Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, December 7, 2014

Waziri mkuu wa Somali atimuliwa

Waziri mkuu wa Somali Abdiweli Sheikh Mohammed Kushoto aliyengatuliwa mamlakani
Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu wa taifa hilo Abdiweli Sheikh Ahmed mamlakani.
Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia.
Waandishi wanasema kuwa serikali ilikuwa imelemazwa na uhasama baina ya kiongozi huyo na rais wa taifa hilo Hassan Sheikh Mohamud.
Wanasema kuwa usalama ulikuwa umezorotoa kutokana na hali hiyo.
Abdiweli ni waziri mkuu wa pili kuwahi kuondolewa madarakani mwaka huu.
Marekani imeshtumu kura hiyo ikisema kuwa haikuzingatia maslahi ya raia wa Somali.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG