- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza na waandishi wa habari wa Zanzibar kwenye ofisi ndogo za
mashirika ya Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar kuhusiana na mafanikio
ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka
2011 na sasa ukiwa ukingoni. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Tanzania, Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mtaalam wa Mahusiano na
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea kufurahishwa
kwake na Serikali Tanzania kwa kupigia hatua katika kutoa ajira nyingi
kwa walimu kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.(Martha Magessa)
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Zaidi ya watoto 3000 waliokuwa
wakikabiliwa na utapiamlo nchini Zanzibar sasa wapo katika hali nzuri
baada ya Umoja wa Mataifa (UN)kwa kushirikiana na wadau wengine
kufanikisha programu ya kusaidia kukabili utapiamlo mkali kwa watoto
hao.kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari uliofanyika hivi karibuni ambapo UN ilielezea mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP) ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja huo ukiadhimisha miaka 69 ya uwepo wake imefurahishwa na maendeleo yaliyopatikana katika maeneo ambayo ilikuwa imejikita kusaidia kukabili umaskini,kuhakikisha utawala bora na kusaidia jamii.
Alisema pamoja na kuendeleza na juhudi za kukabiliana na utapiamlo katika visiwa vya Pemba pia Umoja huo umefurahishwa na hatua zilizofikia katika kukabiliana na vifo vya mama na mtoto na kusema ni wajibu kuhakikisha watoto hawana matatizo ya utapiamlo kwani wao ndio msingi wa taifa la sasa na lijalo.
Alisema hata hivyo upo umuhimu wa kuendelea na washirika wengine wa maendeleo kuona kwamba tatizo la utapiamlo la visiwa vya Pemba kwa watoto linamalizwa.
Alisema
pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa unaendelea na ujenzi wa uwezo
kwa baraza la wawakilishi ili kuhakikisha kwamba baraza hilo linawezesha
kuwepo kwa sheria nzuri na bora na zinazotekelezeka ambazo hazikwazi
kukua kwa demokrasia na ustawi wa jamii.
Aidha
alisema kwa kuzingatia kwamba mwaka huu mwishoni kuna uchaguzi wa
serikali za mitaa na pia uchaguzi mkuu mwakani pamoja na kura ya maoni
ya katiba, Umoja huo unaendelea kufanyakazi na Tume ya uchaguzi ya
Zanzibar kwa kuiwezesha kitaalamu kuweza kufikisha elimu ya uraia kwa
wananchi.
Aidha
katika masuala ya utawala bora Umoja wa Mataifa unashirikiana na taasisi
za sheria kwa ajili ya kufanya mabadiliko katika mfumo wa sheria za
watoto ili kuwepo na usalama mkubwa kwa watoto hasa kutokana na
utamaduni uliopo visiwani kwa sasa.
Aidha
alisema kwamba yamepatikana mafanikio makubwa katika sekta ya tiba na
kuzuia maambukizi ya Ukimwi na kuondokana na unyanyapaa.
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Zanzibar, Talib Ussi akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Aliwahimiza
waandishi wa habari kuwa daraja la kuelezea mafanikio na pia changamoto
zinazotokana na program za Umoja wa mataifa zilizolenga kusaidia
maendeleo ya wananchi wa Zanzibar.
Alisema
matokeo ya program ya kusaidia maendeleo ya Tanzania (UNDAP) ndiyo
yatakayotumika kutengeneza UNDAP 2 ambayo inatarajiwa kuanza katikati ya
mwaka 2016.
Katika
mkutano huo ambapo waandishi walipata nafasi kubwa ya kuuliza masuala
yanayohusu shughuli za Umoja wa Mataifa Zanzibar, Bara na duniani kwa
ujumla Alvaro alizungumzia pia umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika dunia
inayobadilika.
Alisema
pamoja na madhumuni ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, baada ya vita
kuu ya dunia ya pili mwaka 1945 ya usalama na kujenga uchumi baada ya
kuharibiwa na vita yapo palepale, mabadiliko katika utendaji kwa lengo
hilo hilo la usalama na maendeleo ni dhahiri.
Alisema
mathalani malengo ya millennia (MDGs) ambayo yalisanifiwa kwa lengo la
kuleta maendeleo duniani katika demokrasia, utawala bora na ustawi wa
jamii, bado yanatakiwa kuimarishwa kupitia mpango mpya wa maendeleo SDGs
wenye lengo la kutokomeza umaskini uliotopea duniani ifikapo mwaka
2030.
Afisa
Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma
Ledama akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusiana
na mafanikio ya mradi wa kusaidia maendeleo nchini Tanzania (UNDAP)
ulioanza mwaka 2011 na sasa ukiwa ukingoni.
Alisema
ni matumaini yake kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na UN katika
kuhakikisha kwamba mafanikio katika MDGs yanaendelezwa na pia
kukamilisha yale ambayo hayakufikiwa kwa lengo la kutokomeza umaskini
uliotopea ifikapo mwaka 2030.
Alisema
mafanikio ya UNDAP kwenye utawala bora, ustawi wa jamii na uondoaji
umaskini na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania, ni matokeo ya ushirikiano
kati yake ya mamlaka mbalimbali nchini Tanzania na kwamba UN itaendelea
kushirikiana na mamlaka hizo kuhakikisha maendeleo ya kuwezesha amani na
usalama na ukuaji wa uchumi yanapatikana.
Naye
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia
Nkhoma Ledama amesema lengo la kukutana na waandishi wa habari wa
Zanzibar lilikuwa kuangalia mafanikio na namna ambavyo program za Umoja
wa Mataifa katika visiwa vya Zanzibar zinafanyakazi.
Alisema
kwamba shughuli za Umoja wa Mataifa visiwani humo zinaweza tu kujulikana
kwa wananchi kwa kupitia waandishi wa habari ambao wanakuwa wanajua
Umoja huo unafanya nini na wapi.
Mkutano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wa Zanzibar ukiendelea.
Mwandishi
wa habari wa TBC, Kulthum Ally, akiuliza swali kuhusiana namna Umoja wa
Mataifa unavyoweza kuwasaidia Wanawake wa Zanzibar kupata nafasi za
uongozi sawa na wanaume.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (waliokaa
katikati), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira
Rodrigues (kulia) pamoja na Meneja wa Baraza la Habari Zanzibar,
Suleiman Omar (kushoto) katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment