo na ghururi.
Wajibu wa Vijana katika Jamii
Vipawa vingi vya binadamu huchimbuka
katika wakati huu wa ujana. Huwa na
ukunjufu wa wakati na nafsi. Vilevile huwa anamiliki nguvu, uwezo na nishati. Hivi vyote vinampa nafasi nzuri na kumshajiisha kuwa na wadhifa maalum katika jamii.
Hapo mbeleni tuliwahi kuelezea juu ya
matakwa ya kijana yenye kiwi ya kutaka kutekelezwa, na
kupenda kwake kushiriki katika nyadhifa mbalimbali ili ahisi kwamba yuko huru
na awathibitishie wengine uwezo wake na uume wake baada ya kuwa alikuwa mdogo
akiishi katika hali ya kuwanyenyekea wengine na kupondokea kwenye matakwa
yao. Baada ya kuwa
alikuwa akitendewa kama mtoto mdogo, sasa ataka
atendewe na jamii
kama mtu mkubwa, mwenye
heshima yake kamili na mwenye matakwa na irada.
Lau twampa nafasi kijana na kumuacha
kutekeleza nyadhifa na wajibu anazoziweza katika jamii, na tukamwelekeza
kufanya mambo mema Yenye faida na kumsaidia kuujenga utu wake na kuvikuza
vipawa vyake, hakika tutakuwa tumefanya wema kwa kuyajua na kuya pambanua yale
yanayoweza kumdanganya katika wakati wa ubarobaro. Na ikiwa hatutashughulika na masiala haya na ikawa hatutampa nafasi barobaro kutoa
maoni yake na kutekeleza matakwa yake katika nyadhifa za kijamii kupitia
maongozi mema, basi natija itakuwa moja kati ya mambo mawili:
Ima vipawa vya barobaro vitafifia, na
vitazimika au vitakufa na matumaini yake yatazikika, au atajiingiza katika
kutekeleza mambo yaliyopotoka na kufanya mambo maovu ya ufisadi. Na huu ndio
mushkili unaoutatiza umma wetu wa Kiislamu.
Jamli nyingi hazijajua vipi zishirikiane na
vijana wao katika upande huu. Wazee wengi pamoja na
viongozi wale wanaoyatawalia mambo ya wananchi na kushikilia hatamu za uongozi,
aghlabu
yao
hawako tayari kuwapa vijana wao fursa ya kutumia ujuzi wao na vipawa vyao,
hawawapi nafasi yoyote ya kusimamia jambo lolote la kijamii, na hawawaamini,
bali huwazingatia kuwa ni watoto wasiojua kitu na walio dhaifu.
Kutokana na sababu hii vijana wetu
hukua huku wakiwa na juhudi chache
sana na
maarifa
yao
huwa ni ya daraja Ia chini. Hivyo, hupotoka na kuiacha
njia ya utukufu yenye utengevu, hasa wanapochukuliwa na makundi mengine ya
upotevu na kupewa nyanja za kuziamini nafsi zao na kupewa nyadhifa za
kujishughulisha na mambo muhimu yaliyo hatari.
Kitabia, utamwona kijana akivutika kwa
urahisi na kujiingiza katika lile kundi ambalo linashughulikia vyema na
kumthamini
kama mtu mwenye nguvu. Na utamwona
mara moja anawaacha wale watu ambao wanaoshughulikiana naye
kama mtoto mdogo au kijana dhaifu.
Tunasikitishwa
sana kuona ya kwamba jamii yetu
hadi sasa haijaacha kuwapima watu na kuwapa kima (hadhi na heshima) kupitia
kipimo cha umri. Imekuwa kwamba kabla kijana hajakata masafa marefu ya umri,
basi jamii ya watu wakubwa hawamwangalii kwa jicho Ia
uaminifu na heshima, wala hawampi nafasi ya kutaharaki au kuwa na nishati
yoyote.
Mtukufu Mtume ameitangaza wazi rai ya dini ya Kiislamu na
akaelezea waziwazi juu ya kukataa kwake kipimo cha umri na miaka, na akafafanua
kwamba kipimo cha pekee kilicho sahihi ni kipimo cha ujuzi na matendo, na
kwamba kijana mwenye ujuzi na matendo anayestahili na ni bora zaidi na anayo
haki ya kutangulizwa kuliko mwingine yeyote.
Mtume Mtukufu alimtawalisha Ittaab bin Usaid mjini Makka,
juu ya kuwa umri wake wakati huo ulikuwa ni miaka
Ishirini na moja. Akamwamuru kusalisha sala ya jamaa na
kusimamia shughuli nyinginezo kwa niaba ya Mtume Mtukufu. Kijana huyo alikuwa
ni amiri wa kwanza kusalisha jamaa mjini Makka baada ya kukombolewa mji
huo. Mtume Mtukufu alimwambia: "Ewe
Ittaab! Unajua nimekutanguliza kwa watu gani? Nimekutanguliza na
kukufanya mwakilishi wangu kwa watu (waja) wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na lau
ningekuwa namjua aliye mbora zaidi kukushinda wewe ningemteua."
Baadhi ya wakaazi wa Makka
walipopinga uteuzi huo, Mtume Mtukufu alisema: "Mtu asihoji kwa hoja ya udogo
wa umri wake, kwani ukubwa si ubora, bali ubora ndio ukubwa."
(Jawaan, Sheikh
Muhammad Taqi Falsafi; uk. 30).
Vilevile taaluma za Kiislamu zinashajiisha kuvikunjulia
vipawa hivi vya vijana chipukizl ili vivie na
kuendelea. Kwa mfano, utaona katika vitabu vya fiqihi kuna masiala ambayo
yanaruhusu vijana wasiobalighi bado kuwaongoza vijana wenzao katika sala ya
jamaa; na hii ni kwa sababu ya kumpa kijana moyo na kumshajiisha ili akulie na
hisia ya kuiamini nafsi yake, kwani vijana wanapoona kuwa wana sala yao ya
jamaa, watatambua kwamba wamethaminiwa na kwamba wao pia wanaweza kuwa
viongozi kama walivyo watu wazima.
Wakati tunaposoma sera za viongozi wa
Kiislamu na historia ya maisha
yao,
tunaona wazi kwamba wao wanaamiliana na vijana muamala wa kuwashajiisha na
kuwaheshimu. Vilevile huwapa heshima kubwa wale vijana walio na
ujuzi, na mara nyingine huwatwisha majukumu mazito zaidi na ya hatari.
Angalia jinsi Mtume wetu Muhammad SAW alivyomchagua Musa'b
bin Umair, yule kijana mwenye imani na mpiganaji jihadi kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu, awe balozi wake mjini Madina, ili auongoze umma wa huko katika njia ya
Uislamu, autayarishe mji wa Yathrib kuwa makao ya machimbuko ya Uislamu na
makao makuu ya serikali yake changa.
Mus'ab alifika mjini Madina akiikuta katika hali nzito
kutokana na tofauti iliyokuwepo baina ya makabila ya
Aws na Khazraj. Akiwa amebeba ule wajibu mkubwa kuiongoza Madina, Mwenyezi
Mungu amemwafikia kufaulu katika kutekeleza wajibu huo kutokana na imani yake ya kweli, ikhlasi aliyovama moyoni na jihadi
yake thabiti.
Katika tukio jingine
lenye kuthibitisha hakika kama
hii katika uhai wake wa mwisho, Mtume Mtukufu aliandaa jeshi kubwa Ia kupigana
na Warumi mkiwemo ndani mwake masahaba wakubwa na wazee wa Kiislamu. Uongozi wa jeshi
hilo
katika vita hivyo alipewa Usama bin Zaid ambaye alikuwa ni kijana asiyefikia
hata umri wa miaka ishirini. Na wengine waliokuwemo katika jeshi
hilo
lenye kunyenyekea uongozi na amri za Usama walikuwa ni Abubakr, Umar na Abu
Ubaida ibn Jarraah, Abdul Rahman bin Auf, Talha, Zubair, n.k.
Baadhi ya masahaba waliudhika kutokana na uamuzi huo wa
Mtume Mtukufu wa kumtanguliza Usama bin Zaid juu yao kutokana na umri wake
mdogo, habari hiyo ikamfikia Mtume Mtukufu, naye akaghadhibishwa sana na
kitendo hicho cha kumthamini mtu kulingana na kipimo cha umri ambacho kilikuwa
kikitumiwa wakati wa Ujahilia. Kitendo hicho kilimfanya Mtume Mtukufu kutoka na kwenda msikitini kuwahutubia watu, juu ya kuwa na shida
ya maradhi aliyokuwa nayo na kuumwa kwake.
Miongoni mwa yale aliyoyasema
katika hotuba yake siku hiyo ni: "Enyi watu! Ni nini haya maneno
yaliyonifikia yaliyosemwa na baadhi yenu kwa sababu ya
kumtanguliza kwangu Usama? Ikiwa mwapinga kumtanguliza kwangu Usama, hakika
mlitangulia kuupinga (uamuzi wangu wa) kumtanguliza
baba yake hapo mbeleni. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba baba
yake alikuwa anastahiki uongozi, na hakika mwanawe baada yake naye anastahiki
uongozi pia." (an-Nass wal ljtihad,
uk. 9).
Naye Imam Jaafar Sadiq AS alimkuta kijana Hisham bin Hakam kuwa
na vipawa vikubwa na akawa akimdhihirishia mapenzi na
heshima yake juu yake kwa kiasi kikubwa mpaka wazee wakaingiwa na wivu mioyoni
mwao.
Katika kitabu cha Safinatul Bihar imeelezwa kwamba heshima
na cheo cha Hisham bin Hakam vimefikilia daraja Ia juu kabisa mbele ya Abu
Abdillah Jaafar bin Muhammad Sadiq AS na kwamba Hisham alifika kwa Imam katika
Mina, wakati alipokuwa anaanza kubalehe. Katika kikao hicho cha Imam walikuwepo baadhi ya masahaba zake wazee
kama
Hamraan bin Aayun, Qais al-Maasir, Yunus bin Ya'kub, Abi Jaafar al-Ahwal na
wengineo, na Imam akampa Hisham heshima kubwa kushinda wazee wote waliokuwepo
hapo.
Abu Abdillah alipoona kwamba kitendo hicho kilikuwa kikubwa
mbele ya masahaba wake, alisema: "Kijana
huyu ametunusuru kwa ulimi wake, moyo wake na mikono
yake." (jz. 2, uk. 719)
Kauli ya mwisho juu ya maelezo haya
yatakikana ifahamike kwamba haiwezikani kabisa kumwacha au kumtenga barobaro
huku tukivipuuza vipawa vyake. Haimkiniki kumtupa na kumwacha abakie akiwa hana thamani yoyote au atenganishwe
na maisha ya umma. Hakika yatakikana athaminiwe na
aheshimiwe na apewe wajibu muhimu azitekeleze na vilevile aongozwe iIi aujenge
utu wake. Bila shaka, ikiwa sisi tutamshajiisha na
kumpa miongozo yenye kufaa, tutafaidika naye; na hayo yatakuwa ni matayarisho
muhimu ambayo yatamjenga na kumfanya awe chimbuko jema lililo muhimu katika
siku zijazo. Na ikiwa tutampuuza na kudharau rai zake na uwezo Wake na
hatutompa nafasi ya kushughulika na jambo lolote au kumshajiisha na kumtia
nishati na kumwongoza katika njia sahihi, tujuwe wazi kwamba atatekwa na
wengine na kufaidiwa na wengine, na watamtayarisha kulingana na taratibu zao na
miongozi yao miovu yenye kupoteza na kupotosha.
Majaribio mengi yamethibitisha kwamba kijana anapopewa
nyadhifa au shughuli za kijamii kuziendesha au kusimamia wajibu wa kidini, huwa
yuko tayari kutoa juhudi zake zote kuushughulikia umma wake, tena hushikamana
zaidi na kulazimiana zaidi na dini.
Ama kule
kuwahimiza vijana kusali na kufunga na kuwahimiza kusikiliza hotuba
na mihadhara pekee hakutoshelezi hata kidogo kudhamini utengevu wa vijana hao
wala uongofu wao, wala hakutoshelezi kuyalelea maadili
yao na vipawa vyao. Ni wajibu ulioko juu yetu
kuwapa nidhamu na mipango yenye kuwataharakisha na
kuwapa nishati. Nidhamu hizo ziwe nzuri ili ziweze
kuwatambulisha umuhimu wao katika jamii.
Miongoni mwa mambo yanayotia uchungu moyoni ni upinzani unaotoka kwa jamii kuwapinga vijana waumini, au
kikundi chema kilichojitolea kusimamia na kutekeleza nishati muhimu za kijamii
au za kidini.
Umma huwawekea tuhuma na shaka na
huwapinga. Mara ngapi tunayashuhudia makundi ya vijana wema wenye nia
safi kwa umma wao, vijana walio
na hamasa kwa ddini
yao,
wanaotaka kusimamia jambo la kidini au la kijamii, au kuunda kamati za maendeleo
ya kidini na kijamii, lakini kwa masikitiko utaona jamii hufanya ubahili katika
kuwashajiisha na kuwatia moyo. Utaona hawawashajiishi hata
kidogo, bali huzuia misaada
yao katika pande zote na
mara nyingine huwapinga na huwawekea vikwazo. Kwa nini?
Je, ni kwa kuwa baba zetu na viongozi wa jamii hawajui
tabia ya kipindi hiki cha ujana, wala hawajatambua hatari yake? Au ni kwa kuwa hao wazazi na viongozi hawataki kuwaruhusu
vijana washirikiane nao katika kuyaongoza mambo ya kijamii kwa lengo la kuiendeleza
hadhi yake? Basi ni kwa sababu gani? Hakika kufanya
hivyo ni hiana na makosa makubwa.
Mapambano
Dhidi ya Ujinga na Upotevu
Ili kupambana na hali
hii mbaya yenye kusikitisha unaoishi umma wetu wa Kiislamu, panahitajika
sana kuwepo moyo wa kimapinduzi na moyo wa kutaka kuleta mabadiliko na kuwa na
msimamo wa kukataa na kupinga utaghuti (udhalimu).
Serikali za kidikteta na za
kidhalimu zinaendelea kuzitwisha tawala zao kwa mataifa yetu manyonge na
zinayatawala kwa siasa
yao
ya kikoloni na kwa kutumia njama za mataifa makubwa. Vilevile fikra za zamani
zilizoyaweka nyuma mataifa bado zingalimo ndani mwa akili za viongozi wetu na wakuu wetu wa kidini na kijamii, na wakiwa katika wao
wako katika hali
kama hi wanauongoza umma
wetu.
Nazo ada mbaya pamoja na mienendo
iliyo chakaa ingali inazidi kuleta matatizo na vikwazo katika umma wetu.
Kubakia nyuma katika maendeleo kunazidi, na udikteta
unaotawala umetia fora. Haya ndiyo maisha tunayoishi kila siku na ndiyo hali iliyoenea katika umma wetu. Sasa imebakia
tujiulize: Ni nini msimamo wa umma wetu juu ya kuishi
katika hali kama hii na maisha
kama haya? Hali
ambayo inachoma mioyo yetu na kutuudhi?
Hakika ile roho ya kimapinduzi ya kutaka mabadiliko na kukataa kudhalilishwa iliyokuwemo ndani mwa nafsi za
umma wetu imeyeyuka kabisa. Msimamo wa kupinga
ufisadi pia umetoweka. Nafsi zilizothubutu kupinga zimekosekana.
Mioyo yenye ghera na kaa lenye kuwasha utambi wa
upinzani limezimika.
Kila mmoja wetu amekuwa akipuuza kila jambo isipokuwa yale mambo yanayohusiana na maisha yake tu. Hafikiri kitu
isipokuwa mambo yanayohusiana na maslahi yake ya
kibinafsi. Ama kufikiria hali ya umma au hali ya muundo wake wa kisiasa na
kiuchumi, hayo yote ni mambo ambayo fikra yake haimpi nafasi kuya fikiria, wala hamu
yake haiyapi umuhimu wowote.
Hadi hivi sasa tungali tumebakia twaishi katika hali hi ya
kupooza na kukosa thamani. Yawezekana watu wabadilike na mambo pia kubadilika na yakawa mengine, lakini hali yetu
itabakia kuwa ni ileile ya ujinga, upotevu, kubakia nyuma katika elimu na
uchumi na kutengwa kwenye uongozi wa nchi yetu. Tutabakia katika hali ileile
ya kupomoka na kuwa katika dhiki na mateso. Tutabakia
katika maisha haya na hali hii hadi pale roho ya
kutaka mapinduzi na mabadiliko itakapozaliwa upya ndani mwa nafsi zetu na
mioyo yetu, na pale hisia za upinzani zitakapojumuika kwa wingi na tushughulike
na misimamo ya kupinga na kukataa hii hali yetu ya kubakia nyuma katika
maendeleo yanayoenea.
Mwenyezi Mungu Mtukufu asema: "Hakika Mwenyezi Mungu hoyabadili yale
yalioko kwo kaumu (watu) hadi (wao) wabadili yale yaliyomo nafsini mwao."
(13:11)
Ikiwa tunaitamani roho hii ya kimapinduzi na
tunataka kumiliki mioyo yenye kukataa na kupinga, basi katika kipindi cha
ubarobaro ziko mbegu zilizo hai kabisa, na iko hali ya kimaumbile kabisa
inayokubaliana kutekeleza matakwa haya. Na huu ndio wakati unaotakikana kwenda
mbio kuitafuta roho
kama
hii.
Na hii ni
kutokana na sababu zifuatazo:
Kwanza:
Kijana huhisi kuwa na nguvu nafsini na viungoni mwake
baada ya kuwa alikuwa akiishi katika hali ya udhaifu alipokuwa mdogo. Kutokana
na sababu hii hujiona ana jukumu Ia kupinga na
kukataa.
Pili: Tukimzingatia kwa makini
tutamkuta kwamba kijana huanza maisha yake yungali hajavaana nayo bado wala
hana pupa nayo
kama wanavyoyapupia watu
wakubwa, bali inakuwa kinyume chake, yeye hupendelea kujitosa kwenye
ukinzani na kukabiliana na hatari. Haya ndiyo yanayostahiki kuigwa na nafsi inayotaka kumiliki roho ya kutaka mapinduzi na
kukataa.
Tatu: Kijana hana fungamano na maisha haya ya dunia wala hajaonja ladha zake zenye kumfanya
aipondokee. Na hii ni kutokana na muda mfupi aliyoishi
hapa duniani na kwa sababu ya kutokuwepo maslahi mengi yenye kumvuta zaidi
kuyapenda maisha haya.
Ni tabia ya
binadamu kwamba anapoishi katika hali maalum kwa muda
mrefu na maslahi yake yakawa mengi katika hali kama hiyo, huwa inakuwa vigumu
kwake kufikiria kuibadili hali kama hiyo au maisha
kama
hayo, bali mara nyingine hupatwa na babaiko pakiwepo matara jio ya kupatikana
mabadiliko.
(Kwa mfano, Jean Jacques Rousseau alikuwa akiona hali
kama hiyo kwa ufalme wa
Kifaransa. Yasemekana alikuwa akisema kwamba alikuwa akipatwa na babaiko kutokana na kuisawiri Ufaransa ikijiendeleza bila
ya kuwa na mfalme, juu ya kuwa alikuwa ni miongoni mwa wanafikra na wanafalsafa
wakubwa waliowaita watu katika kuendeleza hali ya kisiasa wakati ule. Hii ni kwa sababu Rousseau alikulia katika chombo cha utawala wa
kifalme na kuvuta hewa yake kwa muda wote wa maisha yake).
Vivi hivi utaona
kwamba kundi Ia vijana ndilo kundi ambalo linaelekea
zaidi kuwa na roho ya kutaka mapinduzi na kuleta mabadiliko, na wao ndio watu
ambao wako tayari kabisa kuleta upinzani na kukataa ufisadi na dhuluma.
Ushahidi mkubwa ni hizi hoja
zifuatazo: Tume zote zilizotoka mbinguni, mapinduzi yote ya kijamii
yaliyofanyika yamefaidika na vijana. Vijana walitegemewa kama
viongozi wa kuleta mabadiliko na kuwa
kama
nguzo ya kuyaendeleza mapinduzi.
Ama katika jamii zetu za Kiislamu kuna kosa kubwa
linalotendeka katika kuamiliana na vijana wetu
wanaokulia. Badala ya wao kuzikuza na kuziogoza roho zao ya kutaka mapinduzi na
mabadiliko waliyonayo,
vilevile badala ya
kuiongoza roho ya kupondokea kwao katika upinzani, kuupinga ujinga ulioenea na
upotevu uliotawala, sisi hufanya kila juhudi kuiua roho hii ya kimapinduzi
iliyomo ndani mwa nafsi za vijana wetu. Pia huziua hamasa zao zilizowaka moyoni
mwao ambazo ziko tayari kupambana na hali
kama hizi. Mara nyingine utaona tunashughulika zaidi
katika kutafuta njia za kuwakinaisha na kuwafanya
wasalimu amri na kutii hii miweko ya ufisadi na kukubali kufuata hii miongozo
michafu kwa njia za kuwavunja mioyo na kuzirudisha nyuma azima walizonazo na
kuwakatisha tamaa nafsini mwao. Wakati huu tunapotumia hila za kuwakinaisha
mabarobaro, huwa tunatumia kila mbinu na kila njia
hata ikiwa ni kwa kuyapotoa baadhi ya mafunzo ya Kiislamu ili tu tuwakinaishe
vijana wetu wasiweze kupinga au kukataa lolote analoambiwa.
Miongoni mwa tashwishi za kuvunja moyo ni ile itikadi ya taqiya (ufichaji wa imani), eti taqiya ni
wajibu wa kisheria inayomruhusu mtu amnyamazie au amnyenyekee dhalimu yeyote
anayetawala umma kwa dhuluma na maonevu!!
Eti kupambana ni
kuiingiza nafsi kwenye maangamivu, na kufanya huko ni haramu katika sheria yetu
ya Kiislamu!!
Eti kufanya
mapinduzi au kuleta aina yoyote ya mabadiliko kunahitaji fatwa ya mujtahidi (mufti) ambaye
haoni kuwepo maslahi kwa dini kwa hivi sasa kutoa fatwa!!
Eti fursa ya kufanya mapinduzi imepita kitambo, na ni wajibu kwa waumini kwa hivi sasa kungojea kudhihiri
kwa Imam Mahdi!!
Hebu tafakari kidogo.
Je, haya mafundisho na fikra hizi zisizo nyofu na
zenye kupinga mapinduzi zinakubaliwa na vijana wetu wote? Vijana wanaotaka
kuleta mabadiliko, waliojaa hamasa, walio na matumaini
ya kuasi udhalimu na walio na lengo Ia kuhakikisha kupatikana mapinduzi
watakubali fikra hizo?
La hasha!! Umma wetu na watu wetu
wana akili imara zilizo madhubuti ambazo hufikiria na kuyapima mambo
yanayotolewa na fikra hizi na mafunzo haya. Ndiyo, yawezekana wapatikane baadhi
ya vijana ambao watahadaika na kukubaliana na hali hii
ya ufisadi. Kisha wajiondoe kwenye mkondo wa kutaka
mapinduzi ambapo utawakuta wengine wanaitafuta njia ya mapinduzi popote ilipo
ili waiandame hadi wahakikishe kwamba lengo lao Ia kuleta mabadiliko
limepatikana.
Hii ndiyo fursa wanayoipatiliza makundi ya upinzani na ndiyo nafasi inayopatilizwa na watu wenye hila za
kikoloni ili wawawinde vijana wetu kwa jina Ia kuleta mabadiliko na maendeleo
chini ya wito wa kupinga na kukataa.
Wakati ambapo kijana anapoona njia mbili mbele yake: njia inayomwamuru
kutii na kunyenyekea upotevu na utaghuti
(udhalimu) (kama wanavyoiona baadhi ya wapingamaendeleo), na njia
inayomshajiisha kufanya mapinduzi na kumtia moyo wa kuleta maendeleo na
mabadiliko - ni dhahiri na ni kawaida kwamba vijana wengi watafuata njia ya
pili, kwa sababu njia hiyo inakubaliana zaidi na tabia yao na maumbile yao ya
kutaka mabadiliko. Vilevile njia hi inachukuana na
maumbile
yao ya
kutaka mabadiliko na inaafikiana na maumbile ya mwanadamu ya kutokata tamaa na
kuwa na moyo wa matumaini usiokuwa na kifani.
Kwa hakika, tukizingatia, tutaona kwamba dhati au umbile Ia
Uislamu ni mapinduzi, linapinga kubakia nyuma na
linakataa dhuluma na upotevu. Tamko Ia KiisIamu Ia Laa
ilaaha illa-Ilah (Hapana mungu mwingine anayeabudiwa ila Allah tu) linamaanisha
kuwakufuru na kuwakataa waungu wote wa udikteta na upotevu.
Mafunzo ya Kiislamu yamemfaradhia kila binadamu aliyeukubali
Uislamu kupambana na dhuluma,
kukomesha ufisadi na
ubatilifu, kukataa ujeuri na upotovu, na kuukomesha kabisa.
Lau sisi twasimama kwa nia safi na kufundisha Uislamu
halisi kwa vijana wetu pamoja na kuyaejezea mafunzo yake ya kimapinduzi na
misingi yake ya kuleta mabadiliko, basi vijana wetu wangekuwa walinganifu,
wenye nia safi ya kuuhudumia Uislamu, na wangekuwa wanamapinduzi wenye
kupambana kwa ajili ya kuuhuisha Uislamu na kuujenga umma wenye imani na
wenye kuiongoza dunia.
Barobaro na Kujitolea katika
Njia ya
Mwenyezi Mungu
Njia ya Mwenyezi Mungu ni njia ya
haki, uadilifu na uhuru. Kuitumikia njia ya Mwenyezi Mungu ni
kushughulika katika kuitekeleza haki, kuiandama na kuhakikisha kwamba uadilifu
uko juu na uhuru uko kwa wote.
Matukio ya tarekhe (historia) na mazingira ya maisha
yametufundisha na kututhibitishia kwamba haki, uadilifu na uhuru haviwezi
kupatikana ila kwa njia ya kupambana na kujitoa mhanga. Umma ule unaomiliki
roho yakujitolea, kujitoa mhanga na njia ya mapambano
na mapigano unastahiki kupata uadilifu na uhuru ili ufikie anga Ia kuvuta hewa
iliyojaa haki na usawa.
Ama umma ulio bahili na mwoga,
jazaa yake ni kutawaliwa na tawala za kibatili, kidikteta, na kidhalimu ambazo
zakandamiza umma na kuutia utumwani.
Na wale wanaongojea uadilifu na
uhuru usimame na kuenea kila pahali kwa kuomba dua misikitini, kumnyenyekea
Mwenyezi Mungu, kutamani au kutumaini tu bila ya kusimama na kuyahakikisha hayo
kwa vitendo, hao ni juu
yao
kuzidi kungojea dhuluma, maonevu, madharau, vitisho, n.k.
Uadilifu ni njia ambayo haimkiniki
kuifikia ila kwa kulendea; uhuru wenye thamani haumkiniki kupata ila kwa
kuilipia. Njia ya kupata haki na uadilifu ni mapambano
tu. Thamani ya kupata uhuru ni kujitoa mhanga,
kujitetea na kuinyakua haki hiyo kwa nguvu.
Mtume Mtukufu amesema: "Kheri yote iko upangani. Hakuna kinachowanyorosha
watu isipokuwa upanga, na upanga ndio vishikilio vya Pepo."
Naye Amirul Mu'miniyn Ali bin Abu Talib akiwatahadharisha
wale wanaopenda kujiweka nyuma kuuacha mkondo wa
kujitoa mhanga na kujitolea kusaidia na wanaojitenga na kuiacha njia ya
mapambano na kujikomboa, alisema:
"Jihadi ni mlango miongoni mwa milango ya Peponi. Mwenyezi Mungu
ameifungua kwa wale mawalli Wake mahususi. Ni nguo ya
uchaji Mungu, deraya ya Mwenyezi Mungu iliyo na
hifadhi, na ni Pepo Yake iliyoimarishwa na inayotegemewa. Mwenye kuiacha
(jihadi) kwa ajili ya kuichukia, Mwenyezi Mungu
atamvika nguo ya udhalilifu na balaa itamwenea, na atadhalilika kwa madogo na
matwevu."
Vijana wa umma ndlo walio na uwezo
zaidi wa kupambana na kujitoa mhanga. Umbile lao na
tabia
yao
wanayokuwa nayo katika kipindi hiki cha ujana huwavuta zaidi na kuwapambia
kujiingiza kwenye mambo ya hatari bila ya kuyajali maisha, kwa sababu za
kinafsi tulizotangulia kuzielezea katika faslu zilizotangulia.
Kwa hivyo, ni juu yetu kuihifadhi
hii tabia iliyoko kwa wingi nafsini mwa vijana wetu. Tujibidiishe kuwaongoza
kwenye njia ya kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,
yaani katika njia ya kuhakikisha kuisimamisha haki, kuusimamisha uadilifu na
kuulinda uhuru.
La sivyo, umbile hili laweza kuelekezwa katika upande
uliopotoka, na wakati huo kutapatikana vikundi vya
vitisho na mapote yenye kuleta uharibifu na upotevu. Vipote hivyo vitakuwa na tabia ya kuilingiza kwenye ufisadi bila ya kujali, au
vijana wetu watalelewa na makundi mengine maovu yaliyo kinyume chetu na kuwafanya
wawe ndizo kuni za kuidumisha mipango
yao ya
uadui, au madaraja
yao ya kuwavusha na
kuwafikisha kwenye matakwa
yao
ya kikoloni.
Mafunzo ya
Kiislamu Yazinduayo
Ndiyo
Yanayotakikana Zaidi
Fikra huzinduka na kuamka. Bongo
hufunguka na alama za kuuliza huanza kuambata fikrani
mwa vijana chipukizi. Maswali mengi humjia akilini mwake.
Mimi ni nani? Kwa nini nimekuja
ulimwenguni? Ni nani aliyeniumba na kunipa
uhai? Ni mwisho gani unaonisubiri ambao utakomesha
maisha yangu? Ni nini msimamo wangu katika jamii ninayoishi
nayo?
Maswali kama haya na makumi mfano
wake huchoreka ndani mwa akili ya kijana chipukizi na hubakia katika hali hii
yakitafuta majibu ya maswali hayo ambayo yatapoza na kukinaisha moyo wake. Hi ni kwa sababu kijana huishi katika hali ya upungufu wa fikra
na ni punde tu ambapo bongo
lake
hufunguka na kuanza kuyafikiria
mambo haya kwa makini.
Hi ndiyo fursa inayopatilizwa na makundi yaliyopotoka,
yanayoingilia wakati kama huu ili kusimamia uandalizi wa fikra ya kijana kwa
miongozo iliyopotoka ambayo hutayarishwa kwa ustadi na kwa lengo Ia kutupiga
sisi wenyewe. Makundi haya huijaza fikra ya kijana kwa
kumpa jawabu zenye upotevu ambazo si za haki katika kuyajibu maswali yake
yaliyomo akilini na mawazoni mwake. Kutokana na sababu
kama hizi ndiyo utaona kwamba mafunzo ya
viongozi wa kidini yanatilia mkazo na kututanabahisha juu ya hatari ya kipindi
hiki cha ujana kwa upande huu.
Mafunzo hayo na riwaya hizo zinawakumbusha wazazi, viongozi
na wanavyuoni wa jamii yetu umuhimu wa kufanya haraka kupatiliza kuwaelimisha
watoto na vijana na kuijaza faragha ya kifikra kwa itikadi sahihi za Kiislamu
na kwa mafunzo yake yaliyo salama.
Uislamu unazingatia kwamba kumwelimisha mtoto ni haki mojawapo miongoni mwa haki za mzazi kwa mwanawe.
Baba wa mtoto akiacha kutoa haki hiyo, basi Mwenyezi
Mungu atamhoji na kumwuliza, na ikiwa atapatikana na makosa basi Mwenyezi Mungu
hatasita kumtesa siku hiyo ya Kiyama. Imam Ali bin Husayn Zaynul Abidiyn AS
amesema: "Ama haki ya mwanao, ujue kwamba yeye atokana nawe, na Akhera atawekwa nawe pamoja na kheri na shari zake. Nawe
utaulizwa juu ya yote uliyomfunza katika adabu nzuri na
katika kumthibitishia (Uungu wa) Mola wake Mwenyezi na Mtukufu na kumsaidia
katika kumtii Mwenyezi Mungu. Basi mfanyie mwanao matendo
mazuri na jueni kwamba mtalipwa thawabu kwa kumfanyia vizuri na mtateswa kwa
kumfanyia maovu."
Ali bin Abu Talib AS ameitaja hali ya faragha ambayo kijana
anayekulia huishi nayo. Ameitaja kwa kuashiria kwamba
ni miongoni mwa sababu zinazomwandaa kukubali fikra yoyote anayoelezwa. Akasema:
"Hakika moyo wa kijana ni
kama
ardhi isiyokuwa na kitu (isiyolimwa), chochote kinachoingizwa (kinachopandwa)
hukikubali."
Imam Ja'far Sadiq AS anasisitiza kuharakisha kuelimishwa
vijana wanaokulia ili kuwafutisha fursa mirengo
iliyopotoka na kuwakinga kutokana na misingi inayobomoa. Asema:
"Wapatilizeni watoto wenu wadogo kwa kuwafunza (Qur'ani na Hadithi) kabla
hamjatanguliwa na wapingamaendeleo." Wapingamaendeleo (marjaiyyah) ni kundi lililokuwa na fikra zilizopotoka katika jamii ya
Kiislamu katika zama hizo.
Leo katika zama zetu hizi tunaposhuhudia jinsi mawimbi ya
upotevu yanavyoleta uharibifu na yanavyouweka Uislamu mbali na wengi wa vijana
na mabarobaro wetu, na jinsi yanavyowavuta na kuwakumba vijana wetu waliozama
katika malezi ya Mashariki na Magharibi, huwa hatuna budi ili kufikiria kwa
makini misingi ya matatizo hayo na chanzo chake ili tuweze kupambana na haya mawimbi ya upotofu
ambayo yanahatarisha kwa kiwango kikubwa hali ya usoni ya umma wetu na ujumbe
wa Kiislamu.
Si sahihi wala si kweli kwamba yote haya waliyonayo vijana
wetu yanasababishwa na ubaya na uovu ambao uko ndani
mwa nafsi zao. Vivyo hivyo, haifai kuzikubali fikra zilizochakaa za hao
viongozi wapingamaendeleo ambao wanayafasiri haya yote yanayotokea na
kutendeka kwamba hayana bud
yatokee. Wana dalili kwamba ni lazima
ufisadi udhihiri katika bara na bahari na ujeuri na dhuluma uenee ulimwenguni
kote. Vivyo hivyo, wanasema kwamba haimkiniki kuyazuia yale
yaliyokadiriwa na yaliyojaaliwa na historia.
Kwa jumla, udhaifu wa vijana wetu
wa kutopendelea dini na kutoshikamana na mafunzo yake na badala yake
kushikamana na mafunzo maharibifu yaliyoingizwa kutoka nje, unatokana na
sababu maalum zinazotokana na hali yetu ya kubakia nyuma katika maendeleo ya
kila aina.
Sisi tuna jukumu mbele ya Mwenyezi Mungu na
mbele ya historia katika suala Ia kupotea umma wetu ujao. Kwa sababu sisi ndio
chanzo cha kupotea kwao na kwenda kombo. Kutokana na hali ya kujibakiza kwetu nyuma, kuacha kuwaongoza na
kutojali kuwaelimisha hadi kufikia kiwango sahihi kinachostahili na kinachotakikana.
Uislamu
Uliopotoshwa
Miongoni mwa misingi muhimu na sababu zilizowasababisha vijana
wetu kuyatoroka mafunzo ya dini
yao ni hii hali ya
Uislamu uliopotoshwa katika umma wetu wa kila mahali.
Kijana anapofumbua macho yake na kuiona jamii yake jinsi
iliyotanikatanika katika mila, desturi na tabia, ilivyorudi nyuma katika elimu
na maendeleo kadha wa kadha, ilivyotawaliwa na ubinafsi na ukabaiIa na badala
yake kuthamini utabaka na dhuluma, au atakapoiona jamii hiyo ikiwa na fikra
finyu na huko hayo yote hutendwa kwa jina Ia Uislamu na katika vazi Ia kidini,
basi huchukulia kwamba yule mtawala au kiongozi hutawala kwa jina Ia Uislamu.
Vilevile hudhania kwamba kilichosababisha watu kubakia nyuma ni
mfumo wa Kiislamu.
Kwa kawaida, zile fikra za wale viongozi wapingamaendeleo
zilizoganda hushikilia nafasi ya fikra za wanavyuoni halisi wa
Kiislamu. Zile fikra ambazo hazikushikamana na mafunzo
halisi ya KiisIamu na zilizojaa mafunzo ya woga na kupokonya moyo wa ushujaa,
ndizo ambazo zinatangulizwa mbele ya watu ili zionyeshwe
kama
mafunzo sahihi ya Kiislamu.
Maadamu Uislamu unaonyeshwa na kufundishwa kwa mabarobaro wetu kwa sura
kama hii iIiyochushwa ambayo inaonyesha kwamba ndilo
chimbuko halisi lililosababisha umma kubakia nyuma, basi utakuwaje msimamo wa
hao vijana wetu kuihusu dini hii?
Hapana shaka kwamba watautoroka Uislamu
huu na kuyakataa mafunzo yake, na badala yake
watatafuta njia nyingine waifuate ili waweze kuleta mabadiliko ndani ya umma,
mabadiliko ambayo watayatarajia kulendeleza jamii
yao.
Maisha haya ya kubaki nyuma, kuishi kwa jina na vazi Ia Kiislamu na kushikilia fikra hizo za
kutotaka kuleta mabadiliko ambayo yanatoa picha iliyochafuliwa ya maendeleo ya
Kiislamu, ndiyo sababu muhimu iliyowafanya vijana hao wanaokulia kuacha
kushikamana na dini
yao
ya Kiislamu.
Wanajua Nini katika Dini ya Kiislamu?
Kabla hatujatoa mawaidha ya
kuwashambulia, kuwakufurisha na kuwafanya mafasiki
vijana wetu, ni wajibu juu yetu kujiuliza wenyewe:
Je,
tumejaribu kuueleza Uislamu na kuwafunza kisha wao
wakaukataa?
Jawabu ni la.
Aghlabu ya vijana hawajui chochote katika mafunzo ya mfumo na
misingi ya Kiislamu.Taaluma zote zilizokuwa zikifunzwa katika jamii zetu za
Kiislamu, hazikukeuka hukumu za shaka katika masiala ya hedhi, nifasi, n.k.
ambayo ni miongoni mwa mafunzo ya kifiqihi na kiibada.
Ama kwa upande wa fikra, uchumi,
siasa au elimujamii ya Kiislamu, mafunzo haya muhimu hayakupatikana ila kwa
uchache. Vijana wetu hawakuweza kuyapata mafunzo namna hii kwa
urahisi. Je, haya yote si kweli? Katika hali
kama hii ambapo kumeenezwa kasumba ya kila aina ya
kupotosha na propaganda zinazotangazwa na mashirika pamoja na makundi mbalimbali
potofu, tunataraji nini kwao?
Wengi wa vijana walioyaepuka mafunzo ya dini na kuacha
kushikamana na sheria zake walifanya hivyo kutokana na kutoujua kwao
Uislamu, kutojua umbile
lake tukufu na umuhimu wake. Nasi tujue kwamba Mwenyezi
Mungu atatuuliza kuhusu huu upungufu tulioufanya wa
kutowafunza vijana wetu Uislamu halisi na kuwapa misingi ya mafunzo yake bora.
Vipi
Tuifundishe Dini?
Mfalme aliota ndoto iliyomfadhaisha
sana. Akaamka akiwa na fadhaa na hali ya kuingiwa na hofu. Akamwita mfasiri
ndoto na kumwelezea yote aliyoyaona ndotoni. Akasema:
“Nimeona meno yangu yakidondoka moja baada ya jingine. Hebu
niambie maana yake ni nini?"
Mfasiri ndoto akainamisha kichwa kwa
muda mfupi huku akifikiria, kisha akainua kichwa chake na kusema kwamba
aliyoyaona yatakuwa kweli, na maana yake ni kuwa watu wote wa familia yake
(mfalme) watakufa katika wakati wa uhai wake.
Tafsiri hi kavu yenye kisirani na fali mbaya ilimkasirisha mfalme na kumtia
hofu. Kwa hivyo, akaamuru mtaalamu huyo auawe mara moja.
Kisha akaamuru aletwe mfasiri ndoto mwingine; na
akaletwa haraka mbele yake. Mfalme akamwelezea ndoto ileile; naye mfasiri ndoto
akamjibu jawabu
kama
ile iliyotolewa na mfasiri ndoto wa kwanza, kwamba watu wa nyumbani kwake
watakufa katika wakati wa uhai wake. Jawabu hii pia haikumridhisha, na akaamrisha tena auawe.
Wakamletea mfasiri ndoto wa tatu.
Tena mfalme akamwelezea ile ndoto kwamba ameyaona meno yake yaking'oka moja
likifuatiwa na jingine. Mfasiri ndoto huyo
akamsikiliza kwa makini kisha akainamisha kichwa
kufikiri; na baada ya muda kupita katika kuwaza na kuzingatia, akasema:
"Ikiwa yale uliyoyaona ni kweli, basi wewe utakuwa mtu mwenye umri mrefu
zaidi katika familia yako, inshaallah."
Jawabu hii iliufanya moyo wa mfalme
kukunjuka na uso wake ukaonyesha furaha na kuondokewa na dhiki kutokana na
tafsiri hiyo nzuri. Hivyo, akaamuru mfasiri ndoto apewe
zawadi yenye thamani.
Msomaji mtukufu hebu zingatia kisa
hiki. Je, unaona tofauti yoyote katika maana
baina ya tafsiri hizo mbili? Ukweli ni kwamba
hapana hitilafu. Zote mbili zinathibitisha hakika moja tu, nayo ni kuwa mfalme atabakia baada ya kuwakosa (kufa) watu wake
wote. Basi kwa nini msimamo wa mfalme ulitofautiana
mbele ya wafasiri ndoto hadi akaamuru wale wawili wa awali wauawe, na wa mwisho
apewe zawadi?
Ukizingatia utaona kwamba siri kubwa mefichika katika nija
iliyotumika kueleza, kwani hakika ni ileile moja
haikubadilika, lakini mara ya kwanza ilielezwa kwa njia inayoleta kisirani na
kutisha, na mara ya pili ilielezwa kwa njia iliyojaa bishara, fali njema na
furaha.
Mbinu
ya Kuelezea ni Muhimu
Sana
Katika kisa hicho imetudhihirikia wazi umuhimu wa mbinu ya
kulielezea jambo lolote lile na umuhimu wake katika kuhadidisha msimamo wa
watu kutokana na jambo lililoelezwa. Hata ikiwa jambo moja ni la kweli lakini ikawa halikuelezwa kwa mbinu nzuri, basi hakuna dhamana kwamba watu
watalikubali jambo
hilo.
Vivyo hivyo, ikiwa jambo jingine ni la batili lakini
kukatumika mbinu nzuri katika kulielezea, basi huenda watu wengi wakahadaika na
kulifuata.
Hivi sasa tunashuhudia vile hali ya watu kuelekea katika
dini na kule kupungua katika kushikamana nayo.
Tutaweza vipi kuwavuta na kuwaelekeza kwenye dini
yao na kuwaelimisha
ujumbe wao mtakatifu?
Ninaitakidi kwamba ni dharura mno
kufikiria njia na mbinu nzuri ya kulelezea dini kwa watu. Wabalighi
(wanatablighi) wengi na wanavyuoni hawajafaulu katika
kuchagua ile mbinu nzuri, na kutokana na sababu hi hawakuafikiwa kufaulu katika
shughuli zao, bali mara nyingine matokeo yake huwa kinyume chake na mara
nyingine hutokea kwa baadhi
yao
upinzani na chuki ambavyo husababisha kuitoroka dini.
Qur'ani Tukufu inatuzindua juu ya umuhimu wa
jambo hili katika kulingania Uislamu. Inasisitiza juu ya
kutumia mbinu nzuri katika tablighi. Inasema: "Lingania katika njia ya Mola wako kwa
hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa lile ambalo ni zuri." (16:125)
Pia Qur'ani yatuzungumzia kuhusu maadili (akhlaki) ya Mtume
Mtukufu na taathira yake katika kuwavuta watu katika
dini. Inasema: "Na lau ungekuwa
mkali na mwenye moyo mgumu wangetawanyikatawanyika pembezoni mwako."
(3:159)
Tablighi
na Hali ya Kijamii
Katika zama hizi hupatikana kila
aina ya sababu ya kupotoa. Vyombo vya habari huhadaa kiasi
cha kuathiri sehemu ya maisha ya kila siku. Imani ya kidini ya vijana
wetu wa sasa imetingishika vya kutosha kutokana na
hila za wakoloni na hali yetu ya kubakia nyuma. Hayo yote ni
kwa sababu ya kuvutika kwetu zaidi katika upande wa ulimwengu wa Magharibi na
Mashariki ambao wanamiliki kila aina ya vyombo vya maendeleo, teknolojia na
elimu pamoja na maongozi
yao
ya kuupiga vita Uislamu.
Katika zama kama hizi na katika
hali
kama hii ya ufisadi, ni njia ipi bora
inayoweza kuwavuta zaidi watu katika dini? Njia ambayo inawafanya wajitambue na wayarudie mafunzo
yao
ya Kiislamu? Hapa yapo mambo mengi ambayo ni wajibu
yapatikane katika taratibu za kuielezea dini kwa watu katika zama zetu hizi.
Urahisi na Ufunufu
Sifa muhimu inayojipambanua nayo zama
zetu hizi ni kuongezeka kasi na kufanywa mambo haraka haraka. Masafa ambayo
binadamu alikuwa akiyakata kwa ngamia katika muda wa mwezi mzima sasa anayakata
kwa ndege kwa muda wa saa moja akiwa amekaa juu ya kiti chenye raha na starehe.
Kazi ambayo binadamu alikuwa akiitolea juhudi na
kutaabika kwa masiku, sasa anaifanya kwa masaa machache na kwa njia ya urahisi
kabisa. Yote haya yamemfanya binadamu kupendelea zaidi kasi katika shughuli
zake na hata katika kufikiri kwake. Hii ni kwa sababu amechokeshwa kufanya jambo lolote ambalo
linahitaji atoe juhudi nyingi na kupoteza muda mrefu.
Vilevile, hata katika upande wa
kifikra na kielimu, usahali na ufunufu vimethibiti kuwa ndio wito wa fikra na
elimu katika zama za sasa. Elimu ya falsafa iliyofanywa kuwa ngumu zamani na kusomwa na watu maalum tu walio na viwango maalum vya
elimu, sasa imekuwa ikisomwa na mabarobaro wanaokulia. Vijana wamekuwa
wakiisoma na kuijadili na kufuata msimamo wake
mwenyewe mbele ya elimu hii. Vilevile tata za kielimu ambazo zilikuwa zikitatiza
katika nyanja tofauti tofauti za elimu leo zimepoteza
haiba yake. Zimekuwa zikiandamana na viwango vyote
kutokana na kurahisishwa na kufafanuliwa kunakofanywa na vyuo, magazeti,
majarida, vitabu, vipindi vya televisheni, n.k.
Kwa hivyo, tunapotaka kuyaelezea mambo yetu ya Kiislamu
katika zama zetu hizi za kasi, usahali na uwazi, bila
ya kupatikana uzito wowote, yatakikana tujiepushe na nija ngumu zisizofahamika.
Tuyaelezee mambo ya kidini, kifikra na kielimu kwa
taratibu zilizo funufu na rahisi ili kijana anayekulia aweze kuyafahamu na
kuyashika. Na aghlabu huu ndio utaratibu unaotumiwa na
Qur'ani na uliotumika na Mtume Muhammad SAW katika kulingania kwake na katika
maongozi yake.
Kuna baadhi ya wanavyuoni wanaopendelea kutumia mbinu ngumu na kuonyesha ubingwa wao wa kielimu katika hotuba zao na
mihadhara
yao
na hata katika vitabu pia kwa kutumia misamiati na istilahi ngumu za lugha na
mantiki wakati wanapoelezea mambo ya dini na mafundisho yake matukufu.
Taratibu kama hizi ni vizuri kuzitumia kwa wasomi
walioelimika barabara, watu ambao wako tayari kutoa juhudi kuyatumia mabongo
yao katika kufikiri. Ama
yule mtu wa kawaida na kijana anayekulia, hana haja ya
kuzisoma sentensi ngumu za lugha zisizofahamika. Wao huwa
wamekwishazoea lugha rahisi ya magazeti.
Huenda baadhi ya wanafikra na
wanavyuoni wakapunguza juhudi zao za kuwaandikia watu wa kawaida ambao
hawajapevuka kielimu, lakini ukweli ni kwamba wao wanasahau kwamba watu wa
kawaida ndio wanaohitaji zaidi kuongozwa na ndio wepesi zaidi kupotea au
kupotezwa. Ama kwa upande mwingine, jambo lenyewe
linahitaji kuwa na uwezo fulani wa kifasihi iIi kuzirahisisha fikra hadi
zifahamike. Hii ni kazi ya mwanafikra au mwandishi
kuifafanua fikra zake na kwa njia rahisi ili zifahamike mbele ya watu wa
kawaida. Haitokuwa fahari kwa mwandishi kuyaelezea
maandishi yake kwa mbinu maalum
iliyo ngumu, bali atashukuriwa na kusifiwa sana ikiwa atazielezea fikra zake
kwa mbinu nzuri yenye kufahamika kwa urahisi.
Njia Zenye
Kuathiri
Kuzieleza fikra fulani kwa njia
isiyoeleweka huenda kukasababisha kutoziathiri nafsi au kuzifanya zile fikra
zisivame au zisieleweke. Lau zatumika njia zilizo hai na
zenye kusisimua njia hizi huzipa fikra hizo hisia zenye kuleta athari. Kwa
mfano, kisa kizuri ambacho kimekusudiwa kuielezea hakika fulani
miongoni mwa hakika za kidini, chaweza kukubaliana na nafsi
na
kuleta taathira zaidi kuliko vile yanavyoweza maneno ya kawaida kuathiri.
Watu wengine wamefaidika kiwango kikubwa kwa
kutumia mtindo huu wa visa, wamezijaza maktaba zao kwa sampuli kadha wa kadha
za visa vilivyojaa fikra zao na mafunzo
yao.
Nayo Qur'ani Tukufu imetangulia katika kutumia mbinu
kama hizi. Utaona inaelezea vipande vingi
vyenye kuathiri katika visa vya historia, nayo ina
haki kabisa kuwa ndiyo visa vizuri zaidi. Hakika zilizotumiwa na elimu za kisasa za lugha za kuweka nambari na kudhibiti
hesabu ni njia muhimu miongoni mwa njia za kuathiri katika zama hizi. Kwa
hivyo, ni juu ya wabalighi wanaoongoza kujisaidia kwa
kutumia njia
kama hizi katika kufundisha
hakika za kidini. Vilevile wazitumie njia hizi katika kutolea ushahidi wenye
kuyathibitisha mafunzo haya ya kidini na hukumu zake.
Kwa upande mwingine, ni wajibu juu
yetu tusiuache uwanja wa fani chini ya maongozi ya wakoloni ambao ni msingi wa
ufisadi na upotevu,
kama vile, sinema,
sarakasi na sanaa. Vyote hivyo ni vitu vyenye taathira
kubwa katika nafsi ya mwanadamu. Lakini pamoja na
masikitiko makubwa, vyote hivyo viko chini ya utumishi na utawala wa wafisadi
na wapotofu. Ni juu ya wabashiri, wabalighi na
wanavyuoni kujitahidi katika kufaidika na vitu mfano wa hivi ili kuyatumikia
malengo ya Kiislamu na mafunzo yake matukufu.
Umma Wenye
Lengo
Binadamu wa sasa huishi katika hali
ya kujiamini kusiko na kipimo. Hutaka akifanye kila kitu kimnyenyekee ili ayashuhudie majaribio yake. Hatosheki na
maelezo ya mhandisi juu ya umbo Ia nyumba au sampuli yake. Hata maelezo yake
pia hayamkinaishi, bali mwishowe humtaka mhandisi amchoree
ramani ya nyumba yenyewe ili aione kwa macho.
Akitaka kununua gari au chombo chochote kingine, mwanzo
hutafuta maelezo yake ili akione kwa macho yake ndipo
atoe msimamo wake. Binadamu hutumia njia hizi hata katika mambo ya kijamii.
Kumwelezea uzuri wa nadharia fulani au ubaya wake
hakumtoshelezi, bali hutaka aione nadharia yenyewe imechorwa na kutandikwa
mbele ya uwanja wa kijamii ili aweze kuubaini msimamo wake juu ya nadharia
hiyo. Ikiwa ataelezea juu ya nadharia fulani kisha
baadaye ashuhudie kuwa watu wenye nadharia hiyo wanaishi katika hali iliyo
kinyume chake, hatoweza kuamini kuwa fikra hii ni sahihi au ni sawa.
Kutokana na mantiki hii imekuwa ni
dharura kupatikana jamii yenye imani ya msingi ili iwe ni dalili bora na
ushahidi thabiti juu ya uzuri wa imani hii. Ni wajibu juu ya wanavyuoni,
viongozi na wabalighi wawe ndio mbegu za kwanza kabisa
katika kukuza hiyo jamii inayotakikana. Wayashike maadili ya Kiislamu na adabu zake katika muamala, maingiliano, maendeleo na
maisha
yao ili
wayafanye kuwa ni kielelezo na kiigizo chema cha misingi ya dini na mafundisho
yake.
Ama ikiwa sifa hizo hazitopatikana katika maisha ya
wabalighi na wanavyuoni wa kidini, maneno
yao na vitendo vyao
vitakinzana na kupingana, na kitendo hiki kitatosha kuwakimbiza watu katika
dini na kujiepusha nayo.
Mabarobaro na Uongozi
Wakoloni wanajaribu kutumia kila njia ya kimatendo katika
kutawanya habari na kuwadhihirishia vijana wetu
viongozi waliopotoka ili wawatumie vibaraka hao katika kuzielekeza hima za
vijana wetu kwenye mambo ya kijinga na upotofu. Kwa ajili kama
hii ndio tunaona wanatilia mkazo
sana
kuiongeza idadi ya viongozi wataalam, mabingwa wa riadha na makocha wa
kijinsia. Lengo lao ni kuwapotosha vijana wetu na
kuwafanya wawafuate na wawaige viongozi hao na waandame tabia na mienendo
yao miovu.
Vilevile matangazo hayo ya kikoloni yanapotaka kuwaelezea
vijana wetu maisha ya shujaa fulani mwanamapinduzi na
mtetezi wa haki, au yanapotaka kuelezea msimamo wa kijana shujaa au sira ya
mwanafikra fulani, hujaribu
sana
kutoa habari za viongozi hao kinyume cha ukweli. Hutumia hiana, hila na huipotosha kabisa hakika ya viongozi hao au mashujaa hao
na huwaarifisha kwa njia ambayo haitoleta faida yoyote kwa yule ambaye
anaelezewa historia hiyo.
Ingawa sisi tunaheshimu kila taaluma na tunayatukuza
mapambano yoyote ya kibinadamu, lakini wakati huohuo tunakataa kutenganishwa
na historia yetu tukufu ambayo ni urithi wetu mkuu uliojaa matukio matukufu ya
mashujaa, wapiganaji jihadi na misimamo ya watetezi wa haki waliokuwa na
ikhlasi. Urithi huo umejaa historia ya wanavyuoni wenye hima, nishati na uvumbuzi. Tunakataa kujisahaulisha historia za viongozi na mashujaa wa umma wetu watukufu na badala yake kuwaiga
viongozi wa umma mwingine. Tunakataa kuwaingiza viongozi wengine hapa kwetu na kuwafanya
kama viongozi
kwa vijana wetu. Hii inamaanisha kuing'oa hadhi ya umma wetu na
asili yake na kukata uhusiano baina ya vizazi vya sasa vya umma wetu na vile
vilivyotangulia.
Tukizingatia tena tutaona kwamba mashujaa wa umma mwingine,
viongozi wao, huenda msimamo wao na maongozi
yao hayakuanza pale panapochimbuka misingi yetu ya asili
tunayoiamini. Vilevile harakati zao hazikulingana na
yale maoni tunayoona na kuyaandama, wala hawalazimiani na yale mafunzo ambayo
sisi tunalazimiana nayo. Ikiwa viongozi
kama
hao watakuwa ndio viongozi wa vijana wetu, basi kuna hatari ya kudanganyika na
kushawishika.
Tunapoitupia jicho historia yetu tukufu tunaona kwamba
vijana wetu waliobalighisha (waliosambaza) dini wana kipindi kikubwa cha
kimsingi cha kuzingatiwa katika kuzitilia nguvu nguzo za ujumbe wa Kiislamu na kuujenga umma wa Kiislamu wenye imani na
kutetea haki. Vijana wa Kiislamu ndio waliosimama
msitari wa mbele katika kuyasimamisha mapinduzi ya Kiislamu, kuuendeleza mbele
harakati zake na kuyalinda mafunzo yake.
Vilevile
vijana wetu walikuwa katika kikundi cha mbele katika kuamini na kufuata upesi
huu ujumbe uliotoka mbinguni hadi Mtume Mtukufu akasema: "Ninawausia (mwafanyie) wema mabarobaro, kwani nyoyo zao ni laini
zaidi. Hakika Mwenyezi Mungu amenituma nikiwa ni mbashiri na
mhofishaji na mabarobaro wakaniunga na wazee wakanihalifu."
Kutokana na juhudi zao
safi zenye ikhlasi,
kujitolea kwao kukubwa na kumwaga kwao damu zao takatifu zilizo tohara ndiko
kulikoufanya mti wa Kiislamu kutanda kijani kibichi na matunda yake yakaiva.
Sasa hebu tutoe baadhi ya harakati za vijana waliobalighisha
dini iIi waigwe na vijana wetu wa Kiislamu wa leo
kama viongozi wao.
Kuleta
Mabadiliko katika Umma kwa Njia ya Hekima
Ikiwa tumekadiriwa kuzaliwa katika jamii hii iliyobakia
nyuma, iliyoteseka na kuzidi kujibakisha nyuma, je,
imeandikwa pia kwamba ni lazima tuishi maisha yetu yote tukiwa tunatawaliwa na
hali hii pamoja na mazingara haya? Ni kwa nini
hatusimami kuibadili hali hii ili maisha yetu yawe na thamani na kuweko kwetu
kubakishe athari?
Hakika wale wakuu ambao wanasifika katika historia na kuheshimiwa na kila umma walikataa kuyaacha maisha yakiwa
yanaendelea kuishi katika hali ile waliyoikuta wakati walipokuja duniani. Wao
ndio waliofanya bidii kuubadili umma wao, hali na
mazingira yake, na ndio wale ambao kwamba wameitengeza historia na kuzichora
athari zake. Majina
yao
yakabakia milele na majukumu
yao
waliyotenda na utukufu wao unashuhudiwa. Ama wale watu waliokuja katika jamii na kuondoka bila ya kuacha athari au sifa yoyote kama
walivyokuwa, hao ndio wanafanana na wanyama, bali baadhi
yao wamepotea njia zaidi, yaani hawana majina
yatakayokumbukwa wala athari yenye kubakia.
Hapa upo mfano mzuri wa Mus’ab bin
Umair, kijana aliyeishi katika raha, aliyependwa
sana na wazazi wake na alikuwa mtoto wao wa
pekee. Alikuwa na uwezo wa kufaidika na nafasi hii
katika kuyajenga maslahi yake ya kibinafsi na kuijenga hali ya maisha yake ya
baadaye, lakini alikataa kuishi
kama mnyama
mwenye hamu ya chakula tu. Hivyo, akajishughulisha na
shughuli za kuleta mabadiliko na mapinduzi katika ile jamii ya Ujahilia na
akavitumia vipawa vyake katika njia ya kuijenga jamii iliyokufa kiimani.
Mus'ab akajiunga na harakati za
Kiislamu zilizokuwa zikiendeshwa kwa siri na hadhari katika mji wa Makka chini
ya uongozi wa Mtume Mtukufu.
Kutokana na kujifunga kwake masombo
na kushikamana na Uislamu, ameweza kutekeleza kwa bidii wajibu wake wa uongozi
katika harakati za ujumbe wa Kiislamu. Na kwa ajili
ya juhudi zake hizo, Mtume Mtukufu alimchagua kuwa balozi wake na mwakilishi
wake katika Madina mji ambao baadae ukawa ndio kitovu cha Uislamu na matokeo ya
jamii ya Kiislamu.
Mus'ab alifika Madina akiwa hamiliki silaha yoyote isipokuwa
silaha ya ikhlasi na imani pamoja na malengo yake
matakatifu ya kuleta mabadiliko na kupambana na maovu yaliyoenea.
Kulikuwepo ugomvi na tofauti za
kijamii kati ya makabila ya Madina na hasa baina ya makabila mawili ya Aws na
Khazraj. Kulikuwepo pia makundi ya kidini yaliyokuwa yakipingana
- Mayahudi,
Wakristo na waabudu masanamu (washirikina). Vilevile
ufisadi mwingi ulienea miongoni mwa vijana wa Ujahilia
katika ulevi, kamari na upotevu mwingineo. Lakini Mus’ab yule kijana aliyekuwa
akibeba wajibu wa ujumbe huu mtukufu, hakuwa na
jingine ha kutekeleza wajibu wake katika kuleta mabadiliko katika jamii hiyo
hata pangekuwepo vikwazo na matatizo ya aina gani.
Akaanzisha shughuli yake kwa mpango
wake wenye hekima kupitia maongozi ya kiongozi wa ujumbe, na akaendelea na
shughuli yake kwa ikhlasi na ustawi. Akapambana na
matatizo kwa moyo mkunjufu, ushujaa na imani.
Haukupita muda katika Madina, harakati za ujumbe zilianza
kupata vijana wakakamavu pamoja na umma ulioamini
barabara malengo ya ujumbe. Mji wa Madina ukaanza
kujiandaa kumpokea na kumlaki kiongozi wa ujumbe huu wa Kiislamu ambaye baada
ya kufika tu akatangaza kuasisiwa kwa dola kuu ya Kiislamu.
Vivi hivi ndivyo Mus'ab alivyoweza kuibadili jami ya Madina - kutoka jamii uliyobakia nyuma hadi kwenye
jamii yenye imani na iliyo hai ambayo ilisimama kupasua njia na kuieneza nuru
na ujumbe wa Kiislamu.
Aliuhusisha
Ubarobaro Wake Kuutumikia Uislamu
Watawala walio vibaraka wa wakoloni
wanaendelea katika mbinu za kuwapoteza vijana wetu na kuuharibu ujana wao
ambao ni kipindi kilicho na thamani zaidi maishani mwao. Kwa upande wa masomo,
wanawapotezea wakati wao kwa kuwawekea vipindi na matangazo ya televisheni yenye kuwapotosha na
mambo mengineyo yenye kujaza bongo zao kasumba.
Kwa upande mwingine, binadamu hushangaa kutokana na hivi viwango vikubwa vya pesa vinavyozidi, pesa ambazo
hutolewa na serikali katika uwanja wa michezo na starehe kutokana na uchumi wa
wananchi. Je, yote haya ni kutokana na kwamba eti
serikali hizi zinataka kuwapunguzia wananchi wake baadhi ya shida zao au
zinataka kuwastarehesha?
La hasha! Lau ni kweli kwamba
serikali hizo zinawatakia raha wananchi wake, zingewajengea viwanda
vidogovidogo vya kazi za mikono au kuwafanyia miradi inayohitajika katika
maisha
yao.
Wananchi wengi wanashtakia upungufu wa huduma za siha,
afya na mahitaji muhimu ya kijamii. Hakuna majumba ya kukaa
wala misaada ya kimaisha. Badili ya kusaidia upande huu muhimu, serikali
hutoa misaada kwa ajili ya riadha kwa kadiri kubwa. Kwa nini?
Jawabu liko wazi kabisa.
Inataka kuipitisha bure fursa ya kijana kwa wananchi
ili umma wetu usifaidike naye katika kuujenga mustakbali wake.
Inataka kuzishughulisha nyakati za vijana wetu na kuzipondoa hamu zao ili wasipate wakati wa kufikiria haji
wanayoishi watu wao wala wasifikirie kupanga jinsi ya kuwaokoa.
Inataka kuviyeyusha vipawa na ujuzi
wa vijana wetu ili daima tubaki kuwa ni mateka wa vipawa vya wataalam wa
kigeni.
Inasikitisha
sana
kuona kwamba vijana wetu wengi wameingia kwenye mtego huo mbaya na lengo
hilo bovu lililojaa hila
za wakoloni na mabeberu. Vijana wetu wengi
wanapoteza nyakati zao za thamani na umri wao mtukufu katika riadha na
michezo mingine ya upuuzi. Kwa mfano, hujitahidi kujinyakulia ubingwa katika
kucheza mpira wa miguu, ha mara nyingine huishi katika
hali ya mapambano katika nyanja na vilabu vya riadha badala ya kushikamana na
mapambano ya kiasili ambayo ni wajibu juu yake kujiingiza kwa ajili ya
kuyatetea maslahi ya umma wake na ujumbe wake.
Je, wakati haujafika bado kwa
vijana wetu kutambua upeo wa njama hizi ili wayaache michezo ya upuuzi na
wazielekeze hima zao na vipawa vyao katika mambo yaliyo wajibu maishani mwao?
Ni
viongozi
wangapi waliotajwa katika historia yetu tukufu ambao walishughulikia
kipindi cha ujana wao kwa ajili ya kuuhudumia Uislamu na kuujenga mustakbali wa
jamii zao?
Hebu tumwone Amirul Mu'miniyn Ali bin Abu Talib AS. Akiwa
mdogo bado aliiweka nafsi yake kuutumikia ujumbe wa
KiisIamu. Alikuwa ni kijana wa kwanza kusilimu na
kusadiki Utume wa Mtume Muhammad SAW pamoja na kwamba umri wake haukuzidi miaka
tisa. Wakati watoto wa Makka walipokuwa wakiongozwa na
mafasiki kumwudhi Mtume Mtukufu na kumtupia mawe alipokuwa akitembea
barabarani, Ali alikuwa kijana wa miaka kumi akiandamana na Mtume Mtukufu
njiani akimwondoshea udhia na kuwaadhibu watoto hao wa makafiri.
Vilevile katika usiku wa Hijra,
kijana 'Ali alionyesha upeo wa kujitolea kwake na imani yake thabiti.
Washirikina waliizingira nyumba ya Mtume Mtukufu wakitaka kumshambulia na kumwua Mtume Mtukufu wakati wa alfajiri. Ikawa hapana
budi ila Mtume Mtukufu atoke kwa muda mle nyumbani ili
aweze kuanza safari yake ya Hijra. Mtume Mtukufu akamtaka Ali -nduguye, na binamu yake ambaye wakati huo alikuwa ni kijana mbichi
kabisa, achukue nafasi ya kuwahadaa maadui kwa kulala katika kitanda cha Mtume
Mtukufu hadi asubuhi wakati watakaposhambulia maadui. Pamoja na
kwamba kulikuwepo hatari kubwa katika kuliingilia jambo
kama
hili, lakini hata hivyo alilala juu ya kitanda cha Mtume Mtukufu huku akingojea
panga na mikuki ya maadui kwa moyo thabiti na ushujaa kamili.
Baada ya Mtume Mtukufu kuhajiri Madina,
Ali alikuwa ndiye mwakilishi wake katika Makka. Amana
alizokabidhiwa Mtume Mtukufu akazirudisha kwa
wenyewe. Akasimamia harakati za Kiislamu na kuihami
familia ya Mtume Mtukufu. Kisha naye akagura pamoja na
familia ya Mtume Mtukufu hadi Madina ingawa kwamba kulikuweko na upinzani
mkubwa pamoja na kufukuzwa na washirikina njiani.
Mjini Madina alikuwa pamoja na
Mtume Mtukufu katika shughuli na harakati zake zote. Kutokana na ushujaa wake, Mwenyezi Mungu aliunusuru Uislamu na kuupa
ushindi katika vita vyote alivyoshiriki.
Kijana Ali aliuhusisha ujana wake katika kuuhudumia ujumbe wa Kiislamu hadi akawa mzee na akauawa shahidi katika njia
ya Mwenyezi Mungu.
Karibu na ushahidi wake alisema:
"Hakika nimeanza nao (Uislamu) na mimi nilikuwa chini ya miaka ishirini,
na hivi sasa nimezidi miaka sitini.”
Barobaro
Mwanamapinduzi Shahidi
Alikuwa ni kijana chipukizi mwenye
umri wa miaka kumi na nane. Alikuwa na uzuri wa ajabu,
tabia njema na mwerevu. Alifanana
sana
na Mtume Mtukufu kwa tabia na umbo
kama
alivyosema baba yake Imam Husayn bin Ali AS. Huyo ni
Ali Akbar, mwana wa lmam
Husayn
AS.
Kijana huyo mtukufu aliandamana na
baba yake Husayn katika harakati zake dhidi ya dhuluma na upotevu wa Bani
Umayya. Kuandamana kwake pamoja na baba yake hakukutokana na huruma itokanayo
na fungamano Ia nasaba, bali kulitokana na imani yenye kanaa na lengo, na nia
yenye chimbuko Ia kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Wanahistoria wanaelezea kuwa katikati ya njia walipokuwa
wakielekea kwenye medani ya vita na mapambano,
kiongozi wa mapinduzi, Imam Husayn AS alisinzia kidogo na alipotanabahi akawa
analikariri neno: "Inna Lillaahi Wainna llayhi raaji’unna." (Sisi ni wa Mwenyezi Mungu nasisi tutarudi Kwake).
Mwanawe Ali Akbar alikuwa ubavuni karibu naye, akamwuliza:
"Baba! Kwa nini ulilikariri maneno hayo? Mwenyezi Mungu asikuonyeshe baya." Imam Husayn AS
akamjibu: "Ewe mwanangu! Nimefazaika. Nimemwona
mtu aliyepanda farasi akisema: 'Watu hawa wanakwenda na mauti yanawaandama.'”
Ali Akbar akasema: "Ewe baba! Kwani sisi hatuko kwenye
haki?" Baba yake akamjibu haraka: "Kwa nini! Wallahi sisi tuko kwenye haki!" Ali Akbar akasema:
"Basi wallahi hatutojali tuyaangukie mauti au mauti yatuangukie."
Msomaji tazama! Mambo hayo kwake haya mhusu baba yake bali yanahusiana na haki na kwa ajili ya haki. Kwa hivyo,
kustahamilia yaliyo machungu na kukabiliana na mauti
huwa sahali kwa mtu.
Kwa hakika, askari wa upande wa maadui
walijaribu wawezavyo kumvuta Ali Akbar ili ajiunge nao au kwa uchache wamtenganishe
na askari wa baba yake kwa kupatiliza uhusiano wa nasaba kati ya Ali Akbar na
Yazid bin Muawiya yule mpotevu aliyejibandika kuuongoza umma wa Kiislamu kwa
ubatilifu. Mama wa Ali Akbar ni Layla bint Abu Murrah
bin Urwa bin Masud al-Thaqafi. Mama yake ni Maymuna
bint Abu Sufyan, dada yake Habiba, mke wa Mtume Mtukufu. Kwa hivyo, nyanya wa Ali Akbar ni dada wa Muawiya na ni shangazi wa Yazid.
Baadhi ya makamanda wa jeshi Ia lbn
Saad walimwita katikati ya vita wakati ilipobainika wazi kwamba mwisho wa watu
wa Imam Husayn AS na Ahlul Bait yake ni kifo na ushahidi. Walimwambia Ali
Akbar: “Wewe ni jamaa wa Amirul Mu'miniyn Yazid, na
wala hatupendelei ufikwe na ubaya wowote. Njoo kwetu."
Lakini Ali Akbar kijana mwanamapinduzi,
hakuwa mtu mwenye kuhadaika au kukubali huu wito mwovu wenye hiana.
Akawajibu papo hapo: "Upotevu ni wenu. Ujamaa wa
Mtume wa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi uchungwe kuliko uakraba wa mwana wa mla
maini."
Akawakumbusha kuwa heshima zao za ubatilifu walizoshikana
nazo ni duni kuliko zile alizoshikana nazo yeye -
heshima za haki na uongofu. Wao walikuwa wanautukuza utawala wa
kidhalimu na kuheshimu zaidi fungamano lao na utawala huo huku wakidharau na
kutupa kando fungamano na heshima kwa Mtume Mtukufu na kuhifadhl haki ya
kuunga uzao wake. Kisha akaingia medani katika vita vya jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Akadhihirisha ushujaa mkubwa na kuwashangaza maadui ambao walilazimika kumchagua yule
shujaa wao zaidi kwenda kupambana naye. Mwishowe kijana huyu mtukufu akaanguka
ardhini akiwa amekufa shahidi juu ya ardhi ya ushahidi ili
aandike kwa damu yake wasia kwa vijana wa umma wa Kiislamu utakao kuja karne za
baadae, kwamba wasimame kutekeleza wajibu wao katika kuutetea ujumbe wa
Kiislamu na kuzitetea haki na maslahi ya umma. Vijana wanaharakati watafute
ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wasiogope wala
wasijali kuyaendea mauti au kufikiwa na mauti.
Hadithi
Kuwahusu Mabarobaro
Zifuatazo ni hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume Mtukufu SAW na Maimamu Maasumu AS kuhusu vijana:
Vijana
Wajielimishe
Imam
Baqir
AS: "Lau namjia barobaro miongoni mwa
mabarobaro ambao ni wafuasi wetu, nikamkuta hajifunzi katika dini,
ningemwadhibu." (Safinatul Bihar, jz. 1, uk. 680)
Kujifunza
Ujanani
Mtume Mtukufu SAW:
"Mwenye kujifunza katika ujana wake ni
kama kuchora katika jiwe." (Usuulul Kaafi, jz. 2,
uk. 603)
Qur'ani
Huvaana na Kijana
Abu
Abdillah
AS:
"Mwenye kusoma Qur 'ani akiwa ni kijana muumini,
Qur'ani hutangamana na nyama yake na damu yake, na Mwenyezi Mungu Mtukufu
humweka pamoja na watukufu na watiifu, na Qur'ani itakuwa ni kinga yake siku ya
Kiyama." (k.j., jz. 2, uk. 603)
Upatilize
Ujana Wako
Mtume Mtukufu SAW alimwusia Abu Dharr: "Ewe Abu Dharr!
Yapatilize (mambo) matano kabla ya matano: Ubarobaro wako kabla ya uzee wako;
siha (afya) yako kabla ya ugonjwa wako; utajiri wako kabla ya umasikini wako;
faragha (nafasi) yako kabla ya shughuli zako; na uhai
wako kabla ya kifo chako." (Abu Dharr Thairi 'Adaalatul lslaamiyyah, uk.
23)
Enyi Barobaro
Itakeni Akhera
Salaam bin Miskiyn amesema: "Imam Hasan AS ametuambia:
'Enyi kundi la mabarobaro! jilazimisheni kuitafuta
Akhera; hakika wallahi tumewaona watu waliotafuta Akhera wakapata dunia na
akhera. Wallahi hatujaona mwenye kuitaka dunia akaipata
Akhera.' " (al-Irshad;
uk. 57)
Imam Mahdi
Atakuja akiwa Barobaro
Abu
Abdillah
AS: "Lau Qaim Imam Mahdi AS atasimama watu
watamkataa kwa sababu atawajia akiwa ni kijana kabisa. Na
miongoni mwa balaa ni kuwatokea watu huku akiwa ni barobaro na wao wakimtarajia
kuwa ni mtu mzima." (al-Ghaybatul Kubraa,
uk. 11)
Barobaro ni Mwepesi Kiyaendea ya Kheri
Abu Jaafar
al-Ahwal alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa Imam Sadiq AS aliyekuwa akijishughulisha kuyatangaza mafunzo ya Kiislamu na Ahlul Bait. Siku moja
Imam Sadiq AS alimwuliza: “Je, waionaje hali ya watu katika kulijia jambo hili
(dini) na kuingia ndani yake?" Abu Jaafar akasema: "Wallahi! Hakika ni wachache
sana." Imam Sadiq AS
akasema:
"Jilazimishe
na vijana, kwani wao ni wepesi katika kuyaendea kila
(mambo ya) kheri." Jawaan,
uk. 49)
Upatilize
Uvulana Wako
Imam Ali AS: “Upatilize uvulana wako kabla ya kuzeeka kwako,
na afya yako kabla ya kuugua kwako." (k.j., uk.
60)
Enyi Vijana
Fanyeni Bidii na Mjitahidi
Mtume Mtukufu SAW: "Mwenyezi Mungu anaye malaika ambaye
huteremka kila usiku kutangaza: 'Enyi vijana wa miaka ishirini! Fanyeni bidii na mjitahidi.'
(k.j., uk. 66)
Faragha ya
Kifikra kwa Barobaro
Imam Ali AS: "Hakika moyo wa
kijana ni
kama ardhi isiyokuwa na kitu
(isiyolimwa) chochote, kinachoingizwa (kinachopandwa) ndani yake hukikubali."
(k.j., uk. 69)
Jihifadhini kwa Elimu na Adabu
Imam Ali AS:
"Enyi kundi la vijana! Ihifadhini heshima yenu kwa
kujifunza adabu ya dini yenu na kujielimisha." (k.j., uk. 194)
Barobaro Awe
Mwalimu au Mwanafunzi
Imam
Sadiq
AS:
"Sipendele kumwona kati yenu ila anakuwa katika hali mbili - Ama awe aalim
(mwalimu/mwanachuoni) au mwanafunzi. Ikiwa hakufanya hivyo atakuwa amepoteza
(amepunguza juhudi), na mwenye kupunguza juhudi
hupoteza, na akipoteza hupata dhambi, na akipata dhambi huingia Motoni. Naapa kwa yule aliyemtuma Muhammad kwa haki." (k.j.,
uk. 197)
Barobaro
Huisumbua Nafsi
Imam Ali AS:
"Asiyeisumbua nafsi yake udogoni (kwa kujielimisha) hatokuwa mwerevu
ukubwani.” (k.j., uk. 278)
Ni Nzuri Zaidi
Wakati wa Ujana
Mtume Mtukufu SAW:
"Kutubu ni kuzuri, lakini kwa barobaro ni kuzuri zaidi."
(k.j., uk. 297)
Nani Atambuaye
Ubora wa Ubarobaro
Imam Ali AS: "Hajui ubora wa vitu viwili ila mwenye kuvikosa -
ubarobaro na afya." (Ghurarul Hikom wa Durarul Kalim, uk. 199)
Utaulizwa
Kuhusu Ubarobaro Wako
Mtume Mtukufu SAW: "Hazitanyanyuka nyayo za mja juu ya
sirati siku ya Kiyama hadi aulizwe kuhusu umri wake ameumaliza katika kitu gani
na ubarobaro wake ameuchakaza katika nini?"
(k.j., uk. 7)
Umeupoteza
Wapi Ubarobaro Wako
Imam
Sadiq
AS: "Miongoni mwa mawaidha
aliyotoa Luqmaan kumwambia mwanawe ni:
'Ewe
mwanangu. Jua ya kwamba wewe kesho utakaposimama mbele ya Mwenyezi
Mungu Aliye Mshindi na Mtukufu utaulizwa kuhusu mambo
manne: Ubarobaro wako umekwisha katika nini?
Umri wako umeumaliza katika jambo gani?
Mali yako
umeichuma kutokana na nini? Na
umeyatumia katika nini?'" (k.j., uk. 8)
Barobaro
katika Kivuli cha Mwenyezi Mungu
Mtume Mtukufu
SAW: "Watu saba Mwenyezi Mungu atawafunika katika
kivuli Chake siku ambayo hakutakuwapo kivuli chochote isipokuwa Chake: Imam
mwadilifu, barobaro aliyekulia katika kumwabudu Mwenyezi Mungu..." (k.j.,
uk. 350)
Barobaro
Mwenye Kutubu
Mtume Mtukufu
SAW: "Hakuna kitu kinachopendwa zaidi na
Mwenyezi Mungu kuliko barobaro mwenye kutubu." (k.j., uk. 350)
Kupatiliza
Kuwaelimisha Vijana
Imam Ja'far Sadiq AS:
"Wapatilizeni vijana wenu kwa kuwafunza hadithi kabla hamjatanguliwa
na wapingamaendeleo." (k.j., uk. 352)
Wapingamaendeleo
Huepukwa na Barobaro
Imam Ja'far Sadiq AS: "Enyi kundi Ia vijana! Mwogopeni Mwenyezi
Mungu wala msiwaendee watawaIa (waovu) waacheni (waepukeni) hadi wawe mikia
(wakose thamani) (k.j., uk. 66)
Mabarobaro
Washikamana na Mtume Mtukufu
Mtume Mtukufu SAW:
"Nawausieni mwafanyieni wema vijana, kwani wana mioyo laini zaidi.
Hakika Mwenyezi Mungu amenituma mimi (niwe) mbashiri
na mhofishaji. Vijana wakaapa kushikana nami na wazee wakanihalifu.
. . Na muda wao (wa kuishi duniani) ukawa mrefu na
nyoyo zao zikasusuwaa." (k.j., uk. 248)
Heshima
Hupatikana kwa Elimu
Imam Ali AS: "Jifunzeni elimu mkiwa vijana mtatukuka
kwayo mtakapokuva wakubwa.” (k.j., uk. 400)
Mkitaka
Kuendelea
Imam Ali AS: "Asiyejifunza ujanani hataendelea
ukubwani." (k.j., uk. 400)
Vijana
Wajifunze Nini?
Imam Ali AS: "Yaliyo bora kwa
vijana kujifunza ni yale mambo watakayoyahitajia watakapokuwa wakubwa."
(k.j., uk. 401)
Onyo Juu ya
Kupotoka Barobaro
Mtume Mtukufu SAW: "Mtakuwaje watakapoharibika wake
zenu na vijana wenu kuwa mafasiki, na mkaacha kuamrisha mema na mkaacha
kukataza maovu?" (Tuhaful 'Uquul, uk. 41)
Kutoa Miongozo kwa Vijana
Amirul Mu'miniyn AS amemwusia mwanawe
Hasan
AS
hivi: “Hakika moyo wa kijana ni mfano wa ardhi ambayo haina kitu (mimea) na chochote
kinachopandwa ndani yake hukikubali (hustawi). Kwa hivyo, nimekupatiliza kukufunza
adabu kabla moyo wako haujawa mwovu na kabla bongo
lako halijashughulika, ili uweze kupokea kwa juhudi za rai yako lile jambo
ambalo wamekutosheleza nalo kulitaka na kulijaribu wenye majaribio. Utakuwa
umetoshelezwa taabu ya kutafuta na kuyajaribu
majaribio. Yakakujia kutokana na hayo ambayo tulikuwa
tukiyaendea na yakakubainikia kutokana na hayo ambayo huenda
hayakutufungukia." (k.j., uk. 53)
Ubarobaro
Huenda Ukawa ni Ulevi
Amirul Mu'miniyn AS:
"Ulevi ni wa aina nne: Ulevi wa ubarobaro,
ulevi wa
mali,
ulevi wa usingizi, na ulevi wa ufalme." (k.j., uk. 88)
Hatari ya
Kutekwa Vijana
No comments:
Post a Comment