Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, December 6, 2014

UGANDA yapuuza vikwazo vya Marekani dhidi ya USHOGA


Mwandishi wa BBC mjini Kampala, Isaac Mumena anasema kuwa Balozi Mugume ameelezea kuwa serikali ya Uganda hata hivyo itafanya mazungumzo na Marekani ili kufafanua hatua waliyochukua.
Amesisitiza kuwa wataieleza Marekani sheria hiyo inapinga tabia ambayo sio ya kiafrika na maadili ambayo hayakubaliki katika jamii nyingi za kiafrika.
Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa na athari kubwa kwa nchi hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii kuwa tayari sheria hiyo imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Vikwazo vyenyewe ni pamoja na kufutilia mbali msaada wa kijeshi, kuwapiga mrufuu baadhi ya maafisa wa serikali kusafiri nje na kupiga tanji mali zao.
Maandamano kupinga mapenzi ya jinsia mopja na kumpongeza Rais Museveni kuwa kupitisha sheria hiyo
Kadhalika msemaji wa serikali Ofwono Opondo amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa wananchi wa Uganda wanafahamu kuwa hawatategemea tena msaada wa nchi za Magharibi.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG