Warembo
wa Miss Universe Tanzania 2014 wameanza rasmi kambi katika hoteli yenye
hadhi ya kipekee Golden Tulip Hotel. Hii ni kwa ajili ya kujiandaa na
fainali ya Miss Universe Tanzania 2014 itakayofanyika tarehe 02 mwezi
Octoba.
Miss
Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa
warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake. Mafunzo hayo
yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika Nyanja tofauti.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ndio Mkurugenzi na
Muandaaji mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai
amesema usaili wa mwaka huu umefanyika katika mikoa mitano ya Tanzania
na warembo zaidi ya 70 walisajiliwa kwa mashindano haya.(T.K)
Kambi ya
Miss Universe Tanzania 2014 imekamilishwa na warembo 12 kutoka mikoa
mitano ya Tanzania ambayo ni Arusha , Mwanza, Mbeya, Iringa na Dar es
Salaam, pamoja na mrembo mmoja kutoka Zanzibar.
"Tumechagua
warembo ambao wameonyesha uwezo wa kujitambua na kuelewa umuhimu wa
kushiriki katika mashindano makubwa kama haya. Tuna wanafunzi wa vyuo
wanaosomea udaktari, uhandisi,uhasibu na pia tuna akina dada
wajasiriamali . Tunafurahi kuona kila mwaka warembo wetu wanazidi
kujitambua na kazi yetu kubwa ni kuwaendeleza" alisema Sarungi
Pamoja na
zawadi ya fedha taslimu, mshindi wa Miss Universe Tanzania 2014 atapata
fursa ya kutangaza bidhaa mbalimbali na kufanya kazi za kijamii. Pia
kama ilivyo ada kwa mwaka wa 4 sasa, mshindi atapewa nafasi
(scholarship) ya kusoma New York Film Academy , Marekani. Hivi sasa
washindi wa mwaka 2011 na 2012, Nelly Kamwelu na Winfrida Dominique wako
New York masomoni.
Mashindano
ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake
wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa
Taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa
kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania
iliwakilishwa na Amanda Ole Sulul,2009 Illuminata James ,2010 Hellen
Dausen , 2011 Nelly Kamwelu, 2012 Winfrida Dominique,2013 Betty Boniface
ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.
Mashindano
ya Miss Universe Tanzania yamedhaniwa na Insignia, MeryLight , Golden
Tulip, Compass Communications, AzH Photography, Adams Digicom, Opulence,
Missie Popular blog, Seif Kabelele blog, Urban Rose Hotel, RichBoys
Entertainment (TZ) Ltd na New York Film Academy.
No comments:
Post a Comment