Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, November 3, 2014

PAUL MAKONDA AKANUSHA KUMPIGA MZEE WARIOBA NA KULAANI WALIOANZISHA VURUGU, ASEMA ALIMSAIDIA AMON MPANJU NA MZEE WARIOBA KUTOKA SALAMA UKUMBINI

 M1 Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha vitu alivyokwenda navyo kwenye mdahalo huo ambavyo ni katiba ya sasa na katiba pendekezwa kwa ajili ya kutumia kujibu hoja mbalimbali wakati wa mdahalo huo, Makonda amelaani na kukanusha kuwa hakumpiga Mzee Warioba isipokuwa alikuwa na kazi moja ya kuhakikisha anamsaidia Anold Kayanda mwandishi wa BBC ambaye aliumizwa  katika vurugu hizo na  Mzee Warioba na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba asiyeona Amon Mpanju  wakati wa vurugu zilizotokea katika  mdahalo wa kujadili rasimu ya Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza  jana, ambapo Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari, Dar es Salaam. Pia Makonda amesema kuwa hawezi kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu kama babake mzazi. Amesema kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo
 M3Makonda akisisitiza jambo katika mkutano huo ambapo pia aliwaambia kazi kubwa aliyoifanya wakati wa vurugu hizo, ni kumsaidia Warioba kutoka salama pamoja na Mwanasiasa mwenye ulemavu wa macho Amon Mpanju ambaye pia alikuwa anamuokoa ili asipatwe na dhahama hiyo.
M4Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wakimsikiliza kwa makini.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG