MKURUGENZI REDIO 5 AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUANDIKA NA KUANDAA VIPINDI VYA KILIMO
Posted by M2S on August 16, 2014
Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha Bw Robert Francis akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kufanya halfa fupi iliyofanyika mjengoni kwao ,ya kuwapongeza kwa kushika nafasi ya kwanza katika sekta ya mawasiliano na habari kwa ukanda wa kaskazini maonyesho ya nane nane, Pamoja na David Rwenyagira aliyepata Tuzo za Tanapa hivi karibuni
Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha Bw Robert Francis akiwa anampongeza Mfanyakazi wa kituo hicho David Rwenyagira kwa kupata Tuzo na kushika nafasi ya kwanza upande wa Redio katika eneo la kutangaza utalii wa ndani na mshindi wa pili pekee kundi la kutangaza masuala ya Uhifadhi upande wa Redio zilizotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) hivi karibuni
David Rwenyagira akiwa anatoa pongezi kwa Mkurugenzi wao kwa kuweza kuona mchango wao katika kampuni hiyo ambapo pia aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari hapa Nchini kutoa ushirikiano kwa wanahabari wao katika kuibua habari za kijamii ikiwa nipamoja na kuwaezesha kufika vijijini
Bw Robert Francis akiongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo, ambapo pia alitumia fursa hiyo kuvitaka vyombo vya habari kuandika na kutangaza habari zinazohusu wakulima vijijini hali itakayosaidia kupatikana kwa wataalam wa kuwasaidia katika kilimo ikiwa nikukuza ajira katika upande wa kilimo
Pia amewaomba waandishi wa habari Tanzania kupeleka kazi zao katika mashindano mbalimbali hali itakayosaidia kujipima na kuongeza ujuzi zaidia huku akimtolea mfano mtangazaji wa kituo hicho David Rwenyagira aliyepata TUZO na kushika nafasi ya kwanza upande wa Redio katika eneo la kutangaza utalii wa ndani na mshindi wa pili pekee kundi la kutangaza masuala ya Uhifadhi upande wa Redio zilizotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) hivi karibuni
No comments:
Post a Comment