Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, December 8, 2014

West Ham yaiadhibu Swansea


Mlinda Mlango wa Swansea Lukas Fabianski alitolewa nje kwa kadi nyekundu
Ligi kuu ya England iliendelea tena wiki end hii ambapo kulikuwa na michezo miwili. Katika mchezo wa awali West Ham United waliwakaribisha Swansea huku Leicester City wakisafiri hadi Villa Park kuuamana na Aston Villa.
Katika mechi ya awali kati ya West Ham United na Swansea West Ham waliiadhibu Swansea baada ya kumiminia magoli 3 - 1.
Magoli mawili ya West Ham yalifungwa na Andy Carrol katika dakika ya 41 na 66 na jingine likafungwa na Diafra Sakho.
Goli pekee la kufutia machozi la Swansea lilitiwa kimiani na Wilfried Bonny.
Mechi nyingine ilikuwa ni kati ya Aston Villa na Leicester City ambapo mechi hii imemalizika kwa Aston Villa kutoka uwanjani kifua mbele baada ya kufunga Leicester City magoli 2 -1
Leicester City ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli lililofungwa na Leonardo Ulloa baada ya mlinda mlango wa Aston Villa kutema mpira.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG