Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, January 22, 2015

Matokeo ya uchaguzi yasitishwa Zambia

Wananchi wa Zambia katika upigaji kura
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Zambia, Bi Irene Mambilima jana alisitisha zoezi la kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu akisema tume imefanya hivyo ili vituo vingine 51 navyo vikamilishe utaratibu wa kupiga kura leo.
Hata hivyo Bi Mambilima alikabiliwa na watu wenye ghadhabu wakitaka Tume ya Uchaguzi iendelee kutoa matokeo ya chama kilichoshinda maana tume hiyo ilikuwa tayari imeshatangaza matokeo ya majimbo 14.
Hata hivyo mwenyekiti huyo wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia amesisitiza kuwa uamuzi huo una manufaa kwa wadau wote, ili kutenda haki.
"Tunaendesha uchaguzi katika nchi hii, tunafanya maamuzi na katika kufanya maamuzi hayo hatulazimiki kupokea maagizo kutoka kwa mtu yeyote. Tumefanya maamuzi. Watu wengine wanasema tufikirie tufikirie. Mnaendelea kurudia mambo hayo hayo kila wakati. Hii si jamii ya malumbano. Tumewaambia maamuzi yetu ni nini, unaweza kukubali au kukataa. Tunaendesha uchaguzi katika nchi hii, SAWA? Kwa kuwa hamkubali hakutakuwa na rais,"anasema Bi Mambilima.
Uchaguzi wa rais nchini Zambia unafanyika kufuatia kifo cha rais Michael Sata, aliyefariki dunia mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG