Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, November 8, 2014

NGUMI KUPIGWA JUMAPILI MANZESE UKUMBA WA MANYARA

BONDIA Samsoni Maisha wa kyela Mbeya amewasili jijini Dar es salaam na kutamba kunyakuwa ubingwa wa TPBO kwa kumpiga Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano utakaofanyika novemba 9 mwaka huu katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam
mpambano huo wa raundi kumi kugombania ubingwa wa taifa unaotambuliwa na TPBO utatanguliwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya julius Kisarawe na
Moro Best mpambano wa raundi kumi pia mwandaaji wa mpambano huo Jafari Ndame amesema maandalizi yote yapo tayali hivyo wanasubili siku tu kukamilisha mpango mzima
Aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Karim Ramadhani atapambana na Stevin Kobelo na Robinson Msimbe atamenyana na Fadhili Boika na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG