Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, January 25, 2015

Ivory Coast yanusurika

Mali
Mchezaji Max Gradel wa Ivory Coast alifunga bao la dakika za mwisho la kipindi cha pili cha mchezo dhidi ya Mali na hivyobasi kuimarisha matumaini yao ya kufuzu katika robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika.
Mali ilikuwa kifua mbele huku ikiwa na ishara zote za kuibuka mshindi baada ya Bakary Sako kufunga bao zuri kunako dakika ya saba ya kipindi cha kwanza.
Lakini Gradel alisawazisha katika dakika ya 86 ndani ya eneo la hatari.
Awali Ivory Coast ilinyimwa penalti ya wazi baada ya Wilfried Bonny kuchezewa visivyo na Molla Wague huku Kolo Toure pia akikosa bao la wazi.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG