Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, December 17, 2014

Ukulima wa Nanasi


Kilimo cha nanasi kinastawi zaidi katika ukanda wa nchi za joto. Hapa Tanzania zao hili linastawi sehemu nyingi lakini kwa wingi linastawi mikoa ya Pwani, Morogoro, Shinyanga na Bukoba. Katika mkoa wa pwani, zao hili linalimwa katika wilaya ya Bagamoyo, Mkuranga na Kisarawe. Kwa Bagamoyo linalimwa zaidi katika kata ya Kiwangwa na maeneo ya Gongo.
Kihistoria, zao la nanasi lilianza kulimwa na wakulima wachache waanzilishi katika kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo. Mzee Seluhombo ni miongoni mwa wakulima waanzilishi aliyeanza kulima nanasi katika miaka ya 1980. Baada ya hapo, kilimo cha zao hili kiliongezeka na kuanza kulimwa na wakulima wengi wa eneo hilo.
Nanasi huliwa kama lilivyo linapokomaa (baada ya kumenywa) na pia hukamuliwa maji yake na kunywa kama juisi. Maji ya nanasi yanaweza pia kuanikwa na kukaushwa ambapo huliwa kwa kutafunwa. Aidha, baada ya kukauka husagwa na unga wake hutumika kutengeneza juisi au kuchanganywa katika vilaji vingine.
Zao hili hustawi vizuri zaidi katika ardhi yenye rutuba (firtile soil), kina cha kutosha (deep soil) na udongo wa tifutifu (sio mchanga wala mfinyanzi). Mambo yafuatayo ni muhimu kuyazingatia:
  • Epuka kupanda zao hili kwenye udongo unaotuamisha maji.
  • Epuka kustawisha kwanye udongo wenye kichanga.
  • Epuka kwenye udongo wenye mawe mawe.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG