Mkurugenzi mtendaji wa Miale sanaa Group Bw Nurdin Khamis akihojiwa
Na MatukiodaimaBlog
WASANII wasanii wa Miaele sanaa Group wa mjini Iringa mkoani Iringa waanza kutembeza bakuli kuomba kuchangia kiasi cha Tsh milioni 3 kwa ajili ya kukamilisha uzinduzi wa filamu yao mpya ya 990 wamekufa .
Akizungumza na mtandao wa matukiodaima.co.tz mkurugenzi mtendaji wa kundi hilo Nurdini Khamis alisema kuwa kundi hilo limeendelea kufanya vema katika tasnia ya filamu nchini kutokana na wasanii wake kuifanya kazi hiyo kwa kutumia vipaji halisi vya kuzaliwa na hivyo kuwa tofauti na wasanii wengine ambao wamekuwa wakiifanya kazi hiyo kwa kutegemea elimu ya vyuo vya sanaa.
Alisema kuwa kuanzishwa kwa kundi hilo ni jitihada zake binafsi baada ya kuona mkoa wa Iringa una wasanii wenye uwezo wa kuigiza ila hakuna sehemu ya kuonyesha vipaji vyao na ndipo alipoanzisha kundi hilo mwaka 2009 kwa kuwa na wasanii 30 kabla ya kufanyiwa mchujo .
Khamis alisema kuwa mara baada ya mazoezi makali zaidi wale ambao walifanyiwa mchujo waliweza kuonyesha uwezo mkubwa katika uigizaji na hivyo kulazimika kutoa kazi yao ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Zero Done kwa kuwashirikisha wasanii wakubwa nchini kama Senga , Mwamba , Mzee Pembe , Patcho ,Halima Madiwa , Rado na wengine wengi wenye majina makubwa kazi ambayo ilisambazwa nchi nzima na kuonyesha kupendwa zaidi.
Aidha alisema kutoka na ukata wa fedha wameendelea kufanya kazi hiyo kwa kusua sua japo kwa sasa wanataraji kuibuka na filamu kali kuliko ya 990 wamekufa ambayo inategemewa kuzinduliwa wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya maandalizi kukamilika.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kutokanana na uwezo mdogo wa kipato na aina ya wasanii wanaounda kundi hilo kutokuwa na kazi za kufanya kundi hilo limeendelea kuwa tegemezi zaidi kwa kufanya kazi kwa migongo ya wafadhili mbali mbali na kuwa hata filamu hiyo iliyopo jikoni inategemea kuzinduliwa kwa ufadhili wa kamanda wa UVCCM mkoa Salim Asas , Jackson Kiswaga ambae ni mkazi wa Iringa na mdau wa sanaa katika mkoa wa Iringa aliyechangia kiasi cha Tsh 500,000
Pamoja na kuwashukuru wadau mbali mbali kwa kuendelea kujitolea kusaidia ukuaji wa tasnia ya sanaa katika mkoa wa Iringa bado alisema kuwa ni mategemeo yao kuwa wadau hao wataendelea kutoa ushirikiano zaidi kwao ili kufanikisha kuutangaza zaidi mkoa wa Iringa kisanaa kutokana na uwezo mkubwa wa wasanii wanaounda kundi hilo .
Kwani alisema mipango ya mbeleni kwa kupitia kundi hilo kuanzisha utaratibu wa kutengeneza filamu za kuelimisha jamii juu ya masuala mbali mbali ya kimaendeleo katika mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kulinda hifadhi zetu kutoingiliwa na majangili .
Hivyo aliomba wale wote wenye mapenzi ya dhati na kundi hilo kujitokeza kuchangia chochote kwa kupitia huduma ya M- Pesa kwa namba 0757 698 582 kwa madai kuwa bila kusaidiwa na wadau mbali mbali uwezo wao ni mdogo zaidi kiuchumi ila kisanaa wapo juu ukilinganisha na makundi mengine makubwa nchini.
” Uwezo wa kucheza filamu zenye ubora tunao na ndio maana vituo mbali mbali vikubwa vya runinga ikiwemo Zuku swahili wamekuwa wakirusha kazi zetu baada ya kuona ni bora zaidi”
No comments:
Post a Comment