Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, December 8, 2014

Ndege iliyobeba silaha yakamatwa Nigeria

Halikopta mbili za kijeshi ni miongoni mwa zana za kivita zilizokamatwa kwenye ndege hizo ya mizigo.
Ndege ya mizigo iliyosheheni silaha za kivita imekamatwa katika uwanja wa ndege wa Kano nchini Nigeria.
Licha ya kukanusha awali, Urusi imesema inamiliki ndege ya mizigo iliyozuiwa katika uwanja wa ndege wa Kano kaskazini mwa Nigeria baada ya kugunduliwa imebeba silaha ambazo hazikuwa zimearifiwa.
Hata hivyo, Msemaji wa Ubalozi wa Urusi nchini Nigeria, ambaye aliliambia Shirika la Habari la Urusi TASS kwamba wanamiliki ndege hiyo, amesema silaha hizo ni za kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari wa BBC ndege hiyo bado inashikiliwa uwanjani hapo.
Awali, msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya kati aliiambia BBC kwamba hawafahamu chochote kuhusu helikopta mbili, magari ya kijeshi na silaha nyingine zilizokuwa katika ndege hiyo.
Hata hivyo baadaye alipiga simu kufuta usemo wake kwa kusema kuwa ndege hiyo ilikuwa imebeba silaha kwa ajili ya wanajeshi wao, walioko katika kambi ya N’damena, ambazo zitapelekwa baadaye Ufaransa.
Msemaji wa Ubalozi wa Urusi mjini Abuja alisema pia ndege hiyo ni yao. Akitatanisha taarifa aliyoitoa awali kwamba ndege hiyo si yao.
Kwa nini Ufaransa inatumia ndege ya Urusi kubeba silaha zake? na kwa nini ilisimama katika uwanja wa Kano, wakati ikiwa inaelekea nchi jirani ya Chad na hata Cameroun ikitokea Afrika ya kati? Kwanini baadhi ya silaha hazikuorodheshwa katika ndege hiyo kama zimebebwa?.
Hayo ni maswali yalioulizwa pande zote.
Seriakli ya Nigeria ambayo ndio muhusika mkuu wa tukio hilo, haijasema chochote.
Baadhi ya wachambuzi wanasema Nigeria inamiliki silaha hizo ilizonunua katika soko haramu. Wengine wanasema silaha hizo zilinunuliwa kutoka kwa waasi wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya kati, wakielezea kwanini ndege hiyo imeingia nchini humo kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.
Nigeria imewekewa vikwazo vya silaha kutoka Marekani na nchi hiyo imekuwa ikiarifiwa kutumia njia zisizo halali kupata silaha kwa ajili ya kupambana na wapiganaji wa Boko haram.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG