Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, November 28, 2014

Maelfu ya dola kuikarabati Brisbane

mwenzako
Brisbane mvua yahanikiza
Mji wa Brisbane nchini Australia umekumbwa na dhoruba mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.mji huo ulipigwa na mawimbi makubwa na upepo mkali wenye nguvu ya kilomita mia moja na arobaini kwa saa.
Kimbunga hicho nyenye nguvu nyingi kimeezua mapaa ya nyumba kadhaa,kuvunja madirisha,matofari yalionekana yakinyanyuliwa na kutupwa na kusababisha nyumba takriban elfu sabini kukosa nishati ,ni mwezi mmoja sasa mvua nyingi zinaendelea kunyesha kila siku kwa nusu saa na hivyo magari yanaonekana yakielea kwenye mitaa iliyofurika.
Jeshi nchini humo limeombwa kusaidia kusafisha miji ili kurejea katika hali yake ya kawaida,nayo serikali ya Queensland imekadiria gharama za ukarabati ujao kwamba huenda ukagharimu mamilioni ya dola za kimarekani.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG