Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, November 8, 2014

MSHINDI WA TMT 2014 MWANAAFA MWINZAGU AFAULU MITIHANI YAKE YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2014.


 Pichani (Katikati) ni Mwanaafa Mwinzagu ambae ni Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wafanyakazi na Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya kutangazwa mshindi wa Kitita cha Milioni 50 za Kitanzania katika fainali ya shindano la TMT lililomalizika Mnamo tarehe 30 Aug 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City na Kumtangaza Mwanaafa Kuwa Mshindi kwa Mwaka 2014.
 Mwanaafa Mwinzagu akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa mshindi wa Shindano la TMT 2014 lilifanyika tarehe 30 August 2014 katika Ukumbi wa Mlimani city.Picha na Josephat Lukaza.
Mwanaafa Mwinzagu ambae alishiriki Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) huku akiwa ni Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Tandika iliyopo Mjini Mtwara katika Manispaa ya Mtwara amefaulu mitihani yake ya kumaliza elimu ya Msingi Kwa Kupata daraja C huku Masomo ya Hesabu na Sayansi akiwa kafanya vizuri sana kwa Kupata Daraja B.
 Wakati Shindano la TMT lilipofika Mtwara kwaajili ya kusaka vipaji vya kuigiza Ndipo Mwanaafa alipojiunga na Kuja kushiriki Katika SHindano hilo Kubwa na lenye mvuto wa Pekee Afrika Mashariki na Kati. Wakati akihojiwa mara baada ya Kutoka katika hatua ya Kwanza ya Shindano hilo lililofanyika Mtwara na kuhojiwa Mwanaafa Mwinzago alisema “Hiki ni Kipaji kwahiyo sina haja ya kuficha na pia naweza Kukosa kwenye Shule nikapata Kwenye Kuigiza na ndio maana nimekuja Kushiriki” Vilevile alipoulizwa Je Ikitokea Ukashinda itakuwaje Shule na Sanaa? Alijibu kuwa “Ikitokea nikashinda katika ngazi ya Kanda ya Kusini Nitaenda Kambini Dar Es Salaam na kuacha Shule kwanza, Maana Shule Ipo ila Shindano hili linapita tu Kwahiyo Naweza kupata kwenye Sanaa na nikishinda basi nitarudia Darasa”.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG