Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Tuesday, November 11, 2014

LILIAN KAMAZIMA MISS TANZANIA 2014 BAADA YA SITTI MTEMVU KUJIUZURU NA KUVUA TAJI

2Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu  aliyekua Miss Tanzania 2014 baada ya kuzuka Sintofahamu kuhusu Umri wake, Lundenga amesema Sitti Mtemvu aliandika barua ya kujivua taji na kuiwasilisha kwa kamati ya Miss Tanzania Novemba 5 2014 ambapo kamati hiyo imeridhia kujiuzuru kwake na kumvua taji , Hivyo taji hili na majukumu ya Miss Tanzania sasa yatachukuliwa na mshindi wa pili Lilian Kamazima aliyekaa kushoto katika picha   ambaye taratibu za Miss Tanzania zinamruhusu kuchukua jukumu hilo, Hashim Lundenga ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam leo(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)3Mii Tanzania 2014  Lilian Kamazima  akizungumza na waandishi wa habari kuelezea furaha yake baada ya kamati ya Miss Tanzania kumvisha taji hilo kutokana na kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekuwa Miss Tanzania, Kulia ni Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania.1Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania akionyesha barua iliyowasilishwa kwa kamati hiyo na Bi. Sitti Mtemvu mara baada ya kujiuzuru Umiss Tanzania na kujivua taji hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG