Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, November 27, 2014

Wezi wamwibia Wanyama Uingereza

Mkenya Victor Wanyama kushoto anayechezea kilabu ya Southampton akikabliana na mchezaji wa kilabu ya Villa.Nyumba ya mchezaji huyo ilivunjwa na wezi alipokuwa akishiriki katika mechi hiyo.
Maafisa wa polisi wanachunguza kisa kimoja ambapo wezi walivunja na kuingia katika nyumba ya mchezaji wa kilabu ya Southampton Victor Mugubi Wanyama nchini Uingereza na kumuibia mali yake usiku wa jumatatu.
Shati moja la kiungo wa kati wa timu ya Barcelona Andres Iniesta ,pamoja na nguo za wanamitindo kadhaa pamoja na jozi 20 za viatu ni miongoni ya vitu vilivyoibwa.
Wezi hao pia waliiba gari la mchezaji huyo aina ya Land Rover lenye thamani ya shilingi millioni 8.4 fedha za kenya,fanicha,Runinga pamoja na vifaa vyengine vya kielektroniki .
Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 23 anaishi katika nyumba ndogo na polisi wameshangazwa kwamba majirani zake hawakuamshwa na kelele za uvunjaji huo.
Kikosi cha timu yake ya Southamptom kilikuwa kimesafiri hadi Villa ambapo bao la dakika za mwisho liliifanya mechi hiyo kuwa na sare ya 1-1.
Wanyama ameshiriki katika mechi 14 msimu huu na kufunga mabao matatu huku Southampton ikiendelea kupigania nafasi ya kufuzu katika mechi za UEFA.
Ni mchezaji aliyeuzwa kwa kitata cha juu kutoka Uskochi baada ya Celtic kumuuza kwa pauni 12.5 mnamo mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG