Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, November 15, 2014

Kijana Sande Mwenye Uzito wa kilo 250 ashindwa kwenda kupatiwa Matibabu Nchini India kwa Kukosa nafasi Kwenye Ndege.


Kijana Sande Mrema Mwenye tatizo la uzito wa kilo 250 na umri wa maiaka 25 ameshindwa kusafiri kwenda nchini india katika matibabu yake baada ya kushushwa mara kadhaa kwenye ndege za kimataifa anazotakiwa kusafiria licha ya ndugu zake kulipa Gharama zote za usafiri wake.
Akizungumza kwa Masikitiko eneo la karakana katika moja ya Hoteli anapoishi kwa sasa wakati akisubiri miujiza ya kupatikana kwa Ndege Bwana Sande Mrema aliyehitaji waandishi kumfunika uso wakati wa mahojiano amesema anateseka sana na uzito wake unazidi kuongezeka siku hadi siku lakini hajafanikiwa kusafiri.
 
Dada wa mgonjwa huyo anaeleza namna ambavyo wameteseka kumuhudumia ndugu yao mapaka sasa na Kuomba serikali kuingilia kati kufanyanikisha safari ya ndugu yao kwani ameshawasiliana na Daktari wake na malipo wameshafanya ila tatizo ni kupatikana kwa nafasi katika Ndege.
 
Licha ya ITV kujaribu kutafuta wahusika wa Ndege hizo na kushindikana kwa leo,mama mdogo wa kijana huyu anaelezea ndege walizolipia na kushindikana hivyo kuomba waziri wa afya na ustawi wa jamii,waziri wa uchukuzi na viongozi wengine kuwasaidia ili nafasi ya kusafiri kupatikana.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG