Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, November 13, 2014

RANGERS VS MAJIMAJI KARUME KESHO


index
KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, kesho kinajitupa kwenye Uwanja wa Karume kuvaa na timu ya MAjimaji ya Songea, katika mchezo wa
Ligi Daraja la kwanza.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa timu hiyo Asha Kigundula, alisema kuwa
wanatarajia kuona upinzani mkali kutoka katika timu hiyo ambayo  mpaka sasa ndiyo inaongoza
ligi, wakati wao wakishika nafasi ya pili.
Kigundula alisema kuwa kikosi chao tayari kipo kambini kikijiandaa na mchezo huo, huku
kocha wao Ally YUsuph ‘Tigana’ akijipanga kuhakikisha pointi tatu zinabaki nyumbani.
PIa Kigundula amewataka wapenzi kujitokeza kwa wingi kuipa ushirikiano timu yao ambayo
inapambana kuhakikisha inapanda daraja msimu ujao.
“Kikubwa tukipata ushirikiano kwa wapenzi ambao wamekuwawakijitokeza kutushangilia mwanzo
mwisho tunaomba mjitokeze kutushangilia tufanye vizuri”alisemaKIgundula
Rangers ina pointi 16, baada ya kucheza mechi 8 huku wanaoongozawakiwa Majimaji
wakitofautiana kwa pointi mbili, endapo Rangers itashinda itakuwa ikiongoza kwa tofauti ya 
pointimoja.
Ikiwa imeshinda mechi nne na kutoka sare
mechi nne , huku ikiwa inakimbizana na Majimaji ambayo nayo ina pointi 15.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG