Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, November 5, 2014

Makanisa ya Kikristo ya Mungu
[297]


Ufafanuzi wa Kitabu Cha Zekaria
(Toleo La  2.0 20060820-20120114)

Kitabu cha Nabii Zekaria ni cha muhimu sana ili kujua fundisho la Marejesho Mapya au Kufanywa Upya kwa taifa la Israeli kutakakofanywa na Masihi katika Siku za Mwisho. Angalia pia Sehemu ya II ihusuyo hatima ya Israeli na Yuda itakavyokuwa katika Siku za Mwisho kwenye maandiko ya Zekaria na kwenye Agano Jipya.




Christian Churches of God

PO Box 369,  WODEN  ACT 2606,  AUSTRALIA


Email: secretary@ccg.org


 (Sheria ya Haki Miliki © 2006, 2012 Wade Cox)
(tr. 2012)

Masomo yaliyo kwenye jarida hili yanaruhusiwa kunukuliwa na kuwapa watu bure bila kulipishwa kitu, ikiwa tu kama yatanukuliwa kikamilifu bila kubadilisha au kufuta maneno. Jina la mchapishaji na anuani yake pamoja na tangazo la haki miliki ni lazima viwekwe pia. Hakuna malipo atakayotakiwa mpokeaji kutoa au kuchangia kununua jarida hili au nakala yoyote atakayopewa. Nukuu fupi zilizolazima zaweza kuwekwa kutoka kokote iwapo zitaonekana zitakithi haja ya lugha husika lakini pasipo kukuka maadili ya ya sheria ya haki miliki..

Jarida hili linapatikana Ulimwenguni kote kwenye wavuti yetu ya:http://www.logon.org au http://www.ccg.org

Ufafanuzi wa Kitabu cha Zekaria


Utangulizi
Nabii Zekaria (maana ya jina lake ni Aliyekumbukwa na Yahova) alikuwa mwana wa Berekia (Aliyebarikiwa na Yahova) na ni mjukuu wa Ido.

Alitoa unabii wake kipindi cha utawala wa Dario Mwajemi au pia anaitwa Dario II wa Uajemi wakati wa ujenzi wa Hekalu. Unabii alioutoa katika kipindi chote cha tangia ujenzi wa Hekalu la Pili hadi kukamilika kwake kulikofanywa kwa kulipaka rangi na kulipamba na aliendelea kutabiri hali itakavyokuwa tangia hapo hadi kuteketezwa kwa Hekalu hili. Kwa hiyo, unabii wake unaendelea hadi kufikia kipindi cha Masihi na ujenzi wa Kanisa la Mungu, ambalo ni Hekalu la Kiroho, na aliendelea kuyataja mambo yatakavyokuwa hadi kipindi cha kurudi kwake huyo Masihi. Pia inahusika na matengenezo ya mfumo wa uongozi utakavyokuwa mjini Yerusalemu katika kipindi cha utawala wa Milenia wa Masihi. Ni kazi ya muhimu sana katika Siku za Mwisho na kwa mataifa yatakayoishambulia Yuda.

Mpangilio wa kitabu umegawanyika kwenye vipengele vifuatavyo:
Sehemu ya 1    A. 1:1-6 Unabii alioutoa katika Mwaka wa 2 wa Dario
B. 1:7-6:15 Unabii Kwa Njia ya Alama za Maono (Maono ya mambo Saba)           
C. 7:1-8:23 Unabii wa tangia Mwaka wa 4 wa Dario
Sehemu ya 2    A. 9:1-10:12 Mzigo wa Kwanza Unafumbuliwa
B. 11:1-17 Unabii kwa njia ya Alama au Ufunuo
C. 12:1-14:21 Mzigo wa Pili Unafumbuliwa

Kipindi cha Dario na Manabii
Inadhaniwa kuwa Dari II alitawazwa kuwa mfalme kwenye kipindi cha miaka ya 424 au mapema 423KK. Tangazo la kuanza ujenzi wa Hekalu alilifanya mwaka 422KK (Ezra 6:1 na 4:24) (huenda ulikuwa ni mwaka wake wa pili wa utawala wake). Majuma 70 ya miaka yalitangulia kabla ya kufika siku hii. Kwa mujibu wa Ezra sura ya 5, inaonekana kuwa manabii Hagai na Zekaria walitabiri kwenye miaka ya 423KK na 422KK. Majuma 70 ya miaka ilitangila na kupita tangu mwaka 423/22KK (ambacho ni kipindi cha mwaka wa kwanza wa Yubile mpya). Ujenzi huu wa Hekalu ulikamilika katika mwaka was ita wa utawala wa Dario Mwajemi (Ezra 6:15) siku ya 3 Adari sawa na Machi ya mwaka 418KK. Dario alikufa katika kipindi cha mwishoni mwa mwaka 405 katika kipindi cha majira ya baridi ya mwaka 404 (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)]: Kwa jinsi hii twaweza kusema kuwa kazi ya upangaji wa miaka aliyoifanya Bullinger imekosewa kwa jinsi inavyofanana na nyongeza ya maandiko iliyowekwa.

Kwa hiyo, unabii huu unatuama kwenye kipindi cha ujenzi wa Hekalu na unafanya kuwa ni sehemu muhimu ya dhana ya Ufunguo wa Daudi iliyo kweny maelezo ya unabii huu na maongozi yanayotupeleka kwenye Siku za Mwisho na majenzi mapya ya mwisho ya Hekalu (soma jarida la Sheria za Wafalme: Sehemu ya II; Sulemani na Ufunguo wa Daudi (Na. 282C) [Rule of the Kings: Part III: Solomon and the Key of David (No. 282C)].

Sehemu ya kwanza inaonyesha mwanzoni mwa ujenzi na inaishia mwaka wa 2 wa ujenzi huu na kuachia njiani mwa tukio hili. Sehemu ya pili inaonyesha sehemu ya pili ya ujenzi huu. Kwa hiyo, kila sehemu inajiri kipindi cha miaka miwili kati ya mine iliyotumika kwa ujenzi huu na kwenye unabii imetajwa kuwa ni kipindi cha marejesho ya taifa la Israeli a Yuda wakati wa utawala wa Msihi, na kanisa lililotajwa hapa kwenye maandiko ni lile litakalotawala na Masihi kipindi hiki cha Milenia huko mjini Yerusalemu.

Kwenye unabii wake Hagai anahusisha kipindi hiki kama tulivyojionea.

Ezra na Nehemia walikuwa hawajarudi bado, jambo walilolifanya kwenye siku za utawala wa Artashasta II mwishoni mwa kipindi cha majuma saba ya miaka. Artashasta II ndiye aliyetoa tangazo la kwa ajili ya Hekalu na Nehemia akalijenga. Ezra alifariki mwaka 323KK ambao pia ni mwaka aliokufa Iskanda Mkuu (Alexander the Great). Mkakati wa kuyachunguza maandiko maarufu kama “canon” uliafanywa mwaka 321 na hatimaye ulitangazwa kusitishwa.

Zekaria, sura ya 1
Sura ya 1 inahusika na kuanzishwa kwa huduna ya kinabii na kipindi tajwa ambacho mji ungefanyiwa marejesho lakini ukiwa hauna amani, na kwahiyo Hekalu lisingeweza kujengwa. Mungu aliwakasirikia Yuda kwa kuwa hawakuwafundisha kanuni zake na Amri za Mungu vizuri, na pia hawakuzitenda. Dunia ilikuwa na amani lakini Nyumba ya Yuda hawakuwa na mapumziko ya amani kwa muda wa miaka saba. Mungu hakupendezwa na mataifa wasiyo Waisraeli pia ambayo walijihisi kuwa wako salama. Ni kama tunavyojionea kwenye maandiko, alikuwa amewakasirikia kidogo bali walijiongezea hasira yake jambo lililopelekea wakutane na hukumu kali na mateso, mambo ambayo Mungu hakuwaambia wafanye. Kisha zile pembe nne zilizofanya hila ya kuwatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu zilishughulikiwa, na mafundi seremala wanne ambao ni watumishi wa Mungu walikuja kuwatawanya waende kwenye zile pembe nne zilizofanya hila ya kuwatawanya na kuwagawa Yuda.

Jina hili la Bwana wa Majeshi au Yahova Sabaioti limeandikwa mara hamsini na tatu kwenye kitabu hiki: mara arobaini na nne kwenye sura ya 1 hadi 8 na mara tisa kwenye sura za 9 hadi 14. Mara zote ishirini na tisa zilizoandikwa imehusianishwa na maneno yenye msisitizo ya Yahova Sabaioti pale inaposema “Asema Bwana wa Majeshi” ni sawa na kusema kwamba maneno haya yamesemwa na kuthibitishwa Yahova Sabaioti. Usemi wa “Asema Bwana” unamaana sawa na kusema “Haya ni Maneno yaliyothibitishwa na Yahova” au Matamshi ya Yahova.

Mpangilio wa jinsi maono aliyoyaona mara nane hadi kwenye Zekaria 6:15 yanaonyesha mambo yafuatayo:
Maono ya 1 (Zekaria 1:7-17) Jeshi Lisiloonekana na Farasi Mweusi.
Maono ya 2 (Zekaria 1:18-21) Maadui wa Nje au Pembe Nne
Maono ya 3 (Zekaria 2:1-13) Kusudi la Yahova kwa mwanadamu linaonyeshwa.
Maono ya 4 (Zekaria 3:1-10) Kuonekana kwa Yoshua ambaye ni Chipukizi.
Maono ya 5 (Zekaria 4:1-14) Mpango wa Yahova unaonekana kwenye Kinara cha Taa
Manono ya 6 na 7 (Zekaria 5:1-4, 11) Maadui wa Nje, Gombo Lirukalo na Efa
Maono ya 8 (Zekaria 6:1-6) Magari ya Vita, Farasi
Kwa kuhitimisha, (Zekaria 6:9-15): Inaishia kwa kumfananisha Yoshua ambaye ni Chipukizi.

Mpangilio uliowekwa ni ule wa Israeli na mtawanyiko wao. Wamataifa wanakuwa ni milki ya Israeli kwenye kipindi hiki cha mwisho Yahova anatangaza nia yake ya kuingilia kati mambo yalivyo mjini Yerusalemu (aya za 16,17; Isa. 40:1-5). Mtu aliye kwenye sura ya 1 ni Adonai wa aya ya 9 na ni Malaika wa Yahova kwenye aya za 11,12 na tunaona jinsi nabii alivyoambiwa kwenye jibu lake. Wale wapanda farasi wote wanayeoonekana kwenye aya ya 8 wanatoa habari zao kwa kiumbe hiki ambaye ni Adonai wa Israeli anayetajwa kwenye Kumbukumbu la Torati 32:8. Neno “miongoni” linahusiana na sura ya 6:1.

Zekaria 1:1-21 inasema: 1Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Iddo, kusema: 2“BWANA aliwakasirikia sana baba zako wa zamani. 3Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyo BWANA Mwenye Nguvu asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘Nami nitawarudia ninyi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 4Msiwe kamababa zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyo BWANA Mwenye Nguvu asemavyo: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema BWANA. 5Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele? 6Je, maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata baba zenu?’’ “Kisha walitubu na kusema,BWANA Mwenye Nguvu ametutenda sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia kufanya.’

Miezi mitatu baadae sehemu ya kwanza iliisha.
7Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja,yaani mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa kutawala kwake mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Iddo.8Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe. 9Nikauliza, ‘‘Hivi ni vitu gani bwana wangu?’’ Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi akanijibu, ‘‘Nitakuonyesha kuwa ni nini.’’ 10Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, ‘‘Ni wale ambao BWANA amewatuma waende duniani kote.’’ 11Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa BWANA, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, ‘‘Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani.’’ 12Kisha malaika wa BWANA akasema, ‘‘BWANA Mwenye Nguvu, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?’’

Sehemu ya pili inaonyesha kipindi cha taabu. Pia inaonyesha kurejea kwenye sura ya 7:9; Zaburi102:13; Isaya 14:1; 49:13. maandiko haya hayalihusu Kanisa ambalo ni mama yetu sote, bali zinauhusu mji wa Yeruralemu wenyewe.
13Kwa hiyo BWANA akazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami. 14Kisha malaika yule aliyekuwa akizungumza nami akasema, ‘‘Tangaza neno hili: Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu asemalo: ‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni, 15lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.

Kwahiyo, Mungu anawashughulikia Yuda, lakini mataifa yaliyoongeza maumivu wakati walikuwa hawana la kufanya na hivyo walimchukiza Mungu na atawashughulikia.

Sehemu hii ilikuwa inatazama mbele kwenye mtawanyiko mwingine. Hapa anaongelea kuhusu nyumba yake inayojengwa juu yake, ambayo kwa sasa inaendelea kujengwa. Hata hivyo, tutajionea jinsi unabii huu unavyoendelea hadi kwenye kipindi cha milenia moja na nusu na kinaendelea hadi kwenye vipindi viwili vya kuja kwake Masihi na hadi alipokufa.

Mji wa Yerusalemu utapimwa kwa nia ya kuweka tena utaratibu ufaao kwenye jingo hili. Tendo hili litafuatiwa na Upimaji wa Hekalu ambalo ni Kanisa tuliloliona kwenye Ufunuo 11:2.
 
16‘‘Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo BWANA: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 17“Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Miji yangu itafurika tena usitawi na BWANA atamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’’’ 18Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne! 19Nikamwuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hivi?’’ Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.’’ 20Kisha BWANA akanionyesha mafundi wanne. 21Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?’’ Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.’’

Hapa Mungu anaonyesha kwamba atashughulikia pembe hizi au mamlaka ya wale wote waliowaumiza na kuwatesa Yuda na Israeli na Yerusalemu. Hii haina uhusiano wowote na Kanisa (kamaanavyosema Bullinger, kwenye ufafanuzi wake wa Biblia iitwayo Companion Bible anapoitafsiri aya 16). Mamlaka hizi nne yanajichomoza ili kuyapiga vita mataifa yatakayoishughulikia, kwa nia ya kuyafanyia vitisho.

Zekaria, sura ya 2
Sura hii ya 2 inaonyesha kuwa Yuda wataongezeka na Mungu atakuwa ni ukuta wa moto utakaowazunguka na na utukufu wake utakuwa katikati yao. Andiko hili linaonysha kwamba Mungu, yaani Yahova, Bwana wa Majeshi, alimtuma Yahova ambaye ni Mungu wa Israeli aende mjini Yerusalemu ili akaulinde (Zekaria 2:8). Mataifa mengi yatajiunga na Bwana katika siku ile na watakuwa watu wake Mungu na Yahova atakuwa kati yao. Mungu ataimiliki Yuda, ambayo ni milki yake kwenye Nchi Takatifu na ataupenda na kuuchagua tena Yerusalemu (kana isemavyo Kumbukumbu la Torati 32:8).
Zekaria 2:1-13 inasema: Kisha nikatazama juu, pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake! 2Nikamwuliza, “Unakwenda wapi?’’ Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.’’ 3Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye 4na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo. 5Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema BWANA, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’ 6“Njoni! Njoni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kaskazini,’’ asema BWANA, “Kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,’’ asema BWANA. 7“Njoo, Ee Sayuni! Kimbia, wewe uishiye ndani ya Binti Babeli!’’ 8Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka wewe nyara, kwa kuwa ye yote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake, 9hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtakapojua ya kwamba BWANA Mwenye Nguvu amenituma. 10“Piga kelele na ufurahie, Ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu,’’ asema BWANA.

Kumbuka hapa kwamba Yahova ambaye ni Bwana wa Majeshi atakuwa anaishi Yerusalemu. Anasema kwamba hatimaye tutajua kwamba Bwana wa Majeshi amemtuma. Kwa maneno mengineni kusema kwamba huyu Yahova sio huyu Yahova ambaye ni Bwana wa Majeshi asemwaye kwenye Zaburi 45:6-7 na Waebrania 1:8-9 aliyetumwa na Mungu kwa Israeli. Bali ni Yahova aliyepewa Israeli kuwa ni urithi wake kama isemavyo Kumbukumbu la torati 32:8 (pia soma Biblia ya RSV ili kupata maana halisi). Maneno yasemayo “mboni ya jicho langu” yalibadilisha nakusomeka “jicho lake” kazi ambyo ilifanywa na Wasoferim waliodai ni kwa sababu za kielimu ya kianthropolojia. Yahova ambaye ni Bwana wa Majeshi alimtuma huyu Yahova kwa “Utukufu wake Mwenyewe”.

Maonyo yametolewa dhidi ya wale wote wanaoishi na kumrithia binti wa Babeli wakiepuka kutoka pande ya Kaskazini. Zekaria anaongelea mambo yatakayotokea siku za baadae sana. Babeli itakuwa imeshaanguka tayari kipindi hiki na ni somo kwa dola za Wamedi na Waajemi na imekuwa hivyo kwa karne sasa. Anaongelea kuhusu Siku za Mwisho na binti Babeli anatajwa pia kwenye sehemu nyingine na Kanisa.

Tunajua kuwa hiki ni kitu muhimu kwa kuwa ni unabii na kisha inatangaza umoja wa mataifa mengi na hata Yuda, mambo ambayo hayajatokea bado hata kwa matukio ya kwanza. Anasema kuwa atakaa kati yao nao watajua kwamba Bwana wa Majeshi amemtuma yeye kwao. Mtu huyu anaweza kuwa ni Yesu Kristo atakayekaa kati yao hapo ajapo tena.
11“Mataifa mengi yataunganishwa na BWANA siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwamba BWANA Mwenye Nguvu amenituma kwenu. 12BWANA atairithi Yuda kama fungulake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu. 13Tulieni mbele za BWANA, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.”

Kumbuka maelezo yasemayo kuwa ataimiliki Yuda na kuifanya kuwa ni sehemu yake. Israeli ni milki yake lakini Yuda ni kabila la Masihi. Mtu huyu, Yahova wa Israeli, anaweza kuwa ni Yesu tu ambaye ni Kristro na Masihi.

Zekaria, sura ya 3
Kwenye sura ya 3 ya Zekaria, Bwana Mungu anaonyesha jinsi utakavyokuwa mwanzo wa siku za mwisho pamoja na jinsi atakavyokuwa Kuhani Mkuu atakayekuwa anaitwa Yoshua, kama alivyofanya Masihi ambaye alionekana kama Chipikizi. Shetani amekaa mkono wake wa kulia akikusudia kumzuia na sio kumsaidia. Yoshua amepewa mavazi safi na meupe na mavazi yake ya zamani yameondolewa mbali. Wafuasi na ambao pia watumishi wa Kuhani Mkuu walioketi mbele yake ni watu wanaofanya mambo ya kushangaza. Bwana Mungu anasema kwamba atalileta Chipukizi ambaye ni Masihi. Bwana Mungu anasema kwamba jiwe lililowekwa mbele ya Yoshua lina macho saba kwenye jiwe moja hilihili, ambayo inamaanisha pia kwamba kuna macho saba kwenye kila jiwe moja, na tunajua kuwa maandiko yanatuambia kuna roho saba za Mungu ambazo zinawakilisha pia malaika saba wa makanisa saba ya Mungu na kuna vinara vya taa kwenye makanisa haya yote saba.

Ni Mungu ndiye anayeyafanya mawe haya na kuyaweka macho saba, ambayo inamaanisha pia kuwa ni roho saba. Mungu anayaondoa maovu ya nchi kwa siku moja tu. Alifanya hivyo kupitiakwa Masihi na kuweka roho saba kwenye makanisa saba.

Aya ya 10 inasema: ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 

Jambo hili linaashiria kuanzishwa kwa makanisa ka kipindi chote na kutuleta kwenye ile Siku ya Bwana, siku ambayo imetajwa pia kwenye aya ya 10 kama: “Katika siku hiyo”.
Zekaria 3:1-10 inasema: Kisha akanionyesha Yoshua kuhani mkuu akiwa amesimama mbele ya malaika wa BWANA, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshitaki. 2BWANA akamwambia Shetani, “BWANA akukemee Shetani! BWANA, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?’’ 3Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. 4Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, ‘‘Mvueni nguo zake chafu.’’ Kisha akamwambia Yoshua, ‘‘Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.’’ 5Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.’’ Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa BWANA akiwa amesimama karibu. 6Malaika waBWANA akamwamuru Yoshua: 7“Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa. 8‘‘‘Sikiliza, Ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi. 9Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema BWANA Mwenye Nguvu, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.10“‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 

Ni hakika kabisa kwamba Kuhani Mkuu wa Israeli ni lazima aendane kwa mujibu wa Torati ama Sheria za Mungu. Kazi hii ndiyo aliyoitoa Mungu na kumpa Yoshua, aliye Kuhani Mkuu wa Israeli. Na kama hataifuata Torati hii ya Mungu basi hafai kuwa Kuhani Mkuu.

Zekaria, sura ya 4
Sura hii ya 4 inaendelea kwa kuwaelezea Mashahidi wasimamao upande mwingine wa vile vinara saba vya taa vinavyowaka kwenye kinara chake. Kupitia Zekaria, Mungu anasema hivi: “‘Sikwa nguvu, wala si kwa uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu.” Hawa ndio Mashahidi Wawili wanaosimama mbele za Bwana wa dunia nay ale macho saba ni roho saba za Mungu zinzoenda huku na huko duniani kote. Huyu sio Shetani anayetajwa kama “Mungu wa dunia hii” (2Kor. 4:4) bali ni Masihi ambaye atachukua nafasi yake. Hii ndio sura inayoielezeasana Siku ya Bwana na Ushindi wa Mashahidi wake utakavyokuwa kwenye Siku za Mwisho.
Zekaria 4:1-14 inasema:  Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka katika usingizi wake. 2Akaniuliza, “Unaona nini?’’ Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. 3Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.’’ 4Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?’’ 5Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?’’ Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.’’ 6Kisha akaniambia, “Hili ni neno la BWANA kwa Zerubabeli: ‘Si kwa nguvu, wala si kwa uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 7‘‘Wewe ni kitu gani, Ee mlima mkubwa sanaMbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’’ 8Kisha neno la BWANA likanijia: 9‘‘Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa BWANA Mwenye Nguvu amenituma mimi kwenu. 10‘‘Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli. “(Hizi saba ni macho ya BWANA ambayo huzunguka duniani kote.)’’ 11Kisha nikamwuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?” 12Tena nikamwuliza, “Haya matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni nini?’’ 13Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?’’ Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.’’ 14Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.’’

Mashahidi hawa wawili watakuja mwishoni mwa matukio haya na hawajafananishwa na mtu mginine yeyote tangu hapo hadi leo.

Zekaria, sura ya 5
Gombo la Bwana lililoko kwenye Torati ya Mungu, litapeperuka na kuingia kwenye majumba ya wezi na waongo na litatoa ushuhuda dhidi yao na kuwatawanya na kuwakomesha na kuziteketeza nyumba zao kwa mawe na kwa matofali.

Umuhimu wa kuitunza na kuiamini Torati utarejeshwa upya na Mashahidi hawa wa Mungu katika Siku za Mwisho. Sura ya 5 inafuatia moja kwa moja kwenye kipindi kinachowaelezea wao kwenye Sura ya 4 na haiyarudii mambo ya nyuma. Hali hii bado haijafanyika hadi sasa.

Mashahidi hawa wa Bwana waliharibiwa na kufanywa kuwa kama efa isiyofaa na kuwekwa mdomoni mwa mwanamke anayeishi kwa kutenda matendo machafu, na mkate huu wa efa ukachukuliwa na kupelekwa katika nchi ya Shinari, ambayo ndiyo Babeli.

Ndiyo maana ya kutokea kwamba, mfumo wa dini ya uwongo ukapata nafasi ya kuwa msemaji na kutoa unabii wake, na kuchukuliwa kwenye mfumo potofu wa dini ya Babeli na kisha watahukumiwa katika Siku za Mwisho. Hawa ndio wale waantinomia wanaofundisha leo kuwa Torati na Amri zote za Mungu zimeondolewa na hazima umuhimu tena siku hizi.
Zekaria 5:1-11 inasema: Nikatazama tena, mbele yangu kulikuwa na kitabu kilichoruka! 2Akaniuliza, “Unaona nini?’’ Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka chenye, urefu wa dhiraa ishirinia na upana wa dhiraa kumib.’’3Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi atahamishwa, pia kufuatana na yaliyo upande wa pili, kila aapaye kwa uongo atahamishwa. 4BWANA Mwenye Nguvu asema, ‘Nitaituma hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi na nyumba ya huyo aapaye kwa uongo kwa jina langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu, pamoja na mbao zake na mawe yake.’’’ 5Kisha yule malaika aliyekuwa akizungumza nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone ni nini kile kinachojitokeza.’’ 6Nikamwuliza, “Ni kitu gani?’’ Akanijibu, ‘‘Ni kikapu cha kupimia.’’Kisha akaongeza kusema, ‘‘Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.’’ 7Kisha kifuniko kilichotengenezwa kwa madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile kikapu, kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu alikuweko mwanamke ameketi! 8Akasema, ‘‘Huu ni uovu,’’ akamsukumia ndani ya kikapu na kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu. 9Kisha nikatazama juu na mbele yangu, walikuwepo wanawake wawili, wakiwa na upepo katika mabawa yao! Walikuwa na mabawa kama ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka nacho kati ya mbingu na nchi. 10Nikamwuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, ‘‘Wanakipeleka wapi hicho kikapu?’’11Akanijibu, ‘‘Wanakipeleka katika nchi ya Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake. Itakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa pale mahali pake.’’

Zekaria, sura ya 6
Zekaria 6:1-8 inaelezea kiindi ambacho malaika saba wanaotajwa pia kwenye Ufunuo 7:1-3. Malaika hawa wanne wanaonekana wapo kwa pea iliyopanda farasi Mwekundu, Mweusi na Mweupe nay ule wa nne anaonekana amepanda gari lililotengenezwa kwa vitu mchanganyiko wa rangi za Zambarau au Dam una Hudhurungi (iliyonakshiwa kwa kupakwa neno linalotokana na Kifaransa gris au chuma chenye rangi ya hudhurungi).

Yule aliyempanda farasi mweusi anaelekea upande wa kaskazini mwa nchi, na yule mweupe anaelekea magharibi, na yule wa rangi ya hudhurungi au kahawia-kidogo anaelekea kusini mwa nchi, anaenda huku na huko duniani.

Neno la kuisimamisha roho yangu upande wa kaskazini wa nchi linamaanisha “kunikasirisha [kunikasirisha] nisistarehe kwenye roho yangu (kama alivyoandika Bullinger, kwenye Biblia yake maarufu kama Companion Bible). Kwa hiyo, Mungu anataka kuishughulikia Nchi ya Kaskazini. Hekalu la Bwana ni lazima lijengwe na litajengwa na watu watakaotokea nchi ya mbali (kamainavyosema Isaya 60:10) na ni Chipukizi aitwaye Yoshua, Kuhani Mkuu atakayelijenga Hekalu. Kwa hiyo, anatakiwa awe na Masihi aitwaye Yoshua, ambaye maana yake ni wokovu auMwokozi. Hii itakuja kutokea ikiwa tu kama tutakaza mioyo yetu kumsikiliza na kumtii Mungu.
Zekaria 6:1-15 inasema: Nikatazama juu tena, nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba2Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi,3la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu. 4Nikamwuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, ‘‘Hawa ni nani bwana wangu?’’ 5Malaika akanijibu, ‘‘Hizini roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake. 6Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.’’ 7Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, ‘‘Nenda duniani kote!’’ kwa hiyo wakaenda duniani kote.8Kisha akaniita, “Tazama, wale wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya kaskazini.’’ 9Neno la BWANA likanijia kusema: 10‘‘Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania. 11Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadiki. 12Umwambie, hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga hekalu la BWANA. 13Ni yeye atakayejenga hekalu la BWANA, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’ 14Taji itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya hekalu la BWANA. 15Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kwamba BWANA Mwenye Nguvu amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii BWANA, Mungu wenu kwa bidii.’’

Huyu Chipukizi amepewa heshima ya kifalme katika Israeli na kuhani atasimama kwenye kiti chake cha enzi. Kutakuwa na amani kati yao. Unabii huu unahusu siku zijazo kipindi ambacho Chipukizi huyu atajenga Hekalu lake akiwa na heshima ya kifalme na akiwa ni mtawala atawalaye kama kuhani pia, na mtu huyu ni lazima awe Masihi tu. Taji ya kifalme itakuwa kwenye Hekalu la Bwana. Wateule watatawala na Mungu na taji za kifalme watavikwa ili watawale. Hii ndiyo ahadi lililopewa Kanisa la Wafiladelfia kwenye Ufunuo sura ya 3.

Usemi usemao kuchipushwa kwa chipukizi la Yemach ... yizmach ambayo maana yake ni kusema kwamba chipukizi litachipuka. Bullinger anauona ukweli huu pia na kwenye kitabu chake ameruka maandiko fulani alipokuwa anaelezea hili.

Zekaria, sura ya 7
Katika kipindi hiki cha miaka saba Israeli hawakufunga saumu wala kuomboleza kwa ajili ya kutubia matendo yao ya kuenenda kinyume cha Torati ya Mungu. Na kwa mafungo yao ya mwezi wa Tano na Saba hawakufunga saumu ili kumtii Mungu. Kumbuka kwamba saumu ya siku ya 10 ya mwezi wa Abu waliyoifanya ili kuomboleza kwa ajili ya kuteketezwa kwa Hekalu ilianzhishwa katika Yuda kipindi hiki (kama isemavyo Yer. 52:12,13). Neno la Bwana lilikuwa ni kufanya hukumu ya haki na kuonyesha rehema na huruma kwa kila mtu na jirani yake, na kutowadhulumu wajane na kwa yatima waliofiwa na baba zao na kwa mgeni na kwa maskini na kuwaasa kusiwe na mtu miongoni mwao mwenge kumuwazia moyoni mwake mabaya ndugu (Zekaria 7:9-10). Lakini hawakusikia bali wakazifanya shingo zao kuwa ngumu na kuziba masikio yao ili wasisikilize. Waliifanya mioyo yao kuwa migumu kama jiwe, na kama mwamba, ili wasizisikilize Sheria za Mungu na wasiyasikilize maneno ambayo Bwana wa Majeshi aliyoyaleta kwao akiwatumia  manabii zake aliowapeleka kwao hapo kabla. Kwa ajili hiyo hasira kali kutoka kwa Bwana wa Majeshi iliwaangukia (Zekaria 7:11-12).

Mungu anasema kwamba itakuja kutokea kwamba, kwa kuwa wanakaza kuyaziba masikio yao ili wasisikilize Amri za Mungu alizozileta kwao kwa kupitia manabii waliotangulia, basi Mungu naye atafunga masikio yake asiwasikilize,, na Mungu akawatawanya watoke na waende mbali kwenye mataifa yote ya dunia ili ardhi yao ibaki kuwa ukiwa. Na kwa jinsi hiyohiyo ndivyo Mungu atawahukumu wale wote wanokataa kulisikiliza Neno lake yeye ambaye ni Bwana na na Amri za Mungu katika Siku za Mwisho.
Zekaria 7:1-14 inasema: Katika mwaka wa nne wa utawala wa mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu. 2Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regam-meleki pamoja na watu wao, kumsihi BWANA 3kwa kuwauliza makuhani wa nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?” 4Kisha neno la BWANA Mwenye Nguvu likanijia kusema: 5“Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu? 6Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa mnasheherekea kwa ajili ya nafsi zenu? 7Je, haya sio maneno ya BWANA aliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu’’’ 8Neno la BWANA likamjia tena Zekaria: 9“Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. 10Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’ 11“Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogokwa ukaidi na kuziba masikio yao. 12Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayo BWANA Mwenye Nguvu aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyo BWANA Mwenye Nguvu alikasirika sana13‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 14‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ’’

Katika Siku za Mwisho, Mungu atashughulika na mabaki ya Israeli. Unabii huu uko kwenye sehemu ya pili au ya mwisho maono ya sehemu ya kwanza. Inauonyesha mtawanyiko unaofuatia najinsi Yuda utakavyoachwa unaangamia na jinsi Hekalu litakavyoangushwa na kuangamizwa ambalo walikuwa kwenye mchakato wa kulijenga. Jambo la kujifunza hapa lilikuwa ni rahisi sana. Ni kwamba walitakiwa kuzishika tu Amri za Mungu na Agano lake vinginevyo wangechukuliwa tena kutumikia adui zao. Hekalu hili linawahusu wale tu wanaolituza Agano na kuzishika Amri za Mungu.

Zekaria, sura ya 8
Katika sura ya 8 Zekaria anaonyesha jinsi Mungu anavyoharakisha kurejea Sayuni na kuwakusanya watu wake kutoka nchi liyo upande wa mashariki na wa magharibi. Watarudi na kukaa mjini Yerusalemu kwa hali isiyo na hofu na haki. Kabla ya marejesho ya mwisho hakukuwa na amani na Mungu alimfanya kila mmoja wao amchukie jirani yake. Lakini katika Siku za Mwisho ataifanya dunia itoa matunda yake na Mungu atautendea mema mji wa Yerusalemu na Yuda. Pia Mungu ataifanya upya Jerusalemu na Yuda ili wasiwe laana tena kwa mataifa (Zekaria 8:10-15). 

Hivi ndivyo tunavyotakiwa kufanya. Tunatakiwa kusema kweli kwa majirani zetu na kutoa hukumu ya haki na kuwa na amani malangoni mwetu. Tunatakiwa kuwapenda majirani zetu natusifanye viapo vya uwongo. Yuda watakomesha saumu ya mwezi wa Nne (siku ya 9 wakati mji ulipobomolewa); mwezi wa Tano (siku ya 10 Abu, wakati Hekalu na Nyumba zilipochomwa moto); mwezi wa Saba (siku ya 3 mwezi Tishri wakati alipouawa kwa kuchinjwa Gedalia na Ishmaeli mwana wa Nethania (Yer. 40:8; 41:1-3, 15-18) na mwezi wa Kumi (siku ya 10 Tebethi) wakati mfalme wa Babeli alipokuja kuuhusuru yaani kuuteketeza mji wa Yerusalemu (Ezekieli 24:1-2)) (Zekaria 8:19). Hizi ni saumu zilizotungwa tu na wanadamu na sio saumu alizoziamuru Bwana Mungu.

Katika siku hizo, kipindi cha mwisho kabisa cha zama hizi, watu watashika upindo wa yeye aliye Myahudi anayetoka mbali na taifa na lugha yao, kutoka nchi ya mbali ya dunia nao watakuja Yerusalemu ili kuomba kwa Bwana wa Majeshi (kama ilivyoandikwa kwenye Mwanzo 26:28; Isaya 2:3; Mika 4:2). Watu wa Mungu, (yaani Israeli) watarejeshwa na kufanywa upya.
Zekaria 8:1-23 inasema: Neno la BWANA Mwenye Nguvu likanijia tena. 2Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.” 3Hiii ndilo asemalo BWANA: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa BWANA Mwenye Nguvu utaitwa Mlima Mtakatifu.’’ 4Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake. 5Barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wanaocheza humo.’’ 6Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?’’ asema BWANA Mwenye Nguvu.7Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi. 8Nitawarudisha waje kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama Mungu wao.’’ 9Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya yanayozungumzwa na manabii ambao walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu, mikono yenu na iwe na nguvu ili hekalu liweze kujengwa. 10Kabla ya wakati huo, hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake. 11Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu hawa kama nilivyowatenda zamani,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu. 12“Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao. 13Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya mataifa, Ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.’’ 14Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta maangamizi juu yenu, wakati baba zenu waliponikasirisha na sikuonyesha huruma,’’ asema BWANA Mwenye Nguvu, 15“Hivyo sasa nimeazimia kufanya mema tena kwa Yerusalemu na Yuda. Msiogope. 16Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtukwa mwenzake, mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu, 17usipange mabaya dhidi ya jirani yako, msipende kuapa kwa uongo, nayachukia yote haya,’’ asema BWANA. 18Neno la BWANA Mwenye Nguvu likanijia tena. 19Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Saumu za miezi ya nne, tano, saba na kumi itakuwa sikukuu za furaha na za shangwe kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na amani.’’ 20Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi watakuja, 21na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihi BWANA, na kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu. Mimi mwenyewe ninakwenda.’ 22Pia watu wa kabila nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafuta BWANA Mwenye Nguvu na kumsihi.’’ 23Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watang’ang’ania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ’’

Zekaria, sura ya 9
Tunaanza sasa Mzigo wa Kwanza wa sehemu ya Pili. Hi sasa ni kipindi cha mbali kijacho.

Kwenye Zekaria sura ya 9 hadi 11, maafa yaliikumba miji ya Tiro na Sidoni na Gaza na Akroni na Ashikeloni na Ashidodi na Damscus, na kwenye nchi zinazoizunguka nchi ya Shamu, na nchi yote la Lebanoni, ambayo imetajwa na kushughulikiwa kwa namna rahisi.

Watamwabudu Mungu huko Yerusalemu na Yuda, na watatawala mchi ya Israeli. Watakabiliwa na maangamizo yatakayowafikisha kwenye wongofu na matengenezo mapya. Mungu ataweka makazi yake mjini Yerusalemu na kufanya vita dhidi ya jeshi hili lililokuja kinyume na mji huu (Zekaria 9:1-8).

Imeandikwa kwamba, katika kipindi hiki: Shangilia sana, Ee Binti Sayuni! Piga kelele, Binti Yerusalemu! Tazama, mfalme wako anakuja kwako, ni mwenye haki naye ana wokovu, mpole naye amepanda punda, mwana punda, mtoto wa punda. (Zekaria 9:9). Matukio yaliyoandikwa kwenye herufi nzito yanaonekana pia kwenye Agano Jipya na yamenukuliwa kutoka huko na pia yametabiriwa kwenye Mika 5:2 na yameandikwa pia kwenye Mathayo 2:1 na 21:5. Hay ani maandiko yaliyoandikwa kotekote. Aya ya 10 inaendelea kwa kuelezea unabii wa Kuja kwa mara ya Pili kwa Masihi, akiwa na hukumu ya haki na wokovu, akiwa amepanda gari akitokea kwa Efraimu na farasi kutoka Yerusalemu na uta wa vita. Masihi ataleta amani kwa mataifa wasio Wayahudi na utawala wake utaenea toka upande huu wa bahari hadi kwenye upande wa pili wa bahari na kutoka kwenye mto hadi hadi pande ya mwisho ya dunia. Mungu anasema kwamba atauchukua Sayuni na kuweka agano la damu na kuwafungulia wafungwa kutoka shimoni ambako hakuna maji (Zekaria 9:11-12). Huu utakuwa ndiyo wongofu wa Yuda na Efraimu. Maandiko yanaonyesha kuwa watatumwa kwa wana wa Yavani, ambao wanaaminika kutoka kwenye jamii ya Wayunani tangu mwaka LXX lakini Waebrania wanatamka yavan, usemi unaoeleweka kuwa ni Wayunani-Ioni wa kale, na sio Wayunai wa siku hizi. Na hawatokani na wakazi wa siku hizi wan chi hii ya Uyunani, maarufu kama Ugiriki siku hizi na ambao sio wana wa Yavani kwa namna yoyote (kama ivyoandika kwenye Mwanzo 10:2,4; Isaya 66:19; Ezekieli 27:13; Danieli 8:21; 11:2; Yoeli 3:6; tazama jarida la Kimbuko la Asili la Mataifa (Na. 265) [Genetic Origin of the Nations (No. 265)] na Vita ya Hamoni-Gogu (na. 294) [War of Hamon-Gog (No. 294)].

Watapata nguvu mpya na Bwana atawafanya kuwa imara na watawatiisha maadui zao kwa Roho Mtakatifu aliye asili ya wongofu wao.

Lebanoni na fahari yote ya Yordani vitaletwa. Bwana anasema atalilisha kundi la kondoo wa kuchinjwa. Kwenye sura ya 11, Mungu anaonyesha jinsi jambo hili litakavyokuwa na jinsi atakavyoingilia kati na kulilisha kundi. Kwenye sura hii Mungu anawaonya wanaozitumikia vinyago na kufanya ibada ya sanamu na anaelezea jinsi hukumu yao itakavyokuwa kwa dhambi waliyoifanya ya kuwaacha na kuwatelekeza kondoo na kuharibu umoja wa watu. Hii ni moja ya mambo yatakayofanyika kwenye Ujio wake wa Kwanza kipindi ambacho watumwa wa Uzuri na Njuga walizofungiwa zitakapovunjwa na wachungaji wale ambao walikulia na kuendelea kuwa kwenye Kanisa kengeufu linalowawinda masikini na kuwakokota kwa kwato zao watakapoadhibiwa (kama ilivyoandikwa kwenye Ezekieli 34:1-22).
Zekaria 9:1-17 inasema: Neno la BWANA liko kinyume na nchi ya Hadraki na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika, kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote za Israeli yako kwa BWANA, 2pia juu ya Hamathi inayopakana nayo, juu ya Tiro na Sidoni, ingawa wana ujuzi mwingi sana3Tiro amejijengea ngome imara, amelundika fedha kama mavumbi na dhahabu kama taka za mitaani. 4Lakini Bwana atamwondolea mali zake na kuuangamiza uwezo wake wa baharini, naye atateketezwa kwa moto. 5Ashkeloni ataona hili na kuogopa, Gaza atagaagaa kwa maumivu makali, pia Ekroni, kwa sababu matumaini yake yatanyauka. Gaza atampoteza mfalme wake na Ashkeloni ataachwa pweke. 6Wageni watakalia mji wa Ashdodi, nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti. 7Nitaondoa damu vinywani mwao, chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao. Mabaki yao yatakuwamali ya Mungu wetu, nao watakuwa viongozi katika Yuda, naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.

Kuanguka kwa miji ya Tiro na Sidoni, kwa sehemu kulifanywa na Wababelonia. Hata hivyo, tukio hili lilitokea siku nyingi zilizopita wakati ilipokuwa inaandikwa. Unabii iliangalia mambo yanayokuja baadae kwa Wayunani na Warumi na kisha baadae kidogo kwa Waarabu na Wapigania dini (Wakrusedi) na sasa unajiri kwenye Siku hizi za Mwisho. Ufafanuzi uliofanywa hapa umefanywa kwa sehemu tu na wala sio wote, na kwenye Siku za Mwisho tunajionea wenyewe haya yakifunuliwa na kuwekwa wazi na tukishukudia kwa macho yetu..

Ahadi ziliyoko hapa ni kwamba mataifa haya yatakuwa ni sehemu ya Israeli na yatakuwa ni majimbo ya inchi hii ya Israeli na uukufu au uzuri wao utakuwa ni utukufu wa Bwana, Mungu wa Israeli. Wayebusi walikuwa ni wakazi wa zamani wa mji wa Yerusalemu na mahali alipokuwa anatwangia ngano yaani shinikizoni kwa Arauna ndipo palipokujakuwa hatimaye ndipo Hekalu la Mungu lilipojengwa. Uweza wa kijeshi wa Wafilisti uliondolewa na utawala wao uliondolewa kutoka Gaza maeneo mengine muhimu yaliyokuwa sehemu nyingine ya Wafilisti yaliondolewa au yalifanywa yawe na watu mchanganyiko kama ilivyokuwa mji wa Ashdodi. Hivi ndivyo yanavyosema maandiko na maandiko hayawezi kutanguka.

Mungu atatuambia kwamba hatimaye Masihi atakuja Yerusalemu kama alivyokuja kwa nguvu na ushindi akashinda nguvu za dhambi na mauti. Andiko haliishii hapa tu bali linaendelea kuwaelezea Efraimu naYuda kwa pamoja, ambao ndivyo watakavyokuwa katika Siku za Mwisho. Israeli walikuwa wameshaenda utumwani tangu mwaka 722KK na hawakurudi.
8Lakini nitailinda nyumba yangu dhidi ya majeshi ya wanyang’anyi. Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena, kwa maana sasa ninawachunga. 9Shangilia sana, Ee Binti Sayuni! Piga kelele, Binti Yerusalemu! Tazama, mfalme wako anakuja kwako, ni mwenye haki naye ana wokovu, mpole naye amepanda punda, mwana punda, mtoto wa punda. 10Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu na farasi wa vita kutoka Yerusalemu, nao upinde wa vita utavunjwa. Atatangaza amani kwa mataifa. Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari na kutoka mto Eufrati hadi mwisho wa dunia. 11Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya agano langu nawe, nitawaacha huru wafungwa wako watoke kwenye shimo lisilo na maji. 12Rudieni ngome yenu, Enyi wafungwa wa tumaini, hata sasa ninatangaza kwamba nitawarejesheeni mara dufu. 13Nitampinda Yuda kama nipindavyo upindi wangu, nitamfanya Efraimu mshale wangu. Nitawainua wana wako, Ee Sayuni, dhidi ya wana wako, Ee Uyunani na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita. 14Kisha BWANA atawatokea, mshale wake utamulika kama umeme wa radi. BWANA Mwenyezi atapiga tarumbeta, naye atatembea katika tufani za kusini, 15BWANA Mwenye Nguvu atawalinda, wataangamiza na kushinda kwa mawe ya kutupa kwa kombeo. Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo, watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia kwenye pembe za madhabahu. 16BWANA Mungu wao atawaokoa siku hiyo kama kundi la watu wake. Watang’ara katika nchi yake kama vito vya thamani kwenye taji. 17Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri! Nafaka itawastawisha vijana wanaume, nayo divai mpya vijana wanawake.

Andiko hili linaelekea mbele hadi kwenye Siku za Mwisho wakati Masihi atakaporudi kwa nguvu na utukufu na kuyatiisha mataifa. Anautumia uweza wa Yuda na wa Efraimu kuyatiisha mataifa, na hivi ndivyo ilivyotokea hasa tangia mwaka 1916 na kuendelea (tazama jarida la Kuanguka kwa Misri: Unabii Juu ya Mikono Iliyovunjika ya Farao (Na. 36) [The Fall of Egypt: The Prophecy of Pharaohs Broken Arms (No. 36)]. Hata hivyo, watalazimishwa kwa amani.

Zekaria sura ya 10
Mzigo wa Kwanza unaendelea hadi kufikia andiko la sura 10:12. Hata hivyo, sura nyingine mbili zinazofuatia zinashughulika kuelezea kuhusu dini ya uwongo. Mungu anawaaambia kuwa wanataka baraka zake na sio za terafi, ambaye ni mungu-sanamu ambaye tunaweza kumuona hata leo akiwa na umbo la mwanamke akiabudiwa kama mungu-mke ambaye anajulikana kama “Bikira Mariamu” au pia anatumika kwenye dini ya Buddha na sehemu nyingi nyingine akijulikana kwa majina tofauti tofauti.

Waonaji wanajimu huona uwongo na waota ndoto hukosea wanapotafsiri ndoto zao. Watu hudanganywa na kupotoshwa na dini za uwongo kipindi hiki kinaedelea hadi mwishoni. Wachungaji watahukumiwa kwa ajili ya yale waliowafanyia Yuda na Israeli na walivyowafanyia wateule wa Mungu. Yuda wamewekwa kando ili kuonysha kuwa watarejeshwa upya na dini ya uwongo itaondolewa mbali na kukomeshwa kabisa. Yuda watarejeshwa upya na Yusufu watatiwa nguvu. Hata hivyo, tunapaswa kuelewa kuwa wao ni kina nani kwanza kabla ya kuona kile ambacho Mungu anakwenda kufanya. Kabila hili la Yuda na nyumba ya Yusufu wako Marekani kwa sasa na kwenye mataifa ya Jumuia ya Madola ya Waingereza, isipokuwa kwa dakika moja wanajulikana kama Makabila Kumi Yaliyopote ya Israeli, ambao nim ara kumi zaidi ya vile wanavyojulikana kama Wayahudi leo kwenye mataifa hayo. Kuna Wayahudi wengi nchini Marekani peke yake kuliko walivyo nchini Israeli kwenyewe na wengi wako Marekani na kwenye Mataifa yaliyo kwenye Jumuia ya Madola kuliko walivyo hahala pengine popote duniani. Hawa wote nitaifa kamili na kweli la Israeli leo, bila kuwahesabia wale wanaojulikana kuwa na nasaba ya uzawa kwa Israeli wa kale.
Zekaria 10:1-12 inasema: Mwombe BWANA mvua wakati wa vuli, ni BWANA atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu. 2Sanamu huzungumza udanganyifu, waaguzi huona maono ya uongo, husimulia ndoto ambazo si za kweli, wanatoa faraja batili. Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo walioonewa kwa kukosa mchungaji. 3“Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi, kwa kuwa BWANA Mwenye Nguvu atalichunga kundi lake, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi mwenye kiburi akiwa vitani. 4Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni, kutoka kwake vigingi vya hema, kutoka kwake upinde wa vita, kutoka kwake kila mtawala. 5Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa wanaokanyaga barabara za matope wakati wa vita. Kwa sababu BWANA yu pamoja nao, watapigana na kuwashinda wapanda farasi. 6“Nitaiimarisha nyumba ya Yuda na kuiokoa nyumba ya Yosefu. Nitawarejesha kwa sababu nina huruma juu yao. Watakuwa kama watu ambao sijawahi kuwakataa kwa sababu mimi ndimi BWANA, Mungu wao, nami nitawajibu. 7Waefraimu watakuwa kama mashujaa, mioyo yao itafurahi kama kwamba ni kwa divai. Watoto wao wataona na kushangilia, mioyo yao itafurahi katika BWANA.8Nitawapa ishara na kuwakusanya ndani. Hakika nitawakomboa, nao watakuwa wengi kama walivyo kuwa mwanzoni. 9Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa, hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali watanikumbuka mimi. Wao na watoto wao watasalimika katika hatari nao watarudi. 10Nitawarudisha kutoka Misri na kuwakusanya toka Ashuru. Nitawaleta katika nchi ya Giliadi na Lebanon, napo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha. 11Watapita katika bahari ya mateso, bahari iliyochafuka itatulizwa na vilindi vyote vya mto Nile vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitashushwa na fimbo ya utawala ya Misri itatoweka. 12Nitawaimarisha katika BWANA na katika jina lake watatembea,’’ asema BWANA.
Pia kumbuka kuwa nchi ya Gileadi na Lebanoni zimehifadhiwa kwa ajili ya Efraimu na kama sehemu ya Israeli yote kuu. Mungu anajiandaa kwa kipindi hiki hata sasa. Lebanoni itajumuishwa kuwa kama sehemu ya taifa hili la Israeli na wataishi kwa amani.

Zekaria, sura ya 11
Kisha Mungu anaitaja Lebanoni kwenye unabii huu kwa njia ya ishara. Kwa hiyo wanahusianishwa na kundi na vilio vya wachungaji. Matukio haya yote yanahusishwa na Siku za Mwisho. Vipindi vyote vya kuhusishwa kwa Gileadi na Lebanoni na Israeli na Makanisa ya Mungu vimefungamanishwa pamoja kwenye mlolongo mmoja na Mungu anashughulika na wote hawa.
Zekaria 11:1-17 inasema: Fungua milango yako, Ee Lebanoni, ili moto uteketeze mierezi yako! 2Piga yowe, Ee mti wa msonobari kwa kuwa mwerezi umeanguka, miti ya fahari imeharibiwa! Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani, msitu mnene umefyekwa! 3Sikiliza yowe ya wachungaji: malisho yao manono yameharibiwa! Sikia ngurumo za simba, kichaka kilichostawi sana cha Yordani kimeharibiwa! 4Hili ndilo asemalo BWANA Mungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa. 5Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘BWANA asifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.6Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,’’ asema BWANA. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.’’

Kipindi hiki kimeendelea kwa muda mrefu sana na mfumo wa uwongo uliinuka na kuitawala dunia na wafalme ambao walifanyanao uzinzi. Hii ndiyo dini tunayoitajwa kwenye kitabu cha Ufunuo kuwa ni Babeli ya Siri. Hakuna mtu ambaye Mungu ameweza kumwokoa kutoka mkononi mwao kwa ajuli la ukengeufu wao.

Dini ikafanyika kuwa ni biashara huku ikienea na kuwalaghai watu wake yenyewe. Mungu akakomesha mpango wa Neema na Ushirikiano au Umoja.
7Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi.

Kwa muda wa mwezi mmoja tu Mungu akawaondolea mbali wachungaji wake watatu. Jambo hili limeongelewa vizuri kwenye jarida la Kulipima Hekalu (Na. 137) [Measuring the Temple (No. 137)]. Huu ni mwaka wa tatu wa siku za mwisho zinazoitwa kama ni ya “Maombolezo ya Musa”. Kundi lile linajiangamizwa lenyewe na wale wanaonyenyekeana na kutetemekewa kwa kuogopana na wanaositakiana mashitaka ya uwongo na kushutumiana. Kisha andiko hili linarejea nyuma na kushughulika na Masihi na mshahara wake atakaolipwa kwa ajili ya mwenendo wake kwa vipande thelathini vya fedha.
8Katika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu. Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao 9nikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.’’ 10Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua agano nililofanya na mataifa yote. 11Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo waliodhurika katika kundi waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno la BWANA. 12Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.’’ Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha.13Naye BWANA akaniambia, “Mtupie mfinyanzi,’’ hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika nyumba ya BWANA

Mkataba wa ushirikiano hatimaye ulivunjika kati ya Israeli na Yuda. Hadi kufikia kipindi kile Israeli walikuwa upande wa kaskazini walikopelekwa lakini wengi wao wanaushirikiano bado na Yuda. Hata hivyo, Yuda waliangamizwa na kutawanywa na katika karne hiyohiyo Waajemi na Warumi waliidhoofisha Israeli na washirika wake na wakaenda Ulaya. Ushirikiano wao ukaisha.Hali hii iliendelea kwa kipindi cha miaka 1800 hadi kwenye karne ya Ishirini wakati Mungu alipoanza kushughulika tena na Israeli na Yuda.
14Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja udugu kati ya Yuda na Israeli! 15Kisha BWANA akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu. 16Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao. 17“Ole wamchungaji asiyefaa, anayeliacha kundi! Upanga na uupige mkono wake na jicho lake la kuume! Mkono wake na unyauke kabisa, jicho lake la kuume lipofuke kabisa!”

Mnamo mwaka 1916 Mungu alianza kushughulika na Misri na kuirudisha Nchi Takatifu kwa mkono wa Efraimu mwaka 1917 Yerusalemu ulitwaliwa na nchi asilia ya Wayahudi ikatangazwa kwenye kile kilichojulikana kama ni Azimio la Balfour. Mwaka 1948 Israeli ikatangazwa kuwa ni nchi huru na ikapigana vita yake ya kwanza. Mwaka 1944 Lebanoni ilijitangazia uhuru wake lakini katika mwaka 1948 ilijihusisha na mgogoro wa wakimbizi wa Kipalestina ambao ulishuhudia wengi wao wakikimbilia huko Tiro na maeneo mengine ya Lebanoni. Miaka saba ya Misri ilienda tangia mwaka 1916 hadi 1996. Kanisa la Mungu lilikuwa likijikusanya upya kwa kipindi cha miaka arobaini muda huu wa kuanzia mwaka 1927 hadi 1967. Hawakushughulikia vizuri na masuala ya kundi la watu wa Mungu na waliweza hata kutupwa kwenye mifumo ya wachungaji hawa wanaoabudu na kutumikia vinyago na mnamo mwaka 1967 walijiingiza kwenye mfumo wa siku za mwisho na mataifa ya Israeli hali iliyowalazimu kuwepo kwa mujibu wa ulivyosema unabii bali walishindwa kutoa huduma vizuri. Mzunguko mmoja wa miaka kumi na tisa uliruhusiwa (soma jarida la Miaka Arobaini ya Toba (Na. 290) [Forty Years for Repentance (No. 290)] na Unabii wa Uwongo (Na. 269) [False Prophecy (No. 269)].

Israeli na Tiro na Lebanoni na Gileadi wote walipewa miaka sabini tangu mwaka 1948. katika miaka hiyo mataifa mengine pamoja na kundi la Makabila Kumi wameendelea kubweteka na kuishi maisha yasiyo na utaratibu wala mpangilio.

Kumbuka mikono miwili inayotajwa kwenye unabii wa Mikono Iliyovunjika ya Farao (Na. 36) [Pharaoh’s Broken Arms (No. 36)]. Mikono hii miwili ilikuwa ni kipindi cha miaka arobaini kilichodumu tangu mwaka 1916 hadi 1996. Walitawanyika tangu kipindi cha mwanzo kwa miaka 2520 au kinachoitwa pia kama cha “mara saba”. Kwa hiyo tunajionea pia mikono mingine miwili ambayo inayomaanisha zama ya kipindi cha miaka arobaini cha mataifa haya cha kuanzia mwaka 1948 hadi 2028, ambcho ni kipindi kilichowekwa kwenye mfumo mzima wa kuanzishwa kwa mfumo mzima wa Milenia. Kuanzia kipindi cha mwaka. 2018 hadi 2028 tutajionea mwisho wa kutiishwa kwa mataifa na mchakato wa kuanzishwa kwa mfumo wa milenia.

Mwaka 1967 mwanzo wa mfululizo wa vita ulianza nchini Israeli na sambamba yake, hali ya ukengeufu kwenye Kanisa la Munu uliendelea. Waliendela kuondoa maadhimisho ya kweli ya Pasaka na wakaendelea na mafundisho ya uwongo. Waliyaacha mafundisho ya kweli yenye uzima na kufundisha hadithi za uwongo. Fundisho lau kuhusu asili chanzo ya Mungu likaendelea kufundishwa kuwa yeye anakamilika uungu wake kwa kujumlisha Nafsi Mbili yani Udithei na waliwafundisha watu wao kushikilia hivyo na kuyakataa mafundisho sahihi kuhusu jambo hili. Mnamo mwaka 1997 kipindi cha Utimilifu wa Mataifa kilifungwa na kipindi cha miaka thelathini ya mwisho cha kutiishwa kwa mataifa kilianza (soma jarida la Miaka Thelathini ya Mwisho: Pambano la Mwisho (Na. 219) [The Last Thirty Years:  the Final Struggle (No. 219)].

Mnamo siku ya 1 mwezi wa Abibu 2008 ikiwa ni miaka wa arobaini ya watu hawa ikiwa imekamilika na kisha mlolongo wa mwisho ukiwa unaendelea. Mungu amesema kwamba atautumia mjiwa Yerusalemu katika mkakati wakewa kuyashughulikia mataifa.

Zekaria, sura ya 12
Zekaria sura ya 12 inaelezea kuhusu Yuda na Yerusalemu watakavyokuwa katika Siku za Mwisho. Inasema kuwa Yerusalemu itakuwa ni jiwe kuu na mzigo au kongwa kwa watu WOTE. Wale wote watakaojiunga nao kwa kujipendekeza watakatwa vipande vipande ingawaje watu wote wa dunia wataungana pamoja ma kuweka mikakati kadhaa kinyume chao. Mungu ansema kuwa katika siku hiyo atampiga kila farasi kwa mapigo makuu sana na atawapiga wapanda farasi wao kwa wazimu. Siku hiyo Mungu atafungua macho yake kuuelekea na kuwatazama Yuda. Kwa hiyo, atawachukulia kwa moyo wa upendeleo na atawapiga farasi wa watu hawa ambao ni maadui zao kwa upofu, jambo linaloasiria kuwa kama bahati nzuri kwa kipindi hiki kwa hawa Yuda. Jambo litakalowafanya washindwe kuamua mambo watakayoyachukua na kuanzisha mikakati ya maana na mipangilio yenye manufaa (Zekaria 12:3-4). Katika Siku za Mwisho viongozi waYuda watakuwa kama moto ulao kwa watu wote watakaokuwa upande wa kulia na wakushoto kwao. Watawategemea wakazi wa Yerusalemu watakaokuwa na Masihi na mikakati ya Bwana wa Majeshi, Mungu wao. Kwa hiyo, mashambulizi dhidi ya Yerusalemu yataendelea kama yalivyo hadi kipindi Atakaporudi Masihi. Wateule wataishi kwenye mji huu wa Yerusalemu pamoja naye na na watakuwa ni faraja na nguvu ya wakazi wa Yuda na kuwazunguka.

Zekaria 12:7 inaonyesha kuwa Yuda inaokolewa na wenyeji wa Yerusalemu ili kwamba Yerusalemu isijitukuze dhidi ya Yuda. Zekaria 12:8 inasema kwamba: tates that: Katika siku hiyo aliyedhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu [elohim] kama Malaika wa BWANA akiwatangulia [au mbele ya macho yao]. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba watakuwa Elohim kama Kristo alivyo kichwa chao na Elohim. (soma jarida la Wateule Kama Elohim (Na. 1) [The Elect as Elohim (No. 1)].

Hivyobasi, Mungu anasema (kwenye aya ya 9) kwamba: “Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoushambulia Yerusalemu.”

Zekria 12:10 ni unabii wa kitaswira au unaopingana na taswira. Atakaporudi Masihi watamtazama wale waliomchoma; kwa maneno mengine ni kusema kwamba, huyu ni Masihi waliyemuwamba mtini na kumchoma kwa mkuki. Kulikuwa na uchungu mjini Yerusalemu wakati wa kutoa dhabihu, na ndivyoitakavyokuwa tena wakati watakapogundua kikamilifu kuwa kile walichokifanya kinawahusu wote yaani Yuda na Walawi, na hasahasa wa nyumba ya Daudi kupitia kwa Nathani na Yuda, na kwa nyuma ya kikuhani ya Shimei na Lawi, kwa mzaliwa wao wa kwanza ambaye ni Masihi. Maombolezo makuu yaliyotangulia yalikuwa ni ya huko Hadadrimmon (kwa sasa inaitwa Rummane) magharibi ya Esdraelon karibu na Megido ambapo Mfalme Yosia aliuawa na maombolezo haya hayakutarajiwa. Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, hata yalikuwa ni maombolezo muhimu zaidi ya yote katika historia ya Israeli, na manasababishwa na tendo lao la kufahamu kile walichokuwa wanakifanya na kile walichikikosa au kupungukiwanacho kwa kipindi kirefu.
Zekaria 12:1-14 inasema: Hili ni neno la BWANA kuhusu Israeli. BWANA, Yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema: 2‘‘Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kulewalewa kwa mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia

Kumbuka kuwa Yudaea itaharibiwa wakati maadui watakapouzingira mji wa Yerusalemu. Wale wote wanaojipendelea na kujikinai wataharibiwa kabisa kwa mangamizi makuu.
3Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe. 4Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye kwa uenda wazimu,’’ asema BWANA. 5Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu BWANA Mwenye Nguvu ni Mungu wao.’

Juda watajionea jinsi mji wa Yerusalemu umetiwa nguvu kwenye uwezo wao wa kiroho kwa kupitia nguvu za Mungu. Hii itakuwa ni sehemu mojawapo itakavyokuwa baada ya toba yao.
6“Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake. 7“BWANA atayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda.  

Kumbuka kwamba utukufu wa nyumba ya Daudi na utaratibu wa kiuongozi wa Yerusalemu hautaweza kujitukuza dhidi ya Yuda, kwa jinsi Yuda itakavyopata ushindi kwenye kipindi hiki.

Hii ni siku ya kurudi kwa Masihi: yaani Siku ya Bwana.

Wateule watakuwa kama miungu wadogo siku ile. Watakatifu watakuwa wamefufuka na kuwa watawala au wana wa Mungu na watakuwa kama miungu wadogo, wakiwa ni Wajumbe wenye ujumbe wa Bwana vichwani mwao, na kumsaidia kazi zote Masihi aliye ni mzaliwa wa kwanza wa wafu wote (soma jarida la Mteule kama Elohim (Na. 1) [The Elect as Elohim (No. 1)].
8Katika siku hiyo, BWANA atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa BWANA akiwatangulia.

Kutoka siku hiyo Kristo atayaleta mataifa yote hadi Megido.
9Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoushambulia Yerusalemu. 10“Nami nitamiminia roho ya neema na maombi juu ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma, nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. 11Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadadrimoni katika tambarare ya Megido. 12Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao,13ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao, 14na koo zote zilizobaki na wake zao.

Jamii za Daudi kupitia Nathan na Lawi kupitia Shimei (Luka 3) ni familia za Masihi katika Yuda walioshuhudia Masihi aliuawa.

Kwa hiyo, dhambi za Yuda zitaponywa.

Zekaria, sura ya 13
Sura ya 13 inaema kwamba katika siku hiyo chemichemi zitafunguka kwenye nyumba ya Daudi na kwa Yerusalemu kwa ajili ya dhambi na unajisi. Wakati hili likitokea vinyago vyote vitaondolewa kutoka Yerusalemu na katika Israeli yote na manabii watakatiliwa mbali kwa kuwa Roho Mtakatifu atakuwa amemwagwa kote kwa kiasi kikumbwa sana kiasi kwamba unabii hautahitajika tena kabisa, na wale wanaojifanya kutabiri kwa jina la Bwana watakufa (Zekaria13:3).

Kama mtu hataiona Yerusalemu, itakuwa ni vigumu kuigundua ibada ya sanamu hapo pamoja na vinyago na alama zake na mahali palipo na uwongo na mafundisho mapotofu na yale ya uwongo kila mahali. Watu hudhania kuwa wanamtumikia Mungu wanapojinyenyekesha na kuvibusu mawe na vinyago na huku wakijipigapiga vifuani mwao.

Wakati Mungu alipouondoa uwongo huu toka Yerusalemu na kumwaga Roho wake Mtakatifu manabii watanya kazi ya ukulima na ufugaji. Zekaria 13:7 inaelezea yale yaliyofanyika siku za nyuma katika kuuawa kwha Masihi na kutawanyika kwa wateule katika kukamilisha unabii wa Isaya 53:5-10. Kondoo wataona theluthi mbili wakifa na theluthi waliobakia watatawanyika na kusafishwa kwa kupitishwa kwenye moto (13:8-9).
Zechariah 13:1-9 Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi. 2“Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asema BWANA Mwenye Nguvu. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi. 3Ikiwa yupo ye yote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la BWANA.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo. 4“Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu. 5Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima, ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’ 6Ikiwa mtu atamwuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu. 7“Amka, Ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu, dhidi ya mtu aliye karibu nami!” asema BWANA Mwenye Nguvu. “Mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika, nami nitageuza mkono wangu dhidi ya walio wadogo, 8katika nchi yote,’’ asema BWANA, “Theluthi mbili watapigwa na kuangamia, hata hivyo theluthi moja watabakia ndani yake. 9Hii theluthi moja nitaileta katika moto, nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama dhahabu. Wataliitia jina langu nami nitawajibu, nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ nao watasema, ‘BWANA ni Mungu wetu.’ ’’

Mungu atausafisha kama isafishwavyo dhahabu mji wa Yerusalemu na wakazi wake.

Zekaria, sura ya 14
 Zekaria 14 inaendelea kuitaja Siku ya Bwana (soma jarida la Siku ya Bwana na Siku za Mwisho (Na. 192) [The Day of the Lord and the Last Days (No. 192)].

Muda mfupi kabla ya kuja kwake Masihi, mji wa Yerusalemu utatwaliwa na na nusu ya wakazi wake watachukuliwa utumwani, lakini nusu nyingine watabakia ndani yake na hawataondolewa humu. Kisha Bwana atawapigania na kuwaadhibu mataifa haya. Masihi atasimama juu ya Mlima Sayuni na mlima huu utagawanyika vipande viwili, ukielekea pande mbili za mashariki na kusini na kufanya bonde litakalotokea mashariki na kuelekea magharibi na bonde hili litakuwa na kikomo chake kitakachoitwa Azal (Kwa mujibu wa kitabu cha fafanuzi cha SHD 682 kutoka kifungu cha 680, neno hili atsel linamaana ya uungwana).
 Zekaria 14:1-21 inasema: Siku ya BWANA inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa machoni penu. 2Nitayakusanya mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba zitapekuliwana wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini. 3Kisha BWANA atatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku ya vita.

Milima inayoelezewa kwenye aya ya 5 ni milima miwili iliyotokana na Mlima wa Mizeituni. Tetemeko hili pia linalotajwa kwenye kitabu cha Amosi sura ya 1. Siku ile, elohim wa Israeli atakuja na watakatifu wote pamoja naye (Zekaria 14:5). Masihi atakuwa mfalme atayayetawala dunia hii yote na jina lake litakuwa moja. Mji wa Yerusalemu utakuwa tambarare kutoka Geba, eneo lililo na umbali wa takriban maili sita kaskazini mwa Yerusalemu hadi Rimmon, ambao unaitwa pia Khan Umm er Rumamin (sawa na inavyosema Nehemia 11:29). Mji huu ni wa Ain Rimmon (En Rimmon, Yoshua 15:32). Hapo mwanzo mji huu walipewa kabila la Simeoni (Yoshua 19:7; 1Nyakati 4:32). Uko kusini mwa Yudea kwenye wilaya ya  Negebu karibu na Beer-sheba. Eusebius anaielezea hii kuwa ni kijiji kikubwa kuliko vyote miongoni mwa vile vya Wayahudi, maili za Kirumi kumi na sita upande wa kusini mwa Eleutheropolis katikati ya Darome (upande wa kusini ya Yuda). Khirbet er-Ramin iko maili tisa Kaskazini Mashariki mwa Beer-sheba. Beer-sheba iko eneo la jumla ya maili ishirini na nane Kusihi Magharibi ya Hebron naHebron iko maili kumi na tisa kusini mwa Yerusalemu, n ani maili thelathini na nusu Kusini Magharibi mwa Bethhlehemu. Kwa hiyo, hili bonde linalojumuisha uwanda wa Yerusalemu lina urefu wa maili arobaini na nne (au kilometa 66) urefu wake na linafunika eneo la vilima vya kusini ya nchi ya Yuda. Matukio ya jiolojia kwa hiyo ni makubwa sana.
4Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mzeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini. 5Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda.Kisha BWANA Mungu wangu atakuja, nao watakatifu wote pamoja naye.

Tunaona hapa kwamba kuwa kurudi kwa Masihi aliwa na utukufu mkuu au akiwa ni Mtakatifu Ajaye. Hili ni Kanisa pia.
6Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. 7Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na BWANA. Jioni inapofika nuru itakuwepo. 8Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi, wakati wa kiangazi na wakati wa masika.

Ziwa kubwa lililochini kwa chini lililogundulika hivi karibuni nchini Israeli litaunda mfumo msingi wa maji kwenda nje kuelekea upande wa magharibi na upande wa kusini mashariki.
 9BWANA atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo BWANA mmoja na jina lake litakuwa jina pekee. 10Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwakama Arabaa. Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme. 11Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa salama.
Kwa hiyo, Ktisto akiwa kama Mfalme, na Kanisa, watatawala kwa pamoja kutoka Yerusalemu kwa kipindi cha miaka elfu moja (soma Ufunuo 20).

Watu wanaopigana na Yerusalemu watateseka kwa tauni wakati kwamba miili yao na macho yao na ndimi zao aitaliwa kwa kadiri watakavyokuwa wakisimama. Wote watawainukia kinyume majirani zao na watauana. Utukufu na utajiri wa mataifa wafanyao hivyo, utapelekwa.
12Hii ndiyo tauni ambayo BWANA atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao. 13Katika siku hiyo BWANA atawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana.

Kumbuka kuwa hata Yuda wataupiga vita mji wa Yerusalemu kabla ya kipindi cha kuongoka kwao siku za mwisho.
14Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo. 15Tauni ya aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda nao wanyama wote walio kwenye kambi za adui.

Baada ya tukio hili, au vita kuu ya kipindi cha mwisho, kila ammoja miongoni mwa walioachwa wamataifa atakayekuja kinyume na Yerusalemu kutoka mahali popote duniani, watatuma wawakilishi wao mjini Yerusalemu, mwaka hadi mwaka ili wakamwabudu Bwana wa Majeshi na kuishika Sikukuu ya Vibanda. Na wale wote ambao hawatakwenda huko, mvua haitanyesha kwao kwa kajira yake sahihi na watasumbuliwa na tauni au magonjwa ya Misri. Mkakati wa kilimo cha umwagiliaji hautawaokoa watu hawa waasi. Kwa hiyo, tendo la kuzidharau nakutozishika Amri na Sheria za Mungu na kutozishika Sikukuu zake kutawasababishia maafa na misiba. Njuga za farasi wao zitakuwa zikilia “utukufu kwa Bwana” na vyungu vilivyo kwenye Nyumba ya Bwana vitakuwa kama mabakuli yaliyo mbele ya madhabahu. Wale watoao sadaka na sadaka zao watazipika nyama ndani yake kwa utakatifu (Zekaria 14:16-21). Mtindo na imani ya kutokula nyama bali mbogamboga tu hautakuwa ndio mshika dau kwenye kipindi hiki cha Milenia (soma jarida la Imani ya Kutokula Nyama bali Mbogamboga Kwenye Biblia (Na. 183) [Vegetarianism in the Bible (No. 183)].
16Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 17Ikiwa taifa lo lote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, BWANA Mwenye Nguvu, hawatapata mvua. 18Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. BWANA ataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 19Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.20Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya: SIKU TAKATIFU KWA BWANA, navyo vyungu vya kupikia katika nyumba ya BWANA vitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu. 21Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwa BWANA Mwenye Nguvu na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyibiashara katika nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu.

Ezekieli sura za 26 na 27 zinaielezea pia Tiro na maafa yanayoungojea mji huo. Ulishambuliwa na Wababelonia, na pia ukashambuliwa na Wamakedonia na Wayunani. Ukafanywa kuwa nimakao makuu ya shughuli za uvuvi kwa karne nyingi, lakini maandiko yanasema kuwa utaangamia na kupotea kwa kusombwa na mawimbi ya maji. Hapa tunajionea piwa kwamba merikebu za Tarshish zitatumika kama vivuko vya wafanyabiashara watakaozitumia pia kama meli za kivita. Yavani, Tubali na Mesheki yalikuwa ndio mataifa yaliyofanyao biashara na watu wa Tiro, kwa hiyo walikuwa ni watu wenye nasaba asilia ya Kiyafeti zaidi kuliko ya Kihamu nah ii ndio sababu ya wao vipimovyao vya nasaba ya damu (YDNA) zinasomeka zaidi kwa kuonekana kuwa wao ni wa kundi la K2 na sio wa E3. Ezekieli 28 inamtaja Shetani ikimfananisha kwa kumuita kuwa ni Mfalme wa Tiro.

Lolote kati ya mataifa haya yanayotoa wito wa kuliangamiza taifa la Israeli litakatwa vipande vipande. Na hii inajumuisha wale wote watakaotafuta kuwasaidia wengine katika maangamizo yakekama mataifa tunayoyaona sasa wakiwatuma wengine kuishambulia. Iran na Iraq watalipa gharama pia. Mataifa haya yanayojipendelea na kujiamini yenyewe kwa ajili ya jambo hili yatadanganyika na kujaribu kuushambulia mji wa Yerusalemu. Vita ya kidini ambayo inakuja hivi punde na itakayopelekea kuanzishwa kwa Vita Kuu ya III ya Dunia ambayo itakuwa ni ya hatari sana.

Miaka ishirini kabla ya vita ya mwaka 1967, tarehe 15 Mei 1947, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipiga kura ya kuunda Kamati Maalumu kuhusu Palestina (maarufu kama UNSCOP), ambalo lilianza kazi yake rasmi na kuendelea kwa ajili ya kuanzishwa ka Taifa la Israeli. Jambo hili lilifanyika miaka thelathini baada ya Azimio la kwanza la Balfour la Waziri Mkuu waUingereza aliyeitwa Balfour lililolenga kuanzishwa kwa laita asilia la Kiyahudi mwaka 1917. Azimio la pili la Balfour lilitilia maanani lengo la kikatiba la kuanzishwa kwa Australia. Hatahivyo, azimio la Umoja wa Mataifa lilichelewa sana kuweza kuikoa Yuda kutoka kwenye Mauaji Makuu na Yakuangamiza maarufu kama Holocust. Na kama ilivyotokea,Yuda walilazimika wapigane kiume ili kuanzishwa kwake.

Kwa mujibu wa utaratibu wa mzunguko wa kipindi cha miaka sabini, kutawezekana kuwa na mwaka kwa mwaka unaowiana kati ya hatari inayotokana na Vita Kuu ya II ya Dunia iliyopiganwa kipindi cha miaka ya 1936-1945 na kwenye kipindi cha miaka ya 2006-2015 ambacho kitashuhudia dalili za maafa na mauiaji ya Vita Kuu ya III ya Dunia.

Tangu vita za mwaka 1967 hadi 2007 ni kipindi cha miaka arobaini na kumekuwa hakuna toba yoyote hadi leo, na hata hakuna dalili hiyo wakati hali halisi ya mambo ni kwamba inakaribia kutokea. Maandiko hayawezi kutanguka. Hata hivyo, ni matumaini kwamba watu hawa wanaweza kutubu, lakini hawajachahua kufanya hivyo. Miaka hii sabini tangu mwaka 1948 inaishia mwaka 2018. Miaka themanini ya vipindi viwili vya pamoja vya miaka arobaini arobaini inaishia kwenye mwaka wa kwanza wa Yubile ya Milenia ya mwaka 2028. Kati ya miaka ya 2006 na2018 utaratibu au mfumo wote wa vita utaendelezwa. Tangia mwaka 2006 tunajionea matatizo yakianza na Mungu anashughulikia na nchi za Lebanon na Iraq. Vita hii itaendelea na kuenea hadiSyria na Iran.

Hatua za kijeshi zinazochukuliwa dhidi ya Israeli hazina maana yoyote. Majeshi hayawezi kuwa na mbinu nzuri au ubunifu mzuri wa kuweka uzani wa kufanikisha mikakati ya operesheni za kivita.

Tendo la Umoja wa Mataifa la kuilaani IsraeIi, limeifanya lijiweke lenyewe kwenye kundi hili na utapatwa na maafa hayohayo, na kama muundo wake unavyokusudia kumiliki mahala palipoachwa akiba na Masihi na watu wake.

Bado hatujachelewa sana kufanya toba na kufanyika wapya.
q

Sehemu ya II. Nyongeza kwenye Ufafanuzi wa kitabu cha nabii Zekaria: Kuhusu mataifa ya Yuda na Israeli na uhusiano wao na nabii zilizotolewa kwenye Agano Jipya.


Kuna maswali mengi yanayoulizwa kuhusu jinsi gani ya kuwatambua hawa Yuda na maelekezo ya Kibiblia kuhusu wale wanaojiita Wayahudi kumbe sio na jinsi ya kuwajua watu hawa. Unabii kuhusu mtiriririko wa mwendo wa Kanisa tangu kipindi cha Wasminarna hadi kipindi cha mwisho cha Kanisa la Wafiladelfia. Mateso haya yalikuwa ni kwa ajili ya kurefusha kipindi cha makanisa kutoka kipindi cha Wasmirna hadi cha mateso ya Diocletian hadi kuja kwa Masihi na sio ufafanuzi tu utokanao na maeneo mawili ya kitabu cha Ufunuo yanayohusu makanisa mawili. Maandiko haya yameelezewa pia kwenye maandiko mengine ya Agano la Kale pamoja na kazi za Bwana na mfumo wa dini ya uwongo ambao utabidi uingie huko Yudea. Unabii huu umeonyeshwa pia kwenye kitabu hiki cha Zekaria miongoni mwa maandiko yaliyo kwenye Agani la Kale.

Kwenye maeneo haya mawili tunaona kunasemwa kwamba kuna wale wanaojiita kuwa ni Wayahudi lakini sio bali ni wa Sinagogi la Shetani. Watu hawa wanaenda kufanywa watokee nawawepo kwenye kanisa na hatimaye kujitukuza wenyewe dhidi ya Kanisa la Mungu na kujifanya waonekane kuwa wao wamependwa na kukubalika na Masihi na Mungu na kwamba wamekabidhiwa mamlaka ya kuwasimamia na kuwaongoza watu hawa wote. 
Ufunuo 2:8-11 inasema: 8‘‘Kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika: Haya ndiyo maneno yake Yeye aliye wa Kwanza na wa Mwisho, aliyekufa kisha akafufuka. 9Naijua dhiki yako na umaskini wako, lakini wewe ni tajiri! Nayajua masingizio ya wale wasemao kuwa ni Wayahudi lakini sio, wao ni sinagogi la Shetani. 10Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia Shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu, hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. 11Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatadhuriwa na mauti ya pili.

Ufunuo 3:7-13 inasema: 7‘‘Kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika : Haya ndiyo maneno Yake Yeye aliye mtakatifu na wa kweli, Yeye aliye na ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, wala anachokifunga hakuna awezaye kukifungua. 8Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango uliofunguliwa, wala hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba una nguvu kidogo lakini umelishika neno Langu wala hukulikana Jina langu. 9Nitawafanya wale wa sinagogi la Shetani, wale ambao husema kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali ni waongo, waje wapige magoti miguuni pako, nao watajua ya kwamba nimekupenda.10Kwa kuwa umelishika neno la saburi Yangu nitakulinda hata utoke katika saa ya kujaribiwa inayokuja ulimwenguni pote ili kuwajaribu wote wakaao duniani. 11Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akaichukua taji yako. 12Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo kamwe. Nitaandika juu yake Jina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu, yaani, Yerusalemu mpya, ambao unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Nami pia nitaandika juu yake Jina langu jipya. 13Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa.

Hatahivyo, twaweza kujiuliza kuwa ni kinanani hao na wakowapi? Je, wametoka wapi na wanataka kuwa ni kina nani wao? Je, hii inahusianaje na maandiko matakatifu ya Agano la kale na tunawajuaje watu hawa?

Kama tunavyojua ni kwamba Uzayoni ni dini na sio kikundi cha kikabila. Tumeorodhesha taarifa za vipimo vya nasaba za damu za hawa Yuda zijulikanazo kama YDNA na mtDNA za Wayahudi na za wale wanaodhaniwa kuwa huenda wakahusiana kinasaba zinazotokana na asili yao ya kale kwenye majarida yetu ya Kiini Asilia cha Kinasaba ya Mataifa (Na. 265) [The Genetic Origin of the Nations (No. 265)] na Wana wa Shemu: Sehemu ya 1 (Na. 212) [Sons of Shem: Part I (No. 212A)]Uzao wa Ibrahimu Sehemu ya V: Yuda (Na. 212E) [Descendants of Abraham Part V: Judah (No. 212E)]Uzao wa Ibrahimu Sehemu ya VI: Israeli (Na. 212F) [Descendants of Abraham Part VI: Israel (212F)] na kwenye majarida mengine mengi yaliyo kwenye mtiririko wa majarida yaliyo kwenye nambari 212 yanayojikita kuelezea wazao wengine na makabila ya Ibrahimu na kila mojawapo yaliyo kwenye jedwali lenye kuhusianishwa na nambari hii ya 212G. Kii na asili ya mataifa ya Ulaya imeorodheshwa pia kwenye majarida yahusuyo Wana wa Yafeti (Na. 46A-46H) na pia yale ya Wana wa Hamu (Na. 45A-45E).

Dhana au fikra iliyoko kwenye Makanisa ya Mungu yaliyoko Uingereza kuhusu Waisraeli na kuhusu Waprotestanti wa Kizungu imekosewa kabisa na utaratibu wa vinasaba vya uzao wa watu (DNA) unadhihirisha makosa yao. Majarida yanayoelezea jinsi Israeli livyogawanywa na jinsi inavyotambulika kwenye mataifa ya dunia.

Ukweli wa mambo ni kwamba kiasi cha chini ya 28% ya Wayahudi kwa kweli ni Wasemiti kiasi kingine kinatokana na wana wa Ibrahimu pia. Kwenye kipindi cha mateso cha Diocletian (kilichodumu kwa takriban miaka 284-305), ambayo ni kuanzia mwaka 303- 311 kilichoendelea baada ya usitishwaji wake katika mwaka 305 hadi lilipotolewa tangazo la Azimio la Kuvumiliana mwaka 311;  lililoendelelea hadi kuinuka au kuanza kwa Uislamu mwaka 632BK, Wayahudi walikuwa na nguvu na madaraka huko Uarabuni na wamewaongoa watu wengi na kujiunga na wao kutoka kwenye makabila ya Kiarabu. Wamewaongoa Waedomu na Wana wa Esau kabla ya kipindi cha utawanyiko wao walivyoenda utumwani. Walilitesa kanisa na kujaribu kulimaliza kabisa lakini kanisa lilidumu kuwa imara katika kipindi cha muanza kwa Uislamu ulioanza na baraza la watu kumi na mbili huko Uarabuni likiongozwa na Muhammad (soma jarida la Utambulisho wa Kitabi cha Ufafanuzi wa Koran (Q1) [Introduction to the Commentary on the Koran (Q1)]. Wayahudi walirudi nyuma na kujifanya kuwa ni Waarabu na kuingia Uislamu, ingawaje wengi wao hawakufanya hivyo. Bali walibakia kuwa ni sehemu ya Yuda hadi leo. Hawakuweza kudhibiti makosa au mafundisho potofu ya Wapaulician wa zama za Wapergamo hadi pande za kaskazini pia iliyokuwa kwenye kipindi cha Wabyzanti. Nguvu na ushawishi wao ulifanyika kuwa na umaarufu na ulifanikisha shughuli za biashara.

Zaidi ya 25% ya Wayahudi ni Waba wa Hamu bila kujali kaqma wana nasaba ya Kikanaani au Kimisri waliotokana na Mchanganyiko Mkubwa wa Wakanaani waliochukuliwa na kuingizwa kwenye jamii ya Israeli na kutumikishwa huko.

Takriban 52% ya Walawi wa Kiashkenazi kwa kweli wana alama ya nasaba damu ya R1a inayoonyesha kuwa ni wana wa Yafeti, ambao huenda wanatokana na waongofu wa Kikhazari walioingia kwenye jamii ya Kiyahudi mwaka 740BK. Idadi kubwa ya watu hawa wana alama ya nasaba damu ya R1b ambayo ni ya Wahiti walioendelea kudumu kwenye mtiririko ya uzao wa kifalme wa Mfalme Daudi pi, hususan kwenye mlolongo wa uzao wa Dayan na Salathiel (soma jarida la Wahiti Kwenye Nyumba ya Daudi (Na. 67c) [Hittites in the House of David (No. 67c)].

Hii ndiyo sababu kwa imani ya Kiyahudi kutoamini Ubatizo na haizishiki amri za Mungu na kuifuata Kalenda potofu ya ukengeufu wa Kibabelonia ambayo ilikuwa haitumiki kwenye utaratibu wa Hekalu na ambayo iliingizwa kwenye dini ya Kizayuni mwaka 358BK na mtu aitwaye Hillel II aliyeiingiza ikiwa kinyume kabisa na utaratibu na amri za Mungu na wanavyotakakiwa kuitunza wateule, bila kujalisha kuwa wao ni Wayahudi au la. Yeyote anayeishika Kalenda ya Hillel itokanayo na itikadi ya Kizayuni hazitii amri za Mungu na atakuwa na kujibu kwa kupotosha watu wao jambo hili miongoni mwao ni Makanisa ya Mungu yaliyotokana na mfarakano wa Armstrong na yale ya Wayahudi wanaomwamini Masihi. Karibu wote miongoni mwao hawaishiki Kalenda ya Mungu (soma majarida ya Kalenda ya Mungu (Na. 156) [God’s Calendar (No. 156)]Kalenda Na Mwezi: Uhairishaji au Sikukuu? (Na. 195) [The Calendar and the Moon: Postponements or Festivals? (No. 195)] na Jinsi Kalenda ya Mungu Ilivyobadilishwa Katika Yuda (Na. 195B) [Distortion of God’s Calendar in Judah (No. 195B)].

Kipindi kile ambacho Mashahidi watakapokuja na kuamsha nia na hamasa ya watu kuona umuhimu wa kuzishika amri za Mungu, ndipo Wapalestine/Israeli hawa watakuwa ni wakwanza kusafiwa kutokana na ukengeufu huu. Wayahudi ambao hawabatizwi na wanaoshika Kalenda ya Hillel wataondolewa. Pia Wayahudi wale ambao hawatubu, pamoja na wale wa nasaba-damu ya Yuda wataondolewa pia wasipotubu.

Hata hivyo, ugumu wa mioyo ulioko kwenye mioyo ya Yuda utaondolewa na watatubu na hata wale wanaosema kuwa wao ni Wayahudi kumbe sio ila wana tu ile nasaba-damu ya kijamii ya Kiyahudi inayosomeka kwa kushabihiana kama mtDNA. Fundisho linalosema mtu anaweza kurithi utambilisho wa Kiyahudi kutoka kwa mama halitaweza kukubalika tena na mafundisho ya Yaisraeli, na kama ilivyo kwa mujibu wa maandiko matakatifu ya Biblia. Watakuwa ni sehemu tu ya Israeli wakiwa kama washiriki wa Kanisa la Mungu kwa kupitia ubatizo wao na sehemu kwenye urithi wao ulio kwenye makabila ya Israeli au meingine yaliyo nje ya taifa hili. Kadiri wanavyooa kwenye makabila ya Israeli watakuwa wanafananishwa pia na kuhesabiwa kuwa sawa na hata na wazawa asilia waliozaliwa nchini Israeli. Haakuna hata mmojawao miongoni mwa hawa Wayahudi wenye asili ya Kikabbali watakaoruhusiwa kubakia nchini Israeli. Wakati huohuo, Israeli watakuwa wanarudi na baadhi yao wataachwa nje ya Israeli kwenye milki yao huko, kama walivyokuwa Warubeni, Gadi na Manase. Maeneo hayo yataongezwa pia.

Muundo wa jinsi itakavyokuwa Yuda na Yerusalemu tangia kipindi cha utawanyiko wake hadi kufikia Siku za Mwisho umeelezewa vyema kwenye jarida la Ufafanuzi wa kitabu cha Zekaria (Na. 297) [Commentary on Zechariah (No. 297)].

Kwenye andiko hilo, hususan kwenye sura ya 2, tunaona kwamba Mungu wa Pekee na wa Kweli, Yahova wa Majeshi amemtuma mwnae wa pekee kwa mamlaka yake Yahova, aliye Bwana wa Israeli ilia je na kuulinda mji wa Yerusalemu na kuufanya upya. Taifa hili lilikwenda utumwani kwa sababu ya maovu yake na kuzivunja kwao Amri za Mungu na mfumo wa Hekalu jambo ambalo wanaendelea kufanya hivyo hadi leo. Kutoka kwenye Sehemu ya I hapo juu tuliona kwamba kwenye Zekaria Sura ya 1 inatanguliwa na maonyo na wito wa kumrudia Bwana wa Majeshi kwenye sehemu ya kwanza (Zekaria 1:1-6).

Kwenye maono ya pili (katika Zekaria 1:7) Mungu anaonyesha farasi watakaofanya kazi zao kuiadhibu dunia wakitumwa na Bwana, Mungu kipindi ambacho dunia itakuwa kwenye mapumziko kwakuwa dunia imeutendea vibaya mji wa Yerusalemu na Yuda kipindi kichokuwa hakiitajiki kwao kuufanyia hivyo. Kwa hiyo, baada ya miaka sabini Mungu alianza kufanya kazi lakini Yudana Yerusalemu hawakutubu na walifanywa upya ili kutimiza mchakato wa kurudi kwa Masihi kuendane sawa na jinsi unabii ulivosema.

Mungu atafanya kazi zake ili kuwezesha ujenzi wa hekalu ili kuufanya mfumo wake uanzishwe kwa ajili ya kutengeneza ujio wa Masihi. Baada ya hilo itatakiwa liharibiwe tena sawa na unavyosema unabii wa Danieli 9:25-28 (soma jarida la Ishara ya Yona na Historia ya Ujenzi Mpya wa Hekalu (Na. 13) [The Sign of Jonah and the History of the Reconstruction of the Temple (No. 13)]. Walifanywa upya na kisha walipimwa na kisha walitawanywa tena kama tunavyoona kwenye Sura ya 2 wakati Yahova ambaye ni Bwana wa Majeshi wa Israeli atatumwa kuusaidia na kuulinda mji wa Yerusalemu.

Katika Zekaria 2:1-13 tumeona anatajwa Mungu wa Pekee na wa Kweli ambaye ni Yahova, Bwana wa Majeshi akimtuma Masihi kuurejesha upya mji wa Yerusalemu na kuufanya kwa maranyingine tena kuwa Mji Wake Mtakatifu na Yuda kuwa ni miongoni mwa sehemu iliyo Ardhi Takatifu.
Kwenye maandiko haya ya Zekaria tunaona maendeleo ya mfumo wa Kibabelonia katika Israeli na hususan katika Yuda.
Kwenye jarida la Ufafanuzi wa kitabu cha Zekaria Sehemu ya 1 hapo juu linatakiwa lisomwe kwa undani sana ili ujionee dokezo au dalili ya kile kinachotokea sasa. Kwenye sehemu hii tutashughulika na kujionea kile kinachotokea katika Siku za Mwisho mambo nayayouhusu na kuutokea mji wa Sayuni na Yuda na watu waliojiingiza na kubobea kwenye mfumo huo ambao umefanyika kama dini iliyo nje ya sheria na amri za Mungu na kwa kweli haipo kwenye sehemu ya Israeli na kwa wateule wake Mungu. Sura ya 3 na 4 inamwelezea Kuhani Mkuu na Kinara cha Dhahabu ambavyo vinamwashiria Masihi na Mashahidi Wawili wanaozifanya kazi zao kama alivyokuwa anafanya nabii Eliya na walivyofanya mashahidi wengine. Viumbe hawa wametajwa kwenye kitabu cha Ufunuo sura ya 11 na tendo la Kupimwakwa Hekalu ambalo ni wateule wa Mungu kumeelezewa pia mahali hapa (soma jarida la Mashahidi (Wakiwemo Mashahdi Wawili) (Na. 135) [The Witnesses (including the Two Witnesses) (No. 135)]. Kwenye maandiko haya tunaona kwamba Kuhani Mkuu amerejeshwa upya na kutakaswa ili aweze kuzifanya kazi za Hekaluni tena. Hekalu liliharibiwa na kubomolewa mwaka 70BK ili kutimiza unabii na kwa hiyo tunashughulika na Hekalu lingine lenye Kuhani Mkuu zaidi kamatunavyojionea kwenye Kitabu cha Waebrania.
Sura ya 5 inajikita na kuwa maalumu kuelezea jinsi Yuda na Israeli walivyofanya maovu na kujiharibu kwa kujichanganya na mifumo ya Kibabeloni kupitia kwenye muundo wa dini ya uwongo. Tunaona jinsi walivyojenga nyumba kwa kufuata mfumo wake na kuweka efa chini yake. Sura ya 6 inamtaja mtumishi wa Mungu ambaye ni Chipukizi litakalotengeneza na kurejesha tena Hekalu na kuketi kwenye Kiti cha Enzi na kuhani atakayemweka na kutakuwa na amani. Hali hii itatokea kwenye kipindi ambacho dunia itakuwa kwenye amani. Na kama tuonavyo hapo juu, hii ilifanyika kwanza katika Yuda na Kuhani Mkuu ambaye alikuwa Zerubabeli ambaye alikuwa ni ashirio la Masihi na Hekalu ambalo lilikuwa ni mwili wa Masihi katika Siku za Mwisho. Kuhani Mkuu Yoshua ndiye Yahushua au Yoshua ambaye pia ni Masihi. Kisha Zekaria anaendela kuelezea kipindi cha Marejesho ya Siku za Mwisho na pia Marejesho ya Kalenda na sheria za ulimwengu mzima, kazi atakayoifanya Masihi akiamuru kutoka Yerusalemu. Kumbuka jinsi ilivyoandikwa kwenye andiko la Zekaria 6:9-15:
Zekaria 6:9:15 inasema: 9Neno la BWANA likanijia kusema: 10‘‘Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo nenda nyumbanikwa Yosia mwana wa Sefania. 11Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadiki. 12Umwambie, hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga hekalu la BWANA. 13Ni yeye atakayejenga hekalu la BWANA, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’ 14Taji itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya hekalu la BWANA. 15Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kwamba BWANA Mwenye Nguvu amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii BWANA, Mungu wenu kwa bidii.’’
Tazama kwamba Malaika wa Bwana ambaye ni Yahova wa Israeli anasema kwenye aya ya 15 (na msisitizo umeongezewa) kwamba wale waliombali watakuja kusaidia ujenzi wa Hekalu nasi tutajua kuwa Bwana wa Majeshi amemtuma kwetu. Hapa wanaelezewa wateule wa Mungu walio kwenye hali ya utawanyiko ambao ndiyo nyumba yote ya Mungu walio wateule kwenye Mwili wa Kristo, ambao ndio Hekalu la Mungu.

Kisha sehemu inyofuatia inaendelea kuelezea utawanyiko wa watu usababjshwao na utovu wao wa kutowatii manabii wa Bwana wa Majeshi aliowatuma kwao na ndipo alipowatawanya kwa upepo wa kisulisuli (Zekaria 7:1-14). Kwenye sura ya 8 neno la Bwana wa Majeshi lilitumwa tena kwa Zekaria na tunaona kuwa Yahova, Bwana wa Majeshi anawaambia tena lakini ni huyu Yahova, Bwana wa Majeshi ndiye anayewarudisha Sayuni na kwenda kukaa katikati ya mji wa Yerusalemu. Na Yerusalemu utaitwa kuwa ni mji wa Kweli na Mlima wa Bwana au Yahova wa Majeshi, Mlima Mtakatifun (kama tuonavyo pia imeandikwa kwenye Isaya 2:2; Yeremia 31:23; Ezekieli 40:2; & Mika 4:1).

Kwa hiyo, maandiko haya yanaelezea kuhusu kurejeshwa upya tena kwa Israeli na Yuda kutoka kwenye utawanyiko wao na matokeo yake ya mwisho ya marejesho haya kwao na kwa Yerusalemu ni toba ya mataifa kama tunavyoona katika Zekaria 8:23. Kwa hiyo ni jambo lisilowezekana kwa Yuda kuachwa katika Israeli peke yao na wataunganishwa na makabila au na mataifa ya Israeli katika kipindi hiki watakachokuwa wanarudi kutoka kwenye utawanyiko pamoja na wateule wa Masihi ambao wamefanya Agano thabiti na Mungu.

Kwenye kipindi hiki cha marejesho ya mwisho kutakuwa na maangamizi na maafa makuu kwa kiasi kisichowahi kushuhudiwa kwenye mchi ya Shamu (Syria) yatakayofanywa na Utorokaji mkuu. Wilaya ya Harach iliyoko nchini Syria (jina hili kwa Matamshi na Uandishi wa lugha ya Kishamu hutamkwa ‘arka na limetajwa kwenye kitabu cha Mwanzo. 10:17) na Hamath kutakuwa ni mahali pa amani kwa wote waliochoka kwa kuteswa kwa ajili ya imani yao na kulitii kwao neno la Bwana wao (Zekaria 9:1-2).  Kwa maneno mengine ni kusema kwamba, watakuwa wameongoka na kuwa sehemu ya mwili wa nyumba ya Israeli watakaokuwa na Masihi. Ndvyo pia miji ya Tiro na Sidon na nchi yote ya Lebanon watakumbwa na mchakato huu na Palestineyote na Gaza wataogopa sana na kuona aibu. Baadhi ya miji hii itapunguzwa ukubwa wake kutokana na maangamizo yatakayotokana na matendo yao ya kumchukuza Yahova wa Israeli, na Masihi kwa kuto kutubu kwao. Ni kweli kwamba baadhi yao watakaosalia watatubu na watafanywa kuwa miongoni mwa wataoshikilia nyadhifa za utawala katika Yudea na Gaza (Ekron iiliyo kwenye nchi ya Wafilisti) na kwa Wayebusi. Hawa ni wale watakaosalia huko Yerusalemu yaani Wakaanan wa Kiyebusi ambao hatimaye wamekuwa ni sehemu ya Yuda kama livyofanya Wakaanan. Kwa hiyo, Wayebusi hawa wenye nasaba damu na Yuda (YDNA) wataingia kwenye imani ya kweli kipindi hiki cha Masihi pamoja na wanaume wenye Nasaba-Damu (YDNA) ya kabila la Yuda na watashirikishwa kwenye mpango wa utawala. Yuda wataongoka kama watakavyokuwa waefraim pia (watakaoishi kwenye nchi za Lebanon na Yordan wakienea maeneo yote ya Gileadi na Yurdan ambazo zitakuwa ni sehemu ya Israeli: kama unavyoweza kuona hapo chini). Hawawote, yaani Israeli na Yuda wataushughulikia mfumo wa dini uwongo unaotokana na muungano wa imani za kipagani za Kiyunani na Kirumi kama tulivyoona kwenye sehemu ya 1. Hawatakuwa na silaha na wataongelea amani kwa mataifa na milki yao itakuwa ni kutoka bahari hadi bahari hadi kwenye mwisho wa dunia. Watakuwa ni taji na fahari kwa Bwana Mungu (Zekaria 9: 10-17).

Sura ya 10 inatuelezea kuwa tunapaswa kuomba mvua kwenye kipindi chake cha Mvua Nyingi (kama isemavyo Kumbukumbu la Torati 11:14) ambacho ni kipindi cha mmwagiko wa Roho Mtakatifu kitakachotokea katika Siku za Mwisho. Mmwagiko huu ni wa muhimu kwa ajili ya kushamiri kwa ibada za sanamu kwa wachungaji wanaopenda kusema owongo kwenye unabii wao na mabashiri yao na kufanya ulozi.

Kundi la kondoo limeenda kusiko na mwelekeo bila ya wachungaji (Zekaria 10:2). Mungu aliwaadhibu wachungaji pia na mbuzi (wale ambao sio miongoni mwa wateule wa Mungu), (aya ya 3). Kwenye mmwagiko huu, Roho Mtakatifu anamwagwa juu ya watu wa Yuda na Mungu wa Pekee na wa Kweli, Bwana wa Majeshi na atawandaa kwa vita itakayotokea kwenye kipindi hiki cha mwisho. Wale wanaoitwa Wayahudi wenye itikadi kali wataondolewa na makuhani wao wataondolewa na taifa la Yuda litaanzishwa ili lishughulike na dunia kwenye wongofu wao. Wayusufu watahuishwa tena pia na kuletwa kwenye imani ya kweli na Mungu atawarejesha tena ili “kuchukua nafasi yao” (aya ya 6). Wale walio wa Efraimu watakuwa kama mtu mkubwa na mwenye uwezo na roho zao zitafurahi na watoto wao wataona hivyo. Mungu atakuwa amewakomboa na wataongezeka na kuenea kwenye mataifa yote na watatubu na kurudi tena (aya za 7-9). Efraimu atarudishwa kutoka Misri na Ashuru na wataletwa kwenye nchi ya Gileadi na Lebanon na mahala pao hapataonekana wala kuwatosha wao kukaa (aya ya 10). Kwa hiyo, Efraimu watamiliki nakuunganishwa na Lebanon na Yordan na kuenea kwenye nchi yote. Israeli watatanuka na kuenea kutoka kwenye Mto wa Misri hadi kwenye mto Frati na kwenye Jangwa la Uarabuni hadi kwenye bahari.

Kwa sasa mambo haya yanatokea huko Misri na Ashuru ambao watatiishwa chini na kuandaliwa kwa kazi yao kwenye Ufalme wa Mungu (aya ya 11) na watatiwa nguvu katika Bwana na watatembea juu-chini na kotekote kwa jina lake (aya ya 12).

Mambo haya yote yanaanza kutokea sasa na yataletwa na kuonekana hivi karibuni.

Sura ya 11 inaelezea kuhusu mchakato wa kuvunja kwa umoja wa Israeli na Yuda na kukomeshwa kwa ukuhani na mafundisho yao ya uwongo. Mchakato huu umechukua kipindi kirefu sana na unaishia kwenye kipindi cha wachungaji wajinga. Ole wao watu hawa ambao ni wachungaji wanaotumikia vinyago na kuliacha kundi la kondoo. Wanalipa kwa mikono yao ya kulia na machoyao ya kulia, (aya ya 11:17).

Sura ya 12 inaelezea mzigo wa wito ulio kwenye neno la Bwana kwa Israeli. Ataufanya Yerusalemu kuwa ni kikombe cha kutetemesha kwa wale wote wanaojifunga wenyewe kwake na kwa wote watakaouzingira Yuda na mji wa Yerusalemu. Wale wanaoushambulia watateketezwa. Wakazi wa Yerusalemu wa Yerusalemu wataongoka na kurejeshwa kwa uweza wa Bwana Mungu wao. Wakuu wa Yuda watawatumia watu wa Yerusalemu kuwa ni nguvu na kinga yao wakiwa wamepata uweza huo kutoka kwa Bwana wa Majeshi (12:5-6). Yuda wataokolewa kwanza ilikwamba Yerusalemu na nyumba yote ya Daudi wasijitukuze kwa ajili hii (12:7). Siku hiyo Bwana atawalinda wenyeji wa Yerusalemu, na yeyote mwenye mshangao na hadithi miongi mwao atakuwa kama Daudi, na nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, au kama Malaika wa Bwana mbele yao (au vichwani mwao) (12:8). Andiko hili linaongeleza moja kwa moja kuhusu Ufufuo. Daudi ameshakufa na tena tunaambiwa kuwa yeye na nyumba ya Daudi watakuwa ni miungu wadogo kama alivyo Malaika wa Bwana kichwani mwao ambaye ni Masihi na mtu wa Rohoni au mwana wa Mungu. Kwa hiyo imeandikwa:
‘Nimesema kuwa, ninyi ndinyi miungu?’na Kristo hatimaye akajitangaza kuwa ni Mwana wa Mungu (Yohana 10:34-36).

Kutoka kipindi hiki kutakuwa na chemichemi zitakazofunguliwa kwa ajili ya wale watakaopenda kuongoka na ubatizo ili waweze kuingia kwenye Nyumba ya Bwana, na ulimwengu wote utaanza kuongoka. Sura ya 13 inaendelea kuelezea wazo hili (13:1). Tangu siku ile hakutakuwa na majina mengine tena ya vinyago au ya mapepo yatakayokumbukwa (aya ya 2a). Pia manabii wote na roho zote chafu zitaondolewa katika Israeli. Mfumo wa dini ya uwongo utaondolewa pia pamoja na waalimu wake wa uwongo (aya ya 2b). “Manabii” watakoma au hawatakuwepo kwa kulazimishwa na watu wao wenyewe na watajitangaza kuwa ni wafugaji na kusema kwamba walifundishwa kutunza akiba kwa ajili ya vijana wao (aya ya 3-5).

Kwa sehemu zote mbili wataondolewa mbali na theluthi moja itabakia na theluthi moja nyingine iliyobakia watasafishwa kwenye moto na watatakaswa ili wamtumikie Mungu na (Zekaria 13:8-9).

Ili kufanikisha hilo, tunajionea kwenye Sura ya 14 kwamba Bwana Mungu atayainua mataifa dhidi ya Yerusalemu na mji utatekwa na kuchukuliwa, nyumba zitachomwa moto na wanawake watatekwa na kufanywa vibaya na nusu ya mji watakwenda utumwani na watakaosalia hawataondolewa kwenye mji. Hivyo basi Mungu atausafisha Yerusalemu na wale wasio na imani na waongofu. Na katika kipindi hiki, Yahova ambaye ni Masihi, elohim wetu atarudi pamoja na wateule wote na atasimama kwenye Mlima wa Mizeituni. Mlima utagawanyika vipande viwili nabonde kuu la takriban k.m. 66 litafanyika upande wa Kaskazini na Kusini na mji wa Yerusalemu utakuwa katikati yake kama ilivyoelezewa kwenye Sehemu ya I (aya ya 4-5).

Kipindi hiki kitakuwa ni cha taaruki kubwa na huenda kitakuwa pia cha vita vitakavyopiganwa kwa silaha za nyukilia. Wale waliochwa kama Wayahudi walioongoka watapigana wakiwa mjini Yerusalemu na utajiri wa mataifa utakusanywa na watapewa wao (14:14). Tangu kipindi hiki na kuendelea mataifa yote yaliyoupinga na kuupiga mji wa Yerusalemu watatuma wawakilishi wao waende Yerusalemu kila mwaka ili kuitunza Sikukuu ya Vibanda. Na wale wote ambao hawatawatuma wawakilishi wan chi zao, mvua haitanyesha kwao kwa majira yake mwafaka na watadhikika kwa magojwa ya tauni ya Wamisri (Zekaria 14:16-19).  Hekalu za Sayuni litakuwa Takatifu na kitu cha kupendeza na muhimu sana huko Yerusalemu na katika Yuda na patakuwa ni mahali patakatifu kwa Bwana wa Majeshi. Mfumo utakaoanzishwa pale utakuwa umefanywa vizuri na kwa uangalifu sana na sadaka za kuteketezwa au za kuchinja wanyama zitafanyika kwa usimamizi makini wa makuhani tena kama ilivyokuwa zamani. Maneno haya yanatoka kwenye Maandiko matakatifu, na Andiko halitanguki (Yuhana 10:35).


No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG