Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, November 21, 2014

Kiwanda cha Mtibwa na msimamo wake kwa wakulima


mwenyekiti wa Tucoprocos L.TD
UONGOZI wa Kiwanda cha sukari cha Mtibwa, kilichopoTuriani wilayani Mvomero, umekataa mapendekezo yaliyotolewa na wakulima wa nje wa miwa ya kutaka bei ya ununuzi wa miwa iongezwe katika msimu wa kilimo wa 2010/2011 hadi kufikia shilingi 50,899 kutoka shilingi 39,978.53 ya sasa.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha msingi cha wakulima wa Miwa na Mazao mengine Tarafa ya Turiani (TUCOPRCOS L.T.D) Lucas Mwakambaya,alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho, kwenye mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika ukumbi wa Community Centre wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Alisema uongozi huo ulikataa mapendekezo hayo ya wakulima ya kutaka aongeze bei katika ununuzi wa muwa na baada ya majadiliano ya muda mrefu, alikubali kuongeza shilingi 2000 kwa tani moja katika bei hiyo ya sasa ya shilingi 39,978.53 katika msimu wa mwaka 2010/2011.
Alibainisha kuwa kutokana na makubaliano hayo, mwekezaji huyo amekubali kulipa shilingi 42,000 kwa msimu huu wa kilimo, ingawa malipo hayo bado ni ya hasara, kwani utafiti walioufanya kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria wa chama cha ushirika nchini,(TFC),  umebaini mkulima amekuwa akitumia shilingi 43,000 hadi kuufikisha muwa kiwandani kwa kilimo cha kisasa.
“Mwekezaji pia amekubali kuongeza shilingi  1, 000 kwa msimu uliopita wa 2009/2010 katika bei hiyo ya shilingi 39,978.53  na ameahidi kutoa mbegu kwa wakulima wa miwa ili kufufua upya mashamba yaliyokufa,lakini pia tumehoji kuhusu bei hii kudumu kwa miaka miwili mfulululizo sasa”Alisema Mwenyekiti huyo.
Mwakambaya alisema katika msimu wa mwaka 2010/2011 jumla ya tani 2000 za miwa zilivunwa na kupotelea kiwandani na kwamba zaidi ya asilimia 50 ya mashamba ya miwa yaliyopo wilayani humo yamekufa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo hasara ambayo amekuwa akiipata mkulima katika uzalishaji na miwa mingi imeendelea kushindwa kuvunwa hasa katika msimu uliopita.
Hata hivyo alisema hivi sasa wanaendelea na mazungumzo na benki ya NMB ili wapate mkopo kwaajili ya kufufua mashamba ya wakulima wa miwa yaliyokufa, ili waweze kuzalisha tena miwa kwa faida na tija
Kwa upande wao wanachama hao katika Mkutano huo,walihoji  mbegu za miwa inayozalishwa Turiani iwapo kama zinatofautiana na unaozalishwa wilayani Kilombero, ambapo Mwekezaji wa Kiwanda huko amekuwa akinunua muwa kwa wakulima hadi shilingi 60,000 kwa tani moja.
Wakulima hao pamoja na kuikataa bei hiyo na kusababisha malumbalo yaliyodumu kwa saa kadhaa, baadaye waliridhia na kuuagiza Uongozi wa chama hicho kushirikiana na Serikali ili kuendelea kufanya mazungumzo na mwekezaji huyo na kuhakikisha msimu ujao wa kilimo wa 2011/2012, bei ya miwa inaongezeka.
Mapema akifungua mkutano huo, Mkuu wa wilaya ya Mvomero Bi Fatma Mwasa, alisema tayari Serikali imewasiliana na Mwekezaji wa mtibwa ili miwa ya wakulima inunuliwe kwa kiwango kimoja na bei moja kwani kununua kwa kuzingatia vigezo vya utamu wa sukari iliyomo kwenye miwa (rendement)  kumekuwa kukisababisha wakulima kuchoma ovyo mashamba ili kulazimisha miwa yao ivunwe kwa haraka badala ya kuchelewa na kuiuza kwa hasara kwa mwekezaji.
Aliwashauri wakulima kuangalia mazao mbadala ya kulima badala ya kuendelea kutegemea miwa ambayo kila mara wamekuwa wakilalamikia hasara, ikiwemo alizeti na mpunga ili kupata kipato cha haraka bila kumtegemea mwekezaji mmoja.
Mwasa aliwaahidi kuwatafutia watafiti wa kilimo ili kuangalia iwapo maeneo hayo yatastawi mazao waliyochagua na kuweza kushiriki moja kwa moja katika mkakati wa kitaifa wa kuufanya Mkoa wa Morogoro kuwa ghala la taifa la Chakula.
“Sijawahi kufarijika ninapoongea na wakulima wa miwa, kila mara kumekuwa na malalamiko na manung’uniko kwenye zao hili, inaonekana mambo sio shwari kwa wakulima wa miwa wa hapa Turiani, na sio nia yangu kuua zao hilo, nia yangu ni kuona namna wananchi watakavyoweza kuibuka kiuchumi kupitia zao jingine mbadala litakaloleta ushindani katika kilimo cha miwa”Aliongeza Mwas
a

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG