Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, November 7, 2014

Watu 13 wafariki Kilombero katika ajali ya treni



Watu kumi na watatu wamefariki katika ajali iliyotokea huko Kibereke, Ifakara mkoani Morogoro, kati ya basi la abiria la Al Jabir lenye namba za usajili T725 ATD lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Ifakara na treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero akizungumza na TBC kwa njia ya simu, Hassan Masala amesema:
"Chanzo cha ajali ni basi ambalo limeigonga treni, treni ambayo ilikuwa inakatiza hapo kwa hivyo bahati mbaya ikawa imefika na ikakatiza kwa hiyo ikagongwa kwa nyuma."

Masala amekaririwa akisema kuwa watu waliojeruhiwa ni 40 ambapo 14 wametibiwa na
kuruhusiwa kurudi majumbani mwao huku 26 wakilazwa katika kituo cha afya cha Kibaoni na katika hospitali ya Mt. Francis, huku miili ya marehemu ikihifadhiwa hospitalini hapo.

Naye Kamanda wa polisi Mkoani humo Leonald Paulo amenukuliwa akisema kuwa ajali hiyo ilitokea leo majira ya saa 9:15 alasiri.

Kamanda huyo alisema kati ya watu walioaga dunia, sita wanaume, wanne wanawake na wawili ni watoto wakike wenye umri kati ya miaka mitano na sita. Aliwataja marehemu watatu waliotambulika katika ajali hiyo kuwa ni Frugensia Lusangila (60), Albeta Lusangila (62) wakazi wa Ichonde Mangula na Joseph Kazwila (34) mkazi wa jijini Dar es Salaam.

Dereva wa basi hilo alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea na polisi wanamtafuta wakati uchunguzi ukiwa bado unaendelea.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG