Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, November 13, 2014

SHOGA, MWANAMKE LITAWALE JUKWAA!

Mmh! Mshaanza eti nimeshaingia mama Chaunabe kitanga na njia nisiye na breki kwenye domo langu. Wahenga wanasema kinywa cha mkubwa kinanuka lakini maneno hayanuki. Najua maneno yangu ya shombo huenda hayakufurahishi wewe ambaye kila kukicha unabadili wanaume na kuonekana una hila.
Jamani nia yangu nzuri, shida yangu kukuona unafurahia mapenzi, mpenzi wako umpe limbwata lisilo mzizi wala hirizi.
Leo nataka kuzungumzia matumizi ya sauti kwa mwanamke kama nilivyokwishakueleza mwanzo ukijua kuitumia sauti yako vizuri lazima mwanaume apagawe.Unamkuta mwanamke akiwa peke yake sauti hiyohiyo akiwa na mwanaume haibadiliki. Mwanamke unatakiwa kutumia sauti nyingi ili kutofautisha maeneo.
Unapoitwa na mwanaume lazima uitikie sauti ya kudeka, isilainike sana iwe laini ya wastani, iwe na tofauti na unapoongea na mwanamke mwenzako au mwanaume asiyekuhusu.
Pia unapokuwa faragha na mwanaume lazima sauti yako ibadilike ili uonekane kweli upo naye kama mwanamke anayehitaji kitu. Pia atambue yupo na mwanamke anayefaa kumsisimua muda wote. Usifikiri mpaka umvulie nguo mwanaume ndiyo asisimke hata sauti mwake tu.
Mnapokuwa chumbani saresare maua, ngozi kwa ngozi hapa napo kuna sauti yake, mtoto wa kike sauti itolee ndani, iambatane na pumzi kama umemaliza mbio ndefu au mwenye ugonjwa wa pumu ukisaidiwa na jicho, japo ipo siku jicho nalo nitaliongelea katika kumrusha akili mwanaume.
Kila unapoguswa sehemu moja kwenda nyingine, badili sauti kama kinanda huku ukijilegeza, najua umeshaanza.
“Ooh mbona ulituambia tusijilegeze tunapokuwa kwenye uandaaji wa kilimo.”
Narudia kusema mtoto wa kike kulegea huongeza raha  huku ukiitumia sauti yako kulalamika kuonesha kweli umeshikika. Lakini wakati huohuo nawe lazima umlize kabla ya mpambano.
Hii ipo sehemu mbili  mwanaume anatangulia kutayarishwa kisha mwanamke, hapo una haki ya kulalama huku ukiiomba hukumu inachelewa. Hukumu kwa mwanamke ni haki yake hasa mchicha unapokolea nazi, mwiko ndiyo unaotakiwa kuingia kwenye chungu ili kuugeuza uive vizuri.
Usikae kimya kama bubu, lazima uwe mzungumzaji ili mpenzio akiona kuna mabadiliko akuulize. Itumie sauti uwezavyo kumchanganya mwanaume usipayuke na kuwa karaha bali itoke ndani ikiambatana na pumzi nzito zisizoumiza masikio bali ya kupekecha na kusisimua.
Wanaume ni kama watoto wadogo kitu kidogo ambacho hukikuta kwako humfanya akugande na wewe kujikuta ukiongeza kipato cha mkate wako wa kila siku. Kuna baadhi ya wanawake wananiudhi utamkuta sauti ya kumtoa nyoka pangoni anaitumia mbele za watu.
Basi mtu kama huyo akiingia ndani makelele mtindo mmoja kama kaumwa na nyoka.
Mmh! Jamani basi mtoto wa kike jicho nalo lizungumze lilegee kama unaonewa, wengine huweka na kidole kidogo mdomoni jicho kama linaogopa kuona. Ukimuangalia mwenyewe anasisimka kama yupo juu ya pikipiki basi asichoke kuvuta mafuta kwani spidi mita inakuruhusu, ukanyage mafuta unafikiri ni nini kinafuata kama si kuifurahia safari.
Sauti yako ioneshe basi kweli mtoto wa kike umegusika ulipotaka ndipo, mpe sifa zake, siyo kukaa kimya kama mwanajeshi aliyejificha adui asimuone baada ya kuishiwa risasi.
Mwanamke lazima ujue kukitawala kitanda, na si kitanda tu, ujue kujituma popote mpenzio anapotaka kulianzisha. Unazibana sauti, unaibana pumzi, unamuogopa nani, hebu acha kuniudhi kula nanasi kwahitaji nafasi na mwanamke kujiachie babu wee.
Kwa leo yatosha, Loh! Lione, ushaanza kujilamba kutaka niendelee. Jamani eeh, kitamu kula kwa hamu tukutane wiki ijayo. Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG