Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, November 17, 2014

JK AKUTANA NA JAJI MKUU WA TANZANIA NA UJUMBE WAKE WALIOMTEMBELEA KUMJULIA HALI MAREKANI


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu waTanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake walipomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  

Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Mhe Hussein Katanga.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume. Kushoto ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete. 
 Rais Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG